Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 1 May 2014

VYAMA VYA WAFANYAKAZI VISAIDIE WAFANYAKAZI




Kumekuwa na vyama vingi vya wafanyakazi, lakini kero za wafanyakazi bado zinaendelea kuwapo.
Kwa mfano kuna vyama vya wafanyakazi vyenye lengo la kutetea walimu, hata hivyo bado walimu wengi wanaendelea kuteseka.
Hivi karibuni nilikuwa nazungumza na mwalimu mmoja, anasema anashindwa kuelewa maana hasa ya kuwapo kwa vyama vya wafanyakazi.
Hoja hiyo inaungwa mkono na mwalimu wa Shule ya Sekondari Mbalizi ambaye hakutaka kutajwa jina lake huku akifafanua kwamba kama kweli Chama cha Wafanyakazi (CWT) ingekuwa ni kwa ajili ya wafanyakazi ingefungua kesi kudai madeni ya walimu.
Mwalimu huyo anasema pamoja na kwamba CWT inaongoza kwa kukusanya fedha za wanachama wake, walimu wanaongoza kwa kukopa na kuishi kwenye mazingira magumu zaidi nchini.
Imefikia hatua baadhi ya wafanyakazi wanaona kama vyama vya wafanyakazi vipo kwa ajili ya matumbo yao.
Mfanyakazi wa kampuni ya usafirishaji, Juma Hamisi anasema pamoja na kuwapo kwa chama chao cha Cotwu, lakini waajiri wanawakandamiza wafanyakazi.
Anasema madereva wamekuwa wakipewa Sh20,000 za posho ya safari ya kwenda kulala nje ya kituo cha kazi, je hiyo ni haki?
Pamoja na hoja hizo, Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Elimu ya Juu, Utafiti na Kazi zinginezo (Raawu), Kanda ya Nyanda za Juu, Joseph Sayo anasema wafanyakazi wengi wamefaidi matunda ya kazi za vyama vya wafanyakazi.
Anataja moja ya faida kuwa ni Serikali kuondoa kodi kwa mishahara ya kima cha chini na pia kupunguza walau asilimia moja ya kodi kwa mishahara mingine yote.
Hata hivyo, anasema pamoja na faida hizo ukweli ni kwamba wafanyakazi wengi hawajajiunga kwenye vyama vya wafanyakazi.
Anasema vyama vya wafanyakazi vimefanya mambo mengi mazuri, yakiwamo ya kutetea sheria za kazi zirekebishwe na pia vyama vinasaidia kuendesha kesi nyingi za wafanyakazi.
Mwenyekiti wa Tucta Mkoa wa Mbeya, Alinanuswe Mwakapala anakiri kwamba wafanyakazi wengi wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha nyumbani na hata ya kazini.
Mwakapala anasema mazingira ya wafanyakazi maeneo ya kazi ni mabaya na kwamba waajiri hawataki kutekeleza baadhi ya sheria na hata makubaliano yanayofikiwa.
Anasema sababu za waajiri kuwa na dharau ni kutokana na sauti ndogo ya wafanyakazi inayosikika kutokana na kutojiunga kwenye vyama vya wafanyakazi.
Tanzania inakadiriwa kuwa na wafanyakazi karibu milioni 2, lakini wanachama wa vyama vya wafanyakazi ni asilimia 20 tu.
Hiyo ni sawa na kusema wafanyakazi 400,000 ndiyo wanaopiga kelele wakati wengine milioni 1.6 wamefumba midomo.
Pamoja na sheria kuruhusu kila mfanyakazi kuwa kwenye vyama vya wafanyakazi, watumishi hawana ari ya kujiunga na vyama vya wafanyakazi jambo ambalo ni tofauti na nchi zingine.
Wafanyakazi wa Afrika Kusini asilimia 100 ya wafanyakazi ni wanachama wa vyama vya wafanyakazi na huko Kenya wanachama ni asilimia 80 ya wote.
Katika nchi kama hizo wafanyakazi wana nguvu, umoja, mshikamano wa kweli,’’ anasisitiza.
Ushauri wangu ni kwamba vyama viendelee na jitihada za kuharakisha maendeleo ya wafanyakazi, pia wafanyakazi wajiunge kwenye vyama ili kuunganisha nguvu zao.
CHANZO, MWANANCHI




TUCTA IMEITAKA SERIKALI KUTOKA TAMKO KUHUSU MUSTAKABALI WA ELIMU NCHINI

Nicholaus-Mgaya

Katibu mkuu wa Tucta Bw. Nicolous Mgaya (Kushoto) akitoa hoja mbele ya waandishi wa habari

Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania(Tucta)limeitaka serikali kutoka tamko kuhusu mustakabali wa elimu nchini baada ya kujitokeza kwa kauli mbili tofauti zinazowachanganya wananchi
Akizungumza Jijini Dar es Salaam,Katibu Mkuu wa Tucta,Nicolaus Mgaya alisema kuwa, kujitokeza kwa kauli hizo mbili tofauti kunaonyesha wazi kuwa, serikali imeshindwa kujipanga wakati wa kutekeleza majukumu yake, jambo ambalo linawafanya kutoa kauli zinazokinzana.
“Kitendo cha serikali kutoa kauli mbili tofauti katika suala nyeti la elimu kunaonyesha wazi kuwa wameshindwa kujipanga,hivyo basi wanaweza kuiangamiza elimu kwa vijana wetu,”alisema Mgaya.
Alisema kuwa, hali ya elimu nchini ni mbaya ikilinganishwa na kipindi kilichopita,jambo ambalo linasababisha kuongezeka kwa idadi ya wananchi wanaoshindwa kufanya vizuri kwenye mitihani yao ya mwisho.
Alisema kuwa,hakuna nchi yoyote duniani ambayo itatoa matokeo ya mwisho ya wananchi bila ya kuwepo kwa waliofaulu na waliofeli,kwa sababu matokeo hayo yanaleta changamoto kwa wanafunzi waliofanya vibaya kujituma zaidi ili waweze kufanya vizuri kwenye mitihani inayofuata.
Kwa mujibu wa Mgaya,kutokana na hali hiyo, serikali ilipaswa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo wa elimu ili kujadili mustakabali wa elimu,hasa katika Nyanja ya walipotoka na waendako, jambo ambalo lingeweza kusaidia kupata maoni ambayo yanatoweza kuboreshwa na kuleta mabadiliko katika sekta hiyo.
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo, maoni hayo wangeweza kuwa mwongozo mpya ambao ukitumiwa vizuri utaweza kuwasaidia wanafunzi kufanya vizuri kwenye mitihani yao.
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo,wananchi wangeweza kuona utofauti wa hali halisi ya elimu kwa vijana wao,jambo ambalo lingeweza kuleta maendeleo.
Alisema kuwa, kutokana na hali hiyo, wanapaswa kujifunza kwa yale yaliyotokea na kuanza mchakato wa kushirikisha wadau ili waweze kuleta mapinduzi katika sekta ya elimu ambayo itasaidia uboreshaji wake katika Nyanja mbalimbali ya sekta hiyo.
CHANZO, PT BLOG

VIJANA KATAVI WAPATIWA ARDHI BURE KUPAMBANA NA UMASIKINI

???????????????????????????????
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda,  Paza mwamlima akionesha eneo ambalo linagawiwa kwa vijana na kujihakikishia zoezi linafanikiwa 
???????????????????????????????
Wazazi wa watoto waliogawiwa ardhi wakiwa katika picha ya pamoja wakinyosha mikono juu  na kupongezi zoezi hilo.

(Picha zote na Kibada wa Kibada –Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Mpanda)
………………………………………………………..
Na Kibada Kibada, Mpanda Katavi
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda,  Paza Mwamlima  amezindua zoezi la ugawaji ardhi kwa  vijana  wasiokuwa na ardhi Wilayani humo ili iweze kuwasaidia katika shughuli za uzalishaji kuliko kukaa kijiweni na kufanya shughuli zizokuwa na tija na kujiingiza katika vitengo vya uhalifu.
Uzinduzi huo umefanyika kwenye kitongoji cha Sijonga kilichoko Kijiji cha Kabungu Tarafa ya Kabungu wilayani Mpanda na ni zoezi litakaloendelea katika maeneo yote ya Wilaya ya Mpanda ili kuhakikisha vijana wasiokuwa na ardhi wanapatiwa ardhi na wazazi wao .
Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa jumla ya vijana ni 262 kutoka katika Kata za Mwesevijana 42, Mpanda ndogo vijana 50, Karema vijana 82, na Kata ya Kabungu wapo vijana 90.
Katika ugawaji huo kila kijana atapatiwa kuanzia ekari tatu na kuendelea kulingana na eneo alilokuwa anamiliki mzazi wake na limekaa tu bila kutumiwa.
Akifafanua zaidi alieleza kuwa Mkoa wa Katavi ni moja ya Mikoa iliyojaliwa kuwa na fursa za kila aina,  ardhi ya kutosha yenye rutuba, madini,maziwa, misitu minene,  mbuga ya wanyama lakini ni Mkoa ambao wananchi wake ni masikini sana wakati kuna kila kitu cha kuwawezesha kuwa matajiri.
“Hakuna sababu yeyote ya Mwananchi wa Mpanda na Mkoa wa Katavi kuwa masikini,  ardhi nzuri tunayo, tuitumie. Tunapokuwa masikini wakati ardhi tunayo mungu anachukia”. Alisema Mkuu wa Wilaya Mwamlima.
Awali Kaimu Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kagwira  Zamda Mheka  ambaye  pia ni Afisa Ugani wa kijiji hicho alieleza kuwa katika kijiji chake  vijana 90 wamegawiwa mashamba kutoka katika vitongoji vinavyounda kijiji cha Kabungu na Kitongoji cha Sijonga.
Hata hivyo  pamoja na kufanikiwa kwa zoezi hilo zipo changamoto kadha zilizojitokeza kutoka kwa baaadhi ya wazazi kusema kuwa kugawa ardhi wakati bado wako hai na ni sawa na kujitangazia kifo .
CHANZO,FULL SHANGWE 

WALCOTT: KUSHINDA FA KUTATUPA `MZUKA` ZAIDI WA MAKOMBE



                                                                     Theo Walcott


WINGA hatari wa Asernal, Theo Walcott anaamini kushinda taji la FA itakuwa kichocheo cha kushinda mataji mengi misimu ijayo.

Imepita miaka 9 sasa tangu Arsene Wenger abebe `ndoo` ambapo kwa mara ya mwisho aliifunga Manchester United kwa penati na kutwaa kombe la FA mwaka 2005.

Asernal wanayo fursa ya kufuta ukame huu watakapokutana na Hull City katika mechi ya fainali ya FA mei 17 mwaka huu na Walcott anaamini wakishinda italeta upepo mpya Emirates.

“Kama tutashinda FA kwa kuzingatia jinsi tunavyocheza sasa, wachezaji watakuwa na hamu ya makombe zaidi. Walcott ameiambia Tovuti ya Asernal.

“Nadhani kombe la kwanza ni muhimu- ukishinda, utashinda mengi zaidi. Nina uhakika na hilo”.

“Itakuwa heshima kwa bosi wetu kushinda kombe tena”.

“Ametuami kwa miaka yote. Kama hatuchezi vizuri, siku zote ananyoshewa vidole hata kama ni makosa yetu”.

Asernal walianza kwa kasi msimu huu na kutabiriwa kushinda taji la ligi kuu nchini England, lakini waliyeyuka mithiri ya barafu na kuziachia Chelsea, Man City na Liverpool ziendelee kupambana.

Walcott hajapangwa tangu mwezi januari mwaka huu kutokana na majeruhi, lakini anaamini kurejea kwa  Aaron Ramsey, Jack Wilshere na Mesut Ozil kutaweza kutimiza ndoto zao kuelekea fainali ya FA.

Aliongeza: “Kuwakosa Aaron, Mesut, na Jack, kocha wetu alisema itakuwa ngumu kuzoeana. Ukiwatoa wachezaji hao watatu kwenye kikosi, timu itaathirika”.

“Ilikuwa huzuni kwa kila mtu kuwapoteza wachezaji hawa kwa wakati mmoja, lakini lazima mjitahidi kukaza”.

CHANZO, MPENJA BLOG

KAGERA SUGAR KUTAFUTA MSAIDIZI WA THEM FELIX NJE YA NCHI



Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

WAKATA miwa wa Kaitaba, `Wanankulukumbi` Kagera Sugar wanatarajia kufanya usajili makini ili kuendana na kasi ya ushindani katika mitanange ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu ujao.

Murage Kabange, kocha msaidizi wa Kagera Sugar amebainisha mapungufu kadhaa katika kikosi chao na sasa wapo katika mipango ya kufanyia marekebisho.

“Kwanza majeruhi ya kudumu kwa baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza ni tatizo lilituathiri sana”.

“Pili ubutu wa safu ya ushambuliaji lilikuwa tatizo la kudumu kwa Kagera Sugar mpaka tunapozungumza hivi”.

“Tatu hatukuwa na wachezaji mbadala, kwahiyo kila inapotokea mchezaji muhimu anapata majeruhi, ilikuwa janga kwetu”.

Kutokana na matatizo hayo, Kabange alisema wanatarajia kuongeza nguvu sehemu ya ushambuliaji ambapo wanafikiria kutafuta hata mchezaji wa kigeni.

“Tunadhani ipo haya ya kwenda hata nje ya nchi ili kupata washambuliaji watakaotuongezea nguvu msimu ujao”.

“Lakini tunafirikia kutafuta wachezaji wengi ili tuwe na machaguo mengi zaidi. Tutasajili vijana zaidi ili iwe rahisi kufundishika”. Alisema Kabange.

Kagera Sugar waliomaliza msimu uliopita katika nafasi ya tano kwa pointi 38 walikuwa wanamtegemea mshambuliaji wao nyota, Them Felix `Mnyama` ambaye hata hivyo hakuonesha makali sana, pia Kabange alieleza kuwa wanafikiria kuboresha safu yao ya ulinzi na kiungo.

Kagera Sugar walifungwa mabao 20 katika mechi 26, huku wakifunga mabao 23.

Kwasababu hiyo, Kabange alisema kuna haja ya kupunguza mabao ya kufungwa msimu ujao kwa kutafuta wachezaji watakaoongeza nguvu katika ngome yao ya ulinzi.

Hata hivyo, Kabange alisema mabao 23 ya kufunga katika mechi 26 yanadhihirisha ubutu wa safu ya ushambuliaji na kwa kushirikiana na kocha mkuu, Mganda Jackson Mayanja wameona kuna haja ya kutafuta washambuliaji wakali.

Aidha, aliongeza kuwa msimu ujao wanatarajia kuingia katika mbio za ubingwa au nafasi tatu za juu.

CHANZO, MPENJA

WAZIRI CHIKAWE,IGP MANGU WALA KIAPO KUTUMIKIA TUME YA UTUMISHI YA POLISI NA MAGEREZA

1
2 3 4 5 6 7
Kamishna wa Utawala na Utumishi wa Jeshi la Polisi, Thobias Andengenye akila kiapo cha kuwa mjumbe wa Tume ya utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza  mbele ya Jaji wa Mahakama kuu Mhe. Njengafibili Mwaikugile jijini Dar es Salaam jana .Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari polisi na Magereza.Katikati ni Msajili wa Mahakama kuu Bw.Benedict Mwingiwa (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)




CHANZO,FULL SHANGWE 

HATARI: TANESCO WAAMUA KUCHUKUA UAMUZI WA KUFUNGA NYAYA JUU YA MTI BAADA YA NGUZO KUVUNJIKA

unnamed
Nguzo hii ina zaidi ya Mwezi mmoja ikiwa ndani ya nyumba ya mtu na hatari zaidi kwa sababu imelalia katika miti mibichi.
unnamed (1)
Hivi ndivyo nguzo hiyo inavyo onekana kwa Jirani ikiwa imelalia miti.
unnamed (2)
Hizi  ni waya zilizopita chini kabisa katika Geti la mtu na ndani ya miti.
unnamed (3)
Nguzo ya umeme ya TANESCO ikiwa imekatika katika eneo la Jirani na Daraja la Mlalakuwa ambapo ipo mpaka sasa ikiwa ni zaidi ya mwezi ipo eneo hilo.
unnamed (4)
unnamed (5)
Hii ndio Njia Mbadala waliyo iona TANESCO kutumia kwa kufunga nyaya hizo juu ya Miti baada ya kubadirisha nguzo iliyo haribika.
unnamed (6)
Hizi ni nyaya za umeme ambazo zimepita Chini ,pia ni hatari kwa watembea kwa miguu
*****
Kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni   jijini Dar es salaam ambapo mvua hizo zimesababisha uharibifu mkubwa wa mali na  miundo mbinu mbalimbali .
Uharibifu mkubwa na wahatari  ni katika nguzo za umeme zilizo vunjika  na baadhi ya nyaya zinazo pitisha umeme kushuka chini ambazo ni hatari kwa wananchi.
Katika eneo la Mlalakuwa  mbele kidogo baada ya kulivuka daraja ukiwa unaelekea kawe  pana nguzo tatu ambapo nguzo moja imevunjika  kabisa na nyingine mbili zimelegea  katika nguzo iliyo vunjika ni mali ya Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) liliweza kufika katika eneo hilo wakachukua hatua ya kufungua nyaya za ile nguzo iliyo katika na kuzifunga juu ya mti ulio pandwa pembeni  mti huo si mkavu ni mbichi.
Je shirika la umeme la Tanzania madhara ya umeme wananchi watayafahamu vipi wakati ninyi wenyewe wataalamu wa kazi hiyo mnatupotosha, pili sehemu mulipo fungia na nyaya zilipo legea ni sehemu watu wanapo ishi ,hivi huku nikuwajali wateja wenu ?
Tunaomba  muchukue hatua harakaiwezekanavyo ili kuepusha madhara yanayo weza kujitokeza hapobaadae  kwani ni hatari sana
Picha na Dar es salaam yetu Blog.
CHANZO,FULL SHANGWE 

MOURINHO ACHARAZWA 3-1, FAINALI UEFA NI REAL MADRID V ATLETICO MADRID

article-2617143-1D7BEDE500000578-530_634x450
KWA mara ya kwanza dunia itashuhudia fainali ya kwanza  ya UEFA mei 24 mwaka huu mjini Lisbon, Ureno, itayozikutanisha timu mbili zinazotoka mji mmoja yaani Madrid.

Hii ni baada ya Atletico Madrid kufuzu fainali usiku huu kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Chelsea kwenye uwanja wa Stamford Bridge.
Mechi ya kwanza nchini Hispania katika uwanja wa Vicente Calderon, timu hizi zilitoka suluhu, lakini leo Chelsea wameachia na kutolewa kwa wastani wa mabao 3-1 katika mechi zote mbili za nusu fainali.
Katika mchezo wa leo, Fernando Torres alitangulia kuifungia Chelsea dakika ya 36 kwa pasi ya Azpilicueta baada ya kazi nzuri ya Willian.
Dakika 8 baadaye,  Adrian Lopez akaisawazishia Atletico  kwa pasi ya Juanfran.
Diego Costa katika dakika ya 61 alifunga bao la pili kwa penalti  iliyosababishwa na Samuel Eto`o.
article-2617143-1D7BD5E700000578-98_634x420
Wakati Chelsea wakihaha kusawazisha bao hilo, dakika ya 72, Arda Turan alipiga kidude cha tatu na jahazi la Chelsea kutota kabisa.

Mouringo katika dakika ya 54 alimtoa beki wake,  Ashley Cole na nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji, raia wa Cameroon, Samuel Eto`o ambaye alisababisha penati iliyowapoteza Chelsea.

CHANZO,FULL SHANGWE