Wizara ya ulinzi ya Marekani inasema kuwa jeshi la nchi hiyo limefanya mashambulizi dhidi ya kundi la wanamgambo wa kiislamu la , Al Shabaab nchini Somalia.
Msemaji wa Pentagon Rear Admiral John Kirby amesema kuwa wanatathmini matokeo ya operesheni hiyo kabla ya kutoa taarifa zaidi .
Al Shabaab kwa sasa wanaendesha kampeni dhidi ya serikali ya Somalia na vikosi vya kimataifa vinavyoiunga mkono.
Afisa mkuu wa Marekani amesema kuwa maafisa wakuu wa Al Shabaab ndio waliolengwa kwenye mashambulizi hayo.
Kundi hilo lenya uhusiano na al-Qaeda lilitimuliwa kutoka Mogadishu mwaka 2011 mji ambao kwa sasa unadhibitiwa na wanajeshi wa Muungano wa Afrika.
Hata hivyo kundi hilo bado linadhibiti maeneo ya Kusini ya nchi hiyo.
Tungali tunadadisi hali na matokeo ya shambulizi na baadaye tutaweza kutoa maelezo,'' alisema msemaji wa mkuu wa Pentagon
Wakazi wa kijiji cha Hawai umbali wa kilomita 240 Kusini mwa Mogadishu, wanasema kuwa walisikia milipuko na kisha kuona moshi mkubwa ukifuka.
Mkazi mmoja aliambia BBC kwamba aliona mabaki ya gari moja liliokuwa limelipuliwa ingawa hakuona miili yoyote.
BBC/SWAHILI
No comments:
Post a Comment