Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 24 September 2016

MBUNGE WA JIMBO LA SEGEREA BONNAH KALUWA AONGOZA SEMINA YA WANAWAKE WAJASIRIAMALI JIJINI DAR ES SALAAM

 Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kaluwa (katikati) akiingia kwenye ukumbi wa Nyantale kwa ajili ya kufungua semina ya ujasiriamali ya wanawake eneo la Tabata Bima jijini Dar es Salaam leo.

TAIFA STARS KUJIPIMA NA ETHIOPIA


Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania (Taifa Stars), inatarajiwa kucheza na Ethiopia katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa Oktoba 8, 2016.

MIRADI 45 KUZINDULIWA NA MWENGE WA UHURU MKOANI TABORA


Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Methew Mtigumwe akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey D.J Mwanri (Kulia)

MKUU WA WILAYA YA MPWAPWA AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI (FDC)-CHISALU

Na Mathias Canal, Dodoma
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya wananchi (FDC)-CHISALU amekalia kuti kavu mara baada ya kubainika kuwa ameruhusu udahili wa wanafunzi wanaosoma fani ya utaalamu wa Kilimo na Mifugo ilihali chuo hicho ni maalumu kwa ajili ya mafunzo ya utaalamu wa Maendeleo ya jamii (Community Development).

Friday, 23 September 2016

YANGA, JKT RUVU SASA KUCHEZA OKTOBA 26

Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imepanga mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Young Africans dhidi ya JKT Ruvu, sasa utachezwa Oktoba 26, 2016 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar s Salaam.

KAMATI YA KATIBA, SHERIA KUJADILI KESI 13 KESHO

Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji kesho Jumamosi Septemba 24, 2016 itasikiliza mashauri 13.
Malalamiko hayo ni:
1.    Mchezaji Ametre Richard ambaye atawasilisha mbele ya kamati makubaliano waliyokubaliana kukaa pamoja na kufikia mafaka.

LIGI DARAJA LA KWANZA YAANZA

Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaanza wikiendi hii ambako katika kundi A, mchezo wa kwanza unapigwa leo Ijumaa Septemba 23, 2016 kwa kuzikutanisha timu za Ashanti United ya Ilala, Dar es Salaam na Pamba ya Mwanza katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Karume jijini.

KILIMANJARO QUEENS NEEMA TUPU

Nahodha wa Kilimanjaro Queens, Sophia Mwasikili
Ubingwa Kombe la CECAFA Chalenji kwa timu za mpira wa miguu za wanawake katika nchi za Afrika Mashariki, umewavutia wadau wengi kwa kiwango kikubwa hivyo kushusha neema kwa wachezaji hao wa timu ya taifa ya Tanzania Bara maarufu kama Kilimanjaro Queens ambayo imeandika historia ya kutwaa taji hilo ikiwa ni taifa la kwanza katika mashindano hayo mapya.

MASAUNI AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKAZI WA UNDP NCHINI

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo wakati alipokuwa akizngumza kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara yake na UNDP. Dabo alimtembelea Naibu Waziri Masauni ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Wapili kushoto ni Nirine Kiplagat, Meneja wa Miraji katika Shirika hilo, na Godfrey Mulisa wa UNDP. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MKURUGENZI MTENDAJI WA CRDB BANK DKT CHARLES KIMEI ATUNUKIWA TUZO NA AFRICAN LEADERSHIP, NEW YORK NCHINI MAREKANI

 
Tuzo aliyotunukiwa mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei siku ya Alhamisi Septemba 22, 2016 jijini New York nchini Marekani katika hotel ya St. Regis, New York. African Leadership hutoa tuzo katika kutambua michango unaotolewa na viongozi wa bara la Afrika katika kuleta maendeleo na utendaji wa kazi wenye ufanisi' katika kukuza uchumi kwa kusaidia kukuza na kuwainua wawekezaji wazawa. African Leadership ilishawahi kutoa tuzo kama hilo kwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka April 9, 2014  katika hotel ya St Regis ya Washington, DC. Picha na Vijimambo Blog/Kwanza Production, New York.

TSN YADHAMINI MECHI YA BONGO MOVIE NA BONGO FLAVA KUCHANGIA WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI BUKOBA

Mkuu wa kitengo cha Masoko na Biashara TSN, Jahu Mohammed Kessy akiwakabidhi wasanii jezi kwa ajili ya mechi ya kuchangia maafaa ya tetemeko la ardhi Bukoba
Kampuni ya TSN  Kwa kushirikiana na Wasanii wa bongo fleva na bongo Movie wamejitokeza kuwezesha mechi maalum kuchangia wahanga wa Tetemeko la Ardhi lililotokea Bukoba mkoani Kagera.

KAMPUNI YA TIGO YAENDELEA NA UTOAJI WA MADAWATI MIKOANI

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadiki akimweleza jambo Mkurugenzi wa kampuni ya Tigo kanda ya Kaskazini,George Lugata wakati wa hafla ya kukabidhi madawati iliyofanyika katika shule ya msingi Mandela mjini Moshi. 

TIGO YATOA SIMU 800 ZENYE THAMANI YA TSHS.120M KUSAIDIA ZOEZI LA KUSAJILI WATOTO CHINI YA UMRI WA MIAKA MITANO KATIKA MIKOA YA NJOMBE NA IRINGA


Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Nyanda za juu Kusini Jackson Kiswaga akipeana mkono na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dr Rehema Nchimbi mara baada ya kutoa hotuba wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya zoezi la usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa, uzinduzi huo ulifanyika jana mjini Iringa.

STARTIMES KUWAPAMBANISHA 18 FAINALI ZA SHINDANO LA VIPAJI VYA SAUTI KESHO JIJINI DAR ES SALAAM


Mtengenezaji wa Sauti katika chaneli ya StarTimes Kiswahili, Tracy Luo (katikatio) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza kufanyika kwa fainali za shindano la vipaji vya sauti litakalofanyika kesho katika ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kushoto ni mshiriki wa shindano hilo kutoka Zanzibar,  Safiya Ahmed na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Masoko wa kampuni hiyo, Damien Li. Washiriki 18 kati ya 547 wameingia hatua ya fainali ambapo washindi 10 watajipatia fursa ya kwenda kufanya kazi makao makuu ya StarTimes yaliyopo Beijing, China.

SIKU NDEGE YETU YA KWANZA ILIPOTUA DAR KABLA YA KUANZA SAFARI

Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016.

WAZIRI MHAGAMA AHAMASISHA MAZAO YA MUHOGO NA MAHINDI KYERWA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama akitembelea eneo la kijiji cha Ntare kata ya Itera wilayani Kyerwa kujionea ukame unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi ulivyoathari mazao ya ndizi na kahawa wilaya Kyerwa mkoani Kagera na kuwaomba wananchi wa mkoa huo wabadilike waanze kulima mazao mengine ya chakula yanayokomaa kwa muda mfupi.

NAIBU WAZIRI MASAUNI APANDA MABASI YA MWENDO KASI, JIJINI DAR

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni  akiwa ndani ya moja ya mabasi ya mradi wa mabasi ya mwendo kasi ya UDA-RT jijini Dar es Salaam akitoka kituo cha Ubungo kuelekea katikati ya Jiji, baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Thursday, 22 September 2016

MASAUNI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA STENDI KUU UBUNGO NA KIBAHA, AGUNDUA MABASI MABOVU, AYAZUIA KUSAFIRI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa tai) akielekea Stendi Kuu ya Mabasi ya mikoani Ubungo, jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza yenye lengo la kukagua mabasi mabovu pamoja na usalama wa abiria katika Stendi hiyo pamoja na Stendi ya Kibaha mkoani Pwani. Masauni alilizuia Basi la Shambarai lenye namba za usajili T419 BUF na Basi la Karachani (T253 CLZ) ambayo yalikuwa yanaenda Tanga kutokuendelea na safari zake kutokana na ubovu wa mabasi hayo ambayo yangeweza kuhatarisha maisha ya abiria. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WAZIRI JENISTA AFANYA ZIARA WILAYA YA KYERWA

Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Kanali Mstaafu Shaban Lissu mara baada ya kuwasili wilayani humo kujionea madhara ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo.

TTCL NA TPDC ZATOA MILIONI 30 KUSAIDIA WAATHIRIKA TETEMEKO KAGERA

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu (kulia) akimshukuru Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Kamugisha Kazaura (kushoto) mara baada ya kupokea msaada wa mifuko 600 ya saruji ambayo ni sawa na tani 30 yenye thamani ya Sh. milioni 10.