Hillary Clinton
Maefu ya kurasa za barua pepe binafsi za aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton zilizotumwa kwa anuani binafsi ya Waziri huyo, zimewekwa wazi hii leo na idara za Usalama nchini humo.
Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani imesema kati ya barua pepe hizo, 150 kati yake ni zile zinazodaiwa kuwa na taarifa muhimu na za siri za serikali.
Hata hivyo, Clinton mwenyewe amesema kuwa barua pepe hizo alizituma kimakosa, kwa kutumia anuani binafsi kwa shughuli rasmi za kikazi.
Shirika la Ujasusi la Marekani FBI linachunguza ili kubaini kama ni kweli barua pepe hizo zilitumwa kimakosa.
Tukio hili limekuwa gumzo nchini Marekani hasa wakati huu ambapo Hillary Clinton anatafuta ridhaa ya chama chake kuwania urais wa taifa hilo kubwa katika uchaguzi wa mwaka 2016.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment