Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday, 8 May 2016

RAIS DKT MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI YA KUPAA KWA BWANA KATIKA PAROKIA YA TOLEO LA BWANA JIMBO LA ARUSHJA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia waumini aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.

JK AMUWAKILISHA RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI MAZISHI YA LUCY KIBAKI NCHINI KENYA



Mwili wa mke wa aliyekuwa rais wa Kenya Mwai kibaki , mama Lucy Kibaki ukiwasili kwa hapo jana katika eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri,mjini Nairobi nchini Kenya. 

WABUNGE JAMES MBATIA NA JOSEPH SELASINI WATEMBELEA WAHANGA WA MAAFA YALIYOTOKANA NA MVUA ROMBO.

Wabunge James Mbatia (Jimbo la Vunjo ) na Joseph Selasini wakiwa ofisini kwa Mkuu wa wilaya ya Rombo Lembris Kipuyo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini Brigedia Jenerali Mbazi Msuya alipofika kutembelea wahanga wa mvua zilizonyesha hivi karibuni na kusababisha maafa.

Saturday, 7 May 2016

TASWIRA MBALIMBALI ZA RAIS DKT MAGUFULI WAKATI AKIONGEA NA WANANCHI WA JIJI LA ARUSHA LEO

Tafadhali pokea taswira mbalimbali za Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli alipkuwa akiongea na wananchi wa Arusha wakati akirejea Ikulu ndogo toka Chuo cha Mafunzo ya Maafisa wa Kijeshi cha Monduli leo Mei 7, 2016.

TUZO ZA WANAFUNZI BORA AFRIKA MASHARIKI "ALL-STARS STUDENTS AWARDS"ZAANZISHWA

 Aaron Ally (Dj Aaron Tanzania) Mratibu wa ‘All-stars Students Awards Akiongea Kwenye Kipindi cha Morning Trumpet kuelezea tuzo hizo.
Dj wa zamani wa Clouds FM, Aaron, yeye na Team yake(Ms Chiku Lweno, Mwl. Dany Mtanga) wameanzisha Tuzo walizoziita All-stars Students Awards. 

NAIBU SPIKA ACKSON AFUNGUA SEMINA KWA WABUNGE YA UELEWA WA HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU


 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu), Dk Abdallah Possi (kulia), akiwasilisha mada katika semina ya Wabunge kukuza na kuimarisha usawa wa watu wenye ulemavu nchini, kwenye Ukumbi wa Bunge wa Msekwa mjini Dodoma jana. Kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Bukene, Seleman Zedi (CCM) na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

WATUMISHI WA MAHAKAMA MKOANI MWANZA WA WAAHIDI UFANISI KATIKA UTENDAJI KAZI

Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika MISA tawi la Tanzania, Simon Berege, akifafanua jambo wakati wa Mafunzo Maalumu kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoa wa Mwanza yanayofanyika Jijini Mwanza.

HUJUMA: SERIKALI YAKAMATA TANI 4,579.2 YA SUKARI ILIYOFICHWA


Frank Mvungi-MAELEZO
Taasisi ya kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU) yabaini kuwepo kwa sukari iliyofichwa tani 4,579.2 iliyonunuliwa toka Kiwanda cha Sukari Kilombero.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valentine Mlolowa Taasisi hiyo imeanza uchunguzi dhidi ya swala hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

UWAKILISHI WA NCHI KATIKA MASHINDANO YA KIMATAIFA


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lingependa kutoa ufafanuzi kuwa iwapo Bingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu 2015/16 inayoendelea atashinda pia taji katika fainali za Kombe la Shirikisho maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), ndiye atayeiwakilisha nchi katika michuano ya Ligi ya mabingwa wa Afrika msimu wa 2016/17.

FIFA YAILIMA FAINI SIMBA, YAPANGA KUISHUSHA DARAJA


Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), limeipiga faini ya Franc 2,000 za Uswisi (sawa na Sh 4,582,000 za Tanzania), Klabu ya Simba baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kupuuza maagizo ya Idara ya Utatuzi wa Migogoro (Desputes Resolution Chamber) ya shirikisho hilo.
Kamati ya idara hiyo iliyokutana na Aprili 20, 2016 huko Zurich, Uswis ilitumia Franc 500 (sawa na Sh 1,145,500) hivyo Simba pia imeagizwa kuzilipa ikiwa ni gharama za kikao cha kufuatilia utekelezaji sakata la mchezaji huyo, raia wa Kenya.

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANACHI MBALIMBALI AKIWA SAFARINI KUTOKEA DODOMA KUELEKEA ARUSHA KWA BARABARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia na mamia ya wakazi wa Babati Mkoani Manyara waliomsimamisha sehemu mbalimbali wakati akitokea Dodoma kuelekea mjini Arusha kwa njia ya barabara jana Mei 6, 2016. PICHA NA IKULU

TANZANIA UK DIASPORA TASKFORCE YATOA PONGEZI KWA DKT. ASHA ROSE MIGIRO.

Thursday, 5 May 2016

SNURA MUSHI AOMBA MSAMAHA KWA VIDEO YAKE YA 'CHURA'


Na Beatrice Lyimo- MAELEZO
05/05/2016
Dar es Salaam

Msanii wa kizazi kipya Snura Mushi amewaasa wasanii nchini kujisajili katika mamlaka zote zinazosimamia kazi za sanaa ili waweze kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa, kutambulika na kuiendeleza tasnia ya Sanaa nchini.

BILIONI 6 ZA RAIS DK. JOHN MAGUFULI KUNUNULIA MADAWATI ZAIBUA MAJIPU JESHINI

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Edosama Wood,  Research Center cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam, Edward Maduhu (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, akidai kutapeliwa na maofisa wa Jeshi la Magereza pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), katika utengenezaji wa madawati ya bei nafuu kama Rais Dk. John Magufuli alivyoagiza.

RITA YAANZA KUKUSANYA ADA ZA USAJILI KWA NJIA YA ELEKTRONIKI

Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Sheria na Katiba

Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma
Serikali inaendelea kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli ili kuchangia upatikanaji wa fedha za kusaidia kuimarisha na kuendeleza miradi ya maendeleo nchini. 
Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) imekuwa miongoni mwa taasisi za Serikali ambayo imeanza kukusanya ada zote zitokanazo na huduma inazotoa kwa njia ya kielekroniki kwa wadau wake kufanya malipo kwa njia ya simu au benki kabala ya kupata huduma wanayohitaji.

TANAPA KUBADILI MFUMO WA UTENDAJI KAZI KUTOKA KIRAIA KUWA JESHI USU

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Allan Kijazi (kulia) akimuongoza Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi kuelekea katika uwanja wa Mafunzo katika kambi ya Mlele kwa ajili ya kufunga Mafunzo ya Wahifadhi na Askari wapya waajiriwa wa shirika hilo.

MAREKEBISHO YA KANUNI ZA LIGI KUU 2016/17


Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka (TFF) imezipongeza timu za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kushiriki na kufanya msimu wa Ligi Kuu Bara kuwa ya Vodacom 2015/16 kuwa wenye mafanikio.

ERASTO NYONI AIPONZA AZAM, YANYANG'ANYWA POINTI TATU


Timu ya Azam FC ya Dar es Salaam, imenyang'anywa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu uliyoupata katika mechi Na. 156 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City.

LAMPTEY NDIYE ATACHEZESHA MECHI YA YOUNG AFRICANS, ESPERANCA JUMAMOSI


Mwamuzi Joseph Odartei Lamptey wa Ghana (pichani), Jumamosi Mei 7, 2016 anatarajiwa kuwa mwamzi wa kati katika mchezo wa kimataifa kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika utakaozikutanisha timu za Young Africans ya Dar es Salaam, Tanzania na GD Sagrada Esperanca ya Angola.

Wednesday, 4 May 2016

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI WATAKIWA KUJIPANGA NA KUKAMILISHA MIRADI YA ULGSP


Wakurugenzi wa Halmashauri zinazotekeleza mradi wa Uboreshaji Miji Tanzania (ULGSP) wametakiwa kuangalia maeneo yote yanayokwamisha utekelezaji wa mradi na kuyafanyia kazi kwa kuyaboresha ili kuweza kwenda sambamba na muda uliopangwa kukamilisha utekelezwaji wa mradi huo.

MITANDAO KIBOKO YA VYOMBO VYA HABARI ASILIA (MAGAZETI, RADIO, TV)

Vyombo vya habari vya asilia hususan magazeti vinakufa. Hivi sasa vvyombo hivyo vinajikongoja kutokana na  mauzo hafifu  na mdororo wa mapato kutoka matangazo na kupunguza wafanyakazi. 
Ila wakati idadi ya wasomaji wa habari mtandaoni ikizidi kukua, wanaoperuzi mtandaoni  humo hawatumii muda mwingi kwenye magazeti tando, utafiti wa Pew Research Centre unaeleza. 

TAARIFA KWA WANACHAMA WA TANZANIA BLOGGERS NETWORK (TBN) KUHUSU SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI



Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini 'Tanzania Bloggers Network' – TBN inawaomba wanachama wake wote kutotumia taarifa ama habari au picha yoyote kutoka katika mkutano wa maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari (WPFD) unaofanyika kitaifa mkoani Mwanza.

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA NCHINI (TIRA) YAKUTANA NA WADAU WAKE JIJINI MBEYA .

Meneja wa Kanda Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini  (TIRA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Ndugu Hiraly Maskini akifungua Mkutano wa  wadau wa soko la Bima kutoka Mikoani ya Nyanda za Juu Kusini  (hawapo pichani) katika ukumbi wa Mikutano Mkapa jijini Mbeya Mei 3 -2016 mkutano ambao unalengo la kujadili na kutambua changamoto mbalimbali wanazo kutana nazo wadau hao katika kutekeleza majukumu yao.(Picha Emanuel Madafa,Jamiimojablogu-Mbeya) 

SOMA HOTUBA YA RAIS MAGUFULI WAKATI WA MEI MOSI DODOMA 2016

Rais John Magufuli

HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWENYE KILELE CHA SIKUKUU YA WAFANYAKAZI DUNIANI MEI MOSI 2016 ITAKAYOFANYIKA DODOMA

Mhe. Samia Hassan, Makamu wa Rais;
Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu;
Ndugu Gratian Mukoba, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA);
Mama Nortubunga Maskini, Makamu wa Rais wa TUCTA;
Mheshimiwa Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu;
Mhe. Tulia Ackson, Naibu Spika;
Balozi Injinia John Kijazi, Katibu Mkuu Kiongozi;

Mheshimiwa Jordan Rugimbana, Mkuu wa Mkoa wa   Dodoma;
Waheshimiwa Mawaziri wote, na Waheshimiwa Wabunge mliopo;
Bi. Mary Kawar, Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), Ofisi ya Nchi za Afrika Mashariki;
Waheshimiwa Mabalozi mliopo;
Waheshimiwa Majaji,
Mheshimiwa Almas Maige, Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania;
Dr. Aggrey Mlimuka, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE);
Ndugu Nicholaus Mgaya, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA);
Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi;
Viongozi na Maafisa wa Serikali mliopo;
Wawakilishi wa Vyama vya Siasa mliopo; Mzee Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM
Bwana Kimbisa (Mb), Mwenyekiti wa CCM Mkoa;
Wanahabari;
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma;
Ndugu Wananchi;
Ndugu Wafanyakazi;
Mabibi na Mabwana.
Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa uhai na afya njema na kuweza kukutana hapa. Leo ni siku muhimu sana. Tupo hapa kwa ajili ya kuenzi na kuthamini mchango wa wafanyakazi wa Tanzania, wake kwa waume, walioko sekta binafsi na ya umma, na  ambao kila siku tangu asubuhi hadi jioni wamekuwa wakivuja jasho kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu.

TAASISI YA MISAADA YA KIJAMII YA HAMISI KIGWANGALLA KUMSOMESHA GETRUDE CLEMENT

a32603a8-b5b0-41d7-8533-7baf03333277
Mwanzilishi wa Taasisi ya Misaada ya Kijamii ya Hamisi Kigwangalla, Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha moja na Getrude Clement ambaye atalipiwa ada ya kidato cha tano na cha sita.
Kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa kizazi cha miaka ijayo, Taasisi ya Misaada ya Kijamii ya Hamisi Kigwangalla iliyoanzishwa na Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla imejitolea kumlipia ada Getrude Clement kwa masomo yake ya kidato cha tano na sita.

KUTANA NA ‘GREEN VOICES’, SAUTI ZA AKINAMAMA WAPAMBANAO NA MABADILIKO YA TABIANCHI

Akinamama wanaoshiriki katika mradi wa kupaza sauti za wanawake wanaopambana na mabdiliko ya tabianchi – Green Vocies katika picha ya pamoja na viongozi wa Foundation For Women of Africa na wafadhili wa mradi huo, mara baada ya uzinduzi wa mradi huo Madrid, Spain hivi karibuni.

Mama Maria Tereza (katikati) - Rais wa taasisi ya Foundation for Women of Africa akiwa na waandishi wa habari wanaotekelza mradi wa Green Voices wakati wa hafla ya kuwakaribisha kinamama nchini Spain. Kutoka kushoto ni Secelela Balisidya, Tukuswiga Mwaisumbe, Farida Hamis, Siddy Mgumia na aliyechuchumaa Judica Losai.

Tuesday, 3 May 2016

MAAZIMISHO YA SIKU YA MUZIKI WA JAZZ ILIVYOADHIMISHWA DAR

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza akizungumza na wadau wa Sanaa kwenye maadhimisho ya Siku ya Muziki wa Jazz duniani yaliyofanyika mapema wiki hii katika Ukumbi wa Baraza hilo ulioko Ilala Sharif Shamba jijinI Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Msanii mkongwe John Kitime na Mkuu wa Kitengo cha Matukio kutoka BASATA Kurwijira Maregesi.

MAPOROMOKO YA ARDHI WILAYA YA MOSHI YAMSHTUA MBUNGE WA JIMBO LA VUNJO ,JAMES MBATIA

Mbunge wa Jimbo la Vunjo akisalimiana na mmoja wa waathirika wa mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni na kusababisha kufusi kilichokuwa kando ya nyumba yake kuporomoka na kuhatarisha maisha yake katika kijiji cha Iwa ,Kirua Vunjo katika wilaya ya Moshi.

KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII,MEJA JENERALI GAUDANCE MILANZI AWASILI MKOANI KATAVI KWA AJILI YA KUFUNGA MAFUNZO YA MFUMO WA JESHI USU KWA WAHIFADHI WA SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA)

Ndege ndogo ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) iliyombeba Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Mpanda ,Meja Jenerali Milanzi anatarajia kufunga rasmi Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Askari waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) yaliyofanyika katika Kambi ya Mlele iliyopo Hifadhi ya Taifa ya Katavi.

TAARIFA KWA WATANZANIA WOTE WAISHIO NCHINI UINGEREZA [TUJUMUIKE UK].


Kikosi kazi cha watanzania wanaoishi Falme za UINGEREZA na EIRE YA KASKAZINI (TZUK Diaspora Taskforce, kwa kifupi, TZUK-DTF) kiliasisiwa na Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe mwaka 2014, kutokana na kutokuwepo na chombo/Jumuiya madhubuti ya kuwaunganisha Watanzania waishio hapa Uingereza.

KESSY: WABUNGE WAPENDA RUNINGA NENDENI SALUNI

 
kaimu katibu mkuu wa UVCCM taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa ananyesha baadhi ya kadi za chadema ambazo zilirudishwa katika mkutano huo wa adhara

MRADI WA KUKUZA TEKNOLOJIA KUPITIA WATOTO XPRIZE WAZINDULIWA DODOMA

Profesa-Msanjila
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Simon Msanjila (kulia) akitoa hotuba ya ufunguzi wa mradi wa kukuza teknolojia kupitia watoto XPRIZE uliofanyika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller, Kaimu Mkurugezi wa Elimu ya Msingi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Kassim Kaoneka na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bi. Zulmira Rodrigues. (Picha na Modewjiblog)

MBUNGE WA JIMBO LA VUNJO ATEMBELEA BARABARA YA KILEMA NA KUJIONEA ILIVYO HARIBIKA VIBAYA KUTOKANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA

Mbunge wa Jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitizama barabara ya kuelekea Hospitali ya wilaya ,Kilema Hospital namna ambavyo imeharibika kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha.

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ATUNUKU VYETI KWA WASHIRIKI WA KAMPENI YA SIKU 10 YA USAFI KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA MLIMA KILIMANJARO (KINAPA)

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky akitoa vyeti kwa wawakilishi wa Kampuni mbalimbali zilizosaidia katika kampeni ya siku 10 ya kufanya usafi katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA),Zoezi la utoaji Vyeti limefanyika katika lango la Marangu wakati wa hafla fupi ya kuwapokea washiriki wa zoezi hilo la usafi.

NYASA BOY ASHINDWA KUTOA VIDEO YA CHONGOROA KISA HAJAMZOEA VIDEO QUEEN WAKE

Msanii Chipukizi kutoka Jijini Mwanza, "Nyasa Boy" (Kushoto) amesema ilimchukua miezi minne hadi kuzoeana na Mlimbwende "Mwanne" (kulia) ambae ameshiriki kwenye video ya wimbo wake uitwayo "Chongoroa".

MAZISHI YA MZEE PIUS MKUNJA YAFANYIKA MKOANI MOROGORO

Mazishi ya Marehemu Mzee Pius Joseph Mkunja (90), aliefariki April 25,2016 katika Hospitali ya Rufaa Bugando Mkoani Mwanza yamefanyika Mkoani Morogoro. 

MBUNGE WA VUNJO JAMES MBATIA AKABIDHI MSAADA WA CHAKULA KWA WAHANGA WA MAFURIKO.

Diwani wa Kata ya Kahe, Rodrick Mmanyi akizungumza baada ya Mkurugenzi wa Idara ya Maafa nchini,Brigedia Jenerali ,Mbazi Msuya kutembelea kata hiyo kutizama athari zilizotokana na mafuriko.