Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 31 July 2014

NDANDA FC YAHITAJI ‘BUNDUKI MBILI’ KUJIKAMILISHA MAWINDO YA LIGI KUU

ndanda
Na Baraka Mpenja, Dar es Salaam

NDANDA FC ya Mtwara inaingia kambini leo kuendelea kujiwinda na mikikimikiki ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015 inayotarajia kuanza kushika kasi septemba 20 mwaka huu.
Katibu mkuu wa klabu hiyo, Seleman Kuchele ameuambia mtandao huu kuwa kwa kiasi kikubwa wamekamilisha ripoti ya kocha wao aliyokabidhi baada ya kumalizika kwa ligi daraja la kwanza, na wamebakiza nafasi mbili tu za usajili.
“Sisi tunaendelea kuikamilisha ripoti ya mwalimu. Kocha alikuwa anahitaji wachezaji tisa na mpaka sasa hivi tumesajili wachezaji saba na wawili tupo katika mipango ya mwisho na kwasababu muda umeongezwa, tutakuwa katika wakati mzuri wa kukamilisha,” Alisema Kuchele.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

NGUMI ZILIVYOPIGWA MANZESE SIKU YA IDDI PILI

Bondia Sadick Nuru kushoto akioneshana umwamba na Baraka Mchonge wakati wa mpambano wao ulifanyika Mazese Dar es salaam wakati wa sikukuu ya iddi pili . Nuru alishinda kwa point mpambano huo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Stevin Kobelo kushoto akirusha ngumi kumpiga Karim Ramadhani wakati wa mpambano wao uliofanyika siku ya iddi pili katika ukumbi wa Manyara Park Manzese Dar es salaam, mpambano huo walitoka droo ya kufungana pointI picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia Joseph Gili kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Ibrahimu Tamba wakati wa mpambano wao uliofanyika siku ya Iddi pili katika ukumbi wa manyara park Manzese Dar es salaam , Tamba alishinda kwa T.K.O  ya raundi ya nne Picha na www.superdboxingcoach .blogspot.com
Bondia Julius Kisalawe kushoto akipambana na Ramadhani Kumbele wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa TPBC uliofanyika siku ya Iddi pili katika ukumbi wa Manyara Park Manzese Dar es salaam , Kumbele alishinda kwa pointi na kufanikiwa kuchukua ubingwa picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha mkongwe wa mchezo wa masumbwi nchini,  Habibu Kinyogoli ‘Masta’ kulia akimvisha mkanda wa ubingwa bondia Ramadhani Kumbele baada ya kumdunda Julius Kisalawe kwa point,  kushoto ni Refarii Ally Bakari picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

RAIS KIKWETE ATUNUKIWA TUZO JINGINE LA KIMATAIFA

Rais Jakaya Kikwete

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Kikwete atunukiwa Tuzo jingine la kimataifa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa mara nyingine ametunukiwa tuzo la kimataifa – zamu hii kwa kuwa mshindi waTuzo la Nyota wa Demokrasia Afrika 2014 – Icon of Democracy Award Winner for 2014 in Africa.

Kwa mujibu wa barua aliyoandikiwa Rais Kikwete na kupokelewa Ikulu, Dar Es Salaam, Rais Kikwete amekuwa mshindi wa kwanza, na kwa mbali kabisa, katika mchuano na marais watatu wa Afrika ambao walifikia mwisho mwa mchuano wa kuwania tuzo hilo.

Katika barua hiyo, Mchapishaji na Mhariri Mkuu wa Jarida hilo, Pastor Elvis Iruh, akizungumza kwa niaba ya Kamati ya Tuzo 2014, amesema kuwa uongozi wa Rais Kikwete umekuwa ni hadithi ya kusifiwa ya mafanikio katika Bara ambako hadithi za namna hiyo siyo nyingi.

Tuzo hilo hutolewa na Jarida la The Voice na mwaka jana mshindi alikuwa ni Rais Bai Koroma wa Sierra Leone ambaye alikuwa ni mshindi wa pili wa Tuzo hiyo ambalo ilitolewa kwa mara ya kwanza kwa Rais wa Kwanza wa Zambia, Mzee Kenneth Kaunda.

Sherehe maalum ya kukabidhi tuzo hiyo imepangwa kufanyika Oktoba 17, mwaka huu, 2014, katika Hoteli ya Van der Valk, iliyoko Almere, Uholanzi.

Miongoni mwa sifa nyingine, Rais Kikwete anatunukiwa Tuzo hiyo kwa sababu ya kuwa msimamizi mzuri na wa kweli wa demokrasia, kuendelea kuhakikisha kuwa amani, utulivu na maendeleo vinaendelea kupatikana katika eneo la Afrika ambalo limepitia vipindi vingi vya migogoro na matatizo.

Aidha, gazeti hilo linasema kuwa Rais Kikwete amekuwa kiongozi wa mfano, kimataifa na kikanda, na linatoa mfano wa mchango wake katika kusuluhisha mgogoro mkubwa wa kisiasa nchini Kenya kufuatia uchaguzi mkuu wa 2007.

Rais Kikwete pia anasifiwa kwa mchango wake katika kusimamia maendeleo ya Tanzania katika nyanja mbali mbali – kilimo, elimu, miundombinu, maendeleo ya viwanda, utalii na pia mchango wake katika kuendeleza vijana na kutoa nafasi nyingi kwa akinamama kushika nafasi nyingi za uongozi.

Jarida la The Voice pia limempongeza Rais Kikwete kwa kuimarisha Umoja na Muungano wa Tanzania na kutoa nafasi kwa wananchi kujadili na kukubaliana kuhusu Katiba Mpya ya Tanzania.

Aprili mwaka huu, Rais Kikwete alitunukiwa tuzo la kuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya Afrika kwa mwaka 2013 – The Most Impactful Leader in Africa 2013.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
30 Julai, 2014

NIMEPOTEZA JAMAA WAWILI KWENYE AJALI YA MOROBEST

Maiti zikiwa zimelala huku wananchi wakihangaika kutoa majeruhi kwenye basi la Morobest jana asubuhi.
Majeruhi wa ajali ya basi la Morobest lililogongana na lori Pandambili wakiwa kwenye Kituo cha Afya Kibaigwa.
 Basi la Morobest likiwa limechakaa baada ya ajali mbaya iliyotokea jana Jumatano, Julai 30, 2014 katika Kijiji cha Pandambili wilayani Kongwa.
 Lori lililogongana na basi la Morobest ambapo mabomba yanaonekana yakiwa yameanguka na kuliponda basi hilo katika ajali iliyotokea jana Jumatano, Pandambili wilayani Kongwa. Watu 17 walifariki dunia papo hapo na wengine 52 kujeruhiwa vibaya. (PICHA ZOTE NA JAPHET MALONGO)

Ndugu zangu,
Katika ajali ya jana iliyolihusisha basi la abiria la Morobest na lori kwenye Kijiji cha Pandambili wilayani Kongwa nimepoteza jamaa zangu wawili na wengine watano wamejeruhiwa vibaya sana.
Jamaa zangu walikuwa wakielekea Dar es Salaam wakitokea Mpwapwa, ambako walikwenda kusalimia ndugu na jamaa.
Tuwaombee kwa Mungu awapumzishe kwa amani na wale majeruhi Mwenyezi Mungu awajalie afya na uponyaji wa haraka.
Amina.

Daniel Mbega,
Iringa





VIJIDUDU SUGU VYA MALARIA VYAGUNDULIKA


Mbu wa Malaria

Watafiti wametoa tahadhari kuwa vijidudu vya malaria visivyoweza kuuawa kwa dawa vimetapakaa katika maeneo ya mpakani kusini mashariki mwa Asia vikitishia mapambano dhidi ya Malaria.
Vipimo kwa wagonjwa 1000 katika maeneo ya Cambodia, Burma, Thailand na Vietnam vimegundua vijidudu hivyo havizuiliwi na artemisinin dawa inayoaminika katika vita dhidi ya malaria. Utafiti huo umeeleza kuwa kuyarudia
matibabu baada ya kukumbana na maambukizi inaweza kusaidia kupambana na kusambaa kwa Malaria katika Asia na baadae Afrika ndani ya muda mfupi. Mamia ya maelfu ya watu hufariki kutokana na Malaria kila mwaka hasa katika Afrika.
BBC

BAN KI MOON ALAUMU MASHAMBULIZI YA SHULE GAZA


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amelaumu mashambulizi ya Israel dhidi ya Shule ya Umoja wa Mataifa iliyoko Gaza ambako maelfu ya Wapalestina walikuwa wamejihifadhi kukwepa mashambulizi.
Ban Ki moon amesema hakuna kitu cha aibu kama kushambulia watoto waliolala. Amesisitiza uwajibikaji kwa waliofanya kitendo hicho kilichowaua watu 15 na kuwajeruhi wengine kadhaa.
Msemaji kimataifa umoja wa mataifa Chris Gunness amesema kitendo hicho cha jeshi la Israel hakiwezi kuwa na sababu ya kujitetea tunalaani vikali ukiukwaji huu wa sheria za kiamataifa zilizofanywa na majeshi ya Israel kwa sababu uchunguzi tuliofanya umeonyesha kwamba wanahusika.Marekani nayo bila kuitaja waziwazi Israel wamelaumu kitendo hicho. Hata hivyo msemaji wa Jeshi la Israel Luteni Kanali Peter Lerner amesema lilikuwa tukio la kuumiza mno.
Tulishalionya jeshi la Israel mara 17, tuliwaambia kwa hakika shule ilipo, tukawaambia ilikuwa imejaa zaidi ya watu 3000 ambao walikimbilia mapigano.
Kamishina Pierre Kraehenbuehl amesema shule ilikuwa imehifadhi raia ambao hawakuwa na mahali pa kwenda.
BBCSWAHILI

LIBERIA YAOMBA MSAADA KUHUSU EBOLA


Waziri wa Habari wa Liberia Lewis Brown amesema nchi yake haiwezi kuimudu hali ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola. Amesema Liberia inahitaji msaada toka jumuiya za kimataifa kutuma wataalam wa tiba ili wasaidie.
Brown ameuelezea mlipuko wa ugonjwa huo kuwa si wa kawaida.
“Huu bado ni mshituko. Uwezo wa huduma za afya ya jamii na vifaa vimezidiwa. Maambukizi na kutapakaa ni kwa namna ambayo hatukuwahi kuwa nayo. Tunapungukiwa wahudumu wa afya na kwakweli tunahitaji wataalam zaidi wa afya” alisema Brown
Amesema Liberia inahitaji vifaa vya huduma za kiafya, wataalam wenye uzoefu wa kiafya kutokana na hali ya ugonjwa huo ilivyo,tunahitaji chochote kinachoweza kutusaidia kupambana na ugonjwa wa Ebola amesisitiza
Serikali ya Uingereza imeitisha mkutano wa dharura kupanga hatua za kuchukuliwa kwa ushirikiano na serikali ya Ufaransa na Marekani. Umoja wa Ulaya imetenga dola milioni 2 nukta 5 za ziada ili kupambana na Ebola. Tangu Ebola ilipoanza mwezi Februari mwaka huu, zaidi ya watu 670 wamefariki huko Afrika Magharibi katika nchi ya Sierra Leone, Liberia, Guinea na Nigeria.
BBC

KIJIJI CHAFUNIKWA NA MAPOROMOKO INDIA

Zaidi ya watu 200 wanahofiwa kukwama katika maporomoko ya udongo nchini India, huku 20 wakithibitishwa kufariki dunia katikakijiji cha Malin karibu na mji wa Pune lilikotokea janga hilo.
Kazi ya uokoaji inaendelea katika eneo hilo huku hali ya hewa mbaya ikidaiwa kuchelewesha harakati hizo.
Vikosi vya uokoaji vimeendelea na kazi ya kuwanusuru waliofukiwa na maporomoko ya udogo huo, japo kuwa mazingira magumu na hali mbaya ya hewa vinakwamisha shughuli hiyo.Maporomoko hayo yaliyokikumba kijiji cha Malin India karibu na jimbo la Maharashtra yamesababisha nyumba nyingi kusombwa huku watu wakihofiwa kunaswa pia katika eneo hilo.
Mwandishi wa BBC Devidas Desh pande aliyepo katika eneo la tukio anasema jingo pekee linaloonekana kunusurika na janga hilo ni ya shule pekee, huku maeneo mengine yakiwa tambarale kabisa.
Narendra Modi ni waziri mkuu wa India na hapa anaelezea hatua wanazozichukua.
Maporomoko ya ardhi ni jambo la kawaida kutokea nchini India hasa kipindi cha mvua zitokanazo na pepo za Monsoon ambazo hunyesha kuanzia mwezi june hadi septemba kila mwaka.
BBCSWAHILI

Wednesday, 30 July 2014

UKWELI KUHUSU UGONJWA WA EBOLA




Ugonjwa wa Ebola unasababishwa na Virusi na ni ugonjwa hatari unaoambukiza haraka binadamu na wanyama mwitu (hayawani) kama kima, sokwe, popo, ndege, mijusi, amfibia, na kadhalika. Ugonjwa huu unaosababishwa na virusi aina ya Ebola Virus ni wa mlipuko.
Japokuwa hakuna mazingira maalum ambamo virusi vya Ebola vinapatikana, lakini wataalamu wanasema virusi hivyo vinapatikana kwa mnyama ambaye anapatikana zaidi barani Afrika.
Mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola umetokea katika nchi nyingi na bado unaendelea kupukutisha maisha ya watu wengi hasa barani Afrika. Matukio ambayo yamethibitishwa kuwepo kwa ugonjwa huo ni katika nchi za Liberia, Sierra Leone, Guinea, Ghana, Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Gabon, Sudan, Ivory Coast, Uganda na kadhalika. 
Ugonjwa wa Ebola daima unasambaa ndani ya maeneo ya utoaji wa huduma za afya.Hata hivyo, matukio mengine yamekuwa yakitokea nje ya maeneo hayo na hayafahamiki.

Jinsi ugonjwa huo unavyosambaa:
Namna ugonjwa huo ulivyojulikana kwa mara ya kwanza hakuna anayefahamu kwa hakika. Hata hivyo, ugonjwa wa Ebola unaweza kusambazwa kwa njia zifuatazo:
1. Kugusana moja kwa moja na mtu ama mnyama mwenye ugonjwa huo;
2. Kugusana moja kwa moja na damu ama majimaji (mate au mafua) ya mtu mwenye ugonjwa huo katika familia;
3. Kugusa vifaa vya tiba vilivyo na virusi vya ugonjwa huo kama sindano;
4. Kutumia vifaa visivyochemshwa katika hospitali kama sinano;
5. Kula ama kushika vinyesi vya wanyama wenye ugonjwa huo;
6. Kuvuta hewa yenye virusi vya ugonjwa huo katika mazingira ya hospitali;
7. Kutumia nyama ya wanyama walioathirika kama kitoweo;
8. Kutozingatia tahadhari za kitaalam.

Dalili za Ebola:
Mtu au mnyama mpaka aonyeshe dalili za ugonjwa wa Ebola huchukua kati ya siku 2 hadi 21. Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na:
1. Homa kali
2. Kuumwa kichwa
3. Kuharisha
4. Kutapika
5. Maumivu ya kifua
6. Maumivu ya tumbo
7. Mafua
8. Kikohozi
9. Maumivu ya misuli na viungo, hasa kwenye viungio
10. Kuvimba koo
11. Mwili kuwa dhaifu
12. Mfadhaiko
13. Kuchanganyikiwa
14. Macho kuwa mekundu
15. Kuvuja damu kwa ndani na nje

Nani aliye katika hatari?
1. Watu wanaofuga wanyama mwitu ama wanaoishi katika maeneo yenye wanyama mwitu;
2. Watu wanaotegemea wanyama mwitu kama popo kama chakula chao;
3. Watumishi wa vyumba ya kuhifadhia maiti;
4. Watumishi wa afya wanaowahudumia wagonjwa wa Ebola;
5. Watumishi wa afya katika hospitali ambazo hazina mazingira bora na safi;
6. Wanafamilia wa wagonjwa wa Ebola;
7. Watu wanaohudhuria hospitali ambazo hazina mazingira safi na salama;

Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa Ebola:
1. Epuka kugusa damu/majimaji ya wanyama ama binadamu walio na ugonjwa wa Ebola au hata maiti za watu waliokufa kwa ugonjwa huo kwa kuzingatia haya:
a) Tunza mazingira safi na salama ya hospitali;
b) Watelekeze wagonjwa wa Ebola;
c) Fukia miili ya waliokufa kwa Ebola kwa usalama;
d) Epuka mazishi ya kienyeji kama kuosha maiti za watu waliokufa kwa Ebola;

2. Watumishi wa afya na wanaowatazama wagonjwa wa Ebola wanatakiwa:
a) Kuvaa kwa usahihi vifaa vya kujikinga na nyuso, mikono na macho,
b) Na majoho maalum daima;
c) Kutumia sindano mara moja na kuziteketeza ama kuzifukia;
d) Epuka kutumia zaidi ya mara moja sindano au kutotumia sindano ambazo hazijachemshwa vyema;
e) Epuka kuosha maiti za watu waliokufa kwa Ebola;


***Share na wenzako ujumbe huu

BOKO HARAM YAWAFUKUZISHA KAZI WANAJESHI WAWILI CAMEROON

Rais Biya amewafuta kazi wanajeshi wawili kwa utepetevu
Rais wa Cameroon, Paul Biya, amewafuta kazi maafisa wakuu 2 wa jeshi baada ya wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram kutekeleza mashambulizi ndani ya nchi hiyo.
Katika taarifa iliyopeperusha katika kituo cha redio ya taifa hakuna sababu yeyote iliyotolewa kwa kutimuliwa kazi kwa kanali Youssa Gedeon na luteini kanali Justin Ngonga.
Wadau wa maswala ya usalama katika magharibi mwa Afrika hata hivyo wanashauri kuwa huenda Biya ameanza kuhofia uwezo wa Boko Haram kutekeleza mashambulizi ndani ya Cameroon.
Jumapili iliyopita kundi la Boko Haram lilimteka mke wa naibu waziri mkuu .
Yamkini Boko Haram ilimteka pamoja na msaidizi wake kiongozi mmoja wa kidini pamoja na meya wa mji wa Kolofata.
Mwandishi wa BBC aliyeko Yaounde Cameroon Muhaman Babalala anasema tukio hilo la utekaji nyara lilidhibitisha utepetevu wa maafisa wa usalama nchini Cameroon.
Kundi la Boko Haram linaanza kupanua eneo la mashambulizi yake
Maafisa hao wawili walikuwa wakiongoza doria katika mpaka wa Cameroon na Nigeria.
Kundi la Boko Haram limekuwa likipigania kuundwa kwa taifa la kiislamu kaskazini mwa Nigeria lakini katika siku za hivi punde limetekeleza mashambulizi ndani ya ardhi ya Cameroon.

Wapiganaji hao wamelaumiwa kwa vifo vya wanajeshi wanne mbali na utekaji nyara wa wageni nchini Cameroon.
BBC

AL SHABAAB YAUA MWANAMKE KWA KUTOFUNGA NIQAB

Wanamgambo wa kiislamu wa Al Shabab wamempiga mwanamke mmoja risasi na kumuua kwa kukosa kujifunga niqab kichwani.
Jamaa za mwanamke huyo mwenyeji wa mji wa Hosingow kusini mwa Somalia wanasema mwanamke huyo alikataa kujifunika kitambaa kichwani kuambatana na sheria za dini ya kislamu .
''alikuwa ameonywa ajisitiri lakini wapiganaji hao waliporejea wakashikwa na hasira walipopata kuwa hakuwa amejifunika na hivyo wakampiga risasi''.
Jamaa zake wameiambia BBC kuwa Ruqiya Farah Yarow alikuwa amewafokea wapiganaji hao akiwataka waondoke kwake na kusema kuwa angejisitiri baadaye.
Kundi la Al Shabab linalomiliki asili mia kubwa ya maeneo ya Kusini na Katikati ya Somalia limekuwa likishinikiza kutumiwa kwa sheria kali za kiislamu.
Hata hivyo msemaji wa kundi hilo amekanusha kuwa ni wao waliomuua mwanamke huyo .

Msemaji huyo anasema kuwa licha ya kudhibiti maeneo makubwa nchini humo kundi hilo bado halijatoa maelezo ya vipi wanawake wanastahili kujisitiri.
BBCSWAHILI

SHAMBULIO GAZA LAUA 15 SOKONI

Takriban watu 15 wameuwa na wengine 160 kujeruhiwa vibaya katika shambulizi kali la angani lililotekelezwa na Israeli kwenye soko moja huko Gaza.
Kwa mjibu wa viongozi wa Kipalestina mlipuko mkubwa ulilipua soko moja la Shejaiya la kuuza matunda na mboga ambalo kwa kawaida huwa na idadi kubwa ya watu, mashariki mwa Gaza.
Msemaji wa wizara ya afya Nchini Palestina amesema kuwa idadi kubwa ya wapalestina waliouwawa ama kujeruhiwa walikuwa wakiendesha shughuli za ununuzi wa bidhaa.
Msemaji wa kundi la Hamas, linalothibiti maeneo hayo Sami Abu Zuhri amekatalia mbali muafaka wa amani na kutaja kuwa hauna maana.
Wanahabari wanasema kuwa haijafahamika bayana iwapo wapalestina walikuwa wakijua kuwa watashambuliwa.
Walioshuhudia wanasema kuwa, waliona moshi mkubwa ukifuka kutoka eneo hilo huku magari ya kutoa huduma ya kwanza yakionekana yakiingia na kutoka mahalipa tukio.
Aidha inasemekana kuwa mmoja wa waandishi habari ameuwawa katika shambulio hilo.

Wakati huo huo, majeshi wa nchi kavu ya Israel yamesema yatasitisha mapigano kwa muda wa masaa manne, lakini kauli hiyo haitotumika katika maeneo ambako wanajeshi wake wanaendeleza operesheni.

BBC

KWA HALI HII, WALIOPONA KWENYE AJALI YA MOROBEST WAMRUDIE MUNGU, POLISI YATHIBITSHA WALIOKUFA 17!!




Picha kwa hisani ya JamiiForums

July 30 imesambaa Taarifa ya ajali ambayo imetokea mapema leo na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma ajali iliyosababisha vifo vya watu 17 kati yao wanaume 12, wanawake 5 na majeruhi kwa mujibu wa jeshi la Polisi Dodoma.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 08:00 asubuhi eneo la Pandambili barabara ya Dodoma –Morogoro ambayo imehusisha basi la kampuni ya Moro Best yenye namba T258 AHV ambalo lilikuwa likitokea Mpwapwa kuelekea Dar es Salaam.
Capture3Basi hilo lilikuwa likiendeshwa na SAID S/O LUSOGO liligongana na Lori namba T820CKU / T390CKT lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma likiendeshwa na GILBERT S/O ISAYA NEMANYA.
Taarifa ya kamanda wa Polisi inseam katika ajali hiyo watu 17 wamepoteza maisha kati yao wanaume ni 12 na wanawake ni 5. 
Pia watu 56 wamepata majeraha mbalimbali na wamelazwa katika Hospitali za wilaya ya Kongwa na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma. Miongoni mwa waliofariki ni pamoja na dereva wa lori hilo pamoja na utingo wake.

Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori kutokuwa na tahadhari kwa magari yaliyokuwa yanakuja mbele yake wakati anapita (overtake) gari lingine na kwenda kuligonga busi hilo.

MWANAMKE AFARIKI KATIKA SWALA YA IDD UWANJA WA SAMORA, IRINGA

  Halida Ng’anguli akiwa ameanguka  nje ya  choo  katika  uwanja  wa Samora kabla ya  kufariki dunia (picha na habari na    Francis Godwin Blog)
 Kaimu Sheikh wa Mkoa  wa  Iringa  Abubakar ChalamilaWAKATI  waislamu   nchini  jana  wameungana na  waislamu  wenzao duniani kuswali  sala  ya Iddi mkoani  Iringa swali   hiyo  imemalizika  vibaya  kufuatia kifo  cha  muumini  mwenzao Halida Ng’anguli mkai  wa Mwangata  C ambae ni shangazi wa manahabari wa gazeti la majira  Iringa Zuhura  zuhkeri kufariki  dunia  baada ya masaa machache  toka aanguke chooni uwanja wa  Samora.
Tukio  la  kuanguka kwa mwanamke   huyo  lilitokea majira ya  saa tatu  asubuhi wakati  waumini  wa dini ya  Kiislamu  ambao  walikuwa  wakiswali pamoja  katika  uwanja  wa samora mjini Iringa  kumaliza swala na  kuanza maandalizi ya kuondoka  uwanjani  hapo kabla ya mmoja kati ya  viongozi  kwa kutumia kipasa  sauti  kutangaza  tukio la  kuanguka kwa mwanamke  huyo huku akiwataka  wanawake kwenda  eneo la tukio katika  vyoo vya wanawake  ili  kutoa msaada  zaidi.
Hata  hivyo  jitihada za  waumini  hao wanawake  pamoja na  askari  waliokuwepo  uwanjani hapo  zilifanikisha  kumkimbiza  mweanamke  huyo  hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi.

                    Ibada ya  idd ikiendelea katika uwanja wa Samora mjini Iringa   
Mbali ya  jitihada  kubwa  za madaktari wa Hospitali  hiyo  kutaka kunusuru maisha  yake  bado  hali ilionekana  kuwa mbaya  zaidi kutoka na tatizo ya  ugonjwa wa kisukari lililokuwa  likimsumbua .
Yapata  majira ya saa 4  usiku mwanamke  huyo alifariki dunia  wakati  akiendelea  kupatiwa matibabu  Hospitalini  hapo.
  
Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza wa tatu  kushoto akishiriki ibada ya Iddi
Akithibitisha   kutokea  kwa  kifo  hicho Shangazi wa marehemu  mwanahabari  Zuhura Zukheri alisema  kuwa shangazi yake  alifariki  majira ya saa 4 akiwa katika matibabu na  kuwa  toka  alipofikishwa  Hospitali hapo  hari yake  ilikuwa  mbaya na  hakuweza kupata nafuu.

Zuhura  alisema  kuwa tatizo kubwa  lililokuwa likimsumbua ni ugonjwa wa  Kisukari  na  kuwa shughuli za mazishi  zimepangwa  kufanyika  leo  ambayo ni  siku ya  Iddi pili majira ya saa 10 jionini .

Uongozi  wa chama  cha waandishi wa habari  mkoa  wa Iringa (IPC) unaungana na familia ya  mwanahabari huyo  Zuhura  Zukheri katika  wakati  huu mgumu  wa maombolezo ya  kifo cha mpendwa  wetu  huyo.


Credit: Matukiodaima

MAUAJI YA KUTISHA: MZEE WA MIAKA 75 AUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI

MMG23716

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 30.07.2014
  • MZEE WA MIAKA 75 AUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
  • MTEMBEA KWA MIGUU AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA MAGARI MAWILI KUGONGANA.
 KATIKA TUKIO LA KWANZA: 
MZEE MMOJA MWENYE UMRI WA MIAKA 75 ALITAMBULIKA KWA JINA LA DAIMONI MATATA, MKAZI WA KIJIJI CHA LUSINGO ALIUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA SHINGONI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 02:00 HUKO KATIKA KIJIJI CHA LUSINGO, KATA YA SONGWE, TARAFA YA BONDE LA USONGWE, WILAYA YA MBALIZI, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA TUKIO HILO BADO KINACHUNGUZWA. 

AIDHA MTU MMOJA AMBAYE NI MTOTO WA MAREHEMU AITWAYE WATSON DAIMONI (53) MKAZI WA KIJIJI CHA LUSINGO AMEKAMATWA KWA MAHOJIANO KUHUSIANA NA TUKIO HILI.

MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI – MBALIZI KWA UCHUNGUZI WA KITABIBU. UPELELEZI ZAIDI JUU YA TUKIO HILI UNAENDELEA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL .N. MASAKI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITO KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO. 

AIDHA ANASHAURI FAMILIA ZIWE NA UTAMADUNI WA KUKAA NA KUTATUA KERO NA CHANGAMOTO MBALIMBALI AMBAZO ZINAJITOKEZA KATIKA KAYA ZAO ILI KUEPUKA MADHARA/MATATIZO YANAYOWEZA KUJITOKEZA.

 KATIKA TUKIO LA PILI:
 MTEMBEA KWA MIGUU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA BARAKA ZAWADI MJEMWA (31) MFANYABIASHARA NA MKAZI WA MIKOROSHINI – KYELA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.604 BCS AINA YA TOYOTA NOAH LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE ASAJILE AYUB (35) MKAZI WA KASUMULU KULIGONGA GARI JINGINE LENYE NAMBA ZA USAJILI T.649 ALB AINA YA TOYOTA HILUX LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE MUSA MWALUBANGE (32) MKAZI WA KIJIJI CHA MBUGANI NA KISHA KUPOTEZA MWELEKEO NA KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU HUYO.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 29.07.2014 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA ILAMBO, KATA YA ITOPE, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI BAADA YA GARI T.604 BCS KUTAKA KUYAPITA MAGARI YALIOKUWA MBELE YAKE BILA KUCHUKUA TAHADHARI. DEREVA AMEKAMATWA.

 KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL .N. MASAKI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

Imetolewa na kusainiwa na:
[BARAKAEL .N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

TAMASHA LA USIKU WA MATUMAINI 2014 WABUNGE SIMBA NA YANGA FULL KUKANYAGANA UWANJA WA TAIFA

Makala na Nassor Gallu
SIKU ya Agosti 8, mwaka huu kutakuwa na bonge la mechi litakalopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar ambapo wabunge wanaoshabikia Yanga, watakuwa dimbani kupepetana na wenzao wa Simba.
Wabunge wa timu ya Simba wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Hebu jaribu kuvuta picha katika ubongo wako, waheshimiwa wabunge watakapoweka kando masuala ya ‘Ukawa’ na ‘Tanzania Kwanza’, kisha kukutana katika uwanja kuonyeshana umwamba kwa kusakata gozi la ng’ombe katika  mchezo huu wa kihistoria.
Kila timu tayari imeingia mafichoni kujiwinda na mchezo huo ili kuhakikisha inaibuka kidedea na kujenga heshima mbele ya watani wao huku Simba wakiahidi kulipiza kisago cha bao 1-0 walichokipata mwaka jana kutoka kwa Yanga.
“Tayari tumeingia kambini kujiwinda na mchezo huu ili kuziba midomo na kelele za Yanga ambao wamekuwa wakitamba tangu watubahatishe mwaka jana,” alijinasibu Hamis Kigwangala ambaye ndiye nahodha wa Simba.
Kwa upande wa mlezi wa Yanga ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abassi Mtemvu, alijigamba kuwa ni lazima waendeleze moto wa ushindi kwa kuwa wapo na kikosi imara na tayari wameshaingia kambini kwa kuwa mchezo huu ni siriazi kwao.
“Kwa kweli mchezo huu tumeuchukulia kwa mtazamo wa juu kabisa na lazima tuwapige kwa kuwa tuna damu changa nyingi, hatuna masihara, maana wakitufunga hatutakaa bungeni.
“Tupo katika maandalizi ya mwisho kwa sasa ingawa tulipoweka kambi yetu itabaki kuwa  siri,” alisema Mtemvu kwa kujiamini.
Baadhi ya wabunge wanaounda timu ya Yanga ni pamoja na Abassi Mtemvu, Ridhiwani Kikwete, Freeman Mbowe na  Mwigulu Nchemba, huku kikosi cha Simba kikiundwa na wakali kama Zitto Kabwe, Hamisi Kigwangalla, Wiliam Ngeleja, Juma Nkamia, Amos Makalla na Ismail Aden Rage.
Mbali na mchezo huo ambao utakuwa kivutio kikubwa kwa wadau wa soka, pia kutakuwa na mchezo mwingine wa kusisimua pale Bongo Fleva chini ya mkali wao, Peter Manyika itakapopepetana na Bongo Movie FC chini ya Jacob Steven JB.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Bongo Movie, Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’, tayari ameanika wachezaji wake huku akisema kuwa hahofii kwani kikosi chake kipo kamiligado kuelekea mchezo huo ambao wameuchukulia kwa umakini mkubwa.
“Sisi tumeuchukulia ‘serious’ sana mchezo huu kwa kuwa mashabiki wetu watakuja wengi na hatutakubali kuwaangusha.“Wachezaji waliopo kambini mpaka sasa ni Mzee Majuto, Kingwendu, Bambo, JB, Steve Nyerere, Dk Cheni, Ray, Mtitu, Cloud pamoja na Muhogo Mchungu,” alisema Bi Mwenda.
Wabunge wa timu ya Yanga wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Akijibu mapigo ya wapinzani wao, kocha wa Bongo Fleva ambaye pia anakinoa kikosi cha Yanga, Juma Pondamali ‘Mensah’, alisema Bongo Movie wajiandae kupata kipigo cha mshangao kwa kuwa wao hawatakwenda kuigiza uwanjani.
“Hawa waigizaji wajiandae na kipigo cha ‘sapraizi’, maana pale sisi hatuendi kuigiza, tunaenda kupiga kazi kwa kuwa mpira hauigizwi, unachezwa kila mmoja anaona, sasa acha wapige domo wataona kitakachowakuta,” alisema Pondamali.
Baadhi ya mastaa wanaounda kikosi cha Bongo Fleva ni pamoja na Peter Manyika, H-Baba, Ali Kiba, Rich One, Kalapina na wengineo.
Ukiachana na soka, pia kutakuwa na burudani mbalimbali ambapo mastaa kibao kutoka ndani na nje ya nchi watakuwepo kulipamba jukwaa la Usiku wa Matumaini.
Baadhi ya mastaa hao ni pamoja na Yemi Alade kutoka Nigeria, Madee, Ali Kiba, Roma Mkatoliki, Shilole, Menninah, Juma Nature na kundi zima la TMK Wanaume Halisi.
Mgeni rasmi katika tamasha hili atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal.Tamasha la Usiku wa Matumaini limedhaminiwa na Clouds FM (88.5),  Times Fm (100.5), Vodacom, Pepsi, Azam TV pamoja na Syscorp.

Credit Source: Fullshangwe

ROSE MUHANDO AIBIWA PINDO LA YESU

IMG_6464rose

Na Mwandishi Wetu

MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili, Rose Muhando amelalamika kuwa albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu Albamu anayotarajia kuizindua Jumapili wiki hii imeingizwa mtaani na wezi wa kazi za wasanii, hivyo kuonya wananchi wawe makini kwani albamu yake halisi itatoka Jumapili.
Taaifa kwa vyombo vya habari aliyoitoa Muhando jana, ilieleza kuwa albamu yake halisi bado haijaingia mtaani na kwamba hiyo wanayoiona wananchi sasa ni bandia na mtu atakayewauzia wamripoti polisi.
“Albamu ya Kamata Pindo la Yesu itaanza kuingia mtaani baada ya uzinduzi wangu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Jumapili wiki hii. Albamu yangu ina nembo ya TRA (Mamlaka ya Kodi ya Mapato nchini).
“Hizi CD zinazouzwa hivi sasa si zangu, hao ni matapeli na nawaomba wananchi tushirikiane kudhibiti wizi. Hao ni maharamia wa kazi za wasanii wanataka kunyonyajasho langu, naomba sana wananchi mnisaidie.
“Nasisitiza albamu yangu sijaiachia sokoni bado mpaka uzinduzi ukamilike, Watanzania wenzangu na mashabiki wangu kote duniani mnielewe na naomba tusaidiane katika hili maana CD feki zimezagaa,” alisema Muhando na kuongez akuwa tayari ameripoti taarifa hiyo kwa vyombo vya dola.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions inayoratibu uzinduzi huo, Alex msama naye katika taarifa hiyo ya pamoja alionya wote watakaobanika kuwa CD za albamu ya Rose Muhando watakumbana na mkono wa sheria.
“Inasikitisha sana kuona baadhi ya watu wanataka kutumia jasho la wengine kujinufaisha. Watanzania kuweni macho, msubiri albamu yenyewe ya Rose Muhando Jumapili pale ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam,” alisema Msama.
Albamu hiyo ya Muhando itakayozinduliwa Jumapili ina nyimbo za Bwana Niongoze, Wewe Waweza, Usiniache, Nibariki, Muongo, Kwema, Kamata Pindo la Yesu na Facebook.
Hivi sasa Rose anatamba na albamu yake ya Utamu wa Yesu, ambapo pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi), Jipange Sawasawa, Kitimutimu, Mungu Anacheka na Wololo.

Source Credit: Fullshangwe

ZITTO KABWE AELEZA MSIMAMO WAKE KUHUSU KATIBA MPYA

Jana tarehe 29 Julai, 2014 nimefanya mahojiano katika kipindi cha PowerBreakFast kinachorushwa na Clouds FM. Baadhi ya vyombo vya habari vimeandika mahojiano yale. Napenda nitoe ufafanuzi kidogo kuhusu msimamo wangu kuhusu mchakato wa Katiba.
Kwanza, Mimi sijawahi kuwa UKAWA wala kundi lolote lile katika Bunge Maalumu la Katiba isipokuwa kundi linalotaka maridhiano. Msimamo wangu kuhusu Muungano ni Serikali Tatu Zilizoboreshwa (S3z) ili kuwa na Muungano imara usio tegemezi wala egemezi kwa Washirika wake.

Pili, Mimi niliunga mkono ‘protest’ ya baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupinga lugha za matusi na lugha za kibaguzi zilizokuwa zinaendelea ndani ya mkutano ule. Vilevile niliunga mkono kwamba Rasimu inayopaswa kujadiliwa ni Rasimu iliyotokana na Tume ya Marekebisho ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Sinde Warioba. Nasisitiza umuhimu wa kupata Katiba BORA itakayoimarisha DOLA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tatu, kwa hali ya sasa kuna mkwamo katika kupatikana kwa Katiba Bora. Mkwamo unaotokana na kutokuwepo kwa nia ya dhati ya kupata maridhiano ya pande zinazopingana. UKAWA hawataki mazungumzo na Viongozi wa Bunge la Katiba badala ya kujenga maridhiano kila siku wanawabeza UKAWA jambo ambalo kamwe haliwezi kujenga mwafaka. Ushauri wangu ni kuahirisha mchakato mzima wa kuandika Katiba mpaka mwaka 2016 baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Katiba ya sasa ifanyiwe marekebisho machache kama ifuatavyo;
i) Tume ya Uchaguzi ili iwe huru na ionekane kuwa huru, ikiwemo kuwaondoa watumishi wa Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji katika kusimamia uchaguzi
ii) Kuruhusu mgombea binafsi
iii) Kuondoa Mafuta na Gesi kama Jambo la Muungano ili Zanzibar ianze mara moja kusimamia kwa uhuru utafutaji wa Mafuta katika vitalu vilivyopo upande huo wa Muungano
Mkutano wa Bunge Maalumu utakaofanyika bila kuwepo kwa maridhiano utakuwa hauna maana yeyote na itakuwa ni sawa na kupoteza muda na fedha za walipa kodi ambazo zingeweza kununua madawa vijijini. Mimi binafsi sitahudhuria mkutano wa Bunge Maalumu kama makundi hasimu hayatakuwa yamefikia maridhiano.
Kabwe Zitto, MB/MBMK

Credit Source: Wanabidii

OBAMA ATANGA VIKWAZO DHIDI YA URUSI

Rais Barack Obama wa Marekani ametangaza kupanua uwigo wa vikwazo dhidi ya Urusi kufuatia mgogoro unaoendelea Ukraines.Tangazo hilo la Rais Obama linafuatia vikwazo vilivyotangazwa na Jumuiya ya Ulaya saa chache kabla ya hili la Marekani.
Vikwazo hivyo vilivyotangazwa Marekani imesema itaiwekea vikwazo Urusi katika maeneo ya nishati,silaha na uchumi.
Hata hivyo Rais Obama amekanusha madai kwamba vikwazo hivyo vyaweza kuanzisha vita baridi dhidi ya Urusi, bali amesema kuwa wanalenga kuhakikisha Ukraine inarejea katika hali yake na kufuatia machafuko yanayoendelea hivi sasa.
BBC

MAJIBU YA MH LOWASA KUTOKANA NA KILICHOANDIKA NA GAZETI LA TANZANIA DAIMA


Kukanusha taarifa
Katika gazeti la Tanzania Daima toleo na.3536 la tarehe 30 Julai, kuna habari inayosema Lowassa aibukia ACT na kumuhusisha na Mbunge wa Kigoma Kaskazini(CHADEMA) Zitto Kabwe katika kile gazeti hilo kilichodai mikakati ya siri dhidi ya Chadema.
Habari hizo ni uzushi, na ni muendelezo wa mikakati ya kumchafua na kumgonganisha Mh Lowassa na wanasiasa wenzake wa kada na maeneo mbalimbali. Mh Lowassa kama walivyo wabunge wengine wa CCM amekuwa na uhusiano na wabunge wenzake bila kujali tofauti ya vyama vyao.
Mh Lowassa ni kiongozi makini ambaye hawezi kupoteza muda wake kujiingiza katika masuala yasiyo na tija kwa nchi, wananchi na ustawi wa demokrasia makini na endelevu nchini. Muda wake anautumia kusimamia utekelezwaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM jimboni kwake Monduli.
"Mimi na chama chetu, tuko busy kutekeleza ilani yetu,kuwaletea maendeleo wananchi ili wazidi kutupa ridhaa ya kuwaongoza katika chaguzi zijazo" alisema Mh Lowassa.
Hata hivyo, Mh Lowassa anathamini mchango wa vyama vyote vya siasa nchini pamoja na Chadema katika kujenga demokrasia yenye tija kwa taifa.

Imetolewa na ofisi ya Mh Edward Ngoyai Lowassa(mb)