Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 30 September 2014

BAADA YA 'MCHINA' KUWADHURU, WANAWAKE WA TANZANIA SASA WAFURIKA AFRIKA KUSINI KUTENGENEZA MAKALIO NA MATITI


WANAWAKE wa Tanzania ni miongoni mwa wanawake wengi barani Afrika wanaofurika nchini Afrika Kusini kwa madaktari wa kienyeji kutengeneza matiti ili yafanane na ya Kim Kardashian, makalio kama ya Jennifer Lopez na tumbo kama la Jessica Alba.
Safari za Operesheni hizo nchini Afrika Kusini kwa sasa siyo za matajiri kama ilivyokuwa zamani kwa Wamarekani na Wazungu kutoka Ulaya, na akinadada hao wanatumia mpaka Randi 100,000 (takriban Shs. 25 milioni za Tanzania) kwa ajili ya upasuaji huo.

FACEBOOK YAPATA MPINZANI WA KWELI, NI ELLO!

Ukuta wa Ello

Mtandao wa kijamii wa Ello unapokea maombi 31,000 ya watumiaji wanaotaka kujiunga kila saa moja hali ambayo inaibua ushindani mkubwa kwa mtandao wa Facebook.
Muanzilishi wa mtandao huo Paul Budnitz ameiambia BBC kuwa wakati mtandao huo unaanzishwa ulilenga watu kuhudumia marafiki 90 tu.

RAILA ODINGA ACHAPWA VIBOKO MKUTANONI

Raila Odinga
Hali ya taharuki iliibuka katika mkutano wa hadhara katika jimbo la Kwale nchini Kenya, baada ya mwanamume mmoja kwenda ukumbini na kuanza kumchapa kwa kiboko kiongozi wa upinzani Raila Odinga pamoja na wanasiasa wengine.
Raila alikuwa amejiunga na kikundi cha wanawake waliokuwa wanacheza densi ya kitamaduni kuwatumbuiza wageni, pamoja na gavana wa jimbo la Kwale Pwani ya Kenya Salim Mvuruya katika mkutanmo wa kisiasa.

KESI YA UFISADI YA JULIUS MALEMA YAPIGWA KALENDA HADI AGOSTI MWAKANI

Julius Malema
Kesi ya ufisadi inayomkabili kiongozi wa upinzani, nchini Afrika Kusini Julius Malema, imeahirishwa hadi Agosti mwaka ujao.
Kesi hiyo ilitarajiwa kuanza hii leo lakini wakili mmoja muhimu hakuwepo.
Kiongozi huyo wa zamani wa kundi la vijana wa chama kinachotawala cha ANC anashtakiwa kwa kulaghai, matumizi mabaya ya fedha na kwa kuuza vitu kimagendo.

JENEZA LAIBWA MSIKITINI, LAKUTWA KWA OFISA MTENDAJI!


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela
NA GIDEON MWAKANOSYA
Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linawasaka watu wasiofahamika wanaotuhumiwa kuingia msikitini na kuiba jeneza, Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma.

Baada ya kuiba jeneza hilo, watu hao wanadaiwa kwenda nyumbani kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kitanda, wilayani humo, Fidea Mbawala (30) na kuliweka mlangoni, likiwa limesheheni matofali.

Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Mihayo Msikhela, alisema  tukio hilo lililotokea juzi, saa 12:00 asubuhi, katika kijiji hicho.

TUNDU LISSU ASEMA, MAPAMBANO YA KUDAI KATIBA MPYA YANAANZA UPYA


Na Godfrey Mushi
Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, (pichani) amesema mapambano ya kudai katiba ya Watanzania yameanza upya hata kama Bunge Maalumu la Katiba litaamua vinginevyo.

Amesema uamuzi wowote utakaofanywa, hautakuwa na uhalali na hautaheshimiwa na mtu yeyote kwa kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mawakala wao ndani ya Bunge wana shida ya akidi na ndiyo maana imewabidi wachakachue sheria na kanuni ili kuhakikisha wanaonekana wamekidhi matakwa ya akidi inayohitajika.

Lissu alisema hayo alipokuwa akihojiwa jana asubuhi na kituo kimoja cha runinga kuhusiana na upigaji wa kura ulioanza jana mjini Dodoma kwa ajili ya kupitisha rasimu ya katiba inayopendekezwa na Bunge hilo.

KINANA ALIPOSHAMBULIA JIMBO LA BUMBULI KWA JANUARY MAKAMBA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kata ya Mbuzii (hawapo pichani).Katibu Mkuu leo alianza ziara yake katika kata ya Mbuzii ambapo alishiriki ujenzi wa ofisi ya chama sehemu ambayo inahistoria kwani ilitumika kwa kufanya mikutano ya harakati za kutafuta Uhuru na ni sehemu iliyojengwa ofisi ya kwanza ya Tanu wilaya ya Lushoto.
 Wananchi wa kata ya Mbuzi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi pamoja na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli Mheshimiwa January Makamba wa ofisi ya CCM kata ya Mbuzii ,Mbuzii ndio chimbuko la TANU wilaya ya Lushoto.

MR SUGU AACHANA NA MKEWE FAIZA ALLY, MAMA SASHA ALIA KWA UCHUNGU

Mh. Sugu, mkewe Faiza Ally na mtoto wao Sasha

MUIGIZAJI wa filamu nchini Faiza Ally amemwagana na mwanamuziki mkongwe wa muziki wa kizazi kipya na Mbunge wa Mbeya mjini kupitiaCHADEMA Mhe. Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu !.... Kupiia Instagram Faiza ameandika maneno yanayoonyesha amemwagana na Mh.Sugu. Faiza aliandika hivi...

'AFANDE' TIBAIGANA ASEMA NCHI INAHITAJI RAIS DIKTETA!


Alfred Tibaigana

Na Phias Bashaya, Mwananchi
Muleba. Iko dhana kuwa ili Tanzania ipige hatua kimaendeleo inahitaji kiongozi anayethubutu kufanya uamuzi mgumu hasa kuwawajibisha viongozi wabadhirifu na wazembe, lakini Kamanda wa Polisi mstaafu wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Alfred Tibaigana amekwenda mbali zaidi; anataka rais dikteta.
Kamishna Tibaigana alitoa kauli hiyo katika mahojiano maalumu na Mwananchi nyumbani kwake Buganguzi wilayani Muleba, mkoani Kagera hivi karibuni.

KURA YA 'HAPANA' YALITIKISA BUNGE LA KATIBA


Dodoma. Wajumbe wa Bunge la Maalumu la Katiba jana walianza kupiga kura za kuamua ibara za Katiba inayopendekezwa, huku kura za wajumbe kutoka Zanzibar zikiibua wasiwasi wa iwapo theluthi mbili itapatikana au la.
Dalili za kupiga kura za hapana kutoka upande wa Zanzibar zilianza kujionyesha mapema baada ya taarifa za ndani kueleza kuwa zikikosekana 10 kutoka upande huo wa Muungano hakuna katiba.
Hata hivyo, mapema Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta alisema idadi ya kura zinazohitajika kukidhi theluthi mbili kwa upande wa Zanzibar ni 140 na jana jioni waliokuwamo bungeni walikuwa 142.

DRUG MULES INMATES IN HONG KONG ACCUSE AMBASSADOR ABDULRAHMAN SHIMBO


A general view of Hong Kong’s Stanley Prison. Tanzanian ambassador to China Abdulrahman Shimbo is accused by drug mules imprisoned here of warning them to stop the campaign to deter other Tanzanians keen on drug trafficking. PHOTOS | FILE

Dar es Salaam/Hong Kong. Tanzania’s ambassador to China, Lt General (rtd) Abdulrahman Shimbo, is on the spot following claims he had “threatened” Tanzanian drug mules jailed in Hong Kong.
The China Morning Post reported yesterday that the ambassador is being accused by the inmates of allegedly telling them to end a campaign waged from prison to deter others from the illicit trade.

WATU 270 WANUSURIKA KIFO KWA KUNYWA TOGWA


Na Joyce Joliga, Mwananchi
Songea. Watu zaidi ya 270 wa Kijiji cha Litapwasi, Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma wamelazwa wengi wao wakiwa na hali mbaya katika Zahanati ya Lyangweni na Hospitali ya Misheni ya St Joseph, Peramiho baada ya kunywa togwa inayosadikiwa kuwa na sumu.
Tukio hilo lilitokea juzi mchana kwenye sherehe ya Kipaimara kwa mtoto Dickson Nungu (14) na kuzua hofu kubwa kwa wakazi wa kijiji hicho ambao wanaonekana kutoamini kilichotokea.

Monday, 29 September 2014

MFUMO DUME NA MAWAZO MGANDO KIKWAZO USHIRIKI WA MWANAMKE KATIKA UONGOZI

20140924_085545
Mkurugenzi Mtendaji wa Uvinza FM Radio, Nuru Kalufya akisimamia usajili wa washiriki wa mafunzo ya Maadili, Jinsia na Kuandika Habari za Migogoro yaliyoanza katika kijiji cha Uvinza, wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma tarehe 24 Septemba hadi 01 Oktoba 2014.

Na Mwandishi Wetu, Uvinza
Imethibitishwa kwamba mfumo dume ulioota mizizi katika jamii kwa kisingizio cha mila, desturi na dini unachangia kwa kiasi kikubwa katika unyanyasaji wa mtoto wa kike na mwanamke nchini.
Hayo yalithibitishwa na washiriki wa mafunzo ya maadili na jinsia yanayofanyika katika kijiji cha Uvinza mkoani Kigoma wakati wakichangia mada ya Jinsia na Vyombo vya Habari iliyowasilishwa na mkufunzi kutoka Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi Rose Haji Mwalimu.

HOFU YATANDA ZIMBABWE: ROBERT MUGABE ADAIWA KUTAKA KUMRITHISHA MKEWE MADARAKA

Hofu ya wananchi ni kwamba huenda Mugabe akamrithisha mkewe mamlaka
Kuzaliwa kwa utawala wa kinasaba sio jambo jepesi kubashiri.
Lakini wananchi wengi wa Zimbabwe kwa sasa wanaonekana kushawishika kuwa kuna uwezekano wa familia ya Mugabe kuingia katika orodha hiyo ya kurithishana madaraka.
Rais Mugabe ana umri wa miaka 90. Mke wake, Grace, ana umri wa miaka 49.
Uvumi wa kurithishana madaraka umekuwa gumzo la kisiasa nchini Zimbabwe kwa miaka mingi, lakini Grace Mugabe katika miaka ya karibuni ameibuka kama mtu ambaye ataweza kumrithi mumuwe madaraka ya uongozi wa nchi ya Zimbabwe.

OBAMA AKIRI, WALIIDHARAU NGUVU YA IS

Rais Barack Obama wa Marekani
Rais Obama amekiri katika televishen ya kitaifa kuwa Mashirika ya Marekani yalikosea katika kukadiria hatari ya wapiganaji wa dola ya Kiislam, Islamic State nchini Iraq na Syria.
Amesema kuwa wapiganaji hao wenye uhusiano na Al Qaeda walitumia fursa ya kutokuwepo serikali thabiti nchini Syria na kuongezewa nguvu zaidi na vijana waliojiunga kupigania jihadi kutoka mataifa mengine.

WAANDAMANAJI WAKESHA HONG KONG

Mamia ya waandamanaj wa Hong Kong wamezingirwa na Askari polisi wanaowataka kusitisha maandamano na mkusanyiko wao karibu na ofisi za Makao makuu ya serikali.
Waratibu wa maandamano hayo wamekaidi amri hiyo na kuwataka watu wengine zaidi kujitokeza ili kuwaunga mkono katika madai yao ya kuitaka China iwaachie uhuru wa kumchagua kiongozi wao katika uchaguzi ujao wa mwaka 2017.

UINGEREZA YAONDOA TAHADHARI KWA RAIA WAKE KUINGIA KENYA

Serikali imeondoa tahadhari iliyowekea raiya wake kuingia Kenya
Uingereza imeondoa tahadhari iliyokuwea imetoa kwa raia wake dhidi ya Kusafiri Kenya.
Tahadhari hiyo kwa ukubwa likuwa inalenga maeneo ya mitaa ya mabanda, na baadhi ya maeneo ya Pwani ambako ilihofiwa kuwa raia wa kigeni wanalengwa kwa mashambulio ya kigaidi.

MAMA TUNU PINDA ACHANGISHA SHS. 128.6 MILIONI KUJENGA KANISA

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Morovian Tanzania ( KKMT)  Martin  Mwalyambwile  akimkaribisha  mke wa Waziri Mkuu Tunu Pinda wakati alipowasilia  kwenye Kanisa la Kiinjili la Usharika wa Mburahati jijini Dar es Salaam, jana kwa ajili ya kuongoza harambee ya ya kuchangia  ujenzi wa Kanisa hilo.
 Mke wa Waziri Mkuu Tunu Pinda akielekezwa kitu na  mmoja wa waumini wa Kanisa la Usharika wa Mburahati Yessaya Mwakifulefule wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo iliyoendeshwa na mama Tunu Pinda jumla ya shilingi milioni 128.6 zilipatikana katika harambe hiyo iliyofanyika jana .

SHURA YA MAIMAMU WAIKATAA RASIMU YA SITTA

Sheikh Rajabu Katimba

Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Rajabu Katimba

NA NORA DAMIAN, DAR ES SALAAM
SHURA ya Maimamu Tanzania imetangaza hatua za kuikwamisha Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, kwa kwenda kuwaeleza waumini wa dini ya Kiislamu kupiga kura ya hapana.
Hatua hiyo imekuja baada ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa iliyowasilishwa mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi, Andrew Chenge, kuiweka kando Mahakama ya Kadhi.
Akizungumza na MTANZANIA jana mara baada ya kumalizika kikao cha maimamu wa nchi nzima, Msemaji wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Rajabu Katimba, alisema hatua ya kupiga kura ya hapana ni moja ya azimio lililoafikiwa na kikao hicho.

DIWANI ALIYEHAMIA CCM AWACHANGANYA CUF, SASA KUANDAMANA KUPINGA UAMUZI WAKE!


Chama cha Wananchi (CUF) wilaya ya Tanga kimesisitiza kufanya  maandamano ya amani mwanzo mwa wiki hii ya kushinikiza aliyekuwa Diwani wa chama hicho Kata ya Marungu Mohamed Mambeya, ambaye amehamia Chama cha Mapinduzi (CCM) kuacha kuhudhuria vikao vya Baraza la Madiwani kutokana na kupoteza sifa.

Kwa mujibu wa Katiba ya CUF kifungu cha 9(1) G ya mwaka 1992 toleo la 2003,”Mwanachama yeyote atasita kuwa mwanachama ikiwa atakuwa mwanachama wa chama kingine cha siasa.

Diwani wa Kata ya Mwanzange na Mwenyekiti wa  CUF Wilaya ya Tanga, Rashid Jumbe, alisema Mambeya ameendelea kuvunja kanuni za Halmashauri kupitia Baraza la Madiwani kwa kutaka kwa lazima kushiriki vikao ambavyo kisheria si mjumbe halali wa vikao hivyo.

CHADEMA WAFUNIKA MWANZA. POLISI WAWATAWANYA KWA MABOMU

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe


NA DANIEL MKATE

Baada ya Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza kuzuia maandamano ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katikati ya wiki iliyopita, umati mkubwa wa wakazi jijini hapa jana walifurika katika uwanja wa Shule ya Msingi Mbugani kuwasikiliza viongozi wao wa kitaifa.

Viongozi hao ni Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu.Mkutano huo uliohutubiwa na viongozi hao, pia ulihudhuriwa na viongozi wa mkoa wa Mwanza wa vyama vya NCCR-Mageuzi na Chama cha Wananchi (CUF) ambavyo pamoja na Chadema  wanaunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Baadhi ya wafuasi wa vyama hivyo, walikuwa wamevaa sare za vyama vyao vinavyounda Ukawa na  muda wote walionekana kuwashangilia viongozi wao walipopanda jukwaani.

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUTUMIA REDIO JAMII KUELIMISHA UMMA

DSC_0009
Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye, akiutambulisha ujumbe wa wageni kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini kwa Wenyeviti wa bodi na mameneja wa redio za jamii nchini waliohudhuria warsha ya siku tano ya kuwajengea uwezo katika kuboresha masoko kwenye vituo vyao iliyofadhiliwa na shirika la maendeleo la Sweden (SIDA) na kuratibiwa na UNESCO.

Na Mwandishi Wetu, Sengerema
OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kupitia Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani (DEP) itaanza kutoa elimu inayohusu sheria ya vyama vya siasa na sheria ya gharama za uchaguzi kupitia redio za jamii ili kuwawezesha wananchi kutambua wajibu wao katika kulinda amani ya taifa kuelekea katika uchaguzi na wakati wa uchaguzi.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini, Beatrice Stephano wakati akizungumza na mameneja wa redio hizo katika warsha yao ya siku 5 iliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Sengerema.

TIBAIGANA ASEMA, WAPINZANI WANA HAKI YA KUANDAMANA!


Alfred Tibaigana enzi zake akiwa kazini

Katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake Buganguzi wilayani Muleba, Kamishna Tibaigana alisema suala la maandamano halikumsumbua kwa kuwa alielewa kuwa sheria inayaruhusu, hivyo alichokuwa akifanya ni kuwaita viongozi wa vyama vinavyotaka kuandamana na kufanya nao makubaliano ya namna maandamano hayo yanavyopaswa yafanywe kabla ya kuyaruhusu.
“Pengine hiyo ndiyo sababu sikuwahi kushambuliwa kwa maneno ya kejeli au matusi na wanasiasa kwa kuwa sikuwahi kuzuia maandamano yao bila sababu na hata kama kulikuwa na sababu niliwaita na kuwaeleza na tulikubaliana.
“Kikubwa ni kujenga tabia ya kuwaita viongozi wa waandamanaji na kujadiliana nao, vinginevyo wanaweza pia hata kukufikisha mahakamani wakipinga kuzuiwa maandamano yao,” alisema Tibaigana ambaye alikumbana na sakata la kudai maandamano wakati akiwa Kamanda kwenye mikoa ya Tanga, Arusha na Dar es Salaam.

MBIVU NA MBICHI ZA BUNGE LA KATIBA KUANZA KUJULIKANA LEO

Na Daniel Mjema, Mmwananchi
Dodoma. Wiki ya kufa au kupona kwa Bunge la Katiba, inaanza leo mjini Dodoma wakati wajumbe watakapoanza kuzipigia kura ibara na sura za Rasimu ya Katiba inayopendekezwa.
Shughuli hiyo itaanza huku kukiwa na hofu ya kutopatikana kwa theluthi mbili ya kura kwa wajumbe kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya wajumbe kutoka Zanzibar inayotakiwa kwa mujibu wa kanuni, sheria na Katiba ya nchi.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa wiki iliyopita na Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta, upigaji kura utafanyika kwa siku nne kuanzia leo hadi Oktoba 2, mwaka huu na iwapo itapitishwa, atakabidhiwa Rais kusubiri kupigiwa kura ya maoni mwaka 2016.
Habari kutoka bungeni zinadai kuwa wasiwasi wa kutopatikana kwa theluthi mbili uko zaidi upande wa Zanzibar hasa baada ya wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia Bunge hilo.

MAHAKAMA YA KADHI YAENDELEA KULITAFUNA BUNGE LA KATIBA


Dodoma/Dar. Suala la Mahakama ya Kadhi limechafua hali ya hewa bungeni mjini Dodoma baada ya wajumbe Waislamu kutishia kupiga kura ya hapana kama halitaingizwa katika Rasimu inayopendekezwa.
Wakati Waislamu wakishikilia msimamo huo, wajumbe ambao ni Wakristo nao wamejipanga kupiga kura ya hapana endapo Mahakama ya Kadhi itaingizwa katika Katiba inayopendekezwa.
Dalili za mpasuko huo zilianza kujitokeza jana asubuhi baada ya mjumbe mmoja, Jaku Ayub Hashim kuwasha kipaza sauti akitaka kuzungumza akisema ana jambo muhimu.

Sunday, 28 September 2014

MWANARIADHA MKENYA AWEKA REKODI MPYA YA DUNIA KATIKA MARATHON

Mwanariadha Wilson Kipsang ashinda mbio za Berlin Marathon mwaka uliopita
Mwanariadha wa Kenya Dennis Kimeto amevunja rekodi ya dunia katika mbio za Marathon zilizondaliwa mapema leo mjini Berlin nchini Ujerumani.

JIVU LA VOLCANO LAWAUA WATU 30 JAPAN


Mlima Ontake

Takriban wakwea milima 30 huenda wameaga dunia nchini Japan kufuatia kulipuka kwa mlima wa Volcano siku ya Jumamosi na kusababisha kukwama kwa mamia ya raia hao karibu na kilele cha mlima huo.
Makundi ya uokoaji yanasema kuwa yalipata miili karibu na kilele cha Mlima Ontake.

HURUMA, MAADILI MABAYA CHANZO CHA AJALI BARABARANI

Mojawapo ya ajali za barabarani zilizotokea mwezi Agosti mwaka huu

Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny BlogArusha: IMEELEZWA kuwa baadhi ya ajali ambazo zinatokea barabarani wakati mwingine zinasababishwa na huruma pamoja na maadili mabaya ya baadhi ya askari wa kikosi cha usalama barabarani hali ambayo pia inaongeza vifo.
Hata hivyo huruma hizo ambazo zinatoka kwa askari hao pamoja na maadili mabaya pia chanzo chake ni maslahi duni ambayo wanayapata pamoja na ugumu wa kazi katika vituo vyao.

CONGO WAANDAMANA KUMPINGA JOSEPH KABILA

Joseph Kabila
Maelfu ya watu wameandamana nchini Jamhuri ya Kidemorasi ya Congo wakimpinga rais wa taifa hilo Joseph Kabila.

ACHANA NA IS, KUNDI LA AL-NUSRA FRONT NALO LATANGAZA VITA!

Wapiganaji wa Jihad kutoka kundi la Al Nusra front
Kundi lililo na uhusiano na mtandao wa Al-Qaeda nchini Syria Al- Nusra Front limepinga mashambulizi ya angani yanayotekelezwa na muungano unaoongozwa na Marekani kama vita dhidi ya Uislamu na kusema kuwa nchi za Magharibi na zile za Kiarabu zinazohusika zitalengwa na makundi ya Jihad kote duniani.

SALVA KIIR SASA ATAKA KUSITISHWA KWA VITA SUDAN KUSINI

Rais Salva Kiir na Riek Machar wakibadilishana makubaliano ya kusitisha vita
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amesema kuwa serikali yake imejitolea kumaliza vita nchini nchini humo.
Akiongea kwenye mkutano mkuu wa baraza la umoja wa mataifa mjini New York Kiir ameitaka jamii ya kimataifa kuwashinikiza waasi kuheshimu makubaliano ya kusitisha vita.

KIMBUNGA CHA SERENGETI FIESTA KUIKUMBA MBEYA LEO

Barnaba Classic kuhanikiza katika Uwanja wa Sokoine leo

Kusubiri sasa kumetosha kwa wakazi wa Mbeya na vitongoji vyake, kinywaji cha Serengeti Premium Lager kwa kushirikiana na waandaji wa tamasha la Serengeti Fiesta 2014, Primetime Promotions wameshaingia mjini humo kuporomosha burudani ya aina yake katika uwanja wa Sokoine leo.
Baada ya kugundua kwamba tamasha la Serengeti Fiesta litakuwa mkoani humo mwishoni mwa juma hili, wakazi wa mji wa Mbeya wamejipanga tayari kwa ajili ya kulipokea tamasha hilo na mashabiki wengi wameahidi kufurika katika uwanja huo.

MBINU MPYA ZA MAANDAMANO YA CHADEMA ZAWATESA POLISI, WAANDAMANA DAR ES SALAAM BILA YA KUKAMATWA

 Wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tawi la Kimara Korogwe jijini Dar es Salaam wakiwa katika maandamano ya kupinga vikao vya Bunge la Katiba vinavyo endelea mjini Dodoma.

MADARAKA YA RAIS YAWAGAWA WAJUMBE BUNGE LA KATIBA


Suala la ugawaji wa madaraka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania na Rais wa Zanzibar kwenye Rasimu ya Katiba inayopendekezwa limewagawa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba (BMK).
 
Mgawanyiko huo umehusu zaidi eneo la kuigawa Jamhuri ya Muungano katika mikoa, wilaya na maeneo mengine ya kiutawala.
 
Baadhi ya wajumbe wanataka Rais wa Zanzibar apewe mamlaka kamili ya kuigawa Zanzibar, huku wengine wakitaka asifanye hivyo mpaka pale atakapokuwa amekasimishwa mamlaka hayo na Rais wa Jamhuri ya Muungano.
 
Hayo yalidhihirika wakati Kamati 12 za BMK zikiwasilisha mapendekezo ya marekebisho ya rasimu ya Katiba inayopendekezwa, iliyowasilishwa bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi, Andrew Chenge.

UKAWA WAMSHUKIA KIKWETE, WASEMA YEYE NA CCM HAWAELEWEKI!

Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa

Na Ibrahim Yamola na Goodluck Eliona, Mwananchi
Dar es Salaam. Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umesema kuwa Rais Jakaya Kikwete na CCM hawaeleweki ukidai ni kutokana na kukiuka makubaliano yao kuhusu kuendelea kwa Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma.
Umoja huo pia umedai kwamba Mahakama Kuu ya Tanzania imeshindwa kutoa uamuzi fasaha kuhusu tafsiri ya kisheria ya mamlaka ya Bunge hilo katika kurekebisha Rasimu ya Katiba kwa kuogopa lawama kutoka Ukawa na CCM.
Ukawa unaoundwa na vyama vya Chadema, CUF, DP, NLD na NCCR-Mageuzi ulieleza hayo jijini hapa jana ulipozungumzia Mchakato wa Katiba ulipofikia, hasa baada ya Bunge hilo kufanya marekebisho ya kanuni kwa wajumbe wake kuruhusiwa kupiga kura kwa njia ya mtandao.
Mwenyekiti mwenza wa Ukawa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kuwa makubaliano ya kusitishwa kwa Bunge hilo kati yao na Rais Kikwete yameshindwa kutekelezwa, jambo ambalo wanashindwa kuelewa sababu zake.

KINANA AITINGISHA LUSHOTO, AZOWA WANACHAMA UPINZANI

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahamn Kinana  na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwa pamoja wakiwapungia mkono mamia ya watu waliofurika kwenye uwanja wa mikutano wa kijiji cha Lwandai kata ya Mlola wilayani Lushoto.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Lwandai kata ya Mlola ambapo aliwasisitiza wananchi hao kushiriki kazi za maendeleo na kujiunga kwa wingi kwenye mfuko wa Afya ya jamii.

Saturday, 27 September 2014

SITTA APOKEA MESEJI ZA MATUSI

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta

Na Daniel Mjema, Habel Chidawali, Mwananchi
Dodoma. Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta amesema anapokea meseji za simu zaidi ya 50 kwa siku za kumtukana na kusisitiza ataendelea kupambana kuhakikisha Katiba inayopendekezwa inapatikana.
Sitta alitoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma jana wakati akielezea kutoridhishwa kwake na kile alichodai ni namna hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Saed Kubenea inavyopotoshwa na wanaomchukia.
“Kuna baadhi ya vyombo vya habari wananichukia mimi binafsi. Wasichanganye chuki hizo na mchakato wa Bunge Maalumu,” alisema Sitta na kuongeza;

SUMU YA 'MKOROGO' HUATHIRI PIA WAUME WA WANAWAKE WATUMIAJI



Na Elias Msuya, Mwananchi

Nuru Masoud, mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, amekuwa akijishughulisha na biashara za vipodozi vya asili, maarufu kama mkorogo.
Hata hivyo, biashara hiyo aliisitisha mwaka 2013 baada ya kupata madhara makubwa ya ngozi ambayo yaliambukiza pia familia yake.
“Nilianza kuwashwa ngozi mfululizo, nikadhani nimeathirika na Ukimwi,” anasema akikumbuka jinsi ugonjwa huo ulivyomtesa.
 “Niliamua kwenda Hospitali ya Muhimbili kwa daktari wa ngozi ambaye alichukua kipande cha ngozi yangu na kwenda kuipima na kubaini tatizo ni mkorogo.”

CHUO CHA DINI CHAFUNGWA KENYA, CHATUHUMIWA KUFUNDISHA 'UGAIDI'!

Madrasa ya Ngulini iliyofungwa kwa madai kuwa inafunza itikadi kali za kidini
Maofisa nchini Kenya wameifunga Madrassa au shule ya mafunzo ya dini ya Kiislamu nchini humo kwa madai kuwa inafunza masomo ya itikadi kali.
Madrassa hiyo iliyo mjini Machakos, Mashariki mwa Nairobi, imechukuliwa hatua hiyo baada ya vijana kadhaa waliokuwa wakihojiwa na polisi kuitaja.

KESI YA HOSNI MBARAK YAPIGWA KALENDA

Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak akiwa mahakamani
Uamuzi wa kesi inayomkabili rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak kuhusu mashtaka ya ufisadi na mauaji ya waandamanaji wakati wa mapinduzi ya mwaka 2011 umeahirishwa.
Jaji alisema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na sahabu ya kuwepo kwa ushahidi ambao bado mahakama haijausikiliza.

UNYAMA: MWANAMKE APIGWA MAWE HADI KUFA SOMALIA

Wapiganaji wa Al Shabaab
Mwanamke mmoja ameuawa kwa kupigwa mawe nchini Somalia na kundi la wanamgambo wa Al Shabaab.
Ripoti zinasema kuwa takriban watu 200 akiwemo gavana wa eneo hilo walishuhudia watu wakimpiga mawe mwanamke huyo kwenye mji wa Barowe.
Mwanamke huyo wa umri wa miaka 30 alikuwa ameshutumiwa kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa.

MAAFA MAKUBWA HAYA: WALIOFARIKI NA EBOLA WAFIKIA 3,000

Mwakilishi wa WHO Michael O''leary
Shirika la afya duniani limesema kuwa zaidi ya watu elfu tatu sasa wamedaiwa kufariki kutokana na kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola katika eneo la Afrika Magharibi kati ya visa elfu sita vya ugonjwa huo vilivyoripotiwa.
Liberia imeathiriwa vibaya na ugonjwa huo huku WHO ikisema kuwa kumekuwa na vifo 150 vilivyotokea katika kipindi cha siku mbili pekee.

MBUNGE AZOMEWA NA WANANCHI MBELE YA KINANA

Mbunge wa Korogwe Mjini (CCM), Yusuph Nassir

KATIBA MPYA: WARIOBA SASA KUTUMIA NGUVU YA UMMA

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba

NA ROMANA MALLYA
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, ametangaza rasmi kuungana na umma mpana, kupinga rasimu ya Katiba Mpya inayopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba (BMK).
 
Hatua hiyo isiyotarajiwa, inafuatia Bunge Maalum la Katiba kukamilisha rasimu hiyo Jumatano iliyopita, ikitarajiwa kupigiwa kura mapema wiki ijayo.
 
Akizungumza kwenye adhimisho la miaka 19 tangu kuanzishwa kwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Aidha, Jaji Warioba, alisema Bunge hilo limeondoa mambo ya msingi  yaliyopendekezwa na wananchi yakiwa ni kiini cha kupatikana kwa Katiba Mpya.

DK. DIALLO AONYWA KUHUSU SIASA ZA KUCHAFUANA

Dk. Antony Dialo, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza
Chama cha Mapinduzi (CCM), mkoani hapa, kimekemea siasa za kuchafuana zinazofanywa na Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Mwanza, Dk. Antony Dialo dhidi ya Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa.
 
Kimesema mwenyekiti huyo akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari, alisema Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, hakufanya kazi ya kuleta maji ya Ziwa Victoria na kuyasambaza mkoani Shinyanga. Akizungumza juzi na waandishi wa habari, Katibu wa siasa na uenezi mkoani Shinyanga, Emmanuel Mlimandago, alisema kauli ya Dialo ni ya ulimbukeni wa kisiasa na kujitafutia umaarufu kupitia mgongo wa Lowassa.