Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 11 September 2015

WATOTO 300 SHULE YA MSINGI IBUMBA WASOMEA KANISANI


Na Hastin Liumba, Kaliua

MGOMBEA udiwani kata ya Ufukutwa  wilaya ya Kaliua mkoani Tabora kwa tiketi ya CHADEMA Abdallah Mbuguma amesema katika kitongoji cha Ibumba kuna watoto zaidi ya 300 wanaosoma masomo yao kwa kutumia majengo ya kanisa la Tanzania Assembulies of God  TAG.


Akiongea kwenye uzinduzi wa kampeni za ubunge na udiwani za UKAWA wilayani Kaliua Mbuguma alisema hadi sasa watoto hao hawana chumba cha darasa hata kimoja hivyo hulazimika kutumia majengo ya kanisa TAG kusoma.

Alisema ameamua kusema hayo kwani hapo awali licha ya kukerwa na jambo hilo hakupata nafasi ya wapi asemee kero hiyo hivyo jukwaa hilo ndiko sehemu sahihi yeye kuanika uozo huo

Mbuguma alisema kutokana na hali hiyo ndicho kimemsukuma kugombea udiwani ili aweze kushirikiana na wazazi kuanzisha ujenzi wa vyumba vya madarasa ili watoto hao waweze kupata haki ya kupata elimu.

Alisema kwa kutambua elimu na umuhimu wake tayari ameshanunua mifuko kumi ya Saruji ili kuanza ujenzi wa vyumba vya madarasa haraka iwezekanavyo na wazazi wamekubali kuchangia.

Alisema Ibumba ni kitongoji ambacho kipo katika kijiji cha Sentaali ambapo kuna shule Msingi yenye vyumba viwili vya madarasa ambapo kuna umbali wa kilomita saba ili kuifikia shule hiyo kutoka kitongoji cha Ibumba.

Alisema licha ya watoto hao 300 kusomea kanisani bado kulikuwa hakuna hata mwalimu hali ambayo ilimlazimu yeye binafsi kutafuta walimu wawili ambao hadi sasa wanafundisha kanisani hapo.

Mbuguma alisema walimu aliowatafuta ni wale waliostaafu ambapo kwa sasa mshahara anawalipa yeye toka mfukoni mwake.

Alisema toka walimu hao wastaafu ameanza kuwalipa mishahara yao toka mwezi Mei mwaka huu na hadi sasa ameendelea kuwalipa.

Alisema awali wazazi walimueleza waliwahi kuchangisha fedha na kufyatua tofali za kuanza ujenzi wa vyumba vya madarasa lakini tofali hizo zilikuja kuchukuliwa viongozi wa CCM wilaya ya Kaliua na haikujulikana zilikwenda kujengewa nini.

Mbuguma alisema huu siyo wakati wa kuanza kuulizana ni nani alichukua tofali zile lakini yeye anaomba kura ili aweze kukomboa watoto wale ambao wako kama yatima kwa sasa.

Alisema ana uhakika endapo atashinda kwenye uchaguzi huo atahakikisha kipaumbele chake cha kwanza ni elimu ya kuanzia awali hadi kidato cha nne ikifuatiwa maji kwani kuna hli mbaya ya upatikanaji wa maji na afya.

No comments:

Post a Comment