Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 1 July 2014

ISRAEL YAAPA KULIPIZA KISASI KWA HAMAS

Benyamin Netanyahu,waziri mkuu wa Israel
Israel imeapa kulipiza kisasi dhidi ya kikundi cha wapiganaji wa Hamas wa Kipalestina wanaosemekana kuwateka na kuwaua vijana watatu katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan.
Miili ya vijana hao Naftali Frenkel, Gilad Shaar na Eyal Yifrach ilionekana Jumatatu jioni, baada ya kupotea kwa zaidi ya wiki mbili.
Israel imefanya mashambulio ya anga zaidi ya 30 katika Ukanda wa Gaza usiku kucha.Waziri Mkuu wa Israel, Benyamin Netanyahu amesema: "Hamas wanahusika na Hamas watalipa." Hamas wanakanusha kuhusika na tukio hilo.
Mashambulio hayo yamekuja ikiwa ni kujibu mashambulio 18 ya maroketi kutoka Gaza tangu Jumapili usiku, limesema jeshi la Israel.
Miili ya vijana watatu waliotekwa na kuuawa ilipatikana karibu na mji wa Halhul

Majeshi ya Israel pia yamesambaa katika mji wa Palestina wa Halhul. Miili ilipatikana chini ya kifusi cha miamba karibu na mji huo. Afisa mmoja wa Israel anasema inaonekana kuwa vijana hao watatu waliuawa kwa kupigwa risasi mara baada ya kutekwa kwao.
Israel imewataja watuhumiwa wawili wa utekaji wa vijana hao kuwa ni Ayoub al-Kawasma na Abu Aisheh. Jeshi la Israel limesema lilitegua milipuko iliyokuwa imetegwa wakati wa kuzivamia nyumba za watuhumiwa hao.
Askari wa Israel walitegua milipuko katika nyumba za watuhumiwa wawili wa Hamas. Picha zimeonyesha uharibifu mkubwa uliofanyika katika nyumba ya Abu Aisheh.

Mpalestina mmoja pia aliuawa baada ya kuwarushia kilipuzi wanajeshi wa Israel waliokuwa katika operesheni katika mji wa Jenin ulioko magharibi mwa mto Jordan, mapema Jumanne, limesema jeshi la Israel.
BBCSWAHILI

RIWAYA TAMU: JUDITH…JUDITH…! - 18


INNOCENT A. NDAYANSE (ZAGALLO)

0755 040 520 / 0653 593 546 

UTANGILIZI
Judith amenunua nguo chache za kuanzia, lakini kutwa nzima hakumuona Baraki ambaye baadaye anampigia simu kupitia simu ya muhudumu wa gesti kwamba asingekuja bali wangeonana kesho yake. Kesho yake mapema Judith anaamua kwenda mjini ili akabadili fedha zake. Anafanikiwa kubadili na kukodi teksi kumrudisha Magomeni. Ungana na msimulizi wako upate uhondo wa simulizi hii… 

Dakika iliyofuata Judith alikuwa ameshaachana na teksi hiyo. Akatembea taratibu akiifuata  barabara ileile aliyoitumia asubuhi kuja hapo kituoni. Ni wakati huo ndipo alipoihisi njaa, na akakumbuka kuwa tangu asubuhi alikuwa hajatia kitu tumboni.
Akaangaza hapa na pale na kuona baa moja nyuma ya kituo cha daladala. Watu walikuwa wengi katika eneo hilo, baadhi wakinywa soda, baadhi wakinywa supu na wengine wakinywa bia.
Alikwenda na kuagiza supu, chapati mbili na soda. Wakati akisubiri huduma hiyo, mara akamwona mtu mwingine akija katika meza hiyo. Alikuwa ni mwanamume, kijana mwenye umri kati ya miaka ishirini na mitano na thelathini na mitano. Kijana huyo alipofika alimtazama Judith huku akiachia tabasamu la mbali na kisha akasema, “Samahani, sista, naweza kuketi hapa au mwenyewe katoka?”
Judith akaunyanyua uso na kumtazama mtu huyo. Akavutiwa na utanashati wake; shati jeupe la mikono mirefu, suruali nyeusi na viatu vyeusi vilivyonakshiwa vizuri. Macho ya kijana huyo yalikuwa kitu kingine kilichomvutia kiasi cha kuhisi mshtuko kila walipotazamana.
“Au kuna mtu, sista?” kijana huyo alirudia kumuuliza huku akimtazama kwa makini zaidi, tabasamu likizidi kuchanua.
“Keti tu,” Judith alijibu. “Sidhani kama kuna mtu aliyekuwa hapa. Mie nimekuta meza nyeupe.”
Dakika chache baadaye mtu huyo alikuwa akinywa soda huku Judith akifakamia supu.
“Samahani, anti, tunaweza kufahamiana zaidi?” kijana huyo aliamua kuuvunja ukimya uliokuwa umeitawala meza hiyo.
Judith alimtazama kidogo kisha akayarejesha macho kwenye bakuli la supu. Akachota mchuzi kwa kijiko na kunywa. Akafanya hivyo mara mbili zaidi, kisha akaachia tabasamu la mbali. “Inategemeana ni kufahamiana ki-vipi,” hatimaye alisema.
Kijana yule alilikuza tabasamu lake na kusema, “Ni kwa utaratibu wa kawaida tu.”
“Sijakuelewa,” Judith alisema, safari hii akiunyanyua uso na kumtazama kijana huyo kwa makini, paji la uso wake likiunda mikunjo ya mbali.
“Yaani kwa mfano,” mtu huyo alisema, “Mimi naitwa Edson. Ni jina langu halisi. Ni mzaliwa wa Kigoma. Nadhani mpaka hapo inatosha. Sijui wewe. Au nitakuwa nimegeuka Ofisa Uhamiaji au askari polisi?”
Kicheko cha mbali kilimtoka Judith. Akamtazama tena Edson na kuyasoma macho yake, akitaka kuthibitisha kama kuna uwiano wowote kati ya macho hayo na maneno yake. Akakumbana na macho yaliyong’ara sanjari na tabasamu dhaifu lililolandana na utazamaji wake.
Sasa Judith akajiona ameondokana na upweke. Japo huyu mtu alikuwa mgeni kabisa machoni pake, tofauti na Baraki aliyemwokoa kutoka Rwanda, hata hivyo alijiona kuwa kampata mkombozi halisi.
“Naitwa Judith,” hatimaye alisema. Hakuendelea kutoa utambulisho zaidi, alijiuliza kama ilikuwa sahihi kutoboa undani wa asili yake. Jibu lililomjia akilini ni HAPANA.
Alitambua fika kuwa uraia wa mtu ni jambo linalotiliwa umuhimu katika mataifa mengi duniani. Siyo kwamba raia au mzaliwa wa nchi moja haruhusiwi kuishi nchi nyingine, la hasha. Anaweza kuishi, lakini kwa utaratibu unaokubalika kisheria. Raia wa nchi nyingine, kama yeye Judith, anaruhusiwa kuishi Tanzania ama nchi nyingine yoyote endapo tu atakuwa amefuata kanuni husika ambazo zinatambulika kitaifa na kimataifa.
Kwa hali hiyo, yeye alipaswa kuwa hapo Dar es Salaam huku Idara ya  Uhamiaji ikiwa na taarifa yake. Isingewezekana amtamkie bayana huyu mtu kuwa yeye ni mzaliwa wa taifa la Rwanda . Hilo halikumwingia akilini wakati huo. Akaendelea kufikiria jinsi atakavyojieleza kama ataulizwa swali jingine hususan kuhusu uraia wake.
“Ni jina zuri,” Edson alimkatisha mawazo yake. Akatamka tena kwa sauti ya chini, “Judith…Judith, jina zuri kama ulivyo.”
Tabasamu jingine likamtoka Judith. Akaunyanyua uso na kumtazama kidogo Edson kisha akayaepuka macho na kuyarejesha mezani. Kwa sauti yenye taswira ya aibu, akasema, “Asante.”
“Unaishi maeneo hayahaya ya Magomeni?” Edson alirusha tena swali.
“Ndiyo.”
I see. Ni mpweke kama mimi au…?”
Judith akamtazama tena, safari hii kwa chati sana . Akakohoa kidogo na kunywa tena soda yake, kama vile hajalisikia swali hilo .
“Eti Judi,” Edson alimbana. “Umeolewa?”
“Kwa nini unauliza ivo?”
Edson alicheka kidogo kisha akasema, “Wengine ni waoga wa kupigwa risasi au kuchomwa visu na wenye mali.”
Judith naye akacheka.
Wakatazamana, macho ya kila mmoja yakiwa na kitu fulani kilichozungumza neno moja tu: MAPENZI. Judith akabibitua midomo na kuendelea kunywa supu yake. Kwa mara nyingine ukimya ukapita katika eneo hilo.
Wakatazamana tena, safari hii Judith akaachia tabasamu la kirafiki, zaidi ya urafiki wa kawaida.
“Judith,” Edson alimwita kwa sauti ya chini.
Judith hakuitika kwa sauti, alimtazama kidogo Edson kisha akauinamisha tena uso.
“Judith,” Edson aliita tena na safari hii alionekana kutojali kuitikiwa. Akaendelea, “Samahani kwa hili nitakalokuuliza kama nitakuwa nimefanya kosa.”
“Hapana, hujafanya kosa,” Judith alijibu huku akiyaepuka macho ya Edson.
“Asante. Kwa hiyo?”
“Sijaolewa,” jibu la Judith lilikuwa fupi.
Lilikuwa ni jibu lililomtia ujasiri Edson. Sasa akapata nguvu ya kuendelea kuzungumza.


Itaendelea kesho…

SUAREZ AMUOMBA RADHI CHIELLINI

Mshambulizi wa Uruguay na Liverpool ya Uingereza Luiz Suarez sasa amemuomba msamaha mlinzi wa Italia Giorgio Chellinii kufuatia tukio la kumng'ata timu hizo zilipokuwa zicheza mechi ya mwisho ya makundi huko Brazil.
Suarez aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter ''baada ya kuketi nyumbani na familia yangu na kutulia imenijia kuwa tukio la kumng'ata Chellini ni la kusikitisha na kwamba sitarudia tena .
Suarez alimng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini Uruguay ilipowalaza mabingwa hao wa zamani wa dunia 1-0 jumanne iliyopita.“ninajutia sana tukio hilo na ninamuomba msamaha Chellini .ukweli ni kwamba anauguza jereha la kuumwa baada ya kugongana naye katika mechi hiyo .''
FIFA imeamuru asishiriki mechi yeyote ile kwa kipindi cha miezi minne mbali na kulipa faini ya pauni 65000. (£65,680).
Awali katibu mkuu wa Fifa Jerome Valcke alimtaka Suarez atafute matibabu ya kisaikolojia wakati akitumikia marufuku hiyo.
Hii si mara ya kwanza wala hata ya pili kwa Suarez kukabiliwa na kashfa kama hii ya kuwauma wapinzani wake , msimu uliopita alilazimika kukaa nje kwa mechi kumi baada ya kupatikana na hatia ya kumuuma mlinzi wa Chelsea Branislav Ivanovic Aprili 2013.
Suarez amuomba msamaha Chiellini kwa mara ya kwanza
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alirejea kwa kishindo na akaifungia Liverpool mabao 31 na kuisaidia kumaliza katika nafasi ya pili.
Suarez pia aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa 2013-2014 .

Nyota huyo wa Uruguay alipokelewa kwa shangwe vifijo na nderemo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Carrasco huko Montevideo aliporejea nyumbani kutoka Brazil.
BBC

WACHEZAJI WA UGIRIKI WAKATAA POSHO

Hatutaki marupurupu yetu
Huku timu za Afrika zikilazimika kusafirisha mamilioni ya Dola za Kimarekani hadi Brazil (Nigeria na Cameroon) ili kuzima migomo kabla ya mechi muhimu, timu ya Ugiriki ilifanya kinyume na hayo ilipokataa katakata kupokea malimbikizi ya marupurupu yao kutoka kwa serikali.
Timu hiyo iliyoondolewa na Costa Rica katika mkondo wa pili ilimwandikia waziri mkuu wa Ugiriki Antonis Samaras barua ikimtaka atumie fedha hizo kujenga uwanja mpya wa kandanda utakaotumika kutambua na kukuza vizazi vipya vya kandanda.
Ugiriki iliambulia kichapo cha mabao 5-3 kupitia mikwaju ya penalti mikononi mwa Costa Rica.

Bwana Samaras aliahidi kutekeleza ombi la wachezaji wake alipozungumza kwa njia ya simu na maafisa wa shirikisho la soka la Ugiriki.
BBC

CAMEROON YADAIWA KUPANGA MECHI RAZIL


Wachezaji wa Cameroon wakichapana katika mechi yao uwanjani

Maafisa wa Cameroon watapelelezwa kutokana na madai kwamba saba kati ya wachezaji wa timu ya taifa hilo walihusika katika kupanga mechi katika Kombe la Dunia linaloendelea nchini Brazil.
Kamati ya maadili ya shirikisho la kandanda la taifa hilo litachunguza shutuma za "udanganyifu" wa "wachezaji saba wabaya" katika mechi zao tatu za makundi.
Madai hayo yametolewa na gazeti moja la kijerumani na mtu aliyehukumiwa kwa kuhusika na kupanga mechi nchini Singapore.
Cameroon ilipoteza mechi zote za kundi A, ikiwemo ile waliolazwa na Croatia kwa mabao 4-0.
Mchezaji wa 'The Indomitable Lions' Alex Song, alionyeshwa kadi nyekundu kwa kumgota Mario Mandzukic mgongoni katika mechi hiyo, huku wachezaji wenzake Benoit Assou-Ekotto na Benjamin Moukandjo wakizozana baadaye katika mechi hiyo.
Ripoti kutoka katika shirikisho la kandanda la Cameroon lilisema: "Madai yaliyotolewa majuzi kuhusu udanganyifu katika mechi tatu za mwanzo za Cameroon katika Kombe la Dunia la 2014, hasa kati ya Cameroon na Croatia, na vile vile 'kuwepo na wacheza saba wabaya katika timu yetu ya taifa' hayaambatani na maadili na kanuni zinazopendekezwa na usimamizi wetu, pamoja na kanuni za Fifa na maadili ya taifa letu.
"Tuna nia kuu ya kutumia mbinu zote zinazostahili ili kutatua swala hili linalosumbua kwa muda mfupi iwezekanavyo."
'FIFA yataka uchunguzi wa wazi'
Fifa haikusema iwapo ilikuwa ikichunguza swala hilo au la, kwani bodi hiyo inayosimamia kandanda ulimwenguni "ilitaka uchunguzi uwe wazi".
Hata hivyo, iliongezea kuwa: "kwa ujumla, uadilifu katika mchezo huu ndio swala linalopewa kipaumbele na Fifa, kwa hivyo, tunatilia madai yoyote kuhusu udanganyifu maanani sana."
'Mgogoro wa marupurupu'
Matayarisho ya Cameroon kabla ya michezo hiyo nchini Brazil yalitatizika baada ya wachezaji kukataa kupanda ndege kuelekea Brazil hadi wakati mgogoro uliohusiana na wachezaji hao kulipwa marupurupu yao ulipotatuliwa.
Maelewano ya fedha hatimaye yalifikiwa na shirikisho la kandanda la Cameroon, Fecafoot, lakini safari ya kikosi hicho kuelekea Brazil ilikuwa imecheleweshwa kwa takriban siku nzima.
Walianza michezo hiyo kwa kushindwa kwa bao 1-0 na Mexico kabla ya kulazwa na Croatia na wenyeji Brazil waliowafunga mabao 4-1.
"Wachezaji kadhaa walikosa nidhamu, na ndio sababu tumefungwa mabao manne," mkufunzi wa Cameroon Volker Finke aliambia gazeti la kifaransa la L'Equipe baada ya kushindwa na Croatia.
"Ninajua ni vigumu kucheza na wachezaji kumi, lakini hilo si sababu ya kupoteza katika mkondo huu.
"Mechi ilikuwa sawa hadi tulipoonyeshwa kadi nyekundu. Wacroatia walifanya vizuri mbele ya lango lakini Cameroon pia ilikuwa na nafasi ya kufunga.
"Tabia ya wachezaji kadhaa kwa kweli sio nzuri. Hata tulipokuwa bado na wachezaji 11 kila upande, haikuwa ya kupendeza."

WATAKIWA KUTETEA PENSHENI KWA WAZEE BILA KUJALI ITIKADI ZA VYAMA


Na Mwandishi Wetu, brotherdanny5.blogspot


ARUSHA: VIONGOZI wa kisiasa hapa nchini wametakiwa kuweka itikadi za  vyama vyao pembeni kuhusu Pensheni kwa wazee na badala yake  kwa pamoja wawe na sauti moja ya kuwatetea wazee wa nchi ya Tanzania.
Endapo kama kila mbunge bila kujali itikadi ya chama chake atafanya hivuo ni wazi kuwa ahadi ya pensheni kwa wazee itatimia na nchi itaweza kuokoa maisha yao kwa urahisi sana.
Kauli hiyo imetolewa na Javes Sauni ambaye ni mratibu wa jukwaa la wazee kwa mkoa wa Arusha (JUWA) wakati akiongea na wadau wa jukwaa hilo mapema jana kuhusiana na umuhimu wa pensheni kwa wazee wa Tanzania.
Sauni alisema kuwa umefika wakati wa Serikali kuweza kuona kuwa wazee wanahitaji kwa haraka Penseheni zao lakini ili Serikali iweze kuwasikia ni lazima kwanza viongozi wa siasa wawe  na umoja juu ya suala hilo.
Alisema kuwa suala la kuangalia maslahi ya wazee kama Pensheni haliitaji itikadi ya chama chochcote kile cha siasa bali linahitaji umoja madhubuti kwa viongozi hasa Wabunge na Mawaziri.
“Wawakilishi wa wazee hawa ndio hao wanatakiwa kukumbuka hata katika bajeti ya 2012/2013 Serikali ilidai kuwa italiangalia suala hilo lakini mpaka sasa bado halijatekelezwa sasa wao wanatakiwa kumuhoji Waziri mwenye dhamana hiyo na kama watafanya hivyo watakuwa wametetea maslahi ya wazee wengi sana," alisema Sauni.
Wakati huo huo aliongeza kuwa kutokana na wazee kukosa uangalizi wa kutosha pamoja na pensheni kama zilivyo nchi ambazo zimeendelea duniani kumesababisha changamoto kubwa kwa kundi hilo.
Alitaja changamoto hizo ni kama vile vifo vya aibu ambavyo vinatokea kila wilaya na kila Kata kwa kila saa moja ingawaje serikali bado ina ina uwezo mkubwa sana wa kuwasaidia wazee hao.
“Kama kundi hili la wazee litapata Pensheni ya uhakika basi litaweza kuondokana na vifo vya aibua ambavyo vinawakumba wazee hawa kwa kuwa wakati wanahitaji kitu kama vile dawa huwa wanakosa hivyo wanajikuta wanakufa kabla ya siku zao,kwaiyo kama wakiwa na pensheni wataweza kusaidia kuondokana na vifo hivi vya aibu”alifafanua hivyo.

UKOSEFU WA VYOMBO VYA USAFIRI KWA WACHUNGAJI CHANZO CHA INJILI KUYUMBA, WAUMINI WAAMKA WACHANGA MILIONI 3 KWA AJILI YA UNUNUZI WA GARI


Na Mwandishi Wetu, brotherdanny5.blogspot

ARUSHA: IMEELEZWA kuwa kutokana na ukosefu wa vyombo vy ausafiri kwa wachungaji na viongozi mbalimbali wa makanisa wakati mwingine ndio chanzo kikubwa sana cha injili kutofika sehemu inapohitajika.
Pia ukosefu huo wakati mwingine husababisha hata huduma za kanisa kushindwa kutimia kwa wakati hali ambayo kwa sasa waumini wanatakiwa kuangalia vyombo muhimu ambavyo wachungaji wao wanatakiwa kuwa navyo ikiwemo suala zima la usafiri.
Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji Nkirwa Palangyo kutoka katika Kanisa la Pentekoste imani na matendo lilopo maeneo ya kisongo jijini Arusha wakati waumini hao wakifanya harambee maalumu ya kununua gari la mchungaji wao mapema wiki iliyopita.
Mchungaji Palangyo aliongeza kuwa chombo kama gari kina umuhimu mkubwa sana kwenye maendeleo ya kanisa lolote lile kwani linaweza kurahisisha kazi mbalimbali za huduma hivyo basi ni changamoto kubwa sana kwa waumini kuhakikisha kuwa wanaliangalia suala hilo kwa undani sana. 
Alisisitiza kuwa wakati mwingine Injili inashindwa kufikiwa kwa wakati maalumu tena hasa maeneo ya vijijini kwa kuwa hakuna usafiri wa kufika huko ila kama kukiwa na magari ya kufika huko ni raisi sana wengi kuweza kumpokea bwana Yesu.
"Kanisa kama kanisa likiwa na usafiri wake basi linaweza kueneza injili kwa haraka sana tofauti na sasa ambapo wakati mwingine tunatamani kufika mbali ila tunashindwa kwa kuwa hatuna usafiri ni vema kama waumini wenyewe sasa hata wa makanisa mengine wakajifunza hili na kisha wakaanza utaratibu wa kutafuta magari ya watumishi wao," aliongeza Mchungaji Palangyo.
Awali mgeni rasmi katika harambee hiyo ambayo iliwashirikisha Wakristo kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Arusha Isaya Sizya alisema kuwa Wakristo wengi wanashindwa kubarikiwa kwa kuwa wana mikono mifupi mbele za Bwana (wachoyo) na hivyo kila mara wanajikuta wakiwa wanabaki
maskini.
Sizya alidai kuwa wapo baadhi ya wakristo ambao kwa sasa wapo radhi waweze kuwekeza katika mambo ya dunia zaidi kama ili waweze kuonekana kwa ufarahari lakini kwenye michango ya makanisa wanakaa nyuma sana jambo ambalo sio sawa mbele za Mungu.
"tunatakiwa kujifunza kumtolea bwana sisi wakristo na tuhakikishe kuwa kwenyemichango ya makanisa tunakuwa mstari wa mbele tusibaki nyuma na kisha kuona mambo ya dunia ndio muhimu kwa kweli tutakuwa tunajiharibu sisi wenyewe ni lazima tubadilike sana kwenye hili na tuangalie mahitaji muhimu ya wachungaji wetu;aliongeza Sizya.
Katika harambee hiyo kiasi cha zaidi ya Milioni tatu kiliweza kupatikana kwa ajili ya awamu ya kwanza ya ununuzi wa gari la mchungaji wa kanisa hilo la Pentekoste imani na Matendo.

'WATIENI MOYO WALIOFELI KIDATO CHA NNE'


Na Mwandishi Wetu, brotherdanny5.blogspot

ARUSHA: SERIKALI imetakiwa kuweka utaratibu maalumu wa kuhakikisha kuwa haiwatupi wanafunzi waliofeli kidato cha nne na badala yake wanawatafutia njia mbadala ikiwa ni pamoja na kuwakusanya tena kwa mara nyingine na kuwapa maarifa mapya.
Endapo kama Serikali itafanya hivyo basi taifa la Tanzania litaweza kupunguza idadi ya wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na kidato cha tano na sita ambacho nacho ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa shule ya msingi na sekondari ya Arusha Modern, Philiph Wasike wakati akiongea na wanafunzi wazazi na walezi kwenye maafali ya 12 ya kidato cha nne shule hiyo ambayo yalifanyika juzi jijini hapa.
Wasike alisema kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi ambao wanafeli kidato cha nne wanaonekana kama hawana maana tena mbele za jamii wakati kuna sababu mbalimbali ambazo zinapelekea wanafunzi hao kufeli.
Alifafanua kuwa sababu hizo zinatakiwa ziweze kuangaliwa lakini pia serikali itunge utaratibu maalumu wa kuwakusanya walioshindwa mthiani na kisha kuwapa hata nasaha ambazo zitaweza kuwafanya wasikate tamaa.
"Kufeli kidato cha nne sio kufeli maisha bali sisi kama jamii lakini pia sisi kama Serikali tunatakiwa kuwaonesha upendo wanafunzi hawa na mwanafunzi ambaye ana moyo wa kuendelea huwa anajionesha tu na kama tukifanya hivi idadi ya wasomi wa vyuo vikuu itaongezeka maradufu tofauti na sasa ambapo idadi ya wasomi wa vyuo vikuu hapa nchini bado hairidhishi hata kidogo," aliongeza Wasike.
Kutokana na hilo alisema kuwa shule yake tayari imeshaweka utaratibu wa kuwatia moyo wale ambao wamefeli kidato cha nne ambapo wanapewa mafunzo maalumu kwa ajili ya kufanya vema zaidi mthiani wa taifa jambo ambalo wamefanikiwa kwa kiwango cha juu sana.
"Hawa wanafunzi ambao sisi tumeanza nao toka mwaka 2011 kwa kweli wamefanya vizuri sana na wamepata alama za juu sana kwenye mthiani yao ya taifa sasa huu mpango mimi naweza kusema kuwa unaweza kuwasaidia walio wengi kama utaigwa ila hata wakitumia  shule yetu sisi tupo tayari kuwalea hawa ambao wamefeli kidato cha nne na wakaenda kidato cha tano tena kwa raha sana"aliongeza Wasike.
Alihitimisha kwa kusema kuwa bado shule hiyo inaendelea na mikakati mbalimbali ya kuweza kuhakikisha inapandisha elimu ya Tanzania ili iweze kufika katika viwango vya kimataifa kama zilivyo nchi
zilizoendelea.

MIRERANI KUUNDA MFUKO WA POLISI JAMII


Na Mwandishi Wetu, brotherdanny5.blogspot

MANYARA: KAMATI ya maendeleo ya Kata ya Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, imeazimia kuanzisha mfuko wa kusaidia polisi jamii wa kata hiyo kwa lengo la kuwawezesha ili wafanye kazi zao ipasavyo katika ulinzi shirikishi.
Diwani wa kata ya Mirerani, Justin Nyari akizungumza juzi mbele ya Mkuu wa kituo cha polisi Mirerani, ASP Lwitiko Kibanda, alisema wanatarajia kuomba kibali kwa Mkuu wa wilaya hiyo ili kuchangisha fedha za kutunisha mfuko huo.
“Tunatarajia kuanzisha mfuko huu baada ya OSC wa Mirerani kuleta wazo hili na sisi tuthamini kazi za polisi jamii katika kata yetu, kwani wamekuwa msaada mkubwa kwa wananchi katika kupambana na uhalifu,” alisema Nyari.
Alisema mfuko wa polisi jamii na ulinzi shirikishi utawasaidia kuwapa morali ya kufanya kazi kwa juhudi zaidi tofauti na hivi sasa ambapo hawapati kifuta jasho ili hali wanafanya kazi nzuri za kusaidia wananchi kwenye suala la ulinzi.
Naye, Mkuu wa kituo cha polisi Mirerani, Mrakibu Msaidizi wa polisi, Lwitiko Kibanda alitoa shukurani kwa uongozi wa kata hiyo kujali na kuthamini jitihada za polisi jamii wa eneo hilo, ambao wamekuwa msaada mkubwa kwa polisi.
“Tumekuwa tukiwapa mafunzo polisi jamii zaidi ya 30 hapa kituoni na wamekuwa wakitusaidia katika shughuli za ulinzi na usalama hapa Mirerani, ila tatizo ni namna ya kuwawezesha kwani sisi hatuna fungu hilo,” alisema Kibanda.
Alisema dhana ya ulinzi shirikishi na polisi jamii ilianzishwa na jeshi la polisi baada ya kuona kuwa watakuwa msaada kwa askari kutokana na idadi ndogo ya polisi waliopo nchini hivyo watashirikiana nao kuhakikisha usalama unakuwepo.

MALUMBANO YA KISIASA CHANZO CHA KUYUMBA KWA UCHUMI WA TANZANIA


Na Mwandishi Wetu, brotherdanny5.blogspot


ARUSHA: IMEELEZWA kuwa endapo kama nchi ya Tanzania itaendelea kujikita katika majibizano ya kisiasa zaidi basi nchi uchumi wa nchi utaendelea kuyumba hali ambayo itasababisha pia maendeleo kuwa duni.
Kwa sasa katika vyombo vya habari kitu kikubwa kinachosikika ni majibizano ya kisiasa na wala sio ya maendeleo sasa kama nchi itaendelea hivi baada ya miaka michache ni wazi kuwa bado umaskini utatawala sana.
Kauli hiyo imetolewa na askofu wa kanisa la International Evangelism Dkt Eliud Isangya,lililopo Sakila wilayani Meru wakati akiongea na wanafunzi, walimu na walezi wa chuo  hicho kwenye maafali ya 63 ya chuo hicho  yaliyofanyika jumamosi iliyopita.
Dkt Isangya alisema kuwa haipendezi sana kuona kuwa nchi inajibizana kwenye siasa na kuacha masuala ya msingi ambayo yanagusa tija za wananchi na hivyo sasa wana siasa wanatakiwa kujiangalia kwenye hilo.
"Unakuta wakati mwingine muda wa majibizano ya kisiasa ni makubwa sana kuliko yale ya maendeleo sasa hali hiin inatupa wakati mgumu sana sisi kama viongozi wa dini hawa wanasiasa wanatakiwa kubadilika na kuachana na hilo," aliongeza Dkt Isangya.
Pia alisema kuwa Nchi ya Tanzania bado inakabiliwa na changamoto kubwa sana kwani asilimia kubwa ya mahitaji yake bado hayajaweza kutekelezwa hivyo wanasiasa wanatakiwa kutumia muda huo huo katika kutafuta ufumbuzi wa hayo yote.
Alisisitiza kuwa kama watafanya hivyo basi hata uchumi wa nchi ya Tanzania utaweza kubadilika kwa kiwango cha juu sana tofauti na sasa ambapo nguvu kubwa sana imeelekezwa kwenye majibizano lakini hata bajeti kubwa kwa ajili ya kujibu hoja za kisiasa tofauti na hoja zile za maendeleo ya wananchi.
Nao wahitimu wa chuo hicho walisema kuwa pamoja na kuwa wameweza kupata elimu bora lakini kuna umuhimu mkubwa sana wa Serikali kuangalia changamoto ambazo wanazipata hasa za miundo mbinu kwani wakati mwingine zinasababisha mvutano mkubwa sana.
"pamoja na kuwa hapa tumepewa elimu bure kabisa na hata elimu za kijamii lakini kama barabara kutoka  kikatiti ingekuwa nzuri basi tungefurai zaidi kwa sasa hii barabara inatupa wakati mgumu sana na sisi tungepata elimu wengi zaidi basi nchi ingekuwa na mabadiliko ya kutosha"waliongeza wahitimu hao.

FISI, NYOKA MKUBWA WAJISALIMISHA KWA WANANCHI


Na Mwandishi Wetu, brotherdanny5.blogspot

ARUSHA: KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida wananchi zaidi 300 wamelazimika kumuuua mnyama pori aina ya fisi pamoja na nyoka wa msituni ambaye alikuwa anafugwa kwa imani za kishirikina.
Aidha tukio hilo limetokea wiki iliyopita katika eneo la Kibaoni Kata ya Kingori ambapo wanyama hao walitoka ndanikwa mkazi mmmoja wa eneo hilo mara baada ya kufanyika kwa maombi yaliyowakuitanisha wakazi wa mji wa Kibaoni.
Akiongelea tukio hilo Nabii ambaye amesababisha wanayama hao kutoka ndani walipokuwa wanafugwa, nabii Felix Ole Mpoke alidai kuwa yeye alikuwa kwenye utaratibu wake wa kawaida wa maombi lakini wakati anaomba aliita wanawake kwa ajili ya maombezi kwani wanawake kwa sasa wanakabiliwa na changamoto nyingi sana ikiwemo suala zima la utandawazi.
Alisema, wakati wanawake hao wanakuja kuombewa ndipo familia moja(jinalinahifadhiwa)ilikuja kwa kuwa walikuwa wanasumbuliwa na matatizo ya muda mrefu hivyo waliitaji nguvu na msaada wa mungu zaidi.
Aliongeza kuwa wakati maombezi hayo yakiwa yanaendelea ghafla Fisi ambaye kawaida yake huishi porini alitoka ndani ya nyumba moja ambayo na kukimbia ovyo katika eneo ambalo mkutano wa injili ulikuwa unaendelea hali ambayo ilizua tafrani kubwa sana .
“Maombi yakiwa yanaendelea dhidi ya familia ile kilichotokea ni kuwa fisi alichomoka ndani na kuja katika eneo la mkutano ambalo tulikuwepo na watu kwa kweli wengi wao walikimbia na kuona kama kitu cha ajabu sana," aliongeza Felix.
Wakati huo huo alidai kuwa wakati fisi huyo akiwa anatembeatembea katika eneo hilo pia ghafla naye nyoka ambaye asili yake ni porini naye alitoka ndani humo huku akiwa anamfuta fisi huyo ambaye anasadikika kuwa alikuwa wanaishi pamoja bila familia kujua ingawaje alikuwa anamilikiwa na baba wa familia hiyo .
Alisema kuwa wananchi wenye hasira kali walilazimika kuhoji maswali familia hiyo ambapo utafiti uliweza kubaini kuwa mama pamoja na watoto wa familia hiyo walikuwa hawajui kinachoendelea juu ya  umiliki wa wanyama hao ambapo utafiti uliweza kubaini kuwa ilikuwamali ya baba wa familia ambaye muda mfupi alitoroka mahali ambapo hapajulikana mpaka sasa.
Alibainisha kuwa baada ya hapo watu walillazimika kumburuta fisi huyo ambaye alikuwa na nyoka mkubwa sana mpaka maeneo ya madhabahu ya kanisa hilo ambapo waliweza kuwacbhoma moto hadi kuteketea
Hataivyo wananchi walioweza kuongea nawaandishi wa habari ambao walidhuru maeneo hayo ya kibaoni walisema kuwa ushirikina ndio chanzo kikubwa cha maendeleo kufifia katika eneo hilo ingawa linakaribiana na uwanja wa ndege wa kimataifa(KIA)hivyo jitiada za kupambana na ushirikina zinahitajika zaidi.

KUMEKUCHA TENA...BAADA YA MAFUTA, GESI, SASA MAGADI SODA KUANZA KUVUNWA


Na Mwandishi Wetu, brotherdanny5.blogspot

MONDULI: BAADA ya rasilimali ya Gas kuanza kuchimbwa mkoani Mtwara na kuinufaisha nchi, sasa neema nyingine tena ya uwekezaji mkubwa wa kiwanda cha magadi soda imewajia Watanzania.
Neema hiyo inatokana na Tanzania kuwa nchi ya pili kwa uzalishaji mkubwa wa magadi soda duniani yatakayoiingizia nchi Dola za Marekani milioni 300 kwa mwaka sawa na Sh.bilioni 480, fedha hizo zitatokana na mauzo ya zaidi ya tani milioni moja kwa mwaka.
Tayari utafiti umekamilika na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) limewataka wananchi wa Kata ya Engaruka wilayani Monduli mkoani Arusha kitakapojengwa kiwanda hicho kujiandaa.
Akizungumza kwenye mkutano mkuu maalum wa Kijiji cha Engaruka, Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa NDC Abel Ngapemba alisema, magadi soda hayo yatavunwa kwa miaka 500 ijayo bila kuisha.
Alisema hadi ifikapo Desemba mwaka huu NDC itakuwa imekamilisha taratibu za namna ya kuanza kuvuna madini hayo bila ya kuathiri mazingira yaliyopo eneo husika.
“Mradi ni wa Serikali umepitia hatua zote zinazohusika ili kujiridhisha kwamba hakuna mazingira yatakayoathirika na ndio maana tupo hapa kuwashirikisha na kuwataka mjiandae kwa kuwekena nyinyi.
“Kwa hiyo kinachofanyika sasa hivi ni kuangalia vyanzo vya maji kwa ajili ya kuleta maji katika eneo hili la mradi ambapo tunaamini maji hayo yatawanufaisha,” alisema Ngapemba.
Alisema kukamilika kwa Kiwanda hicho kunatarajiwa kuajiri zadi ya watu 1,000 watakaokuwa wakifanya kazi kiwandani tu aachilia mbali idara na maeneo mengine ambayo yatahitaji wananchi wa eneo la Engaruka kushiriki.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga akizungumza na wananchi hao aliwaambia kwamba kazi yoyote ya maendeleo ya kiuchumi siku zote huwa inahusisha vita.
Alisema Serikali imeona ni vyema kuanza kuzungumza na wananchi kwa kuwapatia elimu ya jinsi ya kujiandaa na kunufaika na ujio wa uwekezaji huo badala ya kukaa pembeni na kujiona kama si mradi wao.
“Kinachowaogopesha jirani zetu ni ukubwa wa mradi kwani tukianza uzalishaji hakuna nchi itakayotufikia ndio maana kelele za kututaka tusifanye mradi huu ni nyingi.
“Na wataalamu wamethibitisha kwamba hapa Engaruka kuna magadi soda mazuri zaidi kuliko yanayopatikana kwingine sas abasi katika mazingira kama hayo jirani yako hawezi kukupenda,” alisema DC Kasunga.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli Twalib Mbasha alitumia fursa hiyo kuwaelimisha wananchi wa vijiji vya Engaruka Juu na Engaruka Chini namna wanavyotakiwa kujipanga ili kunufaika na
uwekezaji huo.
“Tumeshakubaliana suala hili katika vikao vya madiwani na suala la kupima ardhi ya kijiji tumeliweka kwenye mpango wetu wa mwaka 2014 na 2015. Lakini pia tunatengeneza sheria ndogo zitakazo tawala mradi huu,” alisema Mbasha.
Katika mkutano huo wakuu wa Idara za Mifugo na Uvuvi, Idara ya Maendeleo ya Jamii, Usalama wa Raia na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji ya Baraza la Madiwa waliwaelezea wananchi jinsi ya kubadilisha shughuli za sasa kwa kuziboresha ili wanufaike na ujio wa watu wengi.

UFARANSA NA UJERUMANI ROBO FAINALI

Ufaransa 2-0 Nigeria
Ufaransa imefuzu kwa mkondo wa robo fainali ya kombe la dunia baada ya kuilaza Super Eagles ya Nigeria mabao 2-0 katika mechi iliyochezwa Brasilia.
Paul Pogba ndiye aliyeifungia Ufaransa bao la kwanza kunako dakika ya 79 ya mechi hiyo kupitia kichwa baada ya kipa wa Nigeria Vincent Enyeama kuutema mpira wa kona na kumtnuku Pogba na fursa ya kuwaweka vijana wa Didier Deschamps mbele.
Maji yalizidi unga kwa Nigeria ,Dakika chache baadaye Joseph Yobo alipojifunga mwenyewe kufuatia shinikizo la wafaransa Griezmann baada ya Peter Odemwinge kugonga mpira nje na ukawa kona ambayo safu ya ulinzi ilishindwa kuhimili.Nigeria itajilaumu yenewe kwa bao hilo kutokana na makosa ya kimsingi ya safu ya ulinzi ambayo haikumakinika katika dakika za mwishomwisho ya mechi hiyo.
Ufaransa sasa itachuana na Ujerumani katika robo fainali ya kombe la dunia
Kufuatia ushindi huo Ufaransa ilijikatia tikiti ya moja kwa moja hadi kwenye mkondo ujao wa robo fainali ya kombe la dunia ambapo sasa imeratibiwa kuchuana dhidi ya Ujerumani.
Vile vile kuondolewa kwa mabingwa hao wa Afrika sasa kumeiacha bara zima la Afrika bila ya mwakilishi katika mkondo ujao wa robo fainali baada ya Algeria kufurushwa na Ujerumani katika mechi nyengine 2-1.
Ujerumani ilipata mwaliko huo wa robo fainali baada ya kuibana mwakilishi mwengine wa Afrika Algeria ,mabao 2-1 katika mechi iliyoishia katika mmuda wa ziada .

Mechi hiyo ilikuwa imekamilika suluhu bin suluhu katika muda wa kawaida.
BBC

MAREKANI KUONGEZA VIKOSI 200 IRAQ

Obama kupeleka pia ndege za kivita zisizo na rubani 'drones' huko Baghdad

Rais Barak Obama ametangaza kuwa anatuma vikosi 200 zaidi , na pia helikopta zisizoKuwa na ruban nchini Iraq.
Katika barua yake wa baraza la Cogress rais Obama amesema kuwa vikosi hivyo vitatoa msaada wa nyongeza na usala kwa ubalozi mjini Baghdad.
Wataungana na wanajeshi wengine wa Marekani walioko Badghad wanaolinda ubalozi wa Marekani.Rais Obama amesema vikosi hivyo vya ziada vimepewa mafunzo kabambe ya kijeshi na majukumu yao makuu yatakuwa kuwalinda raia wa Marekani na mali zao huko Iraq.
Katika barua yake kwa bunge la Congress, Obama amaesema amepeleka pia helicopters,na ndege zisizo na rubani kuimarisha ulinzi huo.
Tayari Marekani washapeleka washauri wakijeshi wapatao 180 kufanya kazi na jeshi la Iraq.
Hata hivyo idadi ya jumla ya wanajeshi wa Marekani nchini Iraq ni kama 750 pekee.
Huku mapigano yakiendelea kuchacha huko Iraq rais Obama amesisitiza hatapeleka majeshi ya ardhini nchini lakini hatua ya kufanya mashambulizi ya angani dhidi ya kundi la wapiganaji wa ISIS huenda ikachukuliwa.
Wakati huohuo Balozi wa Saudi Arabia katika umoja wa mataifa amekana madai ya Waziri mkuu wa Iraq , Nouri Maliki kwamba nchi yake inatoa usidizi wowote kwa kundi la ISIS na pia kupinga nadharia kuwa usaidizi wa Saudia kwa waasi wa Syriaumechangia kuliinua kundi hilo la ISIS.
Tangazo la kundi hilo la ISIS hapo jana kwamba wataunganisha ardhi walizoziteka huko Iraq na Syria ndio waunde eneo moja wanalolitaja kama 'Islamic Caliphate' litakalotawaliwa na sheria kali za kiislamu, liwawatia tumbo joto mataifa mengi ya mashariki ya kati na mataifa ya kizungu hasa Marekani.
Kwa kipindi cha mda mfupi ISIS imeweza kushambulia na kuyateka maeneo makubwa kwa kasi iliyowashangaza wengi huku serikali za nchi husika zikishindwa kukabiliana nao.

Kuzuka kwa kundi hili kunaleta tisho jipya katika mashariki ya kati ambayo tayari inayumbishwa na vita na vizozo mbalimbali ya kisiasa.
BBC

SOKWE RWANDA KUPEWA MAJINA LEO!

Sokwe

Kwa kawaida Mtoto anapozaliwa katika familia yake huwa inaandaliwa sherehe ya kumpa jina .
Hata hivyo si jambo la kawaida katika tamaduni nyingi hasa za kiafrika kuandaa sherehe za kuwapa majina wanyama. Lakini nchini Rwanda leo zinatarajiwa sherehe kubwa ya kuwapa majina watoto wa sokwe wa milimani.
Sokwe hao ni kutoka mbuga ya wanyama ya Volcano kaskazini mwa taifa hilo. Sekta ya utalii hasa sokwe wa milimani ni ya kwanza kuingizia Rwanda fedha za kigeni.
Tukio la hilo la kuwapatia majina watoto wa Sokwe maarufu kama'' Kwita izina'' limeendela kupata umaarufu ambapo huhudhuriwa na wadau mbali mbali maarufu wa hifadhi ya wanyama pori kutoka nchi mbali mbali duniani.
BBCSWAHILI

ISRAEL YASEMA HAMAS ILIWAUA VIJANA WAKE

Vijana wa Israel waliokutwa wameuawa

Msemaji wa jeshi la Israel amesema kuwa miili hiyo ilikuwa chini ya miamba iliopo kwenye mji wa west Bank wa Hebron.
Israel imepeleka vikosi vyake katika kijiji cha Palestina cha Hal-hul.
Netanyahu amelilaumu kundi la Wapalestina la Hamas, na akaahidi kulipiza kisasi.Katika kikao cha dharura cha mawaziri ,waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema vijana hao walitekwa na kuuawa katika mauji aliyosema yamefanywa na wanyama.
Benjamini Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Hamas imekana kuhusika na mauaji hayo kupitia mshauri rasmi wa rais wa Palestina Mahmoud Abbas -Abdallah Abdallah.

Mwandishi wa BBC aliyeko mashariki ya kati anasema milio ya mashambulizi ya ndege za Israeli imesikika kote katika ukanda wa Gaza .
Kulikuwa na tetesi kuwa Israeli ingeileng maeneo ya Hamas baada ya kikao chake cha mawaziri cha usalama .
Mji wa Gaza umesalia kuwa ngome kuu ya Hamas na ofisi zake katika eneo hilo zimekuwa zikivamiwa katika kipindi cha zaidi ya wiki mbili na nusu.

vifo vya karibu wapalestina watano vimeripotiwa na mamia ya wapalestina wamekamatwa.
BBCSWAHILI

TIMU ZA AFRIKA ZANG'OLEWA BRAZIL

Algeria ilifanikiwa kuingiza bao moja la kufuta machozi dhidi ya Ujerumani

Timu mbili za mwisho za Afrika katika kombe la dunia zimendoka dimbani baada ya kushindwa katika awamu ya timu bora kumi na sita.
Nigeria walicharazwa na Ufaransa mbili bila huku Algeria ikiangushwa na Ujerumani mabao mawili kwa moja katika muda wa ziada.
Algeria na Nigeria walijitahidi kadri ya uwezo wao kuingia katika awamu ya robo fainali ingawa mambo yalikuwa magumu.Ilikuwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika kwa timu mbili kufika awamu ya kumi na sita bora katika kombe la dunia.
Nigeria ilichapwa mabapo mawili bila na Ufaransa
Timu hizo mbili zilionyeshwa mlango baada ya kutofanya vyema. Algeria waliwapa wakati mgumu wachezaji wa Ujerumani ingawa mabao ndiyo yalikataa kuingia.
Katika muda wa ziada walichapwa mabo mawili ingawa walifanikiwa kuingiza bao moja kabla ya muda kumalizika. Matumaini ya kusonga mbele yakaisha.

Katika mechi yao, mabingwa wa Afrika, Nigeria walikula kichapo cha mabao mawili bila dhidi ya Ufaransa na baada ya mechi kumalizika, kocha wa timu yao Stephen Keshi akajiuzulu.
BBCSWAHILI

KITUO CHA BOKO HARAM CHASHAMBULIWA

Jeshi la Nigeria limesema kuwa limekishambulia kituo cha ujasusi cha wapiganaji wa Boko Haram kinachodaiwa kuhusika na utekaji wa wasichana zaidi ya 200 nchini humo.
Hata hivyo taarifa za jeshi hilo zinasema kuwa kiongozi wa kituo hicho cha Boko Haram Babuji Ya'ari amekamatwa.
Ya'ari pamoja na kutuhumiwa kuhusika katika utekaji wa wasichana hao lakini pia alihusika katika mauaji ya kiongozi wa kijadi wa Gwoza, imebainisha taarifa ya serikali.
Jishi hilo pia limegundua kuwa Ya'ari aliyekuwa mfanya biashara alikuwa akijifanya ni mwanaharakati katika kutokomeza kundi la Boko Haram ili kupata nafasi ya kuchunguza harakati za jeshi la Nigeria na mipango dhidi ya kundi hilo la kigaidi.
Anatuhumiwa kuhusika katika maandalizi ya mashambulio kadhaa likiwemo lile lililotokea Maiduguri na makao makuu ya mji wa Borno mwaka 2011.
BBCSWAHILI