Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 30 September 2015

MAGUFULI AAHIDI KUKOMESHA MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI NCHINI


  Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa watu kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo, akiendelea na kampeni zake za kuisaka Ikulu nchini Kote huku akiwaomba Watanzania kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ili aweze kuwatumikia kwa uaminifu mkubwa.PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA

FRIENDS PUB YA SEGEREA NA CHECKPOINT CHANIKA BAA ZA WIKI TUSKER FANYAKWELI KIWANJANI

Mkazi wa Chanika Kay Christopher akipokea zawadi yake ya fulana kutoka kwa Msimamizi wa mauzo ya Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Chanika Tesha Stanslaus (Kulia) wakati wa kuipongeza baa ya Check Point iliyopo Chanika jijini Dar es salaam baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwa mara ya pili kwenye Kampeni inayoendelea ya Tusker Fanyakweli kiwanjani. (Kushoto) ni Mshereheshaji wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Gadner Habash.

MGOMBE AAHIDI KUJENGA KITUO CHA RADIO NA TV



Na Hastin Liumba, Uyui

MGOMBEA ubunge wa jimbo la Tabora Kaskazini wilaya ya Uyui Mkoani Tabora kupitia Chama Cha  Mapinduzi Almas Maige amezindua kampeni za jimbo hilo na kuahidi kuanzisha kituo cha Radio na Televisheni ili kusadia wananchi wa jimbo hilo kupata mawasiliano ya taarifa.

MAAFISA AFYA TABORA WALAUMIWA KWA UCHAFU



Na Hastin Liumba, Tabora

WANACHAMA na viongozi wa umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Manispaa Tabora wameamua kujitolea kufanya usafi katika mji huo kwa lengo la kupunguza mlundikano wa uchafu hali inayoonyesha wahusika wameelewa na kazi za kuweka mji huo safi.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MWANGALIZI WA UCHAGUZI KUTOKA UMOJA WA NCHI ZA ULAYA IKULU DAR, AAGANA NA BALOZI WA MALAWI TANZANIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya, Judith Sergentine (kushoto) na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya Tanzania, Filiberto Cebregondi, wakati walipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujitambulisha baada ya kuwasili nchini. Picha na OMR 

WATANO WAFARIKI DUNIA KATIKA MATUKIO TOFAUTI MKOANI MBEYA, WAMO RAIA WA ETHIOPIA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi.
Na Jamiimojablog.

Watu watano wamefariki dunia   Mkoani Mbeya katika matukio matatu tofauti likiwemo la ajali ya haice iliyosababisha vifo vya watu wanne mkoani hapa.
       
Katika tukio la kwanza gari  lenye namba za usajili  T.519 AKH aina ya Toyota Haice ikiendeshwa na dereva  asiyefahamika kugongana na pikipiki yenye namba za usajili  T.535 AWC aina ya T-Better eneo la Nanenane Jijini Mbeya.      

ZETRIDA EZEKIEL ATOKA NA 'RINGA NA YESU'!


Zetrida Ezekiel ni mwanamuziki mahiri wa muziki wa injili aishiye mkoani Kigoma, amekuwa mwanamuziki wa nyimbo za injili ambaye ni mwana kwaya wa  kikundi maarufu na kikongwe cha nyimbo za injili cha MKE MWEMA cha mjni Kigoma. Zetrida ameolewa na ni mama wa watoto wanne, wa kike wawili na wa kiume wawili.

SHEREHE YA WAFANYAKAZI WA KISSA PHARMACY LTD KIJIJINI MAKANYA, SAME

Mgurugenzi Kissa Pharmacy Ltd Ndugu Gaspar Kilango Singo akizungumza na wafanyakazi wake katika sherehe hiyo iliyofanyika kijijini kwao Mnazi, Makanya Wilayani Same, Kilimanjaro.

DC PAUL MAKONDA AZURU GEREJI YA WACHINA, ALILIA WAFANYAKAZI WAPATE MIKATABA

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati), akizungumza na wafanyakazi wa Gereji ya Spring City Enterprises inayomilikiwa na raia wa China iliyopo Mikocheni B Mlalakuwa  Barabara ya Mwai Kibaki Dar es Salaam leo, alipofika kusikiliza malalamiko yao mbalimbali yakiwemo ya kutokuwa na mikataba ya kazi licha ya kuwa kazini kwa zaidi ya miaka saba. 

DK. SHEIN ANDELEA NA KAMPENI GARAGARA MTONI, ZANZIBAR

Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein. akisalimiana na Viongozi wa CCM alipowasili katika viwanja vya garagara mtoni kwa ajili ya kuendelea na mikutano yake ya kampeni Zanzibar kuomba ridhaa za Wananchi kumchagua tena kuongoza Zanzibar.

WILD BEEST DEATH IN MARA RIVER A NATURAL PHENOMENON




TANZANIA NATIONAL PARKS
PRESS RELEASE

Deaths of Wildebeest in Mara River a natural phenomenon

On 28th September, 2015 Africa Geographic website run a story with a caption “hundreds of wildebeest found dead in Tanzania”. The website posted a number of pictures taken along Mara river displaying dead wildebeest and went further stating that “…the authorities have been contacted and the exact cause of death has yet to be confirmed”. Tanzania National Parks would like to clarify on the story which has also been quoted by other social media as follows:

IT BRIDGE YAWAFIKIA WANAFUNZI 60,000

IMG_3000
Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Na mwandishi wetu
JUMLA ya wanafunzi 60,000 katika shule 150 nchini wamepitiwa na mafunzo ya programu ya Bridge IT yenye lengo la kuongeza ubora wa elimu kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kidijiti (digital technology) katika ufundishaji na ujifunzaji wa Hisabati,Sayansi na Stadi za Maisha.
Hayo yamsemwa na Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya Tehama.

IT BRIDGE YAWAFIKIA WANAFUNZI 60,000

IMG_3000
Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Na mwandishi wetu
JUMLA ya wanafunzi 60,000 katika shule 150 nchini wamepitiwa na mafunzo ya programu ya Bridge IT yenye lengo la kuongeza ubora wa elimu kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kidijiti (digital technology) katika ufundishaji na ujifunzaji wa Hisabati,Sayansi na Stadi za Maisha.
Hayo yamsemwa na Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya Tehama.

MAENDELEO ENDELEVU 17 YA DUNIA YAZINDULIWA TANZANIA

IMG_3349
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women nchini Tanzania, Anna Collins-Falk (katikati) wakipata picha ya kumbukumbu sambamba na mmoja wa wadau wa maendeleo. (Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

Na Mwandishi wetu
UMOJA wa Mataifa kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania wamezindua rasmi malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
Malengo hayo ambayo pia yanajulikana kama malengo ya dunia yamezinduliwa jana Septemba 29 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Uzinduzi huo ulifanywa na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez, Kamishina wa mipango (POPC) Bw. Paul Kessy, na Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame kwa niaba ya serikali, Bi. Fionnuala Gilsenan, Balozi wa Ireland na Bi. Liz Lloyd, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa niaba ya wadau wa mradi wa Project Everyone Partners.
SDGs ni wito wa dunia wa kuchukuliwa kwa hatua za kuufuta umaskini, kuihami dunia dhidi ya uharibifu wa mazingira na kuhakikisha kwamba kila mwanadamu anaishi maisha stahiki katika amani na ustawi.
Katika malengo hayo 17 yapo makusudio 169 yanayotoa ramani ya utengenezaji wa sera za maendeleo na namna ya kutekeleza kwa miaka 15 ijayo.
Malengo hayo yakijengwa juu ya mafanikio ya malengo ya milenia (MDGs), yameingiza vitu vipya kama mapambano dhidi ya tofauti za kiuchumi, ubunifu, mabadiliko ya tabia nchi, lishe, amani na haki. SDGs ni mpango wa dunia unaojikita kwa ustawi wa wanancni na dunia.
IMG_3303
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo (kushoto) na Kiongozi wa mabalozi wa nchi za nje hapa nchini Mheshimiwa Juma Mpango, ambaye ni balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiwa wameshikilia lengo namba 16 na 17 kati ya malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia ambayo yamezinduliwa rasmi nchini Tanzania jana 29, Septemba 2015.

Akizungumza umuhimu wa malengo hayo, Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez amesema: “Kwa mara ya kwanza katika historia ya dunia , serikali zimekutana na kukubaliana kupeana malengo kwa ajili ya kila mtu. Malengo haya yatasaidia mataifa yote kushirikiana katika kuwezesha ustawi, kupunguza matumizi na kuilinda dunia dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.Katika hilo watashughulikia elementi zinazohusu maendeleo endelevu: ukuaji wa uchumi, ustawi wa jamii na kulinda mazingira.”

MO KUANZISHA BENKI YA MIKOPO KWA WAFANYABISHARA WADOGO NCHINI

DSC_0316
CEO wa Kampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akiwa ofisini kwake.

Na Modewjiblog team
Mfanyabiashara Bilionea Mohamed Dewji ambaye hivi karibuni amepata tuzo ya Mfanyabiashara Bora wa Afrika wa mwaka 2015, katika kinyang’anyiro cha tuzo za wafanyabiashara bora wa Afrika (African Business Awards 2015) amebainisha kuwa lengo kuu la kampuni anayoiongoza ya MeTL Group, hadi kufikia mwaka 2022, ni kufikia dola bilioni 5 huku akitarajia kuajiri wafanyakazi zaidi ya laki moja.

MAGUFULI ASEMA ANATAKA USHINDI WA ASILIMIA 99!

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli

Na Joseph Mwendapole, Iringa
Wakati zikiwa zimebaki siku 25 kabla ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema hadi sasa anaona mambo yanamuendea vizuri kwenye kampeni zake na hivyo anataka kupata ushindi wa kishindo wa asilimia 99.
 
Magufuli aliyasema hayo jana kwenye Uwanja wa Samora uliopo Iringa mjini wakati wa mkutano wake wa kuhitimisha kampeni mkoani hapa.

Tuesday, 29 September 2015

JACK WARNER AFUNGIWA MAISHA KUJIHUSISHA NA SOKA

Aliyekuwa Afisa Mkuu wa Shirikisho la Kandanda Duniani, FIFA, Jack Warner, amepigwa marufuku kushiriki shughuli zo zote za kandanda maishani mwake.
Aliyekuwa Afisa Mkuu wa Shirikisho la Kandanda Duniani, FIFA, Jack Warner, amepigwa marufuku kushiriki shughuli zo zote za kandanda maishani mwake.
Kamati ya maadili ya FIFA ilisema kuwa alihusika pakubwa katika shughuli zote za kuwalipa watu pesa za shirikisho hilo kinyume cha sheria.

UCHAGUZI MKUU AFRIKA YA KATI KUAHIRISHWA

Catherine Panza
Bi Panza amewasihi raia nchini CAR kuwa watulivu
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Catherine Samba Panza amesema uchaguzi mkuu nchini humo utaahirishwa kwa sababu za kiusalama.

MATOKEO YA CHUONI HAYATAKUSAIDIA KUPATA KAZI

Matokeo ya chuoni hayatakusaidia kupata kazi
Kampuni ya kusaili watu kwa nafasi za kazi Deloitte imebadilisha sera zake ilikuficha majina ya vyuo walikosomea wafanyikazi watarajiwa.
Hii inalenga kuondoa upendeleo na ubaguzi dhid yao kwa misingi ya vyuo walivosoma.

UTAMUOKOA NANI, MAMAKO AU MPENZI WAKO? HILI NDILO JIBU SAHIHI...

Wazimamoto Kazan, Urusi
Wizara ya Haki baadaye ilichapisha ibu sahihi

Ungelazimishwa kuamua nani utakayemuokoa, ungemuokoa mamako au mpenzi wako kutoka kwa jumba linaloteketea?
Hili ni swali tata linaloulizwa sana Uchina. Na mwaka huu, lilikuwa kwenye mtihani wa kitaifa wa uanasheria, likiulizwa mawakili na majaji wa siku za usoni. Wanaopita mtihani huo ndio pekee huruhusiwa kuhudumu kama wanasheria nchini Uchina.

MMEA HATARI WATUMIWA KUZALISHA KAWI KENYA

Mathenge
Vijana wanalipwa kukata miti hiyo na kuisafirisha hadi kiwandani
Katika kipindi cha zaidi ya miaka kumi iliyopita, jamii ya Njemps iliyoko kaunti ya Baringo nchini Kenya imekuwa ikifuatilia kwa makini kesi iliyowasilisha mahakamani dhidi ya serikali.

MAKANISA MENGINE MANNE YACHOMWA MOTO KAGERA

Kanisa Kagera
Haijajulikana ni nani anayechoma moto makanisa
Makanisa manne yameteketezwa katika mkoa wa Kagera, kaskazini magharibi mwa Tanzania na kufikisha saba, idadi ya makanisa yaliyochomwa moto eneo hilo mwezi huu.

MATAIFA YASHUKU IDADI YA WALIOFARIKI MECCA

Mahujaji
Iran ni moja ya nchi zilizokosoa sana Saudi Arabia kutokana na mkasa huo
Maafisa katika mataifa kadha wamesema zaidi ya watu 1,000 walifariki kwenye mkanyagano karibu na Mecca wakati wa kuhiji.

VPL KUENDELEA VIWANJA SABA


Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea kesho Jumatano kwa timu 14 kucheza katika viwanja saba nchini, ikiwa ni raundi ya tano ya ligi hiyo iliyoanza kutimua vumbi Septemba 12, 2015.

U15 KWENDA TANGA KESHO


Kikosi cha Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) kinatarajiwa kusafiri kesho Jumatano kuelekea jijini Tanga kwa ajili ya mchezo wa kirafiki na kombani ya U15 ya jijini humo.

NYOSO AENDA 'JELA' MIAKA MIWILI

Juma Nyoso akifanya tukio la udhalilishaji dhidi ya John Bocco msimu huu wa ligi kuu Tanzania

Kamati ya masaa 72 ya uendeshaji wa Ligi Kuu iliyokutana leo kupitia ripoti mbalimbali za michezo iliyochezwa ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza nchini imemfungia mchezji Juma Nyoso wa timu ya Mbeya City kucheza mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka miwili na faini ya shilingi milioni mbili (2,000,000) kufutia kitendo cha udhalilishaji alichomfanyia mchezaji wa Azam FC John Bocco.

MAKAMU WA RAIS DK. BILAL ACHANGISHA SHS. 105 MILIONI KUHIFADHI VYANZO VYA MAJI MILIMA YA TAO LA MASHARIKI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo Maalum, Mshauri wa kampuni ya VIP Engineering & Marketing, Fr. James Rugemalira, wakati wa hafla ya Uchangishaji fedha kwa Uhifadhi wa vyanzo vya maji katika Mabwawa ya kuzalisha Umeme ya Mtera, Kihansi, Kidatu, Nyumba ya Mungu na Pangani, iliyofanyika jana usiku Sept 28, 2015 kwenye Hoteli ya Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. Picha zote na OMR

Na Daniel Mbega wa www.brotherdanny.com
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, amewaomba wadau wa maendeleo na uhifadhi wa mazingira kuisaidia taasisi ya Mfuko wa Udhamini wa Hifadhi ya Milima ya Tao la Mashariki (EAMCEF) ili kufanikisha uhifadhi wa vyanzo vya maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme nchini.

MGOMBEA MWENZA WA UKAWA KUPITIA CHADEMA AFANYA MIKUTANO KILWA KUSINI

 Mgombea mwenza wa urais Chadema, Juma Duni Haji akiwapungia mikono wananchi wakati akielekea jukwaani kuwahutubia kwenye mkutano wa kampeni katika kiwanja cha Mandawa Jimbo la Kilwa Kusini mkoani Lindi. (Na Mpigapicha Wetu)

MAGUFULI AENDELEA NA KAMPENI ZAKE, KESHO KUUNGURUMA LIVE UWANJA WA JAMHURI MKOANI DODOMA

 Pichani kati ni Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli akiwa sambamba na Mgombea Ubunge wa jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusinde kwa pamoja wakiwapungia wananchi wa jimbo la Mtera (hawapo pichani),ndani ya mji wa Mvumi wilayani Chamwino mkoani Dodoma. PICHA NA MICHUZI JR-DODOMA

EMIRATES YAPATA MENEJA MPYA NCHINI TANZANIA

Meneja mpya wa Shirika la ndege la Emirates nchini Tanzania, Husain Alsafi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati alipokuwa akijitambulisha, Dar es Salaam jana. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)

WASIMAMIZI NA WARATIBU WA UCHAGUZI MIKOA YA IRINGA MBEYA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA UPENDELEO KWA WAGOMBEA

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (PICHA MAKTABA)


Na Kahema Emanuel, Mbeya

Wito umetolewa kwa Waratibu  wa uchaguzi wa mikoa ,wasimamizi  wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi wa halmashauri mikoa ya kanda za juu kusini  kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa waledi na kwa uadilifu bila kuwa na upendeleo wa chama chochote cha siasa ua mgombea .

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro wakati akifungua mafunzo ya wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi halmashauri ambao ni wakurugenzi wa halmashauri na maafisa uchaguzi katika mikoa  ya Iringa na Mbeya.

UKAWA, CCM KWENYE MCHUANO MKALI TABORA



Na Hastin Liumba, Tabora

UNAWEZA kwa sasa ukasema bila kumung`unya maneno kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 utaacha historia, lakini hata kwa majibo yaliyoko mkoani Tabora licha ya kuwa siku zote hutwaliwa na CCM safari hii lolote linaweza kutokea.
Unaweze ukasema kwa sasa wapiga kura wa leo siyo wale wa chaguzi zilizopita za mwaka 1995, 2000, 2005, 2010 na 2015 yawezekana wamebadilika au ni uzoefu wa kujifunza kupitia chaguzi zilizopita.
Kutokana na hilo niliamua kuzunguka majimbo yote 12 ya mkoa wa Tabora ili kujiridhisha na mchuano ulivyo kwa sasa kipindi hiki kampeni za lala salama.

MAMA SAMIA SULUHU APANGA KUWAPIGANIA WANAWAKE

Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM.
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni inayoendelea nchini akiinadi ilani ya CCM.

MCHUANO wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajia kufanyika Oktoba 25, 2015 unaendelea maeneo mbalimbali ya nchini, huku vyama anuai vilivyofanikiwa kuingia katika ushindani huo wa kisiasa vikinadi ilani na sera zao kwa Watanzania ili kuwashawishi wachaguliwe.

TANZANIA NA POLAND KUKUZA KILIMO, KUANZISHA KIWANDA CHA MATREKTA NCHINI

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Wasira akutana na Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya kutengeneza Matrekta ya Ursus kutoka nchini Poland.

Na Eleuteri Mangi, MAELEZO
29/09/2015
Serikali ya Tanzania na Poland zimeingia makubaliano ya ushirikiano yatakayosaidia kukuza sekta ya kilimo kwa kuwawezesha wakulima kupata zana bora za kilimo kupitia  Kampuni ya kutengeneza Matrekta ya Ursus kutoka nchini Poland itakayoanza kufanya kazi zake nchini Tanzania mwanzoni mwa mwaka 2016.

MRISHO MPOTO AFUNGUKA NDANI YA GLOBAL TV ONLINE, AELEZA KISA CHA KUTEMBEA PEKU

MTEMVU: TUCHAGUENI TUMALIZIE MIRADI YA MAENDELEO YA MIAKA MITANO TULIYOPANGA

 Mgombea ubunge wa Jimbo la Temeke kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abbas Mtemvu (kulia), akipongezana na mgombea udiwani wa Kata ya Keko, Francis Mtawa baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa kampeni viwanja vya Mabembeani Keko jijini Dar es Salaam jana jioni

FASTJET YAONGEZA SAFARI ZAKE KWENDA JOHANNESBURG SASA NI KILA SIKU

 Mkuu wa Biashara wa Fastjet Lan Petrie (kulia), akizungumza katika semina hiyo.
 Meneja Mkuu wa Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati (kulia), akizungumza katika semina ya siku moja ya waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, iliyohusu kuongezeka kwa safari za ndege za shirika hilo kila siku kwenda Johannesburg nchini Afrika Kusini.

BASATA, WADAU WAWEKA MIKAKATI KUUPA HADHI MUZIKI WA REGGAE

 Msanii mkongwe wa muziki wa reggae na Mkurugenzi wa Reggae Production House Innocent Nganyagwa akiongea na wadau wa muziki huo mapema wiki hii kwenye programu maalum ya kujadili hatma ya muziki wa reggae iliyoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kufanyika makao makuu ya Baraza hilo Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Sanaa kutoka BASATA, Augustino Makame na Katibu wa chama cha waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) Hassan Bumbuli .

NG'OMBE WAWEKWA 'REFLECTOR' ZIMBABWE

Ng'ombe Zimbabwe
Wakazi wanasema kamba hizo zitawawezesha madereva kuwaona mifugo hao kutoka mbali
Wakazi wa wilaya moja nchini Zimbabwe wamevumbua njia ya kuzuia ajali za barabarani zinazohusisha ng’ombe wanaoranda randa.

WALIMU KENYA WAKAIDI AMRI YA MAHAKAMA


Mgomo wa walimu washika kasi Kenya
Masomo katika shule za umma nchini Kenya yamekwama licha ya amri ya mahakama ya kuwataka walimu warejee shuleni jana Jumatatu.

MTOTO MMOJA KATI YA WAWILI WANAOZALIWA NI WANAHARAMU

Je ndoa imepoteza hadhi yake?


Je ndoa imepoteza hadhi yake?
Watoto waliozaliwa nje ya ndoa walikuwa wanatambulika kama wana haramu.
Lakini takwimu za hivi punde zinaonesha kuwa mtazamo huo umebadilika kadri walimwengu wanavyoendelea kukubali maisha ya kisasa.

MWEZI USIO WA KAWAIDA WAZUA MSISIMKO

Mwezi mkubwa
Picha hii inaonyesha mwezi mkubwa wa kawaida na mwezi mkubwa ukilingana na kupatwa kwa mwezi kama ilivyoshuhudiwa Wiesbaden, Ujerumani leo

Watu wengi pande mbalimbali duniani wamekuwa wakitazama tukio la kawaida la kupatwa kwa mwezi ambalo limetokea wakati mmoja na kuonekana kwa mwezi mkubwa kwa Kiingereza "supermoon".