Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 25 June 2016

HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA HUENDA IKASHINDWA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS LA UTENGENEZAJI MADAWATI

 Na EmanuelMadafa,Jamiimojablog

Halimashauri ya jiji la Mbeya huenda ikashindwa kutekeleza  agizo la Rais John Pombe Magufuri, lililozitaka halmashauri  kuhakikisha zinamaliza tatizo la uhaba wa madawati shuleni ifikapo Juni 31, mwaka huu kutokanana kutokuwepo kwa msukumo wa kutosha katika  utekelezaji wa agizo hilo.



Halmashauri ya Jiji la Mbeya, imeweza kutengeneza na kukamilisha madawati 1500, wakati uhitaji ni madawati 10,000.

TRA YAZIDI KUBORESHA TIMU YA KUTOA ELIMU YA KODI, YAZINDUA JUMUIYA YA WANAFUNZI WA KODI IFM

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wakati wa uzinduzi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa kodi chuoni hapo (Student Tax Association).

Katika kuhakikisha kunakuwa na wasomi ambao wanakuwa na elimu kuhusu kodi, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imefanya uzinduzi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kodi (Student Tax Association) katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambapo wanachama hao watatumika kutoka elimu kwa wananchi wengine kuhusu kodi.

WACHUMI NA MAAFISA MIPANGO NCHINI WAKUTANA DODOMA KUJADILI MPANGO WA PILI WA TAIFA WA MAENDELEO



Servacius Likwelile, Katibu Mkuu Hazina

Na Benny Mwaipaja, WFM

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile amesema kuwa Tanzania imejipanga kuimarisha mapato yake ya ndani ili kutekeleza kikamilifu Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021.

Dkt. Likwelile, amesema hayo Mjini Dodoma, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku 2 unaowahusisha wataalamu wa Uchumi na Mipango wapatao 170 kutoka nchi nzima.

Friday, 24 June 2016

TOVUTI YA WANANCHI INAVYOTATUA KERO ZA WANANCHI


Na Immaculate Makilika -MAELEZO

Ni ukweli usiopingika kwamba dunia imeingia katika maendeleo ya teknolojia yanayopelekea matumizi ya vifaa vya kisasa na vyenye utaalamu wa hali ya juu katika kufanya shughuli mbalimbali, ambazo hapo awali zilifanywa kwa kutumia nguvu kubwa na idadi kubwa ya watu na kwa muda mrefu.

Maendeleo hayo ya teknolojia yamejidhihirisha katika nyanja nyingi mojawapo ni hii ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano. Ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano umerahisisha mawasiliano na unatoa fursa kwa jamii kwa ujumla kuwa huru zaidi katika kutekeleza majukumu yake.

ZITTO KABWE: KAULI YA DK. MAGUFULI NI VITA DHIDI YA DEMOKRASIA


Kauli ya Rais ya Kuzuia Vyama vya Siasa Kufanya Shughuli za Siasa kwa Miaka Mitano ni Tangazo la Vita dhidi ya Demokrasia na Mfumo wa Vyama vingi Nchini

Tumepokea kwa MSHTUKO na masikitiko makubwa kauli ya Rais kwamba vyama vya siasa havipaswi kufanya siasa isipokuwa wakati wa Kampeni na kupitia bungeni. Kimsingi kauli ya Rais ni kauli yenye nia ya kuvunja Sheria ya Vyama vya siasa inayolinda uwepo wa mfumo wa vyama vingi na kuhimiza vya vya siasa kufanya shughuli za siasa katika msimu wote ili kuthibitisha uhai wao.

ASILIMIA 89 YA WATANZANIA WANAMKUBALI RAIS MAGUFULI


Rais John Magufuli


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAREHE 23/06/2016



                                                        UTAFITI



MIEZI 8 TOKA MHE RAIS JOHN MAGUFULI AMECHAGULIWA KUWA RAIS WA JAMHURI YA     MUUNGANO WA TANZANIA



Ndugu waandishi wa habari habari za leo na pole kwa majukumu mazito ya ujenzi wa Taifa. Taarifa yetu itajikita katika maeneo makuu mawili, Mkutano Mkuu wa CCM na UTAFITI wa Miezi 8 ya Mhe Rais John Magufuli.

Taasisi ya CZI ni taasisi huru isiyo ya kiserikali ambayo inajihusisha na ushauri wa mambo ya HABARI na kijamii, pamoja na tafiti mbalimbali. Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, tulizunguka nchi nzima na kuuliza wananchi maswali ya papo kwa papo, ama kwa njia ya simu ama kwa kuhoji kimakundi kulingana na umri wa wahusika.

Tulihoji Watanzania 2,3oo wa kada mbalimbali katika maeneo kadha wa kadha tuliyotembelea kuanzia umri wa miaka 14 hadi 18 na kuanzia wenye umri wa miaka 18 hadi 30 na kuanzia miaka 30 hadi 60.



KUNDI LA 1 UMRI MIAKA 14-18

Kundi hili baada ya kuhojiwa wanaamini Rais John Magufuli ataleta mageuzi makubwa ya kiuchumi, na atarejesha nidhamu ya masomo shuleni kuanzia shule za awali, msingi nasekondari kwa vijana wenye umri kuanzia miaka 7 hadi 18.

MERCY KITOMARI: MJASIRIAMALI KIJANA ANAYEFIKIRIA MAKUBWA

Mjasiriamali kijana Mercy Kitomari akiwa ofisini kwake wakati wa mahojiano.

Modewjiblog ilipata bahati ya kuzungumza ana kwa ana na Mercy Kitomari mmoja wa wajasiriamali wanawake vijana ambaye anafikiria kuwa na kiwanda kikubwa cha ashkrimu (ice cream) ifikapo mwaka 2020 akizisafirisha na kuziuza Tanzania nzima na Afrika Mashariki. Wapi alipotokea, yuko wapi kwa sasa, ni machungu gani aliyokumbana nayo na anaishauri nini serikali na wajasiriamali wenzake. Haya yote utayajua katika mahojiano haya .Soma…

MODEWJI BLOG: Role model wako nani?
MERCY: Magufuli. You know why?(unajua kwanini?) ametuweka wazi kabisa kwamba maisha ni changamoto na tusikubali kushindwa ni lazima kupambana na kufanyakazi kwa bidii na maarifa kuondoa vigingi vyote vinavyotukwamisha. Amenifanya nifanye kazi kwa bidii. Nataka kuwa mwanamke anayefanya mabadiliko. Hakuna kitu kinachokuja kirahisi. Nataka kuwa mwanamke yule ambaye anaonesha tofauti nataka kuifanya nchi yangu iniringie.

RAIS KAGAME KUFUNGUA MAONESHO YA 40 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM-2016

Ofisa Mawasiliano Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Theresa Chilambo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wakati akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Edwin Rutageruka (katikati), kuzungumza na wanahabari kuhusu maonesho  ya 40 ya biashara ya kimataifa yatakayoanza rasmi Juni 28, 2016 hadi Julai 8, 2016 katika viwanja vya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Ukuzaji wa Biashara, Anna Bulondo.

'NDOA' YA TTCL NA BHARTI AIRTEL YAVUNJIKA RASMI

Msajili wa Hazina, Laurence Mafuru (wa kwanza kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Profesa Tolly Mbwete (katikati) hati ya mauzo ya hisa asilimia 35 za Kampuni ya Bharti Airtel Afrika. Serikali imezinunua rasmi hisa za kampuni hiyo ndani ya TTCL ambapo leo wamesaini mkataba wa mauziano wa hisa hizo. Kulia ni  Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Bharti Airtel Afrika, Christian De Faria akishuhudia.

DK. MENGI ACHANGIA MADAWATI 1,000, ATOA SOMO KWA WATU MATAJIRI

Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi akizungumza katika halfa ya kukabidhi milioni 70 kwa wilaya ya Handeni na Bagamoyo ambazo zitawezesha wilaya hizo kununua madawati 1,000 na kila wilaya kupata madawti 500.

Katika kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kuhakikisha tatizo la madawati nchini linamalizika hadi kufikia Juni, 30 mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa Mashirika ya IPP, Dk. Reginald Mengi ametoa msaada wa milioni 70 kwa wilaya ya Handeni, Tanga na Bagamoyo, Pwani kila moja ikipata milioni 35 kwa ajili ya ununuzi wa madawati 1,000 ambayo yatasaidia kumaliza tatizo hilo katika wilaya hizo.

TANZANIA BADO INAHITAJI WATAALAM WALIOBOBEA KATIKA BIASHARA YA KIMATAIFA

 Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema wakati akifungua mkutano wa wadau mbalimbali wa kujadili program mpya mbili za masomo katika ngazi ya Shahada ya Uzamili katika Biashara ya Kimataifa  na Ugavi, Usimamizi mfumo wa uzalishaji na usambazaji, zinazotarajiwa kuanza kutolewa na chuo hicho.

Wednesday, 22 June 2016

SEKTA ISIYO RASMI KUNUFAIKA NA HUDUMA ZA HIFADHI YA JAMII



Mkurugenzi wa Sheria kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Onorius Njole akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Mpango Maalum wa kutoa huduma ya hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi maarufu kama Informal Sector Scheme ambayo inajumuisha waendesha bodaboda, bajaji na mama lishe. Kulia ni Mkuu wa Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde.

Tuesday, 21 June 2016

Shinda Nyumba: Zimebaki siku chache tu, changamkia mjengo huu!

Nyumba (7) Kushinda ni rahisi sana! nunua Gazeti la Championi, Ijumaa, Uwazi, Amani, Ijumaa Wikienda au Risasi. Jaza kuponi iliyopo ukurasa wa pili kisha tuma kwenye Ofisi za Global Publishers, Bamaga - Mwenge, Dar es Salaam au kwa wakala aliyekaribu nawe na nyumba hii yaweza kuwa yako Juni 30, 2016.

WAAMUZI WA MECHI YA SERENGETI BOYS, SHELISHELI



Waamuzi wanne kutoka Ethiopia, ndio watakaochezesha mchezo wa kimataifa kati ya timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ na Shelisheli utakaofanyika Juni 26, 2016 kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo ni wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17. Waamuzi hao ni Belay Tadesse Asserese ambaye ni mwamuzi wa kati wakati wasaidizi wake ni Tigle Gizaw Belachew upande wa kulia na Kinfe Yilma Kinfe upande wa kushoto huku mwamuzi wa akiba atakuwa Lemma Nigussie. Kamishna wa mchezo huo atakuwa ni Bester Kalombo.

SERIKALI YAREJESHA MISAMAHA YA KODI KWA TAASISI ZA DINI, YATOA MASHARTI MAZITO

Dk. Phillip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango


Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Serikali imelegeza msimamo wake kuhusu kuondoa misamaha ya kodi
kwenye Taasisi za dini badala yake itaongeza udhibiti ili kuzuia mianya ya matumizi mabaya ya misamaha hiyo.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ametoa ufafanuzi huo mjini Dodoma wakati akiongea na vyombo vya habari ili kutoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizotolewa na wabunge wakati wa kujadili bajeti Kuu ya Serikali iliyopitishwa Juzi na Bunge.

WABUNGE, WAANDISHI WA HABARI NA WASANII KUOSHA MAGARI KATIKA TAMASHA LA MEDIA CAR WASH MJINI DODOMA JUMAMOSI HII


KUWA MJASILIAMALI NA TAJIRIKA NA UFUGAJI WA KUKU KUPITIA INCUBATOR



Katika miaka ya hivi karibuni ufugaji wa kuku umekua kwa kiasi kikubwa na kuwa mtaji mkuu wa wajasiriamali wadogo na wakubwa katika kujiingizia kipato.

MACHINGA JIJINI MWANZA WAKUTANA KUAMUA HATIMA YAO

Mgeni Rasmi, Dkt.Kissui Steven Kissui ambae ni Mwenyekiti wa Shindano la Uwezeshaji Kiuchumi na Ajira Tanzania, akifungua Mkutano wa Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) Jijini Mwanza uliofanyika hii leo.
Na BMG

Mkutano huo ambao uliandaliwa na Shirika la Machinga Mkoa wa Mwanza SHIUMA, ulilenga Machinga kujadiliana na wadau wengine wa Uwekezaji ikiwemo taasisi za kifedha, juu ya Kurasimisha biashara zao na kuwekwa kwenye mifumo rasmi ya Kibiashara na Kijamii.

TIGO PESA YATOA FURSA ZA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI

Mkuu wa Huduma za Kifedha za Tigo, Ruan Swanepoel (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Tigo Makumbusho Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu Tigo Pesa kutoa fursa za biashara kwa wajasiriamali. Kulia ni Mkuu wa Masoko wa Tigo, Temitope Ayedum na kushoto ni Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga.

WACHAWI WAVAMIA MKUTANO WA INJILI JIJINI MWANZA

Na Binagi Blog_BMG
Katika hali ya kushangaza, binti mmoja (pichani katikati) ametoa ushuhuda mbele ya waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza na kueleza jinsi alivyoshindwa kumtoa kafara mchungaji wa kanisa hilo, Dk. Daniel Moses Kulola.