Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji akihutubia katika mkutano wa tano wa mwaka wa ESRF wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.(Picha na Said Khalfan wa KVS Blog)
Imeleezwa kuwa ili kumwezesha kila mwananchi wa Tanzania kupata maendeleo na kuondokana na janga la umaskini, Serikali haina budi kutunga sera ambazo zitamgusa kila mwananchi na kuwa na faida jambo ambalo litawasadia kukuza uchumi wao binafasi na taifa kwa ujumla.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana na mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu katika uwanja wa ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa timu ya Bunge,William Ngereja
ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza akizungumzia
maandalizi ya timu ya Bunge kuelekea mashindano ya Afrika Mashariki
yatakayofanyika nchini Kenya.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said (Mpaka Basi) akiwa na mgeni wake Ndg Wilfred Moshi wakiwasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar, kutembelea na kujionea shughuli za Mkutano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ndg Wilfred Moshi ni Mtanzania wa Kwanza kupanda Mlima Mkubwa Duniani wa Evarest ukiwa na Mita 8,848, Mtanzania huyo Ndg Wilfred Moshi amepanda mlima huo mwaka 2012. akiwa ni Mwaafrika wa Tatu kupanda mlima huo na mwafrika wa Pili mweusi kupanda mlima huo Duniani kwa ukubwa.
Katibu Mtendaji wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Fabian Magoma (kulia), akizungumza katika Kongamano la 33 la siku tano la Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) linaloendelea Hoteli ya Kebby Mwenge jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa TPHA anayemaliza muda wake, Daktari Bingwa Elihuruma Nangawe.
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro (kushoto) akisalimiana na mmoja wa wahadhiri wa chuo hicho alipowasili katika ofisi za Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa (UOI), Prof Joshua Madumulla akiwa ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.(Picha zote na Zainul Mzige wa Moblog)
Wananchi wa Kata ya Kitaraka iliyopo katika Halmashauri ya Itigi, Wilaya ya Manyoni, Mkoani Singida, wamemuomba Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mh. William Ole Nasha, kuwapatia shamba linalomilikiwa na Serikali la Tanganyika Packers, ambalo Serikali imeacha kulitumia kwa zaidi ya miaka 20, ili walitumie kwa shughuli za Kilimo na Ufugaji.
Gari la Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe likisukumwa na wananchi wa kijiji cha Sagara baada ya kushusha neema kwa wakazi hao kwa kitendo cha kuwamilikisha shamba la ekari 5,430. Wananchi hao kwa miaka mingi wamekuwa wakitozwa shilingi elfu 30 kwa ekari moja katika msimu wa kilimo. Ushuru huo kwa msimu huu ulipandishwa hadi shilingi 40,000 kwa ekari. Kwa sasa hawatalipa tozo hilo.
Balozi wa India nchini
Tanzania ,Sandeep Arya kushoto akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Thobias Mwilapwa wakati wa kongamano la wafanyabiashara wa pili
kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena
Saidi.
NYUMBA INAUZWA IPO WILAYA YA TEMEKE KATA YA CHAMAZI KARIBU NA UWANJA WA MPIRA WA AZAM NI SEIF CONTAINED NA INA MASTER ROOM NA CHUMBA KIMOJA CHA KULALA, SEBURE, JIKO NA CHOO NA BAFU LA NDANI, BEI NI SHILINGI MILIONI 19 KWA MAWASILIANO PIGA SIMU NAMBA 0687-347676 AU O759-239338.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida (kushoto), akimkabidhi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano ya Kimataifa, Maendeleo na Mafunzo wa Chuo cha Viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, Jia Bo, Dar es Salaam leo asubuhi, ambaye yupo nchini na wajumbe wenzake sita kwa zaiara ya siku saba ya kichama kukitembelea Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George
Simbachawene ameziagiza Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi
wa Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya kuhakikisha kuwa fedha zilizotolewa kwa
kaya zisizokuwa na sifa katika Mpango wa kunusuru kaya maskini unaofanywa kwa
uratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF) kurejeshwa ili ziweze kuwanufaisha walengwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kuhusu kuipitia upya mikataba iliyoingia shirika hilo na Taasisi mbalimbali na watu binafsi kutokana na baadhi yake kugundulika ikiwa na utata wa maslahi ya shirika hilo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu, Fortunatus Kapinga na Kulia ni Katibu wa Shirika, Rochus Assenga. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mwenyekiti
wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa na Mkuu wa Mkoa wa Singida
Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiongoza kikao hicho, kushoto kwake ni
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dokta Angelina Mageni Lutambi, wa kwanza
kulia ni Waziri wa Mambo ya ndani Mwigulu Lameck Nchemba na anayefuata
ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Mhe. Martha
Mlata.
Mwenyekiti
wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa na Mkuu wa Mkoa wa Singida
Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiongoza kikao hicho, kushoto kwake ni
Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dokta Angelina Mageni Lutambi, wa kwanza
kulia ni Waziri wa Mambo ya ndani Mwigulu Lameck Nchemba na anayefuata
ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Mhe. Martha
Mlata.
Naibu
Waziri wa ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa
na serikali za mitaa TAMISEMI Suleiman Jaffo akikagua kitabu cha Risiti
kulia anayemwangalia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani
Sabas Chambasi
Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) imeshirikiana na kampuni ya Getenrgy kuandaa mkutano wa Afrika wa Mafuta na Gesi (GETENERGY VTEC AFRICA 2016) ambao unafanyika nchini kwa siku tatu kuanzia Novemba, 21-23, 2016.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications L.T.D,Maria Sarungi Tsehai (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,kuhusu kuanza kambi kwa warembo wa Miss Universe Tanzania 2016 ambapo fainali itafanyika Novemba 25 katika Hoteli ya Collessium iliyopo Oysterbay. Kulia ni Mkurugenzi wa Hoteli ya Collessium,Mustafa Dhanji na Mratibu wa shindano hilo,Mwanakombo Salim.(PICHA NA ELISA SHUNDA)
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania
(TEMESA), Dkt. Mussa Mgwatu akieleza utendaji kazi kwa Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, alipotembelea Wakala huo,
jijini Dar es Salaam. (Picha na Benjamini Sawe-Maelezo)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati wa kuelekea kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala
katika bara la Afrika.
Mkurugenzi Msaidizi wa Fedha na Mipango, Servus Sagday akielezea madhumuni ya warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) kwa Maofisa Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango nchini iliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua warsha hiyo inayoendelea mjini Dodoma katika ukumbi wa mikutano Hazina ndogo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Miriam Mmbaga amewataka maofisa Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango nchini kufanya kazi kwa uzalendo ili Tanzania iweze kufikia malengo ya maendeleo endelevu (SDG’s) ifikapo mwaka 2030 kama ilivyokusudiwa.
November 25th is the International Day for the elimination of Violence against women in the world. The 16 days up to December 10th the Human Rights Day is a period of global activism dedicated to fight gender violence in all settings.
UZIKWASA, an organization based in Pangani, Tanzania has become known for its innovative interventions that encourage a voice among rural communities and the development of capable grass roots leaders who are committed to fight gender rights violations in Pangani.
UZIKWASA’s multimedia work that has addressed violence against women and girls (VAWG) includes:
-Pangani FM radio programs
*Leadership that Touches (UongoziwaMguso)
*Womens’ Voice (Sauti ya Mwanamke)
-Feature films
*Fimboya Baba (Father’s Stick: Early and forced marriage)
*Chukua Pipi (Sweet deceit, sexual abuse of school children)
*AISHA (Gang rape)
-Comic books
* Varangati
*Halafu series
*AISHA book
-Forum Theatre and Theatre for Development
-A series of TV spots
On December 2 UZIKWASA will participate in the 16 days of activism by launching theMinna Dada Day, abig bang event to create awareness on VAWGin Pangani District.The campaign is designed to start a deep reflection process among the Pangani people and their leaders about atrocities committed against women and girls including Intimate Partner violence.
Minna dada introductory TV Spot
The following four “Minna Dada” TV spots paint a picture of how intimate partner violence affects the lives of local Pangani women. Cinema Zetu of AZAM TV will broadcast the four spots during the next four months.
Wastaafu mbalimbali wakiwa kwenye foleni kusubiri zamu yao
ya kuhakikiwa jijini Dodoma.
SERIKALI imesema kuwa itaendelea na utaratibu wa kuwalipa wastaafu wanaohudumiwa na Wizara ya Fedha na Mipango, pensheni yao kila mwezi kwa mujibu wa sharia ya mafao ya wastaafu Na. 371 badala ya kuwalipa malipo hayo kila baada ya miezi mitatu.
Mkaguzi wa Ndani Mkuu
wa Serikali Msaidizi Stanslaus Mpembe akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari
kuhusu zoezi la Uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa pensheni na Wizara ya Fedha na
Mipango, mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya
Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Jenerali Fan Changlong mara baada ya
kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
MZAZI Sakina Lembo (26) mkazi wa Mbagala Kibonde Maji ambaye alizuiliwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), kutokana na deni la sh. 338,257 baada ya kufanyiwa oparesheni ya uzazi uongozi wa hospitali hiyo umemruhusu kuondoka bila ya masharti yoyote.
Ndege aina ya ATR namba 5H-PWE mali ya Shirika la ndege la Precision Air ikitua kwa mara ya kwanza katika uwanja wa ndege uliopo ndani ya Hifadhi ya taifa ya Serengeti ikiwa na wageni 45 kutoka nchini Afrika Kusini waliofika nchini kwa ajili ya shughul za utalii.
Ofisa Mkuu wa Biashara wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Shavkat Berdiev (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu kampuni hiyo kutangaza ofa ya Krismas ya Smartphone. Kushoto ni Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia
wajumbe wa mkutano wa masuala ya soko la Gesi na Mafuta uliofanyika kwenye
ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Young Africans Sports Club, Yussuf Manji kutokana na kifo cha Makamu Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Isaac Shekiondo ‘Clinton’.
Uchunguzi dhidi ya waamuzi Martin Saanya, Samuel Mpenzu (mechi ya Yanga Vs Simba), Thomas Mkombozi (mechi ya Coastal Union Vs KMC) na Rajab Mrope (mechi ya Mbeya City na Yanga) umekaribia kukamilika.
Hatua ya mwisho ya uchunguzi huo ni wao kufika mbele ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa 72) ambapo watahojiwa ili kutoa ufafanuzi katika masuala mbalimbali yaliyojitokeza katika taarifa zao.
Meza kuu ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, kushoto kwake Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Jackson Lyanivana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, Makamu Mwenyekiti, Nassor Idrissa na Ofisa Habari, Jaffary Idd.
By Abducado Emmanuel
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Paul Makonda, leo mchana amefanya ziara kwenye Makao Makuu wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC akiwa na lengo kuu la kuipongeza kutokana na juhudi kubwa wanazofanya za kuwekeza katika soka la Tanzania.
Mkurugenzi wa Kampuni ya simu za mkononi, Tigo-Tanzania, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jackson Kiswaga, (kulia) akizungumza na wananchi wa Itumba Wilaya ya Ileje, waliofika kwa ajili ya kushudia msaada waliopatiwa kutoka Tigo-Tanzania kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya hiyo, kwa niaba ya kampuni hiyo. Tigo ilikabidhi vifaa vya afya hospitalini hapo ambavyo ni mashuka, mablanketi, Goves, Jokofu na mifagio ambavyo vinagharimu kiasi cha Sh20 Milioni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, ambapo aliwaasa wananchi kuchukua uamuzi wa kupima afya zao na kupatiwa matibatu. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Dk. Hedwiga Swai.
VIJANA 10 wenye umri chini ya miaka 17, wamefanikiwa kuchaguliwa kwenye majaribio ya wazi yaliyoendeshwa na Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, jana Jumamosi katika Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.
Huo ni mwendelezo wa mpango wa mabingwa hao wa kutengeneza timu bora ya vijana wa umri huo kwa ajili ya kuwatumia kwa miaka ijayo na wengine kunufaika nao kwa kuwauza.
Waziri wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Mhe.Mahmood Thabith Kombo, akizungumza kwenye Uzinduzi wa Tamasha la Uoneshaji wa Filamu kwa njia ya Sinema mkoani Geita, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Nape Nhauye.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, (aliyevaa joho jekundu), akiwa nje ya
Ofisi Kuu ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kilichoko
Changanyikeni Jijini Dar es salaam, wakati wa Mahafali ya Pili ya Chuo hicho
ambapo wahitimu 154 kutoka nchi nane Barani Afrika wametunukiwa Astashahada na
Shahada za Takwimu Rasmi zinazotolewa na chuo hicho.
Wanafunzi waliohitimu na kutunukiwa Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara wakishangilia wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira tawi la Dar es Salaam Tudarco yaliyofanyika leo Mwenge, Dar es Salaam. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Frederick Shoo, alitunuku jumla ya wahitimu 733. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG}
Mgeni
Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo cha
Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt.
Philip Mpango (kushoto) pamoja na mkuu wa chuo hicho Prof. Innocent Ngalinda
(kulia) kuingia ukumbini pamoja na wahitimu tayari kwa mahafali.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fesso (kushoto), akizungumza kwenye kikao cha Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita hii leo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Geita. Mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye, aliyewakilishwa na Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Mahmood Thabith Kombo (wa pili kushoto). Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti Chama cha Waigizaji mkoani Geita, Rosemary Michael na anayefuata ni Herman Matemu ambaye ni Kaimu Afisa Tawala mkoa wa Geita.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene, akisalimiana na Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, baada ya kuwasili Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kufunga mafunzo ya uongozi na maadili ya vijana wazalendo 47 yalifungwa chuoni hapo Dar es Salaam leo. Kulia ni Samuel Kasori, aliyekuwa Msaidizi wa Hayati Baba wa Taifa ambaye alipata fursa ya kuzungumza katika hafla hiyo kuhusu suala zima la maadili ya uongozi na uzalendo.