Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 13 January 2017

HALMASHAURI YAIFUNGIA KWA MUDA USIOJULIKANA SHULE YA MSINGI HAZINA MISION KWA KUTOKUWA NA VIWANGO VYA UANDIKISHAJI



Na Woinde Shizza, Arusha

HALMASHAURI ya jiji la Arusha imeifungia kwa muda usiojulikana shule ya
msingi Hazina Mision iliyopo kata ya Baraa mara baada ya uongozi wa shule
hiyo kushutumiwa kwa makosa mbali mbali ikiwemo kuwatelekeza  watumishi
wake pamoja na  mindombinu kuwa chini ya viwango vinavyohitajika katika
uandikishaji wa shule.

Hatua hiyo ya kufungiwa kwa shule hiyo imekuja mara baada  siku chache
zilizopita wamiliki wa shule hiyo kulalamikiwa kuwanyanyasa na kushindwa
kuwalipa mishahara watumishi na walimu  wa shule hiyo na hivyo kutakiwa
kufanya marekebisho na kuwalipa stahiki watumishi lakini wakakaidi kufanya
maagizo hayo kwa muda waliopewa.
Akitoa agizo hilo katika viwanja vya shule hiyo kaimu afisa elimu  shule za
msingi katika jiji la arusha Eunice Elibariki alisema kuwa wameamua
kusimamisha huduma ya utoaji elimu kutokana na shule hiyo kushindwa kufanya
marekebisho waliyotakiwa kuyafanya shuleni hapo.
Alisema kuwa awali kabla hatua hiyo haijafikiwa walipata taarifa kuwa
uongozi wa shule hiyo inawanyanyasa walimu kwa kuwanyima mishahara yao,
kutokuwa na mindombinu kuachilia viwango pamoja na kuwepo uchafuzi wa
mazingira na ndipo uongozi ukapewa muda wa kufanya marekebisho hayo pamoja
na kimaliza migogoro ya kimaslahi lakini walikaidi kutoa ushirikiano hali
iliyopelekea halmashauri hiyo kuchukua hatua ya kusimamisha utoaji huduma.
"Kwa kuwa uongozi  wa shule hii mlishindwa kufanya marekebisho mlioagizwa
ikiwa ni pamoja na kishindwa kumaliza migogoro ya walimu kuanzia sasa
nasimamisha huduma za masomo hadi hapo mtakapoweza kuiweka shule yenu
katika mazingira yanayohitajika kwani lazima shule iwe na viwango na sifa
zinavyohitajika sio tu kuendesha kiholela "alisema Eunice
Wananchi wa eneo hilo akiwemo  Diwani wa kata ya baraa Elifasi Ndetika
akizungumzia  uamuzi wa kufungiwa kwa shule hiyo  alisema kuwa ni halali
kabisa kwani walikuwa na malundano ya muda mrefu baina ya uongozi na walimu
lakini walishindwa kumaliza wenyewe huku akidai kuwa mazingira yalikuwa
hayadhirishi na hivyo kupitia usimamishaji huo unaweza kupelekea
marekebisho yakawepo.

No comments:

Post a Comment