Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 8 December 2016

COASTAL UNION YALIA NA ADHABU YA TFF


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
COASTAL UNION FOOTBALL CLUB (TANGA, TANZANIA)
Uongozi wa klabu ya soka Coastal Union yenye makao yake makuu mkoani Tanga, imepokea kwa masikitiko adhabu iliyotolewa na Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji ya Bodi ya Ligi kutokana na vurugu zilizofanyika katika mechi namba 15B kati ya Coastal Union na KMC ya Dar es Salaam.

AZAM FC KUCHEZA MCHEZO WA KIRAFIKI DHIDI YA MTIBWA SUGAR

Nahodha wa Azam FC, John Bocco, akimiliki mpira mbele ya kiungo mkabaji, Stephane Kingue na beki Bruce Kangwa, wakati wa mazoezi ya timu hiyo leo Jumatano asubuhi.

SBL YAKABIDHI MRADI WA MAJI WA 83M/- MAKANYA WILAYANI SAME

Mkuu wa wilaya ya same Bi Rosemary Semanyole akifurahi pamoja na baadhi ya viongozi wa serengeti breweries Limited .kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasialiano wa SBLJohn Wanyancha  mara baada ya uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha makanya..Hafla ya uzinduzi ilifanyika katika kijiji cha Makanya wilaya ya same mapema jana.

TAMASHA LA SIFA ZA YERIKO ARUSHA



Miaka 25 ijayo, Takribani asilimia 75 ya wakazi wa Afrika Mashariki watakuwa vijana,na hii inamaanisha nguvukazi kubwa itakuwa mikononi mwao. Lakini kama watasalia kuwa idadi kubwa basi na kuwa na maarifa ya kuendesha nchi, basi changamoto itakuwa kwa ukuaji wa nchi.Vijana wao huona kama wana mchango katika jamii, hasa kwenye makusanyiko ya kijamii mathalani misiba, ambapo hutakiwa kuchangamkia kwenye shughuli zenye uhitaji wa nguvu. Lakini kama fursa ya uwepo wa vijana katika jamii itatumiwa vema, basi nyanja zote za maendeleo zitaendeshwa vema, na watakuwa na uwezo wa kutatuza matatizo yaliyo kwenye jamii – sawasawa na malengo endelevu namba 2 na namba 8 za umoja wa mataifa, zinazolenga kumaliza masuala ya njaa, na pia uhakika wa kazi na ukuaji wa uchumi, ikiwemo pia lengo namba 4 – kuwa na elimu bora.

TAASISI YA AFRICAN RELIEF YAANZISHA KILIMO CHA UMWAGILIAJI CHUMBI, RUFIJI


Mkurugenzi wa Taasisi ya African Relief Organization, Samy  Mohammed Elazeb (kulia) akisimamia trekta likilima shamba lenye ukubwa wa ekali 2500 eneo la Khanga, katika Kijiji cha Chumbi C, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki.Taasisi hiyo itaanza uzalishaji wa mazao ya mahindi na mpunga.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

WAHARIRI WAKUTANA KUPITIA SHERIA YA HUDUMA YA VYOMBO VYA HABARI ILIYOPITISHWA NA BUNGE

 Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Theophil Makunga (kulia), akizungumza Dar es Salaam leo wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa wahariri  kupitia sheria ya huduma ya vyombo vya habari uliyopitishwa na Bunge pamoja na kujadili mpango mkakati wa TEF wa kuendeleza tasnia ya habari nchini. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Habari Tanzania (TMF), Ernest Sungura.

MSD YAZINDUA HUDUMA MAALUMU KWA WATEJA WAKUBWA JIJINI DAR

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee naWatoto Dk. Mpoki Ulisubisya (kulia), akizungumza na viongozi mbalimbali wa sekta ya afya wakati akizindua mpango wa huduma maalumu kwa wateja wakubwa Dar es Salaam leo asubuhi.

Tuesday, 6 December 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN, KATIBU MKUU PAMOJA NA NAIBU WAZIRI WA TAMISEMI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwakaribisha Naibu Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo aliyeambatana na Katibu Mkuu wa TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe  kabla ya kuanza kwa kikao chao cha pamoja na Makamu wa Rais  Samia Suluhu Hassan.

WAKAGUZI WA NDANI WATAKIWA KUSIMAMIA UBORA WA MIRADI MIKUBWA YA UJENZI WA MIUNDOMBINU

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika (kulia), akimsikiliza   Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Faraji Kasidi (kushoto) wakati akielezea mafanikio na changamoto zinazokikabili chuo hicho.  Kushoto kwa Mkuu wa Chuo ni Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Bw.  Mohamed Mtonga, Msaidizi wa Mkuu wa Chuo Dkt. Samwel Werema, Mkaguzi wa Ndani Mkuu Msaidizi– Ukaguzi Mamlaka za Mitaa Bw. Mwanyika Musa na Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Kiufundi Bw. Amin Mcharo.

MSD YAZINDUA HUDUMA MAALUMU KWA WATEJA WAKUBWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee naWatoto Dk. Mpoki Ulisubisya (kulia), akizungumza na viongozi mbalimbali wa sekta ya afya wakati akizindua mpango wa huduma maalumu kwa wateja wakubwa Dar es Salaam leo asubuhi.

NAPE AKIRI, BLOGGERS WAMEIRUDISHA CCM MADARAKANI


Mmiliki wa blogu ya www.maendeleovijijini,blogspot.com, Bw. Daniel Mbega, akipokea kadi ya uanachama wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma – PSPF kutoka kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye baada ya kujiunga na mfuko huo leo hii jijini Dar es Salaam. Mhe. Nape alikuwa mgeni rasmi wakati wa ufungaji wa semina na mkutano mkuu maalum wa wamailiki wa blogu Tanzania – TBN, ambapo PSPF walikuwa miongoni mwa wadhamini.

Monday, 5 December 2016

SERIKALI YATAKIWA KUBAINISHA STENDI ZA DALADALA JIJINI MWANZA

 Mwenyekiti wa Madereva Kanda ya ziwa Hassan Dede akihojiwa na waandishi wa habari

CHADEMA YAWANOA VIONGOZI WAKE WA MABARAZA WILAYA YA NYAMAGANA MKOANI MWANZA

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Ziwa, Meshack Micus (kulia), akizungumza juzi kwenye semina kwa viongozi wa Mabaraza ya Chadema Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.

MATUKIO YA UHAKIKI WA WASTAAFU WANAOLIPWA NA HAZINA MKOANI ARUSHA

Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe (kushoto)  akitoa ufafanuzi kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango namna zoezi zima la uhakiki wa wastaafu kanda ya kaskazini linavyokwenda kabla ya uzinduzi wa zoezi hilo. Zoezi hili ni kwa mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga. 

SERIKALI YAITAMBUA RASMI MITANDAO YA KIJAMII (BLOGGERS)

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MKURUGENZI WA MAUZO WA KAMPUNI YA NDEGE YA BOEING, MWAKILISHI MKAZI WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AfDB) PAMOJA NA BALOZI WA CUBA HAPA NCHINI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa mauzo wa kampuni ya Ndege ya Boeing Jim Deboo aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo pamoja na ujumbe wake.

AZAM FC YAOMBOLEZA KIFO CHA MCHEZAJI MBAO

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, leo asubuhi kabla ya kuanza rasmi mazoezi ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utakaoanza rasmi Desemba 17 mwaka huu, wachezaji na benchi la ufundi walisimama kwa dakika moja kuomboleza kifo cha mchezaji wa timu ya vijana ya Mbao, Ismail Khalfan.

WIZARA YA FEDHA YA FEDHA NA MIPANGO YATUNUKIWA TUZO YA TAARIFA BORA YA FEDHA MWAKA 2015

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Prof. Isaya Jairo akizungumza na Wahasibu kutoka Taasisi za umma na binafsi waliohudhuria katika hafla ya kutoa tuzo ya Taarifa bora ya Fedha kwa mwaka 2015, katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (NBAA) kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

TAARIFA YA VIKAO VYA KAMATI KUU NA HALMASHAURI KUU

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kutakuwa na kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kitakachofanyika tarehe 11 - 12/12/2016 na kufuatiwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa tarehe 13/12/2016. Vikao vyote hivyo vitafanyika jijini Dar es salaam.

Wajumbe wote wa vikao hivyo wanaombwa kuhudhuria.
Imetolewa na:- 
                   
SELEMAN Y. MWENDA
Kny: MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
05.12.2016

Sunday, 4 December 2016

MALEZI BORA NI MSINGI WA MAFANIKIO KATIKA ELIMU NA TAIFA

Wanafunzi wa shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings wakionesha umahiri wao katika michezo wakati wa siku ya wazazi na mahafali ya wanafunzi wa elimu ya awali katika shule ya Awali na Msingi ya Genius Kings mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.

Saturday, 3 December 2016

DURU LA KWANZA LIGI YA TFF U-20

Ligi ya vijana kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea katika vituo viwili vya Kagera na Dar Es Salaam ambapo duru la kwanza linatarajiwa kumalizika Desemba 05, 2016.

RIPHAT HAMISI MCHEZAJI BORA WA VPL MWEZI NOVEMBA, 2016

Mchezaji Riphat Hamisi wa timu ya Ndanda FC amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Novemba kwa msimu wa 2016/2017.

WATAALAM WA MIPANGO NA MAENDELEO VIJIJINI WAHIMIZWA UADILIFU NA KUJIEPUSHA NA UFISADI

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (Wa pili kulia), akipata maelezo ya Chuo Cha Maendeleo ya Mipango Vijijini Kampani Kuu ya Dodoma, kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Frank Hawassi (Wa pili kushoto) kabla ya kuanza kwa sherehe ya Mahafali ya 30 ya Chuo hicho kilichoko eneo la Miyuji, mkoani Dodoma.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA KUENDELEZA MAENEO TENGEFU YA VIWANDA VYA USINDIKAJI VYAKULA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati ufunguzi wa mkutano wa Wadau wa kuendeleza maeneo Tengefu ya Viwanda vya Usindikaji Vyakula uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

MWALIMU AFARIKI KATIKA MKUTANO WA CHAMA CHAO CHA CWT JIJINI DAR ES SALAAM

 Mwalimu Tuhobwike Mwinuka Mwakatumbula enzi za uhai wake.

MREMBO ANNA NITWA AFANIKISHA UKARABATI WA CHOO CHA WODI YA KINAMAMA WANAJIFUNGUA WATOTO NJITI HOSPITALI YA DODOMA

 Mlimbwende anayeshikilia Taji la Urembo la Mkoa wa Dodoma (Miss Dodoma 2016/17), Anna Nitwa (wa pili kulia) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (wa pili kushoto) pamoja na madaktari wakati wakielekea kwenye Wodi ya Wazazi wanaojifungua Watoto kabla ya wakati (Njiti), katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Desemba 1, 2016.

KAMA MSANII UNATAKA KUJUA HAKI ZA KAZI ZAKO ZA SANAA.., BASI JUKWAA HILI SIO LA KUKOSA!


WAMA FOUNDATION YAKANUSHA TAARIFA ZA "MTANZANIA"


WANAWAKE NA MAENDELEO FOUNDATION
D A R ES SALAAM | IJUMAA |DESEMBA 2, 2016
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katika gazeti la Raia Mwema toleo No 486 la Tarehe 30 Novemba, 2016 kumeandikwa habari yenye kichwa kilichosomeka “Mali za Salma Kikwete kuuzwa kwa mnada?”.  Katika habari hiyo kumetolewa madai ati kwamba taasisi ya WAMA inayoongozwa na Mheshimiwa Mama Salma Kikwete inao mzigo mkubwa bandarini ambao haujalipiwa ushuru na kodi. Na kwa sababu hiyo, Mamlaka ya Mapato Tanzania imepanga kuuza mali hizo.

Friday, 2 December 2016

RC SINGIDA AWAAGA VIJANA WAHADZABE 43 WANAOENDA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JESHI

Mmoja wa kijana wa kihadzabe Zuhura Ramadhani Longa ambaye alikuwa akiwasindikiza vijana wenzake wanawinda na kurina asali, amesema ameamua kujiunga na jeshi ili aweze kuisaidia familia yake lakini pia aweze kulitumikia taifa.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU ASAINI KITABU CHA KUMBUKUMBU YA MAOMBOLEZO YA FIDEL CASTRO



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha kumbukumbu cha maombelezo ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo na mpigania ukombozi Fidel Castro aliyefariki dunia novemba 25,2016 mjini Havana, aliyesimama kushoto ni Balozi wa Cuba nchini Balozi Jorge Luis Lopez Tormo.

ZAIDI YA MILIONI 340 ZAPATIKANA KATIKA UZINDUZI WA BODI YA UDHAMINI DHIDI YA UKIMWI


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Munngano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye Uzinduzi wa Bodi ya Udhamini dhidi ya Ukimwi uliofanyika tarehe 1 Desemba kwenye hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

TANZANIA BLOGGERS NETWORK (TBN) KUFANYA SEMINA NA MKUTANO MKUU DESEMBA 5 NA 6




TAARIFA YA TANZANIA BLOGGERS NETWORK (TBN) KWA WAANDISHI WA HABARI TAREHE 02 DESEMBA, 2016 KATIKA UKUMBI WA IDARA YA HABARI (MAELEZO)

Ndugu Mwakilishi kutoka Benki ya NMB,
Waandishi wa habari,

Kwa niaba ya Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii nchini 'Tanzania Bloggers Network' (TBN) napenda kuwashukuru kwa kujitokeza katika mkutano huu muhimu. TBN inajua kuwa mnamajukumu mengi ya kuujuza umma masuala anuai, lakini mmechagua kuja kwetu ili kutusikiliza tulichowaitia na baadae tunaamini mtaujuza umma juu ya tukio letu.

PROF. OLE GABRIEL: SIRI YA MAFANIKIO KATIKA TAASISI NI KUFIKIRI KIMKAKATI NA USIMAMIZI BORA

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea na Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST) alipowatembelea akiwa mmoja wa wanachuo wa mwanzao waliohitimu katika chuo hicho ambapo awali kilijulikana na kama Taasisi ya Sayansi na Teknolojia (MIST). Prof. Ole Gabriel amewahimiza viongozi hao wawe msatari wa mbele katika kusimamia taaluma na kuwajengea uwezo wanafunzi wao wajitambue na wawe na utamaduni bora wa kufikiri kimkakati na usimamizi ili waweze kuendana na ulimwengu wa sasa.

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA AENDESHA HARAMBEE YA SH.BILIONI 1 KUSAIDIA MFUKO WA UKIMWI NCHINI

 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati akizundua Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Udhibiti Ukimwi (ATF)  Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam jana.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk.Leonard Maboko akizungumza kwenye uzinduzi huo.

CHAMA CHA AFYA YA JAMII TANZANIA (TPHA) CHAPATA VIONGOZI WAPYA

 Mwenyekiti Mteule wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Shaibu Mashombo (wa nne kushoto), akiwa na viongozi wenzake wateule waliochaguliwa katika mkutano mkuu wa chama hicho 2016 jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Dismas Vyagusa, Violeth Shirima, Dk. Godfrey Swai, Dk.Nderineia Swai, Dk. Feliciana Mmasi,  Dk. Mwanahamisi Hassan na Dk.Elihuruma Nangawe ambaye alikuwa Mwenyekiti wa chama hicho aliyemaliza muda wake.

RC MAKALLA AISHUKURU UN KWA MISAADA NA USHIRIKIANO KWA SERIKALI YA TANZANIA

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (kushoto) akisalimiana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyemtembelea ofisini kwake na kufanya mazungumzo ya kuboresha ushirikiano baina ya Serikali na Umoja wa Mataifa jijini Mbeya.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Thursday, 1 December 2016

RC MTIGUMWE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA SINGIDA



Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Singida SSP Peter Charles Kakamba, baada ya mwili kuagwa Mhandisi Mtigumwe amewaongoza msafara wa waombolezaji kuelekea Mkoani Katavi, kijiji cha Kawajese kwa ajili ya mazishi. Kamanda Kakamba amefariki usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati akipatiwa matibabu.(Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida)

SERIKALI YASHAURI MAJINA YA WAHASIBU WEZI YAWEKWE HADHARANI

 Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango (kulia), akikata utepe kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuashiria kuzindua rasmi Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (APC), kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa  Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Profesa Isaya Jairo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa GEPF, Joyce Shaidi.

PUMA YANG'ARISHA UTALII ZANZIBAR KWA MASHINDANO YA NDEGE KONGWE 22


 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Phillipe Corsaletti (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Rubani wa kike mdogo kuliko marubani wote wa ndege ya zamani, Sara Meehan (18), jinsi injini ya ndege hiyo kutoka Botswana inavyofanya kazi, wakati wa mapokezi  ya ndege hizo 'Vintage Air Rally' kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume, Zanznibar jana. Ndege hizo zilitengezwa kati ya mwaka 1920 na 1930. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

RC SINGIDA AHIMIZA WATUMISHI KUWAJIBIKA

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe (picha ya maktaba).

Mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe, amewahimiza watumishi wa umma hasa wa ngazi ya Vijiji na Kata kuwajibika  na kutimiza vyema majukumu yao kwani wao wako karibu zaidi na Wananchi, ili kutimiza adhma ya Serikali ya awamu ya tano ya kumpunguzia kama si kumuondolea kabisa kero zinazozuilika Mwananchi wa kawaida.

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU ANUSURIKA KUFA BAADA YA KUBAKWA NA KUTELEKEZWA KORONGONI

Image result for KAMANDA WA POLISI
ARUSHA MKUMBO
Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha Charles Mkumbo
  

Na Woinde Shizza, Meru
MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kitefu iliyopo Meru  mkoani Arusha amenusurika kufa mara baada ya kubakwa na kuteketezwa kwenye  korongo la mchanga na kusababishiwa  maumivu makali yaliyomsababishia kushindwa kuendelea na masomo yake kwa muda.

SERIKALI KUFANYA MALIPO KWA MFUMO WA KIELEKRONIKI NCHINI



Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam
Wizara ya Fedha na Mipango imekamilisha ujenzi wa mfumo wa malipo moja kwa moja kupitia akaunti za walipwaji katika mtandao wa malipo wa Benki Kuu ya Tanzania (Tanzania Interbank Settlement System – TISS), katika mkoa wa Morogoro, hatua inayolenga kuongeza ufanisi wa miamala mbalimbali inayofanywa na serikali.

MADIWANI HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA WAINGIA MTAANI KUKUSANYA MAPATO

Meya wa Jiji la Mbeya David Mwasilindi


 Na JamiiMojablog, Mbeya
Halmashauri ya jiji la Mbeya imebuni njia mpya ya ukusanyaji wa mapato  ili kufikia malengo yake ya ukusanyaji wa kiasi cha shilingi bilioni  11 katika  mwaka wa fedha wa  2016/17 .

Katika kufanikisha mpango huo halmashauri imewashirikisha madiwani na wataalmu wake katika kufanya kazi ya ukusanyaji wa mapato kupitia vyanzo vyake vya ndani .


Moja ya njia hiyo halmshauri imeanza kuwatumia Madiwani pamoja na wenyeviti wa mitaa katika ukusanyaji wa fedha kupitia vyanzo vyake vya ndani vya mapato .

Akielezea mkakati huo  Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Ndugu David Mwashilindi amesema katika kuhakikisha halmshauri inafikia lengo lake la ukusanyaji wa mapato imeamua kuongeza nguvu kazi kwa kuwaingiza madiwani na wenyeviti ambao wapo karibu na wananchi.


“ Kazi kubwa  wanayo ifanya madiwani na wenyeviti kwa kushirikiana na wataalam ni kuhakikisha wanavitambua vyanzo vyote vya mapato vinavyostahili kuingia katika mapato ya halmashauri  ikiwa na kubaini mianya iliyokuwa ikitumiwa na wahusika kukwepa kulipa kodi,”amesema Mwasilindi.


Amesema kuziendesha halimamshauri hizi inategemea sana mapato ya ndani hivyo lazima kuweka jitahada za makusudi katika kufikia malengo husika .


Amesema katika kipindi cha nyuma halmasahuri hiyo hali ilikuwa katika hali mbaya kwani kwa mwezi walikuwa wanakusanya kiasi cha shilingi milioni 120 hadi 200 lakini mara baada ya kuanza kwa jitihada hizo imesaidia kupandisha mapato ambapo kwa sasa imefikia kiasi cha shilingi milioni 700 kwa mwezi.


Amesema zoezi hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa ambapo sanjali na kukusanya mapato pia kuna sauala la utoaji wa elimu kwa wananchi ili kuelewa namna ya kulipa  tozo zilizo wekwa kisheria.


Amesema zoezi hilo litadumu kwa muda wa siku tano na mara baada ya hapo kutafanyika kwa tahimini ya pamoja ili kubaini changamoto zilizopo katika zoezi.


MD KAYOMBO AFANIKISHA MRADI SHULE YA MATOSA

 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amepongezwa na walimu pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari Matosa iliyopo Kata ya Goba , Manispaa ya Ubungo kwa kufanikisha kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa mradi wa SEDP II.

DC STAKI AZINDUA HUDUMA YA UPANDAJI MITI MAENEO OEVU KWENYE VYANZO VYA MAJI


Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Rosemary Staki amezindua shughuli ya kupanda miti maeneo oevu/ kwenye vyanzo vya Maji katika Kata ya Bwambo. Zoezi hilo limefanyika kwa ushirikiano na shirika lisilo la kiserikali la Floresta.

WATUMISHI OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA WAPIGWA MSASA

Mshauri Mwelekezi wa Masuala ya Jinsia kutoka “Women Fund” Profesa Ruth Meena akitoa mada.

MUUZA MITUMBA SOKO LA KARUME JIJINI DAR ES SALAAM AFUTIWA LESENI YA BIASHARA KWA KUMDHALILISHA MTEJA WAKE WA KIKE


 Diwani wa Kata ya Mchikichini, Joseph Ngowa (katikati), akihutubia wakati akizindua kampeni ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia iliyoandaliwa na Shirika la Eguality for Growth (EfG), Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Wanawake katika Soko la Mchikichini, Betty Mtewele na kulia ni Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mchikichini, Charles Kapongo.