Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 15 September 2015

HALI YA UCHAFU MKOA WA TABORA INATISHA

Mazingira yalivyo katika eneo la soko la matunda Manispaa ya Tabora lililogeuzwa kuwa dampo pasipo uongozi wa manispaa kuchukua hatua zozote. Picha na  Hastin Liumba.

Na Hastin Liumba, Tabora
MKOA wa Tabora, ni moja ya mikoa yenye sifa ya vivuti vyenye sifa na kwamba ni mkoa wenye historia nzuri kwa viongozi wa taifa hili.


Licha ya hitoria hiyo lakini bado mkoa huo umebaki kama yatima karibu kila kitu kuanzia kiuchumi,kijamii,kisiasa na hahali ya muonekano na mandhari mazuri ya mkoa huu.

Lakini leo naomba kuongelea hali ya usafi mkoani Tabora ambayo iko choka mbaya karibu kila eneo linalozunguka mkoa huu hususani hapa mjini.

Aidha lakini siyo hapa mjini tu huko mawilayani hali ni tete mno uchafu uliokithiri ni hatari zaidi kwani tutake tusitake majira ya masika mvua zitakapoanza Kipindupindu kiko nje nje.

Ikumbukwe kuwa mkuu wa wa kipindi hicho Fatma Mwassa aliwahi kuvalia njuga suala la usafi wa mji huu kiasi cha kutenga siku ya Jumamosi ambapo aliongozana na watenda kadhaa wa ofisi yake na Halmashauri ya Manispaa kuongoza usafi wa mji huu.

Hatua ilifikia mahali  ikapongezwa sana hasa baada ya kuvalia njuga suala la usafi na kutenga siku ya kila siku hiyo kufanya ziara ya kukagua usafi kwa  kata itakayopangwa.

Mwasa  alifikia hatua hiyo baada ya kusikitishwa na hali ya usafi ilivyokuwa toka alipofika baada ya uteuzi wa rais Jakaya Kikwete kumteua kuwa mkuu wa mkoa Tabora.

Ni ukweli usiopingika hapo nyuma kabla ya Mwasa kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Tabora,mji wa manispaa hii ulikuwa umeoza kwa uchafu uliorundikana kila kona.

Licha ya jitihada hizo bado juhudi zinztakiwa kufanywa na watendaji wa manispaa Tabora yalibadilika lakini sasa toka mama huyo kahamishwa mji sasa uko taabani.

Naomba niyaweke wazi maeneo ambayo bado yanatia kinyaa ni Bachu, Isevya, Kiloleni, Chemchem,Barabara ya Mwanza na Kanyenye.

Licha ya changamoto za uhaba wa vitendea kazi,pia uelewa wananchi katika suala zima la usafi wa mazingira nalo likiwa sehemu ya tatizo la uchafu kurundikana.

Na pengine niutupie lawama kubwa uongozi wa manispaa Tabora kwa kushindwa kuzitumia sheria ndogo ipasavyo ili kudhibiti wachafuzi wa mazingira.

Cha kusikitisha ni pale maeneo mengi ya wazi yameuzwa na hakuna sehemu inayoonyesha kuna bustani nzuri inayotunzwa sambamba na eneo la wazi.

Hata hivyo licha kuutupia uongozi wa manispaa Tabora kwa kushindwa kuweka mji safi,jamii nayo inapaswa kupewa elimu ya usafi japo suala la usafi lipo mashuleni na itakuwa aibu kwa wanajamii eti kupatiwa elimu ya usafi.

Nyasi ndefu zilizokauka,mrundikano wa taka ngumu mitaani zilizokuwa zinatoa harufu,maji machafu mitaroni na michanga ilijazana na madimbwi ya maji ni vitu ambavyo vimeunguka manispaa Tabora, huku chupa za maji kunywa,mifuko ya plastiki na karatasi za vocha zilizotumika ni sehemu ya uchafu uliopo mitaani.

Hali hiyo imekuja baada ya watendaji wa manispaa Tabora kushindwa kuweka manispaa katika hali ya usafi kwa visingizio kuwa hawana fedha,vitendea kazi,na watumishi wa kufanya kazi hiyo.

Hii ni aibu sana kwa watendaji kumuacha rais wa mkoa akiingilia kati,suala la usafi wa mji, ilihali watendaji wanaohusika na afya wapo,wakitafuna mishahara kila mwezi.

Pamoja na watendaji hao wa manispaa Tabora,kudai wanashindwa kuweka mji safi kwa visingizio walivyosema,lakini jitihada zilizofanywa na mkuu wa mkoa kipindi kile Fatma Mwassa zilionekana kuzaa matunda kwani hali usafi ilijionyesha.

Sura kwa sasa inasikitisha mno hasa kwenye eneo la soko la Kachoka, na maeneo ya makazi ya watu huku maeneo mengine yenye taka zilizorundikana yakiuuzwa vyakula kama mama lishe,chipsi na Glosari za vinywaji.

Kila mmoja wetu anatambua umuhimu wa usafi hasa katika mazingira tunayoishi, ama usafi wa mtu mwenyewe.

Aidha tunatambua wazi kuwa bila kuzingatia usafi athari zake tunazitambua dhahiri kuwa matokeo yake ni maradhi, hatimaye mauti.

Kipindi kile aliyekuwa mkuu wa mkoa wakati huo Mwassa licha ya mkuu wa mkoa,kusimamia usafi pia, alitoa agizo hilo sambamba na ujengwaji wa mizunguko ya barabarani, (Round About), ambazo zilikuwa zimebomoka na kutia kinyaa.
Hata hivyo leo hii mziunguko hiyo iko hoi kwani hata rangi zimechoka na hazitamaniki.

Ni jambo la aibu kwa mkuu wa mkoa kuwaelekeza watendaji wa manispaa ya Tabora na wale wa Tanroad namna ya kuweka mazingira safi wakati sheria ndogo za usafi zipo,wapo watumishi wa afya wapo wanaopokea mishahara kila mwezi.

Unaweza wakati mwingine ukashangazwa na majibu ya watendaji wa manispaa Tabora,wakiongozwa na mkurugenzi  Sipola Liana, wakidai hawana vitendea kazi kama gari, pipa za uchafu, na watumishi wa kufa kazi hizo,na mara nyingine wanasema hawana fedha za kulipa wafanya usafi.

Ni wazi kuwa watendaji wa manispaa Tabora wako likizo,katika suala la usafi, kwani hali ya usafi inatisha kwani kila kona uchafu umerundikana.

Aidha ukija tazama hata pipa ambazo zimetengwa katika mitaa kadhaa japo hazitoshi mara kadhaa tumeshuhudia zimefirika taka ngumu huku nyingine zikiwa zimetupwa pembeni mwa pipa hizo.

Lakini leo hii baadhi ya pipa za taka zimeoza na kupasuka huku nyingine zikiondolewa kabisa mitaani kwani hazifai tena kukusanyia uchafu.

Kichekesho zaidi ni pale utakaposikia wahusika wa usafi hudai mara kadhaa gari la kubeba taka hizo bovu,ama spea fulani wamekosa na hivyo taka hizo kuwa hatari zadi kwa jamii.

”Hatuna mafuta,gari bovu,tunatafuta spea haijapatikana.......hii ndiyo kauli ya mara kwa mara ya wahusika wanaozoa taka hizo katika pipa kadhaa kubwa ama vijipipa vichache ambapo navyo havina msaada wowote kwani uwezo wa vijipipa hivyo hata kilo 20 za taka, havina uwezo wa kuhifadhi.

lakini kipindi kile kabla ya Mwassa kuingilia kati kulikuwa na sababu lakini leo hii amehamishwa visingizio vimeanza upya mara gari hakuna,bovu na hata mafuta pia hawana.

Hata hivyo bado kuna udhaifu mkubwa kwa watendaji wa mitaa na kata kwani maeneo ya ndani ya mitaa bado machafu sana na wenye wajibu wa himizo kwa wananchi wenyeviti wa mitaa na kata.

Aidha niutupie lawama uongozi wa baadhi ya kata hasa mabwana na mabibi afya,wamekuwa wakipitia kukagua usafi kwenye bar,Glosari na hotel na wameku wakisahau sana kupitia majumbani ambako ndiko kuna hali mbaya ya usafi na taka za maji taka na ngumu

Pia haya baadhi ya nyumba za kulala wageni baadhi yake ziko hoi na uchafu na harufu mbaya vyumbani lakini hakuna hatua zozote za msingi katika kuhakikisha zinakarabatiwa na kupakwa rangi.

Bado hata masoko yote ya manispaa Tabora mindombinu yake iko hoi kwani zipo bidhaa za vyakula zikipangwa chini,mvua zinazonyesha maji machafu huzunguka kila kona ya masoko hayo na wafanyabiashara wamekuwa wakilipa ushuru kila siku lakini hali ya usafi ndani ya masoko hayo ni duni.

Ipo haja sasa watendaji wa manispaa kuamua kutumia sheria ndogo zilizopo kutoa adhabu kwa wachafuzi wa mazingira kwani hii itasaidia mji kuwa safi.

Zipo sheria ndogo kama vifungo jela visivyopungua miezi sita,faini ya sh 50,000 ama adhabu zote kwa pamoja lakini hazitumiki ipasavyo.

Mkuu wa mkoa wa Tabora Ludovick Mwananzila alipotafutwa kutolea ufafanuzi wa hali ya usafi katika mkoa wa wake yalikuja majibu yuko safarini.
hastinliumba@gmail.com-0788390788

No comments:

Post a Comment