Nassor Moyo
Na Mwinyi Sadallah
Zanzibar. Chama cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) kimemfukuza uanachama Mwanasiasa Mkongwe Hassan Nassor Moyo baada ya kubainika amekuwa akifanya vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili ya chama ikiwamo kuhutubia mikutano ya hadhara inayoitishwa na Chama cha Wananchi (CUF) na kukejeli misingi ya Mapinduzi na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar imefahamika visiwani humo jana.
