Baadhi ya watumishi wa kampuni ya Ardhi Plan Limited wakiwa kwenye kazi ya upimaji katika baadhi ya maeneo nchini. (Picha zote na Hastin Liumba).
Wananchi kadhaa wakimsiliza mkurugenzi wa kampuni ya Ardhi Plan Limited Gombo Samandito katika moja ya ikutano na wananchi kabla ya kampuni ya kupima ardhi katika baadhi ya maeneo nchini.
Gombo Sanandito
Na Hastin Liumba, Tabora
KATIKA miaka ya hivi karibuni taifa la Tanzania tumeshuhudia likikumbwa na kukua kwa migogoro mingi inayohusu umiliki na utumiaji wa ardhi hali ambayo inasababisha mapigano kati wakulima na wafugaji ama jamii kwa ujumla.
Aidha migogoro hiyo imesababisha wananchi kupoteza maisha na juhudi za kupunguza migogoro hiyo ambayo imekuwa ikijirudia mara kwa mara katika baadhi ya mikoa mbalimbali ikiwemo Tabora bado haijapata ufumbuzi wa kudumu.
Migogoro ya ardhi hadi sasa imesababisha mauaji ya watu wengi na endapo wadau na serikali watatafuta tiba ya mauaji hayo basi taifa litaondokana na adha hiyo na kusonga mbele kwani ardhu duniani ndiyo kila kitu.
Lakini ndapo kutakuwa utaratibu wa kupima viwanja,mashamba basi hatutakuwa na migogoro isiyo ya lazima kwenye ardhi ikiwemo migogoro ya wafugaji na wakulima.
Gombo Samandito ni mkurugenzi wa kampuni ya upimaji wa ardhi nchini iujulikanayo kama ARDHI PLAN LIMITED alisema hayo wakati akifanya mahojiano na mwandishi wa makala hii eneo la upimaji lilikuwa na mgogoro la Uledi kata ya Ipuli Tabora.
Samandito alisema Ardhi Plan limited inatambulika kisheria na kwamba imsajiliwa mwaka 2004 ikiwa ni zaidi ya miaka kumi sasa, chini ya Business Registration and Licensing Authority (BRELA) yenye makao yake makuu jijini Dar-es-Salaam.
Mkurugenzi huyo anasema wana uzoefu mkubwa katika upimaji viwanja vya wananchi na makampuni mbalimbali hapa nchini.
Uzoefu wa kampuni yake.
Anafafanua kampuni yake ina uzoefu wa kazi hiyo kwa miaka kumi toka kuanzishwa kwake na kwamba wanafanya kazi kwa uadilifu mkubwa hali ambayo imewatea sifa ndani na nje ya serikali.
Anasema hatua hiyo imewafanya waaminike zaidi na kuweza kuitwa maeneo mbalimbali ya nchi kwa ajili ya upimaji viwanja ambapo serikali imekuwa ikiona umuhimu wa kampuni yake.
Kuhusu hatua ya upimaji viwanja
Akielezea upimaji viwanja katika eneo la Uledi kata ya Ipuli,anasema hatua hiyo haikuwa rahisi kwani kulikuwa na mvutano mkubwa kati ya uongozi wa halmashauri ya manispaa na wananchi.
Anasema mvutano huo hatimaye ulikwisha na tayari wamepima viwanja vya wananchieneo la Uledi, kata ya ipuli mkoani Tabora na eneo la hospitali kama wananchi walivyokubaliana katika mkataba wa wazi.
Samandito alisema upimaji umekamilika na hadi sasa licha ya kupima eneo la Hospitali ya wilaya ya Tabora mjini wameshapimia wananchi viwanja 9,800 na kazi hiyo inaendelea kukamilishwa.
Wananchi waridhishwa na upimaji
Wananchi wa eneo la Uledi, Kata ya Ipuli Manispaa ya Tabora 1,013 wamesema kwa kiasi kikubwa wameishuuru kampuni hyo kwa kufanikisha zoezi la kuwapimia viwanja na kila mtu ameridhishwa na eneo alilopimiwa.
Wananchi wa eneo la Uledi, Kata ya Ipuli Manispaa ya Tabora 1,013 wamesema kwa kiasi kikubwa wameishuuru kampuni hyo kwa kufanikisha zoezi la kuwapimia viwanja na kila mtu ameridhishwa na eneo alilopimiwa.
Akizungumza na gazeti hili katibu wa kamati ya watu nane iliyoundwa toka kuanaza kwa migogoro katika ya halmashauri ya manispaa Tabora na wakazi hao Alex Warange alisema kila mmojawapo ameridhishwa na kampuni ya Ardhi Plan Limited kwani hakuna manung`uniko yoyote.
Alisema walifikia hatua mbaya hali ambayo ilitaka kuleta machafuko kwani wananchi walitaka kngia barabarani kudai haki yao na kwamba halmashauri ya manispaa Tabora kwenye mgogoro huo imeonyesha udhaifu na udanganyifu waliotaka kuufanya.
Warange alisema baada ya kudai haki yao ya kimsingi kwenye ardhi yao wamekubali kwa moyo moja kutoa eneo la hekari 42 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya na eneo jingine wametoa kwa ajili ya miundombinu ya barabara na huduma nyinginezo.
Anasema hadi sasa wameshatoa zaidi ya hekari 417 ikiwa ni eneo ambalo watapitisha huduma za jamii kama eneo la ujenzi wa hospitali ya wilaya,shule na barabara.
Alisema wanamshukuru Mungu mgogoro ule ulimalizwa na waziri mwenye dhamana wa wizara ya Ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi na alibariki kampuni ya Ardhi Plan Limited kupima ardhi ya wananchi hao.
Alisema Lukuvi alibariki eneo hilo liendelee la upimaji baada ya kusoma nyaraka za kampuni hiyo na kuona iko kisheria na kwamba kazi zake hufanyika kwa uwazi iko kisheria katuka usajili wa BRELA ambapo kazi hiyo ilianza mwezi Juni 4,2015.
Warange alisema baada ya zoezi kukamilika na mgogoro kwisha kamati yake itaandika barua kwenda halmashauri ya amnispaa kuwajulisha kupewa eneo la hekari 42 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya Tabora mjini.
Alisema wanataka kwenda kisheria zaidi hivyo barua watakayoandika kwa mkurugenzi mtendaji itaandikwa pia ofisi ya mkuu wa mkoa na wizara ya ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi kujulisha hatua iliyofikiwa.
Halmashauri ya manispaa yakubali yaishe.
Uongozi wa halmashauri ya manispaa Tabora umeridhika na kumaliza mgogoro huo ikiwa ni pamoja na kuheshimu agizo la waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi.
Akiongea kwa niaba ya uongozi wa halmashauri ya manispaa,G A Mwakalukwa alisema maridhiano yamefikiwa na wapo eneo ambalo watajenga hospitali ya walaya na tayari upimaji umeshafanyika.
Mwakalukwa aliongozana na maafisa wengine ambao ni Ponda Dundumo,Deo Msilu,Williamu Maganga,Emilia Sanga,Dr Edna Mwakyembe na Dr Ibrahim Salehe.
Mwakalukwa alisema kimsngi tatizo ama mgogoro umeisha na sasa shughuli za kijamii zinaendelea eneo hilo kama kawaida kwa sasa kila upande umeridhika.
Mgogoro ulivyokuwa.
Katibu wa kamati ya kushughulikia mgogoro huo ulioanza toka mwaka 2012 hadi 2015 Alex Warange alisema wakazi wa eneo hilo hawakuwa tayari kusikia kauli ya viongozi wa halmashauri ya manispaa kwani waliona wanaporwa ardhi yao.
Hatua hiyo ilipelekea kuundwa kwa kamati ya watu nane ambao ni Aman Shaban Mbwambo (mwenyekiti),Alex Warange (Katibu),Viane Biseko (mjumbe),Aziz Kikamanwa (mjumbe),Saimo Lameck (mjumbe),Shela Idd (mjumbe),Juma Mganwa (mjumbe) na Masoud Mwilu (mjumbe).
Alisema wakazi hao walifanya mikutano kadhaa katika eneo la Uledi kata ya Ipuli Tabora kwa kauli moja walikuwa Wakiongea kwa nyakati tofauti wananchi hao walisema wako tayari kufa kwa ajili ya kudai haki ya maeneo ambayo wamekuwa wakiyamiliki miaka mingi na Halmashauri ya Manispaa Tabora inataka kuwapora.
Wananchi hao walisema kuwa adui yao namba moja ni diwani wa kata ya Ipuli wakati huo kwani kata hiyo sasa imegawanywa na kupatikana kata ya Mpera, Waziri Mlenda ambaye amekuwa akiwadanganya kuwatetea lakini alikuwa haeleweki.
Wange alisema ilifikia mahali wananchi hao walimkataa diwani wao na kusema hawako tayari kumuona kwani Kampuni ya Ardhi Plan Limited iko kisheria katika upimaji huo.
Alisema kampuni ya Ardhi Plan Limited waliingia nayo mkataba mwezi Februari 2013 ili wapimiwe viwanja vyao lakini uongozi wa halmashauri ya Manispaa Tabora imekuwa ikiingilia zoezi hilo kutaka kukwamisha.
Alibainisha kampuni hiyo ikipima Hekari moja inatoa viwanja vitatu wakati halmashauri ya manispaa ikipima Hekari moja inalipa fidia ya sh 600,000 na hiyo tuliona ni tatizo kwetu ndiyo maana tulitaka kuampuni hii.
Mvutano wetu ulifika mbali kiasi cha baadhi ya viongozi wa halmashauri ya manispaa Tabora chini ya mkurugenzi mtendaji Sipola Liana wakapenyeza uongo kuwa kampuni ya Ardhi Plan Limited ni matapeli kitu ambacho siyo kweli kwani mbinu yao ilitaka kutukwamisha.
.Aidha alisema Manispaa Tabora imepima viwanja maeneo ya Malabi na Malolo ambapo kila Hekari moja wamelipa fidia sh 600,000 wakati kampuni hiyo Hekari moja wanatoa viwanja vitatu.
Alibainisha kuwa yeye kama diwani alishiriki kuitafuta kmpuni ya Ardhi Plan Limted ili wananchi wake wapimiwe maeneo yao lakini anashangazwa na kusikia anawasaliti siyo kweli.
Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa Tabora Sipola Liana alisema yeye ameletewa barua toka wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kusitisha zoezi la kusitisha upimaji unaofanywa na kapumuni hiyo.
Hatua ya kumuona waziri
Hatua ya mwisho iliyofikiwa na wananchi hao walifanya mkutano wakiwa zaidi ya 602 wa eneo la Uledi kata ya Ipuli mkoani Tabora waliunda kamati ya watu saba kwenda kuonana na waziri wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi ili aingilie mgogooro wa viwanja na uongozi wa halmashauri ya Manispaa Tabora.
Aman Shaban Mbwambo mwenyekiti wa kamati hiyo alisema walifanikiwa kuonana na waziri na baada ya kupitia nyaraka zao na malalamiko yote kwa ujumla alibariki kampuni ya Ardhi Plan Limited kuendelea na kazi hiyo ya upimaji ndipo ukawa mwisho wa mgogoro huo.
Aman Shaban Mbwambo mwenyekiti wa kamati hiyo alisema walifanikiwa kuonana na waziri na baada ya kupitia nyaraka zao na malalamiko yote kwa ujumla alibariki kampuni ya Ardhi Plan Limited kuendelea na kazi hiyo ya upimaji ndipo ukawa mwisho wa mgogoro huo.
Alisema wanamshukuru Lukuvi kwani amewasaidia na tayari imeonekana wazi kuwa migogoro ya ardhi chini inasababishwa na baadhi viongozi wa halmashauri kwa maslahi yao binafsi.
Aidha alisema ilifikia mahali hata Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora Moshi Abdulrahaman Nkonkota alisema yupo nyuma ya wananchi hao kuona haki inatendeka kwani uongozi wa halmashauri ya manispaa Tabora wamekuwa sehemu ya kero ya ardhi za wananchi kwenye wilaya yake.
Anasema kero za viwanja ilijitokeza katika maeneo ya kazi ni Malabi,Malolo na Uledi na ilifikia mahali baadhi ya watendaji idara ya ardhi kusimamishwa kazi na wengine walifukuzwa kazi.
Serikali iliingilia kati
Serikali mkoa wa Taora kupitia mkuua wa mkoa Ludovick Mwananzila aliingilia kati na kukutana na kamati iliyoundwa kushughulikia mggoro huo na mambo kadhaa yaliagizwa kwa msaidizi wa RAS idara ya ardhi Longono Kazimoto lakini ulishindikana.
pix namba 505 baadhi ya wananchi wakisiliza kwa makini maelekezo ya upimaji wa ardhi.
Pix namba 545 Watumishi wa kampuni ya Ardhi Plan Limited wakiwa kazini.
pix namba 438 Mkurugenzi wa kampuni ya Ardhu Plan Limited Gombo Samandito akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wananchi moja ya sehemu za ipimaji.(Picha zote na Hastin Liumba).
hastinliumba@gmail.com- 0788390788



No comments:
Post a Comment