Munde Tambwe
Na Hastin Liumba, Tabora
MBUNGE viti maalumu Chama cha mapinduzi (CCM) ambaye anasubiria kuthibitishwa baada ya uchaguzi,Munde Tambwe amesema wanafunzi wa kike wa vyuo vikuu Tabora wanakabiliwa na changamoto nyingi zinazotakiwa kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu.
Tambwe alisema hayo wakati akiongea na wanafunzi wa kike wa vyuo vikuu mkoani hapa ili kusikiliza kero zao na kubadilishana mawazo.
Tambwe Vyuo alivyokutana navyo ni chuo cha utumishi wa umma (TPSC), Theophil Kisanji, VETA, TUMBI-MATI, SAUT,
Tambwe alisema wanafunzi hao serikali na wadau wa elimu tunapaswa kungalia upya namna wanafunzi hao tutakavyo wasaidia kutatua kero na changamoto hizo.
Alisema endapo atapata ridhaa tena kuwa mbunge viti maalumu atakuwa karibu na wanafunzi wa kike vyuo vikuu ili kujua na kutafuta ufunzi wa kero zao.
Alisema wanafunzi hao wanakabiliwa na upungufu wa bweni na hostel,huduma duni za afya,ajira serikalini,ambapo wamelalamika malipo ya huduma bma ya afya ni kubwa ambapo ni sh 50,400 lakini huduma bado ni mbovu.
Aidha alisema changamoto nyingine ni mikopo na ada kubwa kwa ngazi ya Diploma kwa baadhi ya vyuo hasa chuo cha utumishi wa umma (TPSC).
Awali wakisoma katika risala yao waafunzi hao walisema wanakabiliwa na changamoto kadhaa ambazo ni ajira kwa watoto wa kike hali ambayo inawawia vigumu kupata kiasi cha kujiingiza kwenye vishawishi na gharama za masomo kuwa kubwa.
Aidha walisema changamoto nyingine ni kukosekana kwa shule za wasichana zenye hostel za kulala huku shule nyingine zikiwa mbali huku baadhi zikiwa mbali na makazi kiasi cha kuwa katika hatari kwao.
Walitaja nyingine ni jamii kutotambua mtoto wa kike anaweza kuwa kiongozi katika jamii hivyo anapaswa kuhusishwa kwenye masuala mbalimali ya kufanya maamuzi kama ilivyo kwa wanaume.
No comments:
Post a Comment