Msanii wa Reggae Princes Delyla
akiongea na wadau wa Sanaa kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA) mapema wiki hii kwenye makao makuu ya Baraza hilo Ilala Sharif Shamba
jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Msanii Mwasiti Almas na Afisa Sanaa kutoka
BASATA Augustino Makame.
Msanii wa kizazi kipya
Mwasiti Almas akisisitiza jambo wakati akiongea na wadau wa Sanaa kwenye
programu ya Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linalofanyika
makao makuu ya Baraza hilo Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Kushoto
kwake ni Msanii wa reggare Princes Dalyla na Afisa Sanaa kutoka BASATA
Augustino Makame.
Mtafiti na Msanii wa Reggae
Innoncent Nganyagwa akifafanua jambo kwenye Jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa
la Taifa (BASATA) mapema wiki hii. Kulia kwake ni Msanii mwenzake wa Reggae
Princes Delyla.
Msanii Mwasiti akisakata
muziki sambamba na mashabiki wake kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA.
Msanii Princes Dalyla
akitoa burudani kwa wadau wa Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii.
Sehemu wa wadau wa Sanaa waliohudhuria Jukwaa la Sanaa
wiki hii wakifuatilia kwa makini burudani.
Msanii mahiri wa muziki wa
kizazi kipya Mwasiti Almas amewataka wasanii wenzake kuwa wabunifu katika
kutanua mianya ya kujiingizia kipato na kuhakikisha wanazingatia maadili wawapo
jukwaani ili kulinda hadhi zao.
Mwasiti ameyasema hayo
mapema wiki hii wakati akijibu maswali ya wadau wa Jukwaa la Sanaa
linalofanyika kwa mwezi mara mbili ziku za Jumatatu makao ya Baraza la Sanaa la
Taifa (BASATA) Ilala Sharif Shamba.
Wadau hao wa Sanaa walitaka
kujua ni kwa nini wasanii wengi hufilisika mara wanaposimama kufanya shughuli
za Sanaa na wengine wamekosa ubunifu wawapo kwenye maonesho au wanapozalisha
kazi zao hali ambayo inawafanya watumie sehemu za siri za miili yao katika
kutafuta mvuto kwa mashabiki.
“Wasanii wengi
wanang’ang’ania kwenye sanaa pekee. Hawawekezi kwenye miradi mingine. Kuwa na
umaarufu si kuwa na fedha bali umaarufu ni njia tu inayokusaidia kuingia kwenye
sekta na miradi mbalimbali kwa ajili ya kujiimarisha kimapato” alisema Mwasiti
wakati akifafanua suala la wasanii kufilisika mara wanapochuja kwenye Sanaa.
Alizidi kueleza kwamba
wasanii waliopo sasa hawana budi kutambua kwamba hawatakuwepo muda wote bali
kuna leo na kesho hivyo lazima kuiandaa kesho sasa.
“Umri wa wasanii unaenda,
waliopo sasa hawawezi kuwepo kesho kwani kuna wasanii wengi wanaibuka na lazima
wapate nafasi. Ni muhimu sana kwa wasanii kuliona hili. Huko nyuma kaka na dada
zetu walipata shida ilikuwa ngumu lakini kwa sasa wasanii tunapata kipato na baadhi
wanajitahidi kuwekeza” alisema Mwasiti.
Kuhusu wasanii kufanya
maonesho yasiyo na maadili, Mwasiti alisema kwamba inasikitisha sana kwani
katika hali ya kawaida msanii anayejitambua na kuthamini utu na hadhi yake
hawezi akafanya maonesho ya uchi kwani matendo ya wasanii huathiri sana jamii
inayowazunguka.
“Matendo yetu wasanii
huathiri sana jamii inayotuzunguka. Sisi ni binadamu na tuna leo na kesho.
Sipendi siku zijazo watoto wetu waje kuuliza na kushangaa yale tuyafanyayo sasa
maana yataendelea kuonekana” alisema Mwasiti.
Katika Jukwaa hilo BASATA
lilimwalika Mwasiti na wa msanii mwenzake wa kike Princes Dalyna anayefanya
muziki wa reggae ili kueleza historia, changamoto na mafanikio waliyoyapata
katika kazi zao za Sanaa.
No comments:
Post a Comment