Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 22 March 2016

RAIS ZFA KUIONGOZA STARS CHAD


Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Ravia Idarus Faina ndiye mkuu wa msafara wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, anatarajiwa kuondoka Dar es salaam kesho Jumanne alfajiri pamoja na wachezaji wengine kuelekea nchini Chad kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2017.

KIPINDI CHA REDIO CHA 'SHUGA' CHARUDI KWA KISHINDO

Mratibu wa Ukimwi kutoka Tume ya Kudhibiti ukimwi mkoa wa Njombe – TACAIDS   Abubakari Magege  akiongea na washiriki wa kipindi cha redio cha shuga katika uzinduzi rasmi wa msimu mpya wa kipindi hicho kitakachoanza kuruka tena katika redio mbalimbali nchini.

UKOSEFU WA WABUNIFU MAVAZI JIJINI MWANZA, WAPATA UFUMBUZI

Idda Hassan ambae ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Ushonaji wa Mavazi Jijini Mwanza ya Mikaela Professional Tailors akionyesha moja ya mavazi yanayoshonwa na Kampuni hiyo.

Na:George Binagi-GB Pazzo

Tofauti na ilivyo katika majiji mengine kama vile Jijini Dar es salaam, Jiji la Mwanza halina mwamko mkubwa katika ubunifu wa mavazi.

STARTIMES YAKABIDHI MINI PADS 180 KWA WAZIRI NAPE NNAUYE KURAHISISHA UTAFITI WIZARANI

 Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa Na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (wa pili kulia) akipokea moja ya Mini Pads 180 kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Bw. Lanfang Liao (wa kwanza kushoto), Dar es Salaam leo asubuhi kwa ajili ya kurahisisha ufanisi wa kazi kwa wafanyakazi wa wizara hiyo. Wakishuhudia tukio hilo wa pili kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Chini nchini Tanzania, Dk. Lu Youqing na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa. Elisante Ole Gabriel  (kulia).

Monday, 21 March 2016

TIGO YAZINDUA JUKWA LA KUJIFUNZA LA MTANDAO WA SMS KWA SHULE ZA SEKONDARI

Mkurugenzi Mtendaji wa  Shule Direct, Faraja K. Nyalandu (wa kwanza kulia) Meneja wa Huduma za jamii wa Tigo  , Woinde Shishael(wa pili kulia), Mkuu wa Mfuko wa Human Development Innovation Fund (HDIF), David B. McGinty, (wa kwanza kushoto), Mwanafunzi aliyefanya vizuri katika  mtihani wa kidato cha nnemwaka 2015/16 kutokea shule ya wavulana Fezza ya jijini Dar es Salaam, Innocent Lawrence (wa pili kushoto) na Mkurungezi wa Tume ya sayansi na teknolojia Flora Ismail Tibazarwa (wa tatukushoto)wakitazama namna mfumo wa huduma mpya ya wanafunzi kujifunza kupitia ujumbe mfupi wa maandishi, MAKINI SMS unavyoweza kufanya kazi kupitia simu ya mkononi.

WAZIRI NAPE AZINDUA MSIMU MPYA WA MASHINDANO YA UREMBO YA MISS TANZANIA 2016

Nape Nnauye
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwasili kwenye hoteli ya Ramada Resort akiambatana na Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia).(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amezindua rasmi msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania kwa mwaka 2016 katika hafla ya kukata na shoka iliyofanyika kwenye Hotel ya Ramada Resort iliyopo eneo la Kunduchi, Dar es Salaam.

UJUMBE KUTOKA KWA BI. IRINA BOKOVA, MKURUGENZI MKUU WA UNESCO, KATIKA SIKU YA USHAIRI DUNIANI, 21 MACHI 2016

The-director-general-of-UNESCO-Irina-Bokova
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi. Irina Bokova.
Shakespeare, mwandishi maarufu kutoka Uingereza aliyefariki yapata miaka 400 iliyopita, aliandika katika tamthilia yake inayojulikana kama “A Midsummer Night's Dream” kuwa, “Jicho la mshairi, hutazama kwa umakini na undani, kutoka mbinguni hadi duniani, na duniani hadi mbinguni. Na kama vitu vya kufikirika vusivyofahika vinavyoumbika katika mawazo, ndivyo kalamu ya mshairi inavyogeuza mawazo hayo kuwa katika maumbo yasiyoweza kudhaniwa”

VYAMA VYA USHIRIKA HUFA KUTOKANA NA MADENI MAKUBWA

NAIBU SPIKA WA BUNGE AHUDHURIA VIKAO VYA KAMATI ZA BUNGE KATIKA KUMBI ZA BENKI KUU JIJINI DAR

  Naibu Spika wa Bunge, Tulia Mwansasu (kushoto) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo alipohudhuria kikao cha kamati hiyo kilichoketi katika Kumbi za Benki Kuu (BoT Dar es Salaam leo.Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa  kamati hiyo, William Ngeleja.

Sunday, 20 March 2016

TWIGA STARS YANG'OKA, YATOKA SARE NA MIGHTY WARRIORS

Timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania ya Mpira wa Miguu ‘Twiga Stars’ imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji Zimbabwe ‘Mighty Warriors’ katika mchezo uliochezwa jioni ya leo katika uwanja wa Rufaro jijini Harare.

TAIFA STARS YAWASILI D'JAMENA

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kundi la kwanza limewasili salama jijini D’jamena nchini Chad tayari kwa mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2017.
Taifa Stars inayonolewa na kocha mkuu Charles Boniface Mkwasa akisaidiwa na Hemed Morocco kimewasili D’jamena leo majira ya saa 7 mchana kwa saa za huku kwa shirika la ndege la Ethiopia, sawa na saa saa 9 alasiri kwa saa za nyumbani na Afrika Mashariki na kufikia katika hoteli ya Legder Plaza.

MASHINDANO YA MAKAMPUNI YALIYOANDALIWA NA KAMPUNI YA POPULAR SPORTS AND ENTERTAINMENT TANZANIA LTD UWANJA WA DUCE CHANGOMBE JIJINI DAR ES SALAAM YAFANA

 Mchezaji Frank Peter wa Banc ABC (kulia), akijitahidi kumtoka  Kambili John wa Ramada katika mashindano ya makampuni yaliyofanyika Uwanja wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu Dar es Salaam (DUCE), Chang'ombe jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Mashindano hayo yaliandaliwa na Kampuni ya Popular Sports and Entertainment Tanzania Ltd.

MAGUFULI KUANZA KUTUMBUA MAJIPU YA CCM JUNI, JK KUMKABIDHI CHAMA

HOTUBA YA KWANZA YA OLE SENDEKA KAMA MSEMAJI WA CCM

YANGA YATAFUTA ‘DAWA’ DHIDI YA AL AHLY ‘KUPUNGA MZIMU’ WA TIMU ZA MISRI


Mshambuliaji wa Yanga raia wa Uganda, Emmanuel Okwi alikuwa mwiba kwa Al Ahly timu hizo zilipocheza jijini Dar es Salaam mwaka 2014.


Na Daniel Mbega
MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Yanga, sasa wanatafuta ‘dawa’ dhidi ya National Al-Ahly kwani ‘mzimu’ wa timu za Misri umeonekana kuleta upepo mbaya kwa timu hiyo ya Jangwani, mtandao wa www.brotherdanny.com unaripoti.
Na ‘dawa’ hiyo haina budi kupatikana kabla ya Jumamosi, Aprili 9, 2016 wakati timu hizo zitakapopambana jijini Dar es Salaam kwenye mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika ili kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi inayoweza kuwafanya wakwa mabilionea.

Saturday, 19 March 2016

HARUSI YA MISS MILIKA BINAGI NA BWANA SAMWELI CHACHA WA TARIME MKOANI MARA YAFANA.

Kushoto ni Bwana Harusi JOHN SAMWEL CHACHA akiwa pamoja na Bibi Harusi Milika Daniel Binagi, katika hafla ya harusi yao iliyofanyika Juzi Alhamisi Machi 17,2016 Rebu, Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.

WASHINDI WA PROMOSHENI YA KWEA PIPA KWENDA BARCELONA WATANGAZWA


 Mshindi wa  wa Promosheni ya kwea pipa  kwenda kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Hispania maarufu kama La Liga, kati ya Deportivo la Coruna na Barcelona Machi mwaka huu Jamal Othman mkazi wa Lushoto, Tanga akikabidhiwa mfano wa hundi toka kwa Meneja Promosheni wa Tigo Pesa, Mary Rutta na Mkuu wa Idara ya Masoko ya Azam Media, Mgope Kiwanga katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya Tigo Makumbusho jijini Dar es salaam.

TANZANIANS HAPPY WITH IMPLEMENTATION OF THE PROPOSED CONSTRUCTION OF THE tANZANIA-UGANDA CRUDE OIL PIPELINE

Tanzania President Dr. John Pombe Joseph Magufuli announces the crude oil pipeline project to reporters after his meeting with President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda on March 1, 2013 in Arusha in the sidelines of the  The 17th Ordinary East African Community (EAC) Heads of State Summit.

WAFANYAKAZI WA MFUKO WA PENSHENI WA PPF WASHIRIKI BONANZA MAALUM JIJILI DAR

Mfanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Anthony Mkinga, akiruka kujaribu kumkamata Kuku, wakati wa mchezo huo wa kufukuza kuku katika Bonanza maalum la Wafanyakazi wa PPF lililofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, leo Machi 19,2016. Picha na Mafoto Blog.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakichuana katika mchezo wa mbio za Magunia wakati wa Bonanza maalum la Wafanyakazi wa PPF lililofanyika kwenye Uwanja wa Chuocha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, leo Machi 19,2016. Katika mbio hizo Magreth John (mbele) aliibuka kidedea. Picha na Mafoto Blog.

RC PAUL MAKONDA AZUNGUMZA NA WENYEVITI NA MAOFISA WATENDAJI WA JIJI LA DAR

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza na wenyeviti na maofisa watendaji wa jiji la Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu mambo mbalimbali hasu suala la usafi wa mazingira.