Miss Singida 2014 Dorice Mollel akizungumza muda mfupi kabla ya kukabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 1.2 milioni kwenye wodi ya watoto njiti ya hospitali ya mkoa mjini Singida. Miss Singida huyo ambaye mwaka jana alikuwa pia mshindi wa kwanza Miss kanda ya kati na kushika nafasi ya tatu katika shindano la kumsaka Miss Tanzania, amesema ametoa msaada huo kwa sababu na yeye alizaliwa mapacha njiti.
Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Wednesday, 7 January 2015
Saturday, 3 January 2015
MSAMA: AKU! MI SIYO MENEJA WA ROSE MUHANDO
Na Mwandishi Wetu
HATIMAYE Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions ya
jijini Dar es Salaam, Alex Msama ameibuka na kutamka yeye si Meneja wa malkia
wa nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando akisema amekuwa akishirikiana naye
katika mazingira ya kawaida kama ilivyo kwa waimbaji wengine.
HUYU NDIYE MWANAMITINDO ANAYEFANANA NA NAOMI CAMPBELL
Modeli Lystra Adams
Modeli aliyechekwa kwa miaka mingi kwa kuwa mrefu kupitia kiasi sasa amekuwa kivutio cha wengi baada ya kufanana na modeli wa kimataifa Naomi Campbell.
KOCHA: RONALDO ATARUDI OLD TRAFFORD
Cristiano Ronaldo
Aliyekuwa msaidizi wa kocha wa Manchester united Mike Phelan anaamini kuwa Cristiano Ronaldo huenda akaandikisha mkataba wa kurudi katika kilabu ya Old Trafford katika siku sijazo.
MSICHANA ANUSURIKA KWENYE AJALI YA NDEGE
Mtoto mmoja wa miaka saba ametembea hadi katika nyumba moja katika jimbo la Kentucky nchini Marekani ili kuripoti kuanguka kwa ndege aliyoabiri.
MWANAFUNZI ATUPWA JELA KWA KUMTUKANA RAIS KENYATTA
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Mwanafunzi mmoja nchini Kenya amepewa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kumtukana rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika mtandao.
WAVULANA 40 WATEKWA NA BOKO HARAM
Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakr Shekau. Kundi hilo limedaiwa kuwateka vijana 40 katika kijiji cha Malari kaskazini mwa Nigeria
Takriban wavulana 40 na vijana wadogo wameripotiwa kutekwa nyara na wapiganaji wa kundi la Boko haram Kazkazini mashariki mwa Nigeria.
RAGE ATOA MISAADA WA SHS. 2.7 MILIONI KWA WAHANGA WA MVUA
Ismail Aden Rage
Na Hastin Liumba, Tabora
MBUNGE wa jimbo la Tabora
mjini Ismail Aden Rage ametoa msaada wa Shs milioni 2.7 kwa wahanga
27 waliobomokewa nyumba zao kata ya Tumbi kufuatia mvua kubwa
iliyonyesha wiki iliyopita.
MSHUKIWA WA MAUAJI KENYA NA TANZANIA AFARIKI
Abu Anas al-Liby
Mmoja wa watu waliopanga mashambulizi ya kigaidi kwenye balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998 ameaga dunia kabla ya kufikishwa kizimbani mjini New York.
MWANAMFALME AHUSISHWA NA UNYANYASAJI UINGEREZA
Mwanamfalme Andrew
Kasri ya Buckingham imepinga madai kwamba mmoja ya wana wa malkia Elizabeth mwanamfalme Andrew amekuwa alijihusisha katika tabia mbaya baada ya kubainika kwa nakala za mahakamani nchini Marekani zinazomuhusisha na madai ya unyanyasaji wa kijinsia.
WAZEE 4,612 WAUAWA KWA USHIRIKINA
mabaki ya nyumba ya mzee ambayo ilichomwa kutokana na imani za kishirikina. Picha na Maktaba
Na Herieth Makwetta, Mwananchi
Madai ya kuroga mvua, upigaji ramli, ugomvi ndani ya ndoa, tamaa ya kurithi mali, ardhi na ng’ombe ni miongoni mwa mambo yanayoelezwa kusababisha ongezeko la mauaji ya wazee vikongwe katika baadhi ya mikoa nchini.
ATANGAZA KUUZA FIGO KWA SHS90 MILIONI
Aprili mwaka jana, gazeti hili lilifanya uchunguzi na kubaini kuwa wapo Watanzania wanaouza figo zao kiholela kwa ajili ya kujipatia fedha. Picha na Maktaba
Na Florence Majani, Mwananchi
Mkazi wa Morogoro, Andrew Germanis Chimulimuli ametangaza kuingiza sokoni figo yake ambayo amesema anaiuza Sh90 milioni ili kukabiliana na ugumu wa maisha.
SALUM MWALIMU AMSIMAMISHA KAZI KIONGOZI CHADEMA
Naibu Katibu Mkuu Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu akihutubia mkutano wa hadhara mjini Nansio Wilaya ya Ukerewe, Mwanza lengo kushukuru wananchi kwa kukipatia ushindi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopita. Katika wilaya hiyo Chadema imepata viti 47 vya Serikali za Vijiji huku CCM ikipata 27 na CUF viwili. Picha na Jovither Kaijage
Na Jovither Kaijage, Mwananchi
Ukerewe. Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu amemsimamisha kazi mjumbe wa kamati ya utendaji ya chama hicho Wilaya ya Ukerewe, Wilbrod Machemli kwa kushindwa kutimiza wajibu wake, ikiwa ni pamoja na kutotangaza ujio wa kiongozi huyo.
PANYA ROAD WATINGISHA DAR, WAFANYA UPORAJI, WANANCHI WAKIMBIA OVYO
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova
Na Waandishi Wetu, Mwananchi
Dar es Salaam. Kwa mara nyingine tena, taharuki, hofu na wasiwasi mkubwa viliwakumba wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwa saa mbili baada ya kundi maarufu la waporaji la Panya Road, kuvamia mitaa mbalimbali na kupora mali.
KILIMANJARO FC YAITAMBIA HAI CITY
Na Fadhil Athumani, MoshiKOCHA wa Klabu ya Kilimanjaro FC ya mjini Moshi, Ally Chandika, amesema atahahakikisha timu yake inavuna pointi muhimu kutoka kwa vinara wa ligi daraja la Tatu, hatua ya sita bora, klabu ya Hai City ya wilayani Hai, katika mchezo wa kumalizia mzunguko wa kwanza, utakaopigwa kesho (Jumapili), kwenye uwanja wa Ushirika mjini Moshi.
Friday, 2 January 2015
SALAMU ZA DK. KIGWANGALLA KWA WATANZANIA KWA MWAKA MPYA 2015

Ni Mwaka Mpya Tena! Dr. Hamisi Kigwangalla, MB.
Ndugu Watanzania wenzangu,
Kwa heshima na taadhima na kwa moyo wa kiutumishi, najisikia furaha kuwatumia salamu za Mwaka mpya 2015. Kwa hakika Mungu amekuwa mwema sana kwangu na kwako mwaka 2014 kwa namna nyingi mbalimbali, ila kwa kiasi kikubwa kwa kutujalia zawadi ya uhai, mafanikio kwenye kazi zetu, uvumilivu tulipoanguka, nguvu tulipokutana na changamoto mbalimbali, na uwezo wa kupambana nazo tulipolazimika kufanya hivyo, na zaidi kwa kutusimamisha pamoja kwenye kamba ya mshikamano wa kitaifa kwa sisi sote kama Watanzania.
KWA TAARIFA YAKO: TANGA SCHOOL NDIYO SHULE YA KWANZA TANGANYIKA
Na Daniel Mbega
Tunazungumzia kuhusu maendeleo ya
elimu nchini – kupanda au kuporomoka. Hata hivyo, hatuna budi kujikumbusha tu
kwamba, elimu hii ilianzia wapi hasa.
Kwa kifupi, Wajerumani ndio walioanzisha
elimu rasmi nchini mwetu, na hii ilikuwa mwaka 1892 wakati walipojenga shule ya
kwanza kabisa, Tanga School, ambayo leo inaitwa Old Tanga High School. Jengo
kubwa la shule hiyo lilikarabatiwa na Tanga Heritage Centre kutokana na fedha
za msaada kutoka Serikali ya Ujerumani.
MAJUU HAMNAZO: MKULIMA AJENGA NYAMBIZI YAKE NA KUIWEKA MAJINI
Mkulima wa Kichina ametimiza ndoto yake ya miaka mingi ya kujijengea nyambizi inayofanya kazi.
Tan Yong, 44, kutoka mji wa Danjiangkou katika Jimbo la Hubei, daima alitamani kuona maisha yalivyo akiwa chini ya maji.
HAPPY BIRTHDAY: CUBA GOODING JR, LOIC REMY, TOMMY MORRISON
CUBA GOODING JR.
Mcheza sinema huyu aliyezaliwa Januari 2, 1968 jijini New York, leo
anatimiza miaka 47. Alitwaa Tuzo ya Academy kama Mwigizaji Bora
Mshirika (Best Supporting Actor) kwa ushiriki wake
kwenye filamu ya Jerry Maguire. Pia aliigiza kama Abraham Lincoln Haines katika
filamu ya mwaka 1992, Gladiator, na kama Meja Emanuel Stance kwenye filamu ya Red
Tails.
UNAZIKUMBUKA ENZI HIZI?!
Enzi za utotoni zina raha yake, mojawapo ikiwa ni kuwinda ndege, iwe kwa manati au ulimbo. Vijana hawa walionaswa na kamera ya BrotherDanny mjini Kibaya wakiwaandaa manati kwa ajili ya mwindo ya ndege.
VYAMA 10 VILISIVYO NA UWAKILISHI BUNGENI VYAWATAKA VIONGOZI WA DINI KUTOJIHUSISHA NA SIASA
Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kwa niaba ya vyama 10 visivyo na uwakilishi wa wabunge Bungeni wakati wakitoa tamko kuhusu viongozi wa dini kutojihusisha na masuala ya siasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu 2015 . Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Sauti ya Umma (Sau), Ali Kaniki na Katibu Mkuu wa Chama cha Wakulima Tanzania (AFP), Rashid Rai.
HIZI NDIZO SABABU ZA SARATANI!
Kifaa cha kubaini saratani
Utafiti mpya unasema aina nyingi za ugonjwa wa saratani ni matokeo ya bahati mbaya, kuliko malezo ya vinasaba, mazingira na mtindo wa maisha.
WAGONJWA WANYANYASWA KINGONO UINGEREZA
Mlipuko wa kisiri wa unyanyasaji wa kingono katika hospitali za Uingereza umegunduliwa huku takwimu mpya zikionyesha zaidi ya mashambulizi 1600 yaliripotiwa kwa polisi katika kipindi cha miaka mitatu iliopita.
BUSH MWINGINE AUTAKA URAIS MAREKANI
Jeb Bush ni mwana wa Rais George Bush na nduguye George W Bush waliokuwa marais wa Marekani
Aliyekuwa Gavana wa Florida kupitia tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani Jeb Bush ameripotiwa kujiuzulu kutoka nyadhfa zake zote za bodi akijiandaa kuwania urais mwaka ujao.
WATU 20 WAFARIKI HARUSINI AFGHANISTAN
Mmoja ya watoto waliojeruhiwa wakati bomu liliporushwa katika nyumba moja iliokuwa ikifanya sherehe ya harusi mkoani Helmand nchini Afghanistan.Takriban watu 20 waliaga dunia
Sherehe moja ya harusi nchini Afghanistan, imeshambuliwa kwa mzinga uliorushwa na roketi na kusababisha mauaji ya watu 20 na kuwajeruhi wengine zaidi ya kumi na mbili.
MSIKITI WASHAMBULIWA SWEDEN
Polisi nchini Sweden wanamtafuta mshukiwa mmoja katika kile ambacho wanamini kuwa shambulizi jengine kwenye msikiti likiwa ni la tatu wiki hii.
WATU 76,000 WAUAWA SYRIA 2014
Mwaka 2014 ulikuwa mwaka mbaya kuliko yote katika mgogoro wa Syria uliodumu kwa miaka minne, ambapo mwaka jana watu zaidi ya 76,000 waliuawa. Wanasema wanaharakati.
Thursday, 1 January 2015
COASTAL UNION YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA JKT RUVU
NA OSCAR ASENGA, TANGA
TIMU ya Coastal Union imeanza maandalizi kabambe ya kuhakikisha inajipanga vema ili kuhakikisha timu hiyo inapata pointi tatu muhimu kwenye mechi yake ya Ligi kuu dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa Jumamosi wiki hii kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani kutokana na umahiri wa kikosi cha timu hiyo.
SAMSON MWIGAMBA HAJATIMULIWA ACT - TANZANIA
Siku ya Jumatano tarehe 31 Desemba 2014 Mwenyekiti wa Muda wa Taifa wa ACT-Tanzania Ndugu Kadawi Lucas Limbu aliitisha mkutano wa waandishi wa habari. Katika mkutano huo, pamoja na mambo mengine, alitangaza kuwavua uanachama Katibu Mkuu wa Muda wa ACT Tanzania ndugu Samson Mwigamba pamoja na wanachama wengine kadhaa. Ndugu Limbu alieleza kwamba maamuzi aliyoyatangaza yalifanywa na Kikao cha Kamati Kuu ya ACT Tanzania ambacho alidai kilifanyika tarehe 30 Desemba 2014.
MBUNGE ATUHUMIWA KUGAWA ZAWADI KWA MBIO ZA MWAKANI
Catherine Magige
Mbunge wa Viti Maalum kupitia UVCCM Mkoa wa Arusha, Catherine Magige, amelalamikiwa kwa kuwagombanisha viongozi wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT)mkoa wa Arusha kutokana na kinachodaiwa ni mbio zake za ubunge kupitia jumuiya hiyo mwakani.
SHEIKH SHARRIF MIKIDADI MATONGO ATABIRI KIFO CHA KIONGOZI MKUBWA WA SERIKALI
Shekh Sharif Matongo, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ndoto aliyoota juu ya Tanzania mwaka 2015 jijini Dar es Salaam jana. PICHA: HALIMA KAMBI
Siku chache baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) kutangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu wa mwaka huu, Shekh Sharif Matongo ameibuka na kusema kuwa mmoja wa kiongozi mkubwa anayewania nafasi hiyo katika chama hicho atafariki dunia.
ACT YADAI KUWATIMU PROFESA KITILA, MWIGAMBA
Katibu Mkuu wa chama cha ACT, Samson Mwigamba
Na Muhibu Said, Dar es Salaam
Chama cha ACT-Tanzania kimedai kutengua uongozi na uanachama wa Katibu Mkuu, Samson Mwigamba na Mshauri wa chama hicho, Prof. Kitila Mkumbo, kwa madai ya kuanzisha chama ndani ya chama na kula njama za kutaka kukikabidhi kwa mafisadi.
Chama cha ACT-Tanzania kimedai kutengua uongozi na uanachama wa Katibu Mkuu, Samson Mwigamba na Mshauri wa chama hicho, Prof. Kitila Mkumbo, kwa madai ya kuanzisha chama ndani ya chama na kula njama za kutaka kukikabidhi kwa mafisadi.
MTUHUMIWA WA DAWA ZA KULEVYA WA SIERRA LEONE AUAWA NA ASKARI MAGEREZA KWEUPEEE
Na Thobias Mwanakatwe, Dar es Salaam
Mtuhumiwa wa kesi ya dawa za kulevya, raia wa Sierra Leone (33), Abdul Koroma, amepigwa risasi na kufa baada ya kujaribu kutoroka akiwa chini ya ulinzi wa askari wa Jeshi la Magereza, jijini Dar es Salaam.
Mtuhumiwa wa kesi ya dawa za kulevya, raia wa Sierra Leone (33), Abdul Koroma, amepigwa risasi na kufa baada ya kujaribu kutoroka akiwa chini ya ulinzi wa askari wa Jeshi la Magereza, jijini Dar es Salaam.
CCM KUTUMIA PANGA LA MWAKA 2005
Dar es Salaam. Vigezo 13 vilivyowekwa na CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2005 kumpima mwanachama anayefaa kugombea urais, ndivyo vitakavyotumika kuwaengua makada wanaoendelea kujitokeza kuwania nafasi hiyo mwakani, imefahamika.
ZITTO KABWE AAHIDI KUMUUNGA MKONO MBOWE
HAKI SAWA: Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Zitto Kabwe wakiwasili kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara jana, ambako walihutubia mkutano wa hadhara. Picha na Ibrahimu Yamola
Mtwara. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe amesema atamuunga mkono Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman Mbowe pale atakapowasilisha hoja yake bungeni kuhusu ufisadi wa zaidi ya Sh1 trilioni katika mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.
MWAKA WA UCHAGUZI, RAIS KIKWETE ATOA SALAMU ZA MWISHO WA MWAKA 2014
Rais Jakaya Kikwete
Na Fidelis Butahe na Goodluck Eliona, Mwananchi
KWA UFUPI
- Daftari la Kudumu: Tume ya Taifa ya Uchaguzi mwezi huu itaanza kuandikisha wapigakura kwa kutumia mfumo wa utambuzi wa alama za mwili (BVR) ambao hata hivyo katika majaribio umezua malalamiko.
- Kuvunja Bunge: Bunge la 10 litatimiza muda wake wa miaka mitano katika mkutano wake wa 20 utakaomalizika kwa Bunge hilo kuvunjwa mwezi Julai.
HAPPY BIRTHDAY: MZEE WA MCHINGA, JACK WILSHERE NA COLIN MORGAN
MUDHIHIR MOHAMMED
MUDHIHIR

Mbunge wa zamani wa
Mchinga. Elimu ya msingi aliipata katika shule za Mchinga (1958 hadi 1959),
Msinjahili (1959 hadi 1961) na Mangamba Middle School (1962 hadi 1965) kabla ya
kujiunga na shule ya sekondari Lindi (1966 hadi 1969). Baadaye akajiunga na
Chuo cha Ualimu Marangu kwa mafunzo ya Cheti cha Ualimu Daraja A (1973 hadi
1974). Kati ya mwaka 1981 na 1982 alisoma kidato cha tano na sita katika shule
ya Kujitegemea (Private School). Mwaka 1988 na 1989 alihitimu Cheti cha Sheria
katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mwaka 2000 alijiunga na masomo ya shahada
ya kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Washington, Marekani lakini hakumaliza.
NGUNA YA WANAUME HII! UPOOOO!
Kweli kazi na Dawa! Hawa ni wavuvi katika Bwawa la Mtera ambao wanapika ugali, wapate nguvu kabla ya kurejea tena majini kutafuta samaki wa kitoweo na biashara.
MATAMU EEEH!...
Kamera ya BrotherDanny iliwanasa wanafunzi hawa wa Shule ya Msingi Kapunga wilayani Mbarali katika Mkoa wa Mbeya wakigugumia maji bombani wakati wa mapumziko.
IRINGA WANAKULA HATA PUNDA!
Jamani hala hala mti na macho! Nyie mlio waroho wa nyamahasa muwapo safarini. Siyo kila nyama choma ni ya ng'ombe au mbuzi, mnapaswa kuwa makini. Tazama huyu bwana aliyeuficha uso wake ambaye ni mkazi wa Izazi wilayani Iringa anachokifanya.
MAJUU HAMNAZO: MWANAMKE MWENYE ASHKI MAJINUNI ALALA NA WANAUME 140 NA KUWEKA ORODHA YA VIWANGO
Sandy Nardo, 53, kutoka Dublin, Scotland anawapima wanaume waliooa, mapenzi ya mtungo na hata mumewe wa zamani kwa viwango vya mapenzi tangu alipopoteza bikira yake akiwa na miaka 19 kwa mwanamuziki wa Kitaliano.
RAIS WA GAMBIA ARUDI NYUMBANI
Rais wa Gambia Yahya Jammeh
Ripoti kutoka Gambia zinasema kuwa rais Yahya Jammeh amerudi nchini humo kutoka ziara ya ughaibuni kufuatia njama ya kutaka kumpindua.
WAKAZI WA KANO WAPOKEA MWAKA MPYA KWA MARA YA KWANZA
Mwaka mpya 2015 ulivyopokelewa Hong Kong
Mwaka mpya wa 2015 umepokewa kwa kishindo katika maeneo mbali mbali duniani na barani Afrika.
PAPA AKEMEA UFISADI ROMA
Papa Francis
Papa Francis ametumia sherehe za kuupokea mwaka wa 2015 kuzungumzia tatizo la rushwa katika mji wa nyumbani wa Rome nchini Italia.
WATU 35 WAFARIKI CHINA MKESHA WA MWAKA MPYA
Umati wa watu waliokanyagana na wengine kufa nchini China wakati wakiupokea mwaka mpya 2015
Sherehe za kuupokea mwaka mpya 2015 zimeguka kuwa majonzi baada ya watu thelathini na watano kufa kwenye taharuki ya kukanyagana kwenye msongamano wakati wakiiupokea mwaka mpya.
HAKYANANI, MVUA ZA MWAKA HUU BALAA!
Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt Agnes Kijazi akiongea na vyombo vya habari kuhusiana na mwelekeo wa utabiri wa hali ya hewa kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Februari 2015.
Subscribe to:
Posts (Atom)








