Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha
na Elimu na Sayansi (UNESCO) litaungana na wasanii mbalimbali nchini na wadau
wa Sanaa kuadhimisha siku ya muziki wa Jazz duniani ambayo kwa mara ya kwanza
itaadhimishwa nchini Mei 2, 2016.
Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Saturday, 30 April 2016
KONGAMANO YA DICOTA 2016 DALLAS, TEXAS LAENDELEA TENA IJUMAA
Bwn. Lunda Asumani akitoa maelekezo kwa wadau mbalimbali waliokuja kuongea kwenye kongamano la DICOTA 2016 linalofanyika Dalas, Texas nchini Mrekani. Picha na Vijimambo/Kwanza production.
KUSANYIKO LA KUMUENZI MAREHEMU ANDREW NICKY SANGA KUFANYIKA LEO 30.04.2016, TRIPLE 7 KAWE
Ndugu
zetu pamoja na Marafiki zetu, wakati huu tukiendelea kuomboleza msiba
wa mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga, tunapenda kutoa shukrani za dhati
kwa ushiriki wenu wa hali na mali katika kuandaa safari yake ya mwisho.
Katika kumuenzi na kukumbuka urafiki wake wa kipekee, Kamati ya Maandalizi ya Dar es Salaam inawaalika na kuwakaribisha katika kusanyiko la kumuenzi jioni ya tarehe 30 April 2016 kuanzia saa 11 jioni pale Triple 7 (@777). Kusanyiko hili ni mahsusi kwa mambo mawili makubwa, moja likiwa ni kukumbuka na kuenzi maisha yake katikati yetu na pili kupashana habari za kuhitimisha maandalizi ya Safari ya kumuweka katika nyumba yake ya Milele.
Naomba tujumuike wote na tunaamini hata huko aliko atafurahi tunapomkumbuka.
Bwana ametoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe
Imetolewa na Dr. George Longopa
KNY Kamati ya Maandalizi ya Dar ES SALAAM
Simu 0754 870969
Katika kumuenzi na kukumbuka urafiki wake wa kipekee, Kamati ya Maandalizi ya Dar es Salaam inawaalika na kuwakaribisha katika kusanyiko la kumuenzi jioni ya tarehe 30 April 2016 kuanzia saa 11 jioni pale Triple 7 (@777). Kusanyiko hili ni mahsusi kwa mambo mawili makubwa, moja likiwa ni kukumbuka na kuenzi maisha yake katikati yetu na pili kupashana habari za kuhitimisha maandalizi ya Safari ya kumuweka katika nyumba yake ya Milele.
Naomba tujumuike wote na tunaamini hata huko aliko atafurahi tunapomkumbuka.
Bwana ametoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe
Imetolewa na Dr. George Longopa
KNY Kamati ya Maandalizi ya Dar ES SALAAM
Simu 0754 870969
Ikiwa unataka tengenezewa Blog, Tukiko lolote la Harusi,Msiba, Mahafali, Tamasha, Matangazo auHabari yoyote usisite kututumia kupitia whatsapp 0765056399 au Barua Pepe fredynjeje@live.com. Follow me instagram @fredynjejeblog Twitter @Fredynjeje
BOHARI YA DAWA YAFAFANUA KUHUSU DAWA NA VIFAA TIBA KUSAFIRISHWA KWA MIAKA MINNE
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu akionesha moja ya nyaraka inayoonesha upelekaji wa dawa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, wakati akitoa ufafanuzi kuhusu dawa za shilingi bilioni mbili kuwa njiani kutoka MSD Keko kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu mwaka 2012.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Victoria Elangwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Sako Mwakalobo.
Ofisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka (kulia), akizungumza katika mkutano huo wakati akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa MSD (kushoto), kuzungumza na wanahabari.Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda, Terry Edward.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea
Na Dotto Mwaibale
BOHARI ya Dawa (MSD) imetoa ufafanuzi kuhusu dawa za sh.bilioni mbili kuwa njiani kutoka Bohari ya Dawa ya Keko kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu mwaka 2012.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema hakuna dawa ambazo ziko njiani tangu mwaka 2012 kutoka Bohari ya Dawa kwenda Muhimbili kama ilivyodaiwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bungeni.
Bwanakunu alisema kuwa ripoti ya CAG ilionesha dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya sh.bilioni 2.03 havikuwa vimefika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu Mei 2012 licha ya kuonekana kwenye ankara 23 na Bohari ya Dawa.
"Tunapenda kutoa ufafanuzi kuwa ankara hizo sio kwamba dawa hazikufika hospitalini hapo, bali hazikuonekana kwenye vitabu vya kupokelea mali vya Hospitali ya Muhimbili" alisema Bwanakunu.
Alisema kwamba baada ya kupitia nyaraka zake, Bohari ya Dawa mpaka sasa imefanikiwa kupata uthibitisho wa hati za kupelekea mali za dawa na vifaa tiba vyote vilivyopokelewa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambavyo ni pamoja na dawa za figo na moyo ambazo zilikwishapelekwa Muhimbili.
Aliongeza kuwa pamoja na juhudi za MSD imewasiliana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili kuainisha taarifa za kwenye ankara na shehena ya dawa na vifaa tiba vilivyopelekwa hospitalini hapo kwani utaratibu wa kupeleka na kukabidhi dawa hospitalini unamlazimu mpokeaji kusaini ankara ya kupeleka mali ambazo zote zipo MSD.
Akitolea ufafanuzi kuhusu picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii za gari aina ya lori lenye herufi "MSD" na kutoa maelezo kuwa ni gari la MSD amesema nembo inayoonekana kwenye gari hilo siyo ya Bohari ya Dawa.
Katika ripoti ya CAG ilionesha kwamba madawa na vifaa tiba ambavyo havikupokelewa kwa muda mrefu kutoka MSD vilikuwa vyenye thamani ya sh.bilioni 2.03 ambapo katika hali ya haikutajiwa kuchukua zaidi ya wiki moja kufikishwa sehemu husika ukizingatia ofisi zao ziko Dar es Salaam.
TANAPA YAKABIDHI MABATI 2800 WILAYANI SERENGETI
Mbunge wa Jimbo la Serengeti Mhe. Marwa Ryoba (kushoto) akipokea msaada wa mabati kutoka kwa Meneja Ujirani Mwema wa TANAPA Bw. Ahmed Mbugi (Kulia) wilayani Serengeti.
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
29.04.2016, Dar es Salaam
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limekabidhi jumla ya mabati 2800 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara kusaidia ujenzi wa maabara 15 za shule za sekondari na zahanati zilizo katika Kata mbalimbali za wilaya hiyo.
WANANCHI JIJINI MBEYA WAJITOKEZA KUPATIWA DAWA ZA KINGA TIBA KWA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE
TIGO YATOA VISIMA 12 VYA MAJI KATIKA VIJIJI 12 SINGIDA
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge (katikati)akikata utepe katika makabidhiano ya visima 12 vyenye thamani ya millioni 174 kutoka Kampuni ya Tigo akiwa na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata(kulia),na kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe, katika kijiji cha Mtinko, mkoa wa Singida juzi.
JAJI MKUU MOHAMED CHANDE OHMAN KUWA MGENI RASMI KATIKA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI
Mwenyekiti wa MISATAN, Simon Berege akizungumza na waandisshi wa habari kuhusu SIku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari. Kushoto ni Afisa Mafunzo wa TMF, Raziah Mawanga na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri na Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile.(Picha na Modewjiblog)
Siku za Uhuru wa Vyombo vya Habari ambayo hufanyika Mei 3 ya kila mwaka inataraji kufanyika jijini Mwanza kwa mwaka huu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman na kuhudhuliwa na viongozi wengine nchini na wengine kutoka nje ya nchini ambapo kwa mwaka huu kaulimbiu ni KUPATA TAARIFA NI HAKI YAKO YA MSINGI.
WATU WATATU WANAOSADIKIWA KUWA MAJAMBAZI WAUAWA MKOANI MBEYA
TIGO, MGAHAWA WA SAMAKI SAMAKI WAINGIA UBIA
MKUU WA WILAYA YA MOSHI, NOVATUS MAKUNGA AAJIONEA ATHARI YA MAFURIKO
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza jambo na wataalamu alioongozana nao katika uwanja mdogo wa ndege wa Moshi kwa ajili ya kuruka na ndege ndo ya Shirika la Hifadhi za taifa (TANAPA) kwa ajili ya kujionea hali ya mafuriko.
WANAFUNZI INTERNATIONAL SCHOOL OF TANGANYIKA WATEMBELEA UN TANZANIA
Mmoja wa wafanyakazi wa UN Tanzania (aliyesimama), akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika-IST) kuelezwa namna ofisi hiyo inavyo pambana kutetea haki mbalimbali za msingi kwa watoto popote duniani. Wanafunzi hao walitembelea ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kujifunza mambo anuai.
MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ,SAID MECKY SADICK AFANYA ZIARA YA UTAMBURISHO WILAYA YA HAI.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadickyakitia saini katika kitabu cha wageni alipotembelea ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Hai.
Tuesday, 26 April 2016
SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA WANAHABARI NCHINI
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akichangia Hotuba ya
Ofisi ya Waziri Mkuu 25/04/2016 jioni bungeni mjini Dodoma na kusisitiza kuwa
Serikali inaendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na wanahabari nchini.
JESHI LA POLISI KILIMANJARO LANASA BHANGI MISOKOTO 4500, BASTOLA NA ZANA NYINGINE ZA KUFANYA UHARIFU.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi, Wilbroad Mutafungwa akionyesha misokoto ya Bhangi iliyokamatwa baada ya wahusika kufanikiwa kuwakimbia askari Polisi.
POSSI: SERIKALI KUBORESHA MAKAZI YA WATU WENYE ULEMAVU NA WENYE MAHITAJI MAALUM.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe Dkt.
Abdallah Possi akiwasilisha hoja za masuala ya Watu wenye
Ulemavu wakati wa Mkutano wa Bunge wa kujadili Bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha
2016/17 kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,
Vijana na Ajira) Mhe. Antony Mavunde tarehe 25 Aprili, 2016.
CAG AKABIDHI RIPOTI
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG), Profesa Juma Assad akionesha ripoti ya ukaguzi ya mwaka wa
fedha unaoishia Juni 30, 2015 kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo
mjini Dodoma ili iweze kujadiliwa na wabunge katika Bunge la bajeti ya mwaka
2016/2017.
PSPF YAWAELIMISHA WAJASIRIAMALI KUHUSU UCHANGIAJI WA HIARI
Mtangazaji wa kipindi cha wanawake
live kulia Bi. Joyce Kiria akionyesha kitambilisho chake cha uchangiaji wa hiari kutoka kwa
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa
mfuko wa PSPF Bi. Mwanjaa Sembe kushoto wakati wa mafunzo kwa
wajasiriamali yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
YANGA KUCHAGUANA JUNI 05, 2016
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) jana imetangaza Juni 05, 2016 kuwa siku ya Uchaguzi Mkuu wa viongozi ndani ya klabu ya Young Africans SC ya jijini Dar es salaam.
STARS KUJIPIMA NA HARAMBEE STARS MEI 29
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na timu ya Taifa Kenya (Harambee Stars) Mei 29, 2016 jijini Nairobi.
WANANCHI WA KIGOGO WANUFAIKA NA UPIMAJI BURE WA AFYA KUTOKA FAZEL FOUNDATION NA TAHMEF
Mwanzilishi wa Taasisi ya Fazel, Dkt. Sajjad Fazel akisalimiana na Diwani wa Kigogo, Bw. Manyama wakati wa funguzi wa huduma ya upimaji wa afya bure kwa wakazi wa Kigogo. Katikati ni Imam wa Msikiti wa Al Ghadir, Sheikh Jalala.(Picha na habari na Modewjiblog)
Kwa kuhakikisha jamii inakuwa katika hali ya usalama wa kiafya, Taasii ya Fazel Foundation kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya Afya na Madawa (TAHMEF) wametoa huduma ya upimaji wa magonjwa mbalimbali kwa wananchi wa Kigogo, Dar es Salaam.
MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA AZUNGUMZA NA WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA WERUWERU.
Wahitimu wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Wasichana ya Weruweru wakiimba wakati wakielekea ukumbini kwa ajili ya kuanza rasmi kwa sherehe ya kuwaaga.
WAZEE WASIOJIWEZA KITUO CHA BUKUMBI MWANZA WAIOMBA SERIKALI KUIMALISHA HUDUMA ZA AFYA KITUONI KWAO
Wauguzi wa zahanati ya kituo cha ustawi wa Jamii cha Bukumbi kijiji cha Kigongo kata ya Idetemya wilayani Misungwi mkoani Mwanza wakiwaongoza waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliofika kuwatembelea wazee wanaoishi katika kituo hicho kujua jinsi wanavyoishi na kuwa kutambua suala la uzazi wa mpango. Ziara hiyo ya waandishi wa habari iliyofanyika wiki iliyopita iliratibiwa na taasisi inayojishuhulisha na ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango (TCDAA) wakishirikiana na Marie Stopes Tanzania. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
WAZIRI UMMY MWALIMU AADHIMISHA SIKU YA MALARIA DUNIANI KWA KUPIMA MALARIA KWA KUTUMIA mRDT
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiwaonesha waandishi wa habari kipimo cha haraka cha kupima malaria(mRDT) wakati akitoa tamko la maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani leo kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha udhibiti wa Mbu waenezao Malaria Charles Dismas kutoka mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria.
PAULINA MGENI: NAHITAJI MENEJA WA KUSIMAMIA KAZI ZANGU ZA UREMBO
Paulina Mgeni ndio Miss Utalii Mkoa wa Iringa mwaka 2013 mpaka sasa kabla mashindano hayo hayaja simamishwa; ila kwasasa anafanya kazi za mitindo akiwa kama Mwanamitindo (Model), lakini anahitaji meneja wa kusimamia kazi zake hizo za Urembo (Modeling).
MAKAMBA: HOJA ZA MUUNGANO NA HATUA ZA UTATUZI
Waziri January Makamba
TAARIFA YA WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA) KUHUSU UTATUZI WA CHANGAMOTO ZA MUUNGANO
HOJA ZA MUUNGANO NA HATUA ZA UTATUZI
1. UTANGULIZI
Katika kuhakikisha kuwa changamoto za Muungano zinatatuliwa, Serikali ilianzisha Kamati ya Pamoja ya SMT na SMZ chini ya uwenyekiti wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Maagizo hayo yalitolewa na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2006 na kuwataka Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi kukutana na kujadili namna ya kutatua changamoto zinazoukabili Muungano wetu. Katika kipindi hicho Ofisi ya Makamu wa Rais iliratibu vikao viwili (2) kati ya Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, tarehe 22 Mei, 2006, Dar es Salaam na tarehe 21 Novemba, 2006, Zanzibar.
Hata hivyo, mwezi Februari 2008, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alifanya marekebisho ya kiutendaji serikalini ambapo Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kushughulikia masuala ya Muungano iliwekwa chini ya Uongozi na Uenyekiti wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa kuzingatia utaratibu huo, kikao cha kwanza chini ya Uenyekiti wa Makamu wa Rais kilifanyika tarehe 15 Mei 2008 Dar es Salaam, na vilivyofuata vilikuwa ni: tarehe 11Oktoba, 2008, Zanzibar; tarehe 19 Mei, 2009, Dar es Salaam; tarehe 2 Juni, 2010, Zanzibar; tarehe 28Januari, 2012, Dar es Salaam; tarehe 13 Januari, 2013, Zanzibar na tarehe 23 Juni, 2013, Dodoma.
Monday, 25 April 2016
TANAPA YAZINDUA KAMPENI KILIMANJARO YENYE KAULIMBIU “ WEKA MLIMA SAFI, TUNZA MAZINGIRA YAKUTUNZE”
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Mecky
Sadiki akiongea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro
iliyokuwa na kaulimbiu “ Weka Mlima Safi, Tunza Mazingira Yakutunze”
katika lango la Marangu mwishoni mwa wiki. Wengine pichani ni Mkurugenzi
Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi (kati) na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya
Kilimanjaro Betrita Loibooki.
BENKI YA CRDB YATANGAZA AJIRA KWA KIDATO CHA SITA JITEGEMEE JKT SHULE YA SEKONDARIBENKI
Meneja wa Huduma Mbadala wa Benki ya CRDB, Joseph Wite (katikati), akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT, Brigedia Jenerali mstaafu Lawrence Magere (kushoto), hundi yenye thamani ya sh.milioni 2.5 kwa ajili ya kusaidia kujenga mifumo ya maji shuleni hapo katika Mahafali ya 22 ya kidato cha sita yaliyofanyika Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy.
CHAMA CHA UDP CHAPATA PIGO VIGOGO WAKE WAWILI WAKIMBILIA CCK
Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati akiwapokea waliokuwa viongozi wa Chama cha UDP, waliokihama chama ambao ni Salum Makunganya aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara na Mkurugenzi wa Uchaguzi Taifa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu na Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam na aliyekuwa Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya chama hicho , Joachim Mwakitiga waliotangaza kujiondoa katika chama hicho na kujiunga CCK jijini Dar es Salaam leo asubuhi mbele ya waandishi wa habari.
UK DIASPORA CONFERENCE 2016
Dear all,
Please come and join us at The Tanzania Diaspora Conference and the Tanzania Diaspora achievement awards UK 2016
WHERE: Coventry University School of Engineering
TIME: 11AM-8PM
DATE:30TH APRIL 2016
For more information please contact +447960811614
You are allwelcome
Sunday, 24 April 2016
WAZIRI MUHONGO ATUA JIJINI DAR JIONI HII AKITOKEA NCHINI UGANDA KUKAMILISHA DILI LA BOMBA LA MAFUTA
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kati) akiwasili jijini Dar es salaam jioni hii, akitokea Jijini Kampala alikoenda kukamilisha dili la bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga, alioongozana nao ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Juliana Pallangyo.
Saturday, 23 April 2016
WIZARA YA UJENZI ,UCHUKUZI NA MAWASILIANO YAENDELEA NA MCHAKATO WA UKUSANYAJI MAONI JUU YA UBORESHAJI SERA YA TAIFA YA (TEHAMA) MKOANI MBEYA
DENMARK YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MUZIKI KWA TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBA)
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari ,Utamaduni, Sanaa,na Michezo Leah Kihimbi akizindua mradi wa vyombo vya muziki kati ya Taasisi ya
Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) na
Kituo cha Utamaduni na Maendeleo cha Watu wa Denmark (CKU), uzinduzi huo ulifanyika
katika Chuo cha Sanaa mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
MHANDISI MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM NA WASAIDIZI WAKE WATUMBULIWA MAJIPU
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akizungumza na wanahabari kuhusu kumvua madaraka Mhandisi wa Manispaa hiyo kwa kufanyakazi chini ya kiwango pamoja na wasaidiziwake wawili.
MATOKEO UTAFITI WATU WENYE UWEZO WA KUFANYA KAZI KUTUMIKA KUFANYA MABORESHO YA SERA ZA KUKUZA UCHUMI NA KUPUNGUZA UMASIKINI
Kaimu
Meneja wa Idara ya Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
Bi. Ruth Minja akitoa ufafanuzi kwa wahariri wa vyombo vya Habari kuhusu matokeo
ya Utafiti wa Watu wenye uwezo wa kufanya Kazi leo jijini Dar es salaam.
Matokeo hayo yataiwezesha Serikali kuangalia upya tija ya utendaji kazi katika
shughuli zinazofanywa na makundi mbalimbali ili kubaini mchango wake katika
kukuza Pato la Taifa.
TIGO WAKABIDHI MADAWATI 400 KWA WILAYA YA MWANGA KATIKA SHULE 8
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Meck Sadiki akikabidhi madawati 400 yenye thamani ya shilingi milioni 66 kwa mwenyekiti wa halmashauri ya Mwanga Theresia Msuya yaliotolewa na Kampuni ya Tigo, Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata. |
CHAIRMAN OF UBA GROUP PLC, TONY ELUMELU HONOURED WITH LIFETIME ACHIEVEMENT AWARD IN ABIDJAN
At the 5th edition of the annual forum, CGECI Academy 2016, the Ivorian National Council of Employers, General Confederation of Enterprises of Côte d'Ivoire (CGECI) presented African businessman and investor, Tony Elumelu, with its 2016 CGECI Lifetime Achievement Award on April 21, 2016 in Abidjan, Côte d’Ivoire. The formal presentation was to honour Mr. Elumelu on his leadership and key role as an African business champion. The event was attended by over three thousand delegates across Africa including top government officials, business leaders, established and aspiring entrepreneurs.
TIGO YATANGAZA VIDEO ZA YOU TUBE KUPATIKANA BURE USIKU KWA WATU WOTE
Mkuu wa Kitengo cha Vifaa vya Mawasiliano wa Tigo, David Zacharia (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam kuhusu huduma iliyoanzishwa na kampuni hiyo ya kutiririsha video za YouTube bure ambayo itakuwa inapatikana kwa wateja wote wa Tigo kuanzia saa 6.00 usiku hadi saa 12.00 alfajiri. Kulia ni Meneja Mawailiano wa Tigo, John Wanyancha.
SERENGETI BOYS KUFUNGUA DIMBA NA MAREKANI MICHUANO YA VIJANA INDIA
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini India (AIFF) limetoa ratiba ya michuano ya vijana (AIFF Youth Cup 2016 U-16) itakayoanza kutimua vumbi Mei 15 -25 katika mji wa Goa nchini India kwa Serengeti Boys kufungua dimba na Marekani.
Michuano ya AIFF inashirikisha timu tano za vijana wenye umri chini ya miaka 17 kutoka nchi za Korea Kusini, Marekani, Malysia, Tanzania na wenyeji India.
WAZIRI UMMY MWALIMU AWASIMAMISHA WATENDAJI WA NHIF KWA UBADHIRIFU WA FEDHA
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (pichani) amewasimamisha kazi kupisha uchunguzi kwa watendaji Wakuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa ubadhirifu wa fedha za mfuko huo kwa Mkoa wa Mara.
MKUU WA WILAYA YA TEMEKE, SOPHIA MJEMA AZINDUA MICHUANO YA UMISETA UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema ambaye alikuwa mgeni rasmi wa uzinduzi wa Michuano ya Shule za Sekondari Nchini (UMESETA), akipiga dana dana wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Subscribe to:
Posts (Atom)