Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 25 October 2013

WAZIRI DK. NCHIMBI AZINDUA MIRADI YA MAENDELEO SONGEA

Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa barabara ya lami ambayo inamaliziwa kujengwa yenye urefu wa mita 600 iliyopo katika Kata ya Mjini, Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. Barabara hiyo imegharimu zaidi ya Sh75 milioni. Dk Nchimbi yupo mjini Songea kwa ziara ya siku tano akikagua pamoja na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo jimboni mwake.

ASALAAM ALAYKUM AFRICA!

Wanachota maji mtoni, Chimala, Mbeya kabla ya kuingia darasani.


Thursday, 24 October 2013

SIKU BOLI ZOZO ALIPOIBUKIA JANGWANI!

Kikosi cha Yanga cha mwaka 1994. Kutoka kushoto waliosimama ni Salum Kabunda 'Ninja', Constantine Kimanda, Steven Casmir Nemes, Kenneth Pius Mkapa, Selemani Mkati. Waliochuchumaa kutoka kushoto ni Nico Bambaga 'Machine', Sekilojo Chambua, Edibily Lunyamila, James Tungaraza 'Boli Zozo', na Said Mwamba 'Kizota'.

Na Daniel Mbega
YOUNG Africans, ambayo mwaka 1993 iliteswa sana na wapinzani wake wa jadi, Simba, baada ya kutamba misimu miwili ya nyuma, hatimaye Jumamosi Februari 26, 1994 iliingia kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwakabili ‘wanyama hao wakali’ wa Msimbazi, ambao mwaka huo walikuwa wameongeza makucha yao kwa kuwasajili wachezaji mahiri na wauaji wa mabingwa hao watetezi wa Tanzania Bara, Yanga.

ASALAAM ALAYKUM AFRICA!

Watoto na nishati ya kuni. Itamboleo, Iringa.

Wednesday, 23 October 2013

WAZIRI WA KILIMO KATIKA ZIARA UINGEREZA

Bi Rachel Turner wa shirika la Maendeleo DFID Uingereza akihutubia.

MNALIKUMBUKA SCUD LA JANGWANI LILILOBOMOA MSIMBAZI MARA MBILI 1991?

Said Sued 'Scud' (wa tano kutoka kulia) akiwa na kikosi cha Yanga 1991


Na Daniel Mbega

ZIKIWA zimesalia siku tatu tu kabla ya pambano la Simba na Yanga, mashabiki wa timu hizo walikuwa wamepamba moto kucharurana mitaani, lakini wadadisi wa mambo walikuwa wamefikia uamuzi kwamba, pambano hilo lingekuwa kama fainali ya ligi hiyo, kwa sababu, timu yoyote ambayo ingeshinda Jumamosi Agosti 31, 1991 ingekuwa vigumu kuzuiwa na timu nyingine huko mbele isitwae ubingwa wa Tanzania Bara msimu huo.

ASALAAM ALAYKUM AFRICA!

"Yanaliwa haya, halafu wanayapenda Wazungu!"
Kaole, Bagamoyo

Tuesday, 22 October 2013

MJADALA WA WAZI TAREHE 23/10/2013;MADA: UCHIMBAJI WA MADINI YA YURANI


SEMINA ZA JINSIA NA MAENDELEO
UNAKARIBISHWA KATIKA JUKWAA LA WAZI LA MFULULIZO WA SEMINA ZA JINSIA NA MAENDELEO (GDSS) KILA JUMATANO, AMBAPO WIKI HII  MTOA MADA NI A. LUKANGA.
MADA:UCHIMBAJI WA MADINI YA YURANI KATIKA MUKTADHA WA SOKO HURIA:  JE, KATIBA MPYA ITADHIBITI UPORAJI NA KULINDA MASILAHI YETU?
Lini: Jumatano Tarehe 23/10/2013
Muda: Saa 09:00 Alasiri – 11:00 Jioni
MAHALI:  Viwanja vya TGNP, Barabara ya Mabibo Karibu na Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji Mabibo Sokoni 
WOTE MNAKARIBISHWA

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

“PRESS RELEASE” TAREHE 22. 10. 2013.
WILAYA YA  CHUNYA – KUPATIKANA NA SARE ZA  ASKARI WANYAMA PORI NA PINGU.
MNAMO TAREHE 18.10.2013 MAJIRA YA  SAA 13:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA BITIMANYANGA, KATA YA  MAFYEKO, TARAFA YA KIPEMBAWE WILAYA YA  CHUNYA MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO  KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI WANYAMAPORI WALIMKAMATA SAMWEL S/O VITALIS @ MANDE , MIAKA 34, MNYATURU, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA BITIMANYANGA  AKIWA NA SARE PAIR MOJA “KOMBATI”  ZA ASKARI WA WANYAMAPORI PAMOJA NA PINGU MOJA. MBINU NI KUTUMIA VIFAA HIVYO KATIKA UWINDAJI HARAMU.  TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUMILIKI MALI ZA SERIKALI  ISIVYO HALALI KWANI NI KOSA LA JINAI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MTU/WATU AU KIKUNDI KINACHOMILIKI MALI ZA SERIKALI /WAWINDAJI HARAMU AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI  WAHUSIKA WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA  MBEYA MJINI  – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI[GONGO].

KAMANDA WA POLISI JAMES KOMBE AFARIKI DUNIA

SOURCE: bashir-nkoromo.blogspot
 

RAIS KIKWETE ATEMBELEA MGODI WA CHUMA WA LIGANGA


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Meneja mradi wa Maganga Matatitu Resource Development limited Bw. Lawrence Manyama  kuhusu mlima huo uliosheheni mashapu ya chuma alipotembelea eneo lenye utajiri wa chuma la  Liganga wilaya ya Ludewa mkoani Njombe leo Oktoba 22, 2013.

SHINDA MAHELA KWA KUSOMA GAZETI LA CHAMPIONI

Changamkieni

ASALAAM ALAYKUM AFRICA!

Mupooooooooo!

Monday, 21 October 2013

DK. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MABUNGE YA SADC

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia vikundi vya sanaa vya ngoma za aina mbalimbali alipowasili katika Jengo la Ukumbi wa mikutano A I C C mjini Arusha kwa ajili ya kufungua mkutano wa siku 11 wa 34 kwa Mabunge ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya SADC leo Octoba 20, 2013.

YANGA FUNGA, SIMBA RUDISHA - KAMA 1996 VILE!

Picha kwa hisani ya jestina-george.com

SIMBA na Yanga zimetoka sare. Ni sare ambayo haikutegemewa na mashabiki wa Yanga waliokuwa wanaamini timu yao ingeweza kupata ushindi wa mabao mengi baada ya kuongoza kwa mabao 3-0 hadi timu zinakwenda mapumziko.

ASALAAM ALAYKUM AFRICA!

Mupooooooooo!!!!

ZIARA YA RAIS KIKWETE WILAYANI MAKETE

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiongea na Bi Sarah Mageni Sanga, mlemavu ambaye Rais alimpa pikipiki ya Bajaji pamoja na mtaji wa pesa taslimu wa shilingi milioni mbili Oktoba 28, 2009 baada ya kuguswa na mkasa wa maisha ya mkaazi huyo wa kijiji cha Lupalilo wilaya ya Makete mkoa wa Njombe alipomuona akohojiwa katika TV na kueleza kuwa maisha yake ni magumu mno baada ya ndugu na jamaa zake wote kuteketea kwa maradhi ikiwa ni pamoja na UKIMWI. Pichani Bi Sanga akimshukur Rais kwa msaada huo ambao amesema umebadili kabisa maisha yake kwani sasa anaishi kama mtu yeyote kijijini hapo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia ubora wa shati lililotengenezwa na wanafunzio wa Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA cha Wilaya ya Makete baada ya kukifungua rasmi chuo hicho mwishoni mwa juma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi  Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA cha Wilaya ya Makete mwishoni mwa juma.

Sunday, 20 October 2013

WATUMISHI WA MAHAKAMA WAASWA KUZINGATIA SHERIA, MAADILI

 
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki akisisitiza umuhimu wa kutoa adhabu mbadala kwa watuhumiwa baada ya hukumu zao kukamilika alipokuwa anaongea na watumishi wa Mahakama ya Mwanzo ya Kerege (hawapo pichani) iliyopo Wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani kwenye ziara yake ya siku moja wilayani humo. Wa kwanza kushoto ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa PwaniBahati Ndeserua, wa kwanza kushoto ni Msajili Mahakama kuu, kanda ya Dar es salaam Projestus Mhagama.
 

Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Bagamoyo Liadi Mohamed Chamshama akimwonesha Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki (mwenye gauni kitenge) na ujumbe wake eneo la mahakama ya Mwanzo ya Kiwangwa alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ya siku moja wilayani mkoa wa Pwani. (Picha zote na Eleuteri Mangi- Maelezo).