Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 15 September 2015

MUSOMA UTALII WAKALIMILISHA BONANZA KUSAKA VIPAJI

Displaying MUSOMA UTALII.3.jpg
Waziri wa maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akiwa na mkurugenzi wa chuo cha Musoma Utalii mkoani Tabora Shaban Mrutu  mara baada ya kuzindua chuo hicho mapema mwaka jana.
Displaying MUSOMA UTALII.4.jpg
Waziri wa maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akisalimia baadhi ya wahitimu wa chuo cha Musoma Utalii Tabora.
Displaying MUSOMA UTALII.7.jpg
Mkurugenzi wa chuo cha Musoma Utalii Tabora Shaban Mrutu akiongea na waziri wa maliasili na Utalii ofisini kwake. Mrtu ameanzisha mashindano ya michezo mbalimbali kusaka vipaji chuoni hapo. (Picha na Hastin Liumba).

Na Hastin Liumba,TaboraMTU makini siku zote huangalia alichokifanya siku za nyuma kwa nia ya kuongeza ubora wa matunda ya kazi yake katika siku zijazo na faida ya kazi nzuri hufurahiwa na kila aliyetoka jasho katika upatikanaji wake.

Ule upungufu wote uliojiwa nia ya kujitokeza ambao ulichangiwa katika kuipunguza faida  kubwa zaidi ambayo ingeweza kupatikana,pia hutakiwa kufanyiwa kazi kwa nia ya kuboresha ufanisi mzima.

Kampuni,chuo ama taasisi yoyote ile inaweza kufurahia mapato makubwa baada mwaka wa biashara kumalizika na wahusika wakanywa na kula kwa furaha,lakini uko udhaifu katika utendaji wa kazi ambao kama ukiweza kushughulikiwa,basi faida kubwa zaidi itaweza kupatikana baada ya mwaka mwingine.

Haya ni maneno ya mkurugenzi wa chuo cha Musoma Utalii kulichopo kata ya Ipuli mkoani Tabora Shaban Mrutu wakati akiongea na mwandishi wa habari kwenye mahojiano maalumu baada ya kumalizika kwa Bonanza la chuo hicho.

 Mrutu anasema leo maneno haya ameyatamka baada ya kuanzisha mashindano haya bila udhamini wowote lakini amekutana na changamoto nyingi.

Changamoto hizo ambazo angepenga kuzitaja ili hata wasomaji wengine wakisoma wataona kuwa ipo haja tuungane wana Tabora kufanya kile ambayo nitahitaji kuungwa mkono wa dhati ili mkoa wetu ufikie malengo ya kimichezo.

Mrutu alisema Bonanza hilo amelianzisha mwaka 2013 na hadi sasa lina
miaka mitatu na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa mwaka hadi mwaka.

Alisema mapema baada kuanzisha mashindano haya alitegemea kupata washiriki wengi kwenye michezo ambayo alikuwa ameilenga.

Mrutu anasema amesikitishwa sana kutokana na michezo mingi kadhaa kushindwa kufanyika hasa kwa kukosa washiriki,huku bajeti kwa kiasi fulani kukwama na wadau wa michezo kadhaa kushindwa kumunga mono kufanikisha kile ambacho kingekuwa ni faida kuu kwa taifa na vijana kwa ujumla.

Mkurugenzi huyo anasema vijana wanaopenda michezo wengi huishia mitaani kwa kukosa wadau wa kuwaendeleza kimichezo na kufikiwa kwa malengo yao na baadaye kuwa wazururaji lakini bado niliona ipo haja kuanisha haya ili siku zijazo tutakuwa na kitu cha kujivunia kwa vijana wetu.

Aidha rekodi nyingi zinaonyesha mkoa wa Tabora tuko nyuma kwa mambo kadhaa lakini tunapaswa kujitoa kwa ajili ya vijana wetu na kizazi kijacho na ili tutuoke hapa tulipo tunahitaji kuwa kitu kimoja kufikia malengo yetu kama wanaTabora

Mrutu alitaja michezo ambayo alikuwa ameianzisha na ipo iliyofanyika na mingine haikufanyika ambayo ni michezo ya Mpira wa Miguu,mpira wa Pete na mpira wa Wavu.

Michezo mingine ni Riadha,Sarakari,Kuvuta Kamba,kuruka Kamba na mashindano ya Umisi kwa wanawake na wanaume,(Miss and Mr Musoma Utalii College).

Michezo iliyofanyika.

Michezo ambayo ilifanyika ni mpira wa soka,Miss Musoma Utalii College tu ndiyo michezo ambayo imefanyika na washindi walipataikana na kukabidhiwa zawadi zao.

Michezo ambayo haikufanyika.

Hata hivyo mashindano ya Mr Musoma Utalii College hayakufanyika kwani fedha iliyokuwa imetengwa bajeti yake ilivurugika ambayo nitafafanua ni kwa nini ilitokea hivyo licha ya washiriki kujitokeza kushiriki lakini tuliomba radhi kwa hilo.

Mrutu alibainisha mchezo ambayo haikufanyika kutokana na washiriki kushindwa kujitokeza ni Riadha,mpira wa wavu,mpira wa Pete,Sarakasi,kuvuta kamba,kuruka kamba.

Hata hivyo michezo ambayo haikuwa rasmi lakini ilifanyika ni Burudani ya kuonyesha umahiri na vipaji cha kuimba nyimbo za kiasili na kizazi kipya.

Michezo iliyofanyika ina vipaji.


Akielezea mashindano yalivyofanyika Mrutu alisema licha ya michezo michache iliyofanyika ni kugundua uwepo wa vipaji vilivyojidhihirisha ambavyo ana mipango ya kutafuta ufumbuzi wake.

Alisema katika mpira wa soka kulikuwa na washiriki ambao ni wanachuo ngazi ya Astashahada na Stashahada ambapo bingwa alikuwa ni Stashahada ambaye ataunganishwa na timu zinazoshiriki mashindano ya ngazi hiyo kupitia cha soka Tabora (TAREFA).

Alisema hii itatokana na mashindano ambayo yataendeshwa wakati huo na chama soka mkoa wa Tabora (TAREFA).

Aidha kwa upande wa mashindano ya Miss Musoma Utalii College washidi wataangaliwa namna ya kusaidiwa ikiwa ofa za kutembelea hifadhi za taifa watakapokuwa kwenye mafunzo ya vitendo.

Ushiriki wa wadau/wafadhili.

Kuhusu ushiriki wa serikali wadau na wafadhili mbalimbali kupitia makampuni alisema hakupata sapoti yoyote licha ya kutoa taarifa za uendeshaji juu ya mashindano hayo.

Alisema pamoja na hayo bado hatachoka kuendelea na mashindano hayo kwani mwisho wa siku atakuja kuungana na wale wote watakaokubali hasa pale amtakapofikia malengo aliyokusudia kwani mwanzo ni mgumu.

Hata hivyo anakiri kuwa bado kulikuwa na uhamasishaji mdogo hivyo mashindano ya msimu ujao yatazingatia hilo kwani mashindano hatyo ni endelevu kwa kila msimu.

Changamoto alizoziona.


Mrutu alisema licha muelekeo mzuri lakini bado kulikuwa na changamoto kadhaa ambazo ni upungufu vifaa,vifaa vingi kuwa vibovu na visivyo na ubora,vifaa vingi vikiwa na gharama kubwa na washiriki wengi kushindwa kujitokeza.

Mwalimu wa michezo.


Mwalimu wa michezo Chuo cha Musoma Utalii Saimon Masaganya anaelezea mashindano yalivyokuwa ya Bonanza hilo.


Zawadi za mashindano.

Akizungumzia mashindano hayo na zawadi zake alisema washindi wa mchezo wa soka mshindi alikuwa ni washiriki wa masomo ngazi ya Stashahada ambao walipata Mbuzi mmoja na kreti mbili za soda.

Hata hivyo washindi hao kabla ya kukabidhiwa zawadi zao walicheza mechi na walimu wa chuo ambapo stashahada waliibuka washindi kwa goli 3-0 na kupewa rasmi zawadi zao mshindi wa pili kreti tatu za soda na
wa tatu atapata sh 20,000.

Kuhusu mashindano ya mamisi (Miss Musoma Utalii College) 2015 mshindi wa kwanza Elizabert Alex  alikabidhiwa fedha taslimu sh 300,000,mshindi wa pili Hadija Mohamed sh 200,000  wa tatu Specioza Gido sh 150,000.

Alisema kwa upande wa wanaume (Mr Musoma Utalii College) 2015 pamoja na kwamba hayakufanyika bajeti ilibana lalkini tulipanga kutoa zawadi za mshindi wa kwanza sh 300,000 na kompyuta ya mkononi,wa pili sh 200,000 wa tatu sh 150,000 na hali kadhalika wengine nao watapata kifutajasho.

Masaganya alibainisha michezo mingine ilipangwa zawadi zake kuwa hivi lakini washiriki hawakujitokeza ni  mpira wa Wavu,kuruka Kamba,kuvuta Kamba, Riadha na Sarakasi washindi wake wangejinyakulia tiketi za kuingia wenye mashindano ya Miss and MrMusoma Utalii College.

Masaganya alisema pia kulikuwa burudani ya wimbaji na wacheza disco wa kike na kiume kutoka chuoni hapo ili kuendeleza kukuza vipaji vyao ambapo washiriki walilipwa kifuta jasho ambacho tuliona umuhimu wake japo bajeti ilibana zaidi.

Changamoto kama mwalimu wa michezo.


Akitaja changamoto katika eneo lake kama mwalimu wa michezo chuo cha Musoma utalii alisema ni vifaa vya mashindano ya Miss Musoma Utalii College washiriki kadhaa hawakuwa na viatu na nguo.

Alisema chuo ilibidi kingie gharama ili kununua viatu na nguo hali ambayo iliuruga kabisa bajeti hasa ukizingatia hatukuwa na udhamini wowote.

Changamoto nyingine ni chuo kwenye mashindano hayo kukosa wadhamini kama ilvyo kwenye mashindano ya Miss Tabora kwani tuliendesha mashindano kwa shida sanjari na ufinyu wa bajeti

Malengo ya kuanzisha kituo cha maichezo.

Alisema yeye binafsi malengo ya kuanzisha kituo cha vijana cha michezo kiko palepale licha ya changamoto zilizojitokeza na ana imani atafanikiwa.
Mashindano haya yameanza mwezi Agosti 7,mwaka huu na yamehitimishwa mwezi Agosti 14,2015 yaliendeshwa katika eneo la viwanja vya Chuo cha Musoma Utalii Tabora.
hastinliumba@gmail.com-0788390788.

No comments:

Post a Comment