Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 10 September 2015

MWANA WA MFALME AJITOSA TENA URAIS FIFA

Mwana mfalme Ali Bin Al Hussain (kushoto) akiwa na Rais wa FIFA Sepp Bltter
Mwanamfalme wa Jordan Ali Bin Al-Hussain ametangaza kuwa atasimama kuwania nafasi ya Urasi wa Shirikisho la kandanda duniani FIFA kurithi nafasi ya Rais wa sasa anayestaafu Sepp Blatter.
Wakati wa uzinduzi wa kampeni zake mwanamfalme huyo aliahidi kufanya mageuzi katika uongozi wa soka,kupambana na rushwa na kuimarisha soka la wanawake.Alipoteza ushindi mwezi Mei ambapo Sepp Blatter alishinda kabla ya kutangaza kujiuzulu wadhifa huo.
Maafisa wa ngazi ya juu ya FIFA wanatuhumiwa kuhusika na rushwa na mamlaka za Marekani mapema mwaka huu.
Rais wa shirikiso la soka barani Ulaya Uefa Michel Platini na Chung Mong-joon wa Korea Kusini kwa pamoja wameonesha nia yao kuwania nafasi hiyo ambao uchaguzi wake utakua mwezi Februari mwaka 2016.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment