Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday, 1 June 2014

WANASIASA WAKWAMISHA ZOEZI LA USAFI

Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot.com, Arusha

MWENYEKITI kamati ya usafi mkoa wa Arusha Adolf Ulomi amesema kuwa zoezi la usafi wa Jiji la Arusha bado unakabiliwa na changamoto kubwa hasa ya baadhi ya wanasiasa kuingiza siasa kwenye usafi jambo ambalo wakati mwingine linafanya Jiji kuonekana bado chafu.
Ulomi aliyasema hayo jana katika eneo la Kwa Murombo wakati Kamati hiyo ikiendelea na usafi wa Jiji na kuhusisha wananchi pamoja na wafanyabiashara wa eneo hilo.
Alisema kuwa pamoja na kuwa kamati hiyo ya usafi imejidhatiti katika kuhakikisha kuwa Jiji la Arusha linakuwa safi lakini baadhi ya wanasiasa wa Mkoa wa Arusha wanatumia vyeo vyao kupotosha maana halisi ya Kamati hiyo lakini pia umuhimu wa jiji kuwa safi.
Alifafanua kuwa baadhi ya wanasiasa hao mara nyingine wanadai kuwa wanawaonea huruma wananchi hasa wale ambao wanaharibu mazingira huku baadhi ya wananchi hao nao wakitumia muda huo kuchafua hali ya usafi wa  jiji  kwa kisingizo kuwa wamepewa ruhusa na wanasiasa wao.
“Pamoja na kuwa kweli tunajitaidi sana katika kuhakikisha kuwa lakini tukipita tu na kufanya usafi kisha kuwaambia wananchi umuhimu wa kufanya mazingira na miji yao basi wanasiasa nao  wanarudi na kuwapa moyo wananchi waendelee kuchafua kwani wanaonewa sasa hali hii kweli inatukwamisha sana," alisema Ulomi.
Pia alisema wanasisasa wanatakiwa kuiga mfano wa usafi kwenye miji mingine ambayo imeendelea duniani na hata baadhi ya Miji hapa Nchini ukiwemo mji wa Moshi jinsi ambavyo wameungana na kisha kuwabana baadhi ya wananchi wanaochafua mazingira jambo ambalo limekubalika na limejengeka kuwa usafi ni wa jamii na wala sio wa Serikali.
Aliishauri Serikali kuwa inatakiwa kuwa bunifu zaidi kwenye sekta ya uwekezaji kwani kama sekta hiyo ikiwa ni kubwa hata wafanyabiashara wadogowadogo(Machinga) ambao wakati mwingine wanauza bidhaa zao bila kujali usafi wa Mji wataweza kuwa na ajira.
Ulomi alifafanua kuwa kwa sasa katika mji wa Arusha asilimia kubwa ya wafanyabiashara wadogo wanafanya biashara zao kila kona ya Mji wa Arusha lakini kama kungekuwa na fursa za uwekezaji nyingi basi wangezitumia vema hivyo hata usafi ungeimarika zaidi.
Alimalizia kwa kusema kuwa hata wafanyabiashara hao ambao wanajitafutia riziki zao za kila siku pembezoni mwa Jiji wa Arusha wanatakiwa kuuza bidhaa zao lakini wakiwa wanazingatia kanuni za usafi ili kuweza kutoa sifa kwa mji wa Arusha ambao unasifika duniani kote.

WANAWAKE 100 WAELIMISHWA UJASIRIAMALI ILI KUACHANA NA 'UGOLIKIPA'


Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha
ZAIDI ya wanawake 100 wa Kanisa la Sinai Healing Center lililopo ngusero wamenufaika bure  na elimu ya ujasiriamali wa kutengeneza bidhaa mbali mbali  zitakazowawezesha kuachana na hali ya utegemezi kwa waume zao.
Aidha wanawake wakiacha kuwa tegemezi taifa la kesho  litaendelea tofauti na sasa ambapo wengi wao wamekuwa magolikipa hali inayoangusha familia zao na taifa kwa ujumla.
Nabii Debora Haruna wa kanisa hilo alisema kuwa yeye aliamua kuchukua jukumu hilo la kujifunza kutengeneza bidahaa mbali mbali na hatimaye akajitolea kuwafundisha wanawake hao ili kuwawezesha kujikwamua katika hali ngumu ya maisha.
Alieleza kuwa kabla ya kuchukua hatua hiyo ya kutoa elimu hiyo ya ujasiriamali alikuwa anapokea malalamiko toka kwa wanawake hao kuwa hawajaachiwa matumizi na waume zao huku wengine wakishindwa hata kuhudumia familia zao kutokana na wao kukosa shughuli za kuwaingizia kipato.
Nabii Haruna aliongeza kuwa kutokana na elimu hiyo aliyowapatia akinamama hao imeasaidia klwa kiwango kikubwa kuwasaidia kuweza kujikimu kimaisha huku wakiweza hata kuwasaidia wanaume zao katika kuendeleza familia zao tofauti na hapo awali walipokuwa wakisubiria tu kutoka kwa wanaume.
“Hawa wanawake nimewafundisha ujasiriamli ili wasaidiane katika maisha kwa kuwa waliumbwa kama wasaidizi na sio magolikipa hali itasaidia sana hata familia zao kuinuka haraka kutokana na vipato wanavyojipatia kutokana na hizi bidhaa wanazozitengeneza wenyewe,” aliongeza Debora.
Alizitaja bidhaa wanawake hao walizonufaika kuzitengeneza kuwa ni pamoja kutengeneza batiki, sabuni za maji, keki za harusi, gesi, mishumaa,shampoo,dawa za chooni,dawa za kutoa machunusi, crips pamoja na vitu vinginevyo ambavyo kwa asilimia kubwa vimekuwa na mafanikio makubwa kwao na hivyo kuwafanya kuachana na hali ya utegemezi.
Vile vile nabii alieweza kutoa elimu hiyo ya ujasiriamali pamoja na mitaji  kwa watoto wenye umri wa kuanzia mika 15 hadi 17 ili kuwawwezesha kuepuka vishawishi wanavyokumbana navyo kwa kuwa mara nyingi watoto haswa wa kike wanadanganyikana kutokana na wao kukosa huduma wanazostahili  hivyo kupitia mitaji hiyo itawawezesha kujikimu kimaisha.

HISTORIA TAREHE KAMA YA LEO: MGODI WA MAKAA YA MAWE WALIPUKA NA KUUA 236 JAPAN


Tarehe kama ya leo mwaka 1965 mgodi wa makaa ya mawe wa Yamano jirani na Fukuoka, Japan ulilipuka na kuua watu 236. Janga hilo lingeweza kuepukwa kama waendeshaji wa mgodi huo wangeweka hata tahadhari za msingi. Miaka sita nyuma, wachimbaji saba walipoteza maisha yao na wengine 24 kujeruhiwa vibaya kwenye mgodi huo kutokana na kutokuwepo na njia za kiusalama. Lakini bado Juni Mosi, 1965, jumla ya wachimbaji 559 waliingia kwenye mgodi ambao haukuwa na vipimo vya methanometer – ambavyo vinatumika kudhibiti kiwango cha mentane – wala kuwa na ving’amuzi vya colorimetric, ambavyo vinabaini kiwango cha kemikali kwenye hewa. Yoshio Sakarauchi, waziri wa biashara na viwanda wa Japan, alijiuzuru kwa kashfa hiyo.

JUNI 1, 1980 – CNN YAANZA RASMI


KATIKA tarehe kama ya leo mwaka 1980, Kituo cha Luninga cha CNN (Cable News Network) cha Marekani, ambacho ni cha kwanza kabisa duniani kurusha matangazo yake kwa saa 4, kilianzishwa rasmi. Kituo hicho kilianza kurusha matangazo hayo majira ya saa 12 za jioni kwa saa za Mashariki – EST (saa 8 usiku kwa saa za Afrika Mashariki) yakitokea kwenye makao yake makuu jijini Atlanta, Georgia. Habari iliyoongoza siku hiyo ni jaribio la kutaka kuuawa kwa kiongozi na mtetezi wa haki za binadamu Vernon Jordan. CNN ilibadili mtazamo kwamba taarifa zinaweza kutangazwa kwa wakati maalum tu kwa siku. Wakati CNN inaanzishwa, habari za luninga zilikuwa zimetawaliwa na vituo vikubwa vitatu - ABC, CBS and NBC- ambazo zilikuwa zinatangaza kwa dakika 30 tu usiku. Awali ikitazamwa na Wamarekani milioni mbili tu majumbani, kwa sasa CNN inatazamwa na Wamarekani milioni 89 na zaidi ya watazamaji milioni 160 ulimwenguni kote.
CNN ilikuwa wazo la Robert "Ted" Turner, mfanyabiashara aliyeitwa “Mdomo wa Kusini”. Turner alizaliwa Novemba 19, 1938 mjini Cincinnati,Ohio, na familia yake ilihamia Georgia akiwa motto mdogo ambapo baba yake alikuwa anamiliki kampuni kubwa ya matangazo ya mabango. Baada ya baba yake kujiua mwaka 1963, Turner alichukua jukumu la kuiongoza kampuni hiyo. Mwaka 1970 alinunua kituo cha televisheni cha Atlanta ambacho kilikuwa kinaelekea kufa, kikiwa kinatangaza filamu za zamani, lakini yeye akakiimarisha na kuwa kikubwa. Turner pia alinunua timu ya baseball ya Atlanta Braves na ile ya mpira wa kikapu ya Atlanta Hawks na kuonyesha michezo yake kwenye kituo cha TBS (Turner Broadcasting System).


HABARI ZA MAUAJI KWENYE KAMBI YA JESHI WAKATI WA VITA KUU YA PILI ZAJULIKANA HADHARANI KWA MARA YA KWANZA
Mojawapo ya magari yaliyotumiwa na utwala wa Kinazi wa Hitler kuwaua Wayahudi huko Chelmno, Poland.

Tarehe kama ya leo mwaka 1942, gazeti change la mjini Warsaw, Poland, Liberty Brigade, linaripoti hadharani taarifa za kuuawa kwa gesi ya sumu kwa makumi ya maelfu ya Wayahudi huko Chelmno, kambi ya mauaji nchini Poland—karibu miezi saba baada ya zoezi la kuwaua wafungwa kuanza wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Mwaka mmoja nyuma, ulikuwa umeanzishwa mpango wa "Final Solution," wa kuwaua Wayahudi wa Ulaya ambapo Wayahudi 700 waliuawa kwa gesi ya sumu kwenye gari ambamo walikuwa wakisafirishiwa kupelekwa katika kijiji cha Chelmno, Poland. Gari hili la gesi ndilo likaja kuwa chemba ya mauaji ya Wayahudi 360,000 kutoka katika jumuiya 200 nchini Poland. ‘Faida’ ya mauaji hayo ilikuwa ni ya kimya kimya na haikuonekana.
Mwezi mmoja kabla ya mkutano wa Wannsee wa mwezi Januari 1942, ambapo maofisa wa Kinazi waliamua kuzungumzia rasmi mauaji ya Wayahudi, magari ya gesi ya sumu huko Chelmno yalitumika kuua hadi Wayahudi 1,000 kwa kutwa.
Mnamo Juni 1, 1942, habari ya kijana wa Kiyahudi, Emanuel Ringelblum, (ambaye alitoroka kwenye kambi ya mauaji huko Chelmno alikokuwa amelazimishwa kuzika miili ya watu waliokuwa wanamwagwa na magari yenye sumu), ikachapishwa na gazeti change la Kisoshalisti nchini Poland la Liberty Brigade. Ndipo Mataifa ya Magharibi yalipobaini unyama uliokuwa ukifanywa na Wanazi.

BENEDICT ARNOLD AFIKISHWA MAHAKAMANI WAKATI WA MAPINDUZI YA MAREKANI


Usikilizaji wa kesi ya Benedict Arnold ulianza huko Philadelphia, Pennsylvania. Baada ya kuonekana na rekodi safi huko nyuma mwanzoni mwa Mapinduzi ya Marekani, Arnold akashtakiwa kwa makosa 13 ya ukosefu wa uadilifu, ikiwemo kutumia vibaya magari ya serikali na kununua na kuuza vitu kwa magendo.
Japokuwa Arnold alifutiwa mashtaka yote, Jenerali George Washington akatoa amri ya kumweka ndani.
Wakati akiwa safarini katika kituo muhimu cha West Point kuona namna wanavyoweza kukabiliana na majeshi ya Uingereza, Arnold aliamua kumpuuza Washington na Wamarekani. Aliona kwamba hakuwa amezawadiwa au kushukuriwa kutokana na mafanikio yake ya kijeshi kwenye vita hivyo. Akaanza kuwasiliana na majasusi wa Uingereza kwa lengo la kuasi ili West Point iingie mikononi mwa Waingereza ambao tayari walikuwa wanaushikilia mji wa New York, hivyo kwa kuutwaa West Point wangeweza kuwa na nafasi ya kuzuia majeshi ya Marekani yaliyokuwa New England.
Mnamo Agosti 1780, Sir Henry Clinton alimpatia Arnold Pauni 20,000 kwa kuwapatia Waingereza askari 3,000 wa Marekani pamoja na kuusalimisha West Point. Arnold akamweleza Jenerali Washington kwamba West Point ilikuwa tayari kukabiliana na Waingereza wakati ukweli haukuwa hivyo. Pia alijaribu kuweka mtego wa kukamatwa kwa Jenerali Washington, mpango huo ungeweza kufanikiwa lakini taarifa yake ilichelewa kuwafikia Waingereza na Washington akatoroka. Mpango wa West Point kuangukia mikononi mwa Waingereza nao ulifeli wakati kanali mmoja wa Marekani alipopuuza amri ya Arnold ya kutoishambulia meli ya Waingereza.
Siri ya Arnold kusailiti ilifahamika kwa Wamarekani wakati ofisa mmoja wa Uingereza John AndrĂ©, aliyejifanya kama mesenja, alipokamatwa na kikosi cha AWOL cha Wamarekani waliokuwa msituni kaskazini mwa New York City.


WAJERUMANI WASHAMBULIA VIKOSI VYA UINGEREZA YPRES SALIENT

SIKU kama ya leo mwaka 1916, wakati vikosi vya wanamaji vya Ujerumani na Uingereza vilipopambana katika Bahari ya Kaskazini wakati wa Vita ya Jutland na Wafaransa wakipambana kuhakikisha Wajerumani hawautwai mji wa Verdun, vikosi vya Ujerumani vikaanzisha mashambulizi makubwa dhidi ya Uingereza huko Ypres Salient katika eneo la Western Front. Hii ilikuwa na wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.

KAMPUNI YA MAGARI YA NISSAN YAANZISHWA

Juni Mosi kama leo, mwaka 1934, kampuni ya Jidosha-Seizo Kabushiki-Kaisha (kwa Kiingereza Automobile Manufacturing Co., Ltd.) ya jijini Tokyo, yapata jina jipya na kuitwa: Nissan Motor Company.
Jidosha-Seizo Kabushiki-Kaisha ilianzishwa Desemba 1933. Nissan ilitengeneza gari lake la kwanza aina ya Datsun kwenye mtambo wake wa Yokohama mnamo Aprili 1935 na mwaka huo ikaanza kusambaza magari yake kwenda Australia. Kuanzia mwaka 1938 hadi wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Nissan ikaanza kutengeneza malori na magari ya vita. Majeshi ya Washirika yalikiteka kiwanda cha Nissan mwaka 1945 na hayakukirejesha hadi miaka kumi baadaye.
Mwaka 1960, Nissan ikawa kampuni ya kwanza ya magari ya Kijapani kutwaa tuzo ya Uhandisi ya Deming. Aina mpya ya magari ya Datsun kama Bluebird (1959),  Cedric (1960) na Sunny (1966) yaliweza kuongeza mauzo ya Nissan ulimwenguni.
  
WAMUUNGA MKONO NIXON VIETNAM

Jun 1, 1971: Tarehe kama ya leo mwaka 1971 kundi la Vietnam Veterans for a Just Peace linajitokeza hadharani kuunga mkono uamuzi wa Rais Richard Nixon wa kuendesha vita vya Vietnam.

VIGOGO WAKUTANA KUJADILI VIETNAM

Tarehe kama ya leo mwaka 1964 maofisa wa juu wa Marekani wakutana mjini Honolulu kwa siku mbili kujadiliana kuhusu Vita ya Vietnam. Waliohudhuria ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje Dean Rusk, Waziri wa Ulinzi Robert McNamara, Balozi Henry Cabot Lodge, Jenerali William Westmoreland, Jenerali Maxwell Taylor, na Mkurugenzi wa Idara ya Kijasusi ya Marekani (CIA) John McCone. Mjadala huo ulihusisha hali ya vita Kaskazini mwa Vietnam, ikiwemo maeneo 94 muhimu ya kushambulia.

VITA YA COLD HARBOR YAANZA

Tarehe kama ya leo mwaka 1864, majeshi ya Uingereza (Confederates) anavishambulia vikosi vya Union katika eneo la Cold Harbor, Virginia, karibu maili 12 kutoka Richmond. Hii ilikuwa wakati wa Vita vya Mapinduzi.
Tangu kuanza kwa mwezi Mei 1864, Jenerali wa Jeshi la Union Ulysses S. Grant alikuwa amejipanga kulishambulia Jeshi la Robert E. Lee Kaskazini mwa Virginia karibu na Richmond. Hali hiyo ilikuwa na madhara kwa Jeshi la Grant huko Potomac, ambapo watu 60,000 waliuawa.


URUSI YAMSHTAKI SHCHARANSKY KWA UHAINI

Tarehe kama ya leo mwaka 1977 wakati wa Vita Baridi, serikali ya Urusi ilimfungulia mashtaka ya uhaini Anatoly Shcharansky, kiongozi wa kutetea hali za Wayahudi na mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Russia. Kitendo hicho kilitazamwa na mataifa ya Magharibi kama changamoto ya moja kwa moja kwa Rais wa Marekani Jimmy Carter kuhusiana na sera yake mpya ya mambo ya nje kuhusu haki za binadamu na kupinga ukandamizaji wa Urusi.
Shcharansky, aliyekuwa na miaka 29 na mtaalam wa kompyuta, alikuwa mashuhuri katika kundi lililojiita ‘Helsinki Group’ katika Muungano wa Kisovieti. Kundi hilo lilianzishwa mwaka 1975, baada ya kusainiwa kwa Sheria ya Usalama ya Ulaya (European Security Act) ambayo pia inajulikana kama Helsinki Accords. Mkutano huo uliofanyika jijini Helsinki, Finland uliwahusisha viongozi wa Marekani na Urusi ambao waliamua kuwaalika viongozi wa nchi nyingine 35.
Shcharansky alishtakiwa kwa uhaini, hususan kwa kupokea msaada wa fedha kutoka CIA ili kuanzisha machafuko nchini Urusi. Baada ya mwenendo wa mashtaka, akahukumiwa kifungo cha miaka 14 jela. Baadaye akaachiliwa huru Februari 1986, baada ya yeye na wafungwa wengine wane walipobadilishana na majasusi wanne wa Urusi waliokuwa wamefungwa huko Magharibi. Hiki kilikuwa ni kipindi cha utawala wa Mikhail Gorbachev ambaye wakati anaingia madarakani mwaka 1985, aliahidi kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa ili kupoza hali ya hewa nchini Urusi. Pamoja na hali hiyo, wanachama wa kundi la Helsinki na vikundi vingine waliendelea kudai uhuru na demokrasia na haki za binadamu hadi Muungano wa Urusi ulipovunjika mwaka 1991.

Jun 1, 1941:

WAJERUMANI WATWAA MJI WA CRETE 1941

Tarehe kama ya leo mwaka 1941 wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, mji wa Crete, ambao ulikuwa ngome ya Majeshi ya Washirika nchini Ugiriki, unatwaliwa na Wajerumani katika mapambano makali.
Mwisho mwa mwaka 1940, jeshi la Ugiriki, likisaidiwa na jeshi la anga la Uingereza, lilifanikiwa kuizuia Italia isivamie nchi hiyo. Lakini Aprili 1941, ushindi huo ukawa kipigo wakati kiongozi wa Nazi, Adolf Hitler alipoliongoza jeshi lake ambalo halikuwa limepigwa ili kuishambulia Ugiriki. Jeshi la Ujerumani lilikwenda haraka na kuishambulia Ugiriki  kiasi kwamba Waingereza waliahirisha mpango wao wa kutuma vikosi vyao kuisaidia Ugiriki.
Aprili 23, mfalme wa Ugiriki na serikali yake walihamia Crete, kisiwa kilichoko kusini mwa Ugiriki, na Aprili 24 vikosi vya Majeshi ya Washirika vilihamia kisiwani humo. Wajerumani walishambulia meli hizo na kuua askari na mabaharia 15,000 wa vikosi vya Washirika. Hadi kufikia Aprili 29, askari 50,000 wa Uingereza, Ugiriki, Australia na New Zealand walikuwa wametua kisiwani humo.
Wiki tatu baadaye Wajerumani walianzia harakati za kuivamia Crete, na zaidi askari 20,000 wa miavuli wa Ujerumani walikuwa wametua kisiwani humo. Pamoja na mapambano makali, Wajerumani walifanikiwa kuutwaa mji huo na kufikia Juni 1, askari 20,000 waliosalia wa Vikosi vya Washirika walikuwa wametoroka.

Jun 1, 1900:

HOOVER ATEKWA KATIKA MACHAFUKO CHINA

Tarehe kama ya leo mwaka 1900, Herbert Hoover ambaye baadaye alikuja kuwa Rais wa Marekani, pamoja na mkewe Lou walikamatwa katikati ya machafuko nchini China maarufu kama Boxer Rebellion.
Baada ya kufunga ndoa mjini Monterey, California, mnamo Februari 10, 1899, Herbert na Lou Hoover waliondoka kwenda fungate nchini China, ambako Hoover alitarajiwa kuanza kazi mpya kama mshauri wa uchimbaji madini kwa mtawala wa China akiwa na kampuni ya Bewick, Moreing and Co. Wanandoa hao walikuwa wameoana katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja wakati kundi la wanaharakati la China lilipoasi dhidi ya wakoloni, wakwawakamata Wazungu 800 kwenye mji wa Tientsin. Hoover aliwaongoza wazungu wenzake kujenga kingo katika makazi yao ya mji huo wakati mkewe Lou alikuwa akisaidia katika hospitali. Inaelezwa kwamba, wakati wa machafuko hayo yaliyodumu kwa mwezi mmoja, Hoover aliwaokoa watoto wa Kichina katikati ya mapigano.
Baada ya vikosi vya majeshi ya ushiriki kuwaokoa akina Hoover na kuwasafirisha wazungu wengine nje ya China, Herbert Hoover akawa mmoja wa wamiliki wa Bewick, Moreing and Co. alikuwa waziri wa biashara chini ya marais Warren Harding na Calvin Coolidge kuanzia mwaka 1921 hadi 1924. Akawania urais mwaka 1928 na kushinda.


Jun 1, 1871:

JOHN WESLEY HARDIN AWASILI ABILENE 




Tarehe kama ya leo mwaka 1871, John Wesley Hardin, mmoja wa wahalifu wakubwa katika historia ya Marekani, aliwasili huko Abilene, Kansas, ambako alijenga urafiki wa muda na Marshal Wild Bill Hickok.
Hardin alianza tabia ya fujo na ugomvi tangu akiwa mdogo. Wakati akiwa na miaka 14, nusura amuue kijana mmoja wakati wakigombea msichana, akimchoma mara mbili kwa kisu. Mwaka mmoja baadaye akamuua mwanamume mwenye asili ya Kiafrika wakati walipopambana katika mieleka. Wakati anakwenda kufungwa jela mwaka 1878, Hardin alidai kwamba alikuwa amewaua watu 44.
Mwaka 1871, wakati Hardin akiwa na miaka 18, mmiliki mmoja wa ranchi wa Texas akamwajiri kijana huyo kuongoza kundi la ng’ombe kutoka Chisholm Trail kwenda Abilene, Texas. Hardin alikuwa anatamani kuondoka Texas, kwani siku chache kabla, alikuwa amemuua polisi wa Texas aliyekuwa akimsafirisha yeye kumpeleka Waco kusikiliza kesi yake. Hardin alitaka aishi maisha ya kujificha, lakini akashindwa kuzidhibiti hasira zake kwa muda mrefu. Wakati akiswaga ng’ombe, kundi la ng’ombe wa jamaa mmoja wa Mexico likachanganyika na ng’ombe aliokuwa nao Hardin. Alipolalamika kwa Mexico aliyekuwa akiswaga ng’ombe hao, wakashindwa kuelewana, hivyo akaamua kumpiga risasi ya kwenye moyo.
Wakati Hardin alipowasili Abilene, Kansas, siku kama ya leo mwaka 1871, kiongozi wa mji huo, Wild Bill Hickok, hakuwa na haja ya kumshtaki mtu aliyeua nje ya himaya yake. Badala yake akawa amempenda kijana huyo ambaye alikuwa amemzidi miaka 16 na wakawa marafiki, japo urafiki wenyewe ulikuwa wa mashaka. Kama ilivyokuwa kwa wanasheria wa magharibi, Wildd Bill Hickok alikuwa amefanya mauaji kadhaa. Lazima alikuwa ameona kitu ndani ya Hardin ambacho kilimvutia, akiamini kwamba kwa tabia yake ya hasira angeweza kumtumia. Kwa upande wake, Hardin alifurahi kuwa rafiki wa mtu huyo maarufu kwa upigaji bunduki.
Kwa wiki kadhaa, Hickok na Hardin walikunywa pamoja na walichangia wasichana, lakini imani ya Hickok kwa kijana huyo ilikuwa ndogo. Wakati akiwa Abilene, Hardin alikodi chumba katika hoteli ya Amerina House. Usiku mmoja, mgeni mmoja wa chumba cha jirani alikuwa anakoroma sana. Hardin alikerwa mno na kitendo hicho hivyo akaanza kufyatua risasi ili kumnyamazisha. Risasi ya kwanza ilimshtua mgeni huyo, lakini ile ya pili ilimnyamazisha moja kwa moja.
Hardin akabaini kwamba urafiki wake na Hickok wala usingemsaidia. "Niliamini," Hardin alisema baadaye, "kwamba kama Wild Bill angenikuta katika hali nisiyo na msaada, wala asingesikiliza maelezo, bali angeniua ili aongeze kwenye orodha yake." Akiwa amevaa singland, Hardin alitoroka kupitia dirisha la hoteli na kuingia mitaani. Usiku huo akajificha kwenye jumba la kufugia farasa, alfajiri na mapema akaiba farasi mmoja na kwenda kwenye kambi ya ng’ombe. Siku iliyofuata akaelekea Texas, hakurudi tena Abilene.

Alikufa mwaka 1895 baada ya kupigwa risasi mgongoni na polisi wa El Paso. Alikuwa na miaka 42.

BURIANI ZAMANI: HELEN KELLER, GEORGE MIKAN

GEORGE MIKAN AFARIKI DUNIA


Mnamo Juni 1, 2005, mchezaji mkongwe wa mpira wa kikapu aliyekuwa kwenye Orodha ya Wakongwe wa mchezo huo (Hall of Fame), George Mikan, alifariki dunia akiwa na miaka 80. Kivutio halisi cha mchezo wa kikapu wa kulipwa, Mikan aliwavutia mashabiki wengi kwenye mechi za NBA katika kipindi ambacho ligi ya mchezo huo haikuwa na uhakika kama ingeweza kushamiri.
George Lawrence Mikan alizaliwa Juni 18, 1924, mjini Joliet, Illinois, na alikuwa na urefu wa futi 6 na inchi 8 wakati anamaliza shule. Alijiunga na Chuo Kikuu cha DePaul, ambako kocha Ray Meyer alifanya kazi ya ziada kumbadili ‘ngongoti’ huyo kuwa nyota. Alimhamasisha Mikan kujenga stamina yake na kuruka kamba ili awe mwepesi. Akiwa chini ya Meyer, Mikan alibadilika na kuwa mchezaji asiyezuiliwa ndani ya DePaul, ambako alikuwa akiharibu muvu za wachezaji wa timu pinzani kiasi kwamba mwaka 1944 NCAA ikaamua kuweka sheria ya kudhibiti “ugolikipa”. Mwaka 1945, Mikan aliiongoza DePaul kupata ushindi dhidi ya Bowling Green na kutwaa taji la NIT na akatangazwa kuwa Mchezaji Mwenye Thamani Kubwa wa mashindano hayo.
Baada ya kumaliza chuo, Mikan alikwenda kucheza Ligi ya Taifa ya Basketball (NBL) akiwa na klabu ya Chicago Gears, ambayo aliiongoza ikatwaa ubingwa wa NBL mwaka 1947. Pamoja na urefu wake wa futi 6 na inchi 10 bado aliendelea kuwa mchezaji mahiri zaidi wa kikapu nchini humo. Alichezea klabu ya Minneapolis Lakers mpaka ligi ya kikapu ilipoanza kuitwa NBA.
Mwaka 1950, shirika la habari la Associated Press lilimtangaza Mikan kama mchezaji bora wa kikapu wa nusu karne ya 20.


HELEN KELLER AFARIKI

Mnamo Juni 1, 1968, Helen Keller, mwandishi na mwalimu aliyekuwa kipofu na kiziwi tangu utoto, alifariki dunia akiwa na miaka 87. Ulemavu wa macho na kutokusikia haukuweza kumzuia Keller kuwa mwandishi maarufu ulimwenguni.
Helen Adams Keller alizaliwa Juni 27, 1880, katika shamba karibu na Tuscumbia, Alabama. Akiwa mtoto alipata ugonjwa wa scarlet fever  akiwa na miezi 19 tu, ambao ukamfanya kuwa kipofu na kiziwi. Kwa miaka minne aliishi nyumbani tu. Elimu maalum kwa vipofu na viziwi ndiyo kwanza ilikuwa inaanza wakati huo, na ilikuwa hadi alipofikisha miaka sita ndipo wazazi wake wakampeleka kwa daktari bingwa wa macho. Daktari huyo akawaambia wazazi wa Keller wakamuone Alexander Graham Bell, mvumbuzi wa simu na muasisi wa kufundisha lugha za alama kwa vipofu. Bell akamchunguza Helen na akaweka utaratibu wa kuwa na mwalimu ambaye atakuwa anakwenda nyumbani kwa akina Keller akitokea Taasisi ya Vipofu ya Perkins mjini Boston.
Mwalimu huyo, Anne Sullivan aliyekuwa na miaka 20, naye alikuwa na uone hafifu, lakini alikuwa amepewambinu za kufundisha vipofu.
Keller aliendelea kufanya vizuri katika elimu yake na kupelekwa katika shule mbalimbali za wenye ulemavu wa macho mpaka akamalicha chuo cha Cambridge huko Massachusetts. Mwaka 1900, akakubaliwa kujiunga na chuo cha Radcliffe, kikiwa chini ya kitivo cha Chuo Kikuu cha Harvard. Akiwa kwenye chuo hicho ndipo alipotoa kitabu chake cha kwanza cha The Story of My Life, ambacho kilichapishwa mfululizo kwenye jarida la The Ladies Home na baadaye kitabu kamili.

Baada ya kumaliza chuo, Keller akawa mwandishi mahiri na kutoa vitabu kama The World I Live In (1908), Out of the Dark (1913), My Religion (1927), Helen Keller's Journal (1938), na Teacher (1955). Mwaka 1913, akaanza kufundisha kwa msaada wa mfasiri, mwanzoni kwa niaba ya American Foundation for the Blind. Kazi zake nzuri kwa niaba ya viziwi zilimfanya katunukiwa nishani ya Presidential Medal of Freedom, ambayo ni nishani ya juu zaidi kwa taifa hilo kwa watu wa kawaida, na alitunukiwa na Rais Lyndon B. Johnson.

Moderator anasema: Tutumie picha na maelezo kwa ajili ya kumbukumbu za wapendwa wetu, nasi tutazitundika mtandaoni bure bilashi.

'HAPPY BIRTHDAY' MARILYN MONROE, EPHRAIM MADEJE, JAVIER HERNANDEZ ‘CHICHARITO’, MORGAN FREEMAN!


MARILYN MONROE

Huyu alikuwa mwigizaji aliyezaliwa Juni Mosi, 1926 huko Los Angeles, California, Marekani. Alifariki Agosti 5, 1962 akiwa na miaka 36.
Mwanamama huyo aling’ara katika filamu ya Some Like It Hot na akawa mwanamke mashuhuri zaidi duniani katika miaka ya 1950. Filamu yake nyingine maarufu I pamoja na ile iliyotoka mwaka 1955 iitwayo The Seven Year Itch na zile za mwaka 1953 - Gentlemen Prefer Blondes na How to Marry a Millionaire.
Alikuwa mwanamitindo wa Blue Book kabla ya kubadili jina lake kutoka Norma Jeane Mortenson kuwa Marilyn Monroe, baadaye alibatizwa na kupewa jina la mama yake Norma Jeane Baker. Alikuwa ni msichana kutoka kijijini, lakini akawa mwanamke mrembo na mashuhuri ndani ya Hollywood ambaye alikuwa na uhusiano na JFK na Robert Kennedy. Aliolewa na Joe DiMaggio mwaka 1954, lakini ndoa hiyo ilidumu kwa miezi tisa tu. Alishirikiana na Tony Curtis katika filamu ya Some Like It Hot.
Mnamo Juni 1962, kampuni ya filamu ya 20th Century Fox aliyokuwa akiifanyia kazi ilimfukuza mwigizaji huyo baada ya kutoonekana mara kadhaa katika maandalizi ya filamu ya Something’s Got to Give. Mnamo Agosti 5, 1962, Monroe alikutwa amekufa baada ya kujiovadozi na madawa akiwa nyumbani kwake Brentwood, California.

EPHRAIM NEHEMIA MADEJE



Alizaliwa Juni Mosi, 1946. Leo hii ametimiza miaka 68. Huyu ni Mbunge wa zamani wa Dodoma Mjini tangu mwaka 2005 hadi 2010 alipodondoka. Elimu ya Msingi aliipata katika shule za Chamuhawi, Mpwapwa (1953 hadi 1956) na Mpwapwa Middle School (sasa Mtejeta) kati ya mwaka 1957 na 1960. Akajiunga na Mkwawa Sekondari kwa masomo ya Kidato cha Kwanza hadi cha Nne (1961 hadi 1964) na baada ya kufanya vizuri akajiunga na Kibaha Sekondari (1965 na 1966). Kati ya mwaka 1981 na 1984 alihitimu shahada ya kwanza katika Uchumi kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Miaka yote ya utumishi wake serikalini alikuwa mwajiriwa wa Shirika la Posta na Simu (TPTC) tangu mwaka 1967 hadi mwaka 1993 akipanda ngazi kutoka Mdhibiti wa Mihuri hadi Mkurugenzi wa Operesheni. Mwaka 1994 aliajiriwa na Tume ya Mawasiliano Tanzania akiwa Mkurugenzi hadi mwaka 2005 alipostaafu.

MORGAN FREEMAN


Mcheza sinema huyu mahiri alizaliwa Juni 1, 1937 huko Tennessee, Marekani na leo ametimiza miaka 77. Yeye ni mwigizaji, muongozaji, na msimuliaji ambaye alishinda Tuzo ya Academy katika eneo la Best Supporting Actor kwenye filamu ya Million Dollar Baby mwaka 2005. Huyu nguli ameshiriki filamu nyingi sana kama Bruce Almighty, The Dark Knight Trilogy, The Sum of All Fears, Thick As Thieves, Dolphin Tale na ile ya mwaka 2013 ya The Olympus Has Fallen.
Wakati akiwa na miaka tisa tu, alicheza nafasi ya mshiriki mkuu kwenye mchezo wa kuigiza shuleni kwao. Aliitosa scholarship ya kusomea uigizaji kwenye Chuo Kikuu cha Jason State na kwenda kufanya kazi kama fundi makanika wa rada katika Jeshi la Anga la Marekani mwaka 1955.
Mwaka 1967 alimuoa Jeanette Adair Bradshaw lakini wakaachana mwaka 1979. Baadaye akamuoa Myrna Colley-Lee mwaka 1984, lakini wakatengana mwaka 2010.

JAVIER HERNANDEZ ‘CHICHARITO’


Mshambuliaji wa Manchester United na timu ya Taifa ya Mexico, maarufu kama Chicharito, alizaliwa siku kama ya leo mwaka 1988 na ametimiza miaka 26.
Dogo huyu aliweka rekodi ya pekee kwa kuwa mchezaji wa kwanza wa Mexico kuichezea Man United wakati alipojiunga nayo mwaka 2010. Mechi yake ya kwanza kuichezea Man United ilikuwa mwaka 2010 dhidi ya Newcastle United alipoingia kuchukua nafasi ya Wayne Rooney.
Alianza kuichezea timu ya taifa ya Mexico mwaka 2009 na amekuwa mmoja wa wafungaji hodari wa kipindi chote wa timu ya taifa.
Alicheza kucheza soka la kulipwa la vijana akiwa na miaka 15 katika klabu ya C.D. Guadalajara. Mwaka 2011 katika mashindano ya CONCACAF Gold Cup aliibuka mfungaji bora kwa kupachika mabao 7, akachaguliwa Mchezaji Muhimu Zaidi (MVP) wa mashindano hayo.
Baba yake, Javier HernĂ¡ndez Gutierrez, alikuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Mexico. was a Mexican international striker.

BRIAN COX

Mwigizaji huyu wa filamu alizaliwa siku kama ya leo nchini Scotland mwaka 1946 na ametimiza miaka 68.
Amecheza filamu nyingi lakini miongoni mwa filamu hizo ambazo zilimpatia umaarufu mkubwa ni ile ya mwaka 2004 iitwayo Troy 2004 na filamu ya historia ya vita Braveheart ya mwaka 1995. Alicheza kama Hannibal Lecter kwa mara ya kwanza katika filamu ya Manhunter mwaka 1986.
Alilelewa na dada zake wanne baada ya wazazi wake kufariki akiwa na miaka 8. Alipofikisha miaka 14, akawa mwanachama wa Dundee Repertory Theatre.
Ametajwa mara kadhaa katika tuzo za Golden Globe kutokana na kushiriki mfululizo wa tamthiliya ya Nuremberg ya mwaka 2000.
Alimuoa mkewe wa pili, Nicole Ansari, mwaka 2002 baada ya kutalikiana na Caroline Burt mwaka 1986. Miongoni mwa watoto wake wanne ni mwigizaji na mshindi wa Tuzo ya Emmy, Alan Cox. Alishirikiana na Hugh Jackman akicheza kama adui katika filamu ya X2: X-Men United.

DANIELLE HARRIS


Mwigazaji huyo mrembo aliyezaliwa jijini New York mwaka 1977 leo anatimiza miaka 37.
Alipata umaarufu zaidi na kuwa malikia wa filamu za kutisha aliposhiriki filamu ya Halloween. Pia alishiriki katika mfululizo wa filamu ya Hatchet akicheza kama Marybeth Dunston.
Safari yake ilianzia katika kufanya kazi za urembo. Akiwa mdogo alipata zawadi ya kusafiri kwa wiki mbili baada ya kushinda mashindano ya urembo. Mama yake anaitwa Fran na dada yake anaitwa Ashley.
Alishiriki pamoja na Christina Applegate katika filamu ya vichekesho iitwayo Don't Tell Mom the Babysitter's Dead.


FRANK MORGAN


Mwigazaji huyo alizaliwa siku kama ya leo mwaka 1890 jijini New York. Alifariki dunia Septemba 18, mwaka 1949 akiwa na miaka 59.
Anakumbukwa vyema jinsi alivyofanya vizuri akiigiza kama mchawi katika filamu ya The Wizard of Oz. ndani ya filamu hiyo pia alicheza kama Profesa Marvel, kocha na mlinzi wa Oz.
Alianza kuigiza akiwa na miaka 26 akipewa nafasi ndogo katika filamu ya The Suspect ya mwaka 1916.
Alichaguliwa mara mbili kuwania Tuzo za Academy katika maisha yake, ikiwemo ya Mwigizaji Bora kwa kushiriki filamu ya The Affairs of Cellini ya mwaka 1934.
Yeye na mkewe Alma Muller, waliyeishi kwa miaka 45, walibahatika kupata mtoto mmoja, George.
Mwaka 1940 alicheza pamoja na James Stewart katika filamu ya mapenzi na vichekesho ya The Shop Around the Corner.

BRIGHAM YOUNG


Kiongozi huyu wa dini wa Marekani aliyezaliwa siku kama ya leo mwaka 1801 alikuwa Rais wa The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints kutoka mwaka 1847 hadi Agosti 29, 1877 alipofariki akiwa na miaka 76.
Pia anakumbukwa kutokana na kusaidia kuanzishwa kwa taasisi ambazo kwa sasa zinajulikana kama Vyuo Vikuu vya Utah na Brigham Young.
Mwanzoni kabisa alianzisha jumuiya ya Wamormon huko Kirtland, Ohio mara tu baada ya kufariki ka mkewe wa kwanza.
Siyo tu kwamba alianzisha Salt Lake City Utah, bali pia anahusika na kuanzishwa kwa Hekalu la Mormon.
Pamoja na kuwa kiongozi wa dini, lakini alikuwa bingwa wa kuoa mitala kwani alikuwa na wake 55 na watoto 56.
Millard Filmore alimteua kuwa msimamizi wa masuala ya Wahindi-Wamarekani katika himaya ya sasa ya Utah.

OLIVER JAMES


Mwigizaji huyu leo anatimiza miaka 34 tangu alipozaliwa na kukulia Surrey, England mwaka 1980.
Ni mwanamuziki, mtunzi na mwigizaji mahiri aliyeng’ara katika filamu ya What A Girl Wants. Pia alishiriki katika filamu za Roadkill, Without a Paddle: Nature's Calling, na Raise Your Voice.
Kabla ya kuwa staa, alionekana katika kipindi cha The Afternoon Play cha BBC ambamo alicheza kama Dave. Katika filamu ya Raise Your Voice alicheza na Hilary Duff na katika filamu ya What A Girl Wants alicheza na Amanda Bynes.

DAYANA MENDOZA


Mwanamitindo huyu alizaliwa siku kama ya leo mwaka 1986 nchini Venezuela. Yeye alizaliwa na kukulia Caracas, Venezuela. Huyu ni mlimbwende ambaye aliwahi kushinda taji la Miss Venezuela mwaka 2007 na Miss Universe mwaka 2008. Aliwahi kuwa jaji latika mashindano ya Miss USA 2012.

JUSTINE HENIN


Mchezaji tennis nyota wa kike duniani ambaye alizaliwa siku kama ya leo mwaka 1982 nchini Ubelgiji ambaye leo ametimiza miaka 32. Bingwa wa Ubelgiji ambaye alivuna pointi 7,626. Aliwahi kushika namba moja duniani, lakini kwa sasa amestaafu mchezo huo.
 Alifiwa na wazazi wake akiwa na miaka 17. Aliolewa na Pierre-Yves Hardenne mnamo Novemba 2002.

KELVIN


Mwanandinga Mbrazili aliyezaliwa mjini Parana siku kama ya leo mwaka 1993 na anatimiza miaka 21. Yosso huyo anachezea klabu ya FC Porto ya Ureno aliyojiunga nayo mwaka 2011 akitokea Parana, akafanikiwa kutwaa ubingwa wa soka wa Ureno (Primeira Liga) msimu wa 2012-2013. Alianza kusakata kabumbu katika timu ya vijana ya Parana kabla ya kuingia kwenye kikosi cha kwanza. Katika msimu wa 2011-2012 alicheza kwa mkopo katika klabu ya Rio Ave.

JACQUES MARQUETTE


Mpelelezi na Mmisionari huyu wa Kanisa la Jesuit alizaliwa tarehe kama ya leo mwaka 1637 huko Ufaransa. Alifariki Mei 18, 1675 akiwa na miaka 37. Yeye ndiye aliyegundua makazi ya kwanza ya Wazungu huko Sault Ste. Marie, Michigan nchini Marekani. Alikuwa ametumwa na kanisa lake katika eneo la Quebec mwaka 1666. Marquette na Louis Jolliet walikuwa Wazungu wa kwanza kuuona na kukatisha eneo la kaskazini la Mto Mississippi mwaka 1673. Alikulia Ufaransa akilelewa na mapadre na watawa. Chuo Kikuu cha Marquette University nchini Marekani kiliitwa kwa jina lake.

SAIGON


Rapa wa Marekani aliyezaliwa New York tarehe kama ya leo mwaka 1977. Jina lake halisi ni Brian Carnard. Yeye pia ni mwigizaji ambaye anatumia jina hilo katika kipindi cha luninga cha Entourage cha TV ya HBO. Mwishoni mwa miaka ya 1990 alishtakiwa kwa makosa ya kumshambulia mtu. Aliamua kutumia jina la Saigon baada ya kusoma kitabu cha mwandishi Wallace Terry kuhusu Vita ya Vietnam akiwa gerezani. Ana binti anayeitwa Rayne Dior Carenard.

POWERS BOOTHE



Mwigizaji huyu wa luninga ambaye anatumia jina la Lamar Hampton katika kipindi cha Nashville alizaliwa tarehe kama ya leo mjini Texas mwaka 1948. Alijiunga na Tamasha la Oregon Shakespeare kushiriki katika nafasi mbalimbali za michezo ya kuigiza ukiwemo wa Henry IV. Alicheza nafasi ndogo katika filamu maarufu ya The Avengers. Amemuoa Pamela Ann Boothe. Filamu yake nyingine ni ile ya Blue Sky aliyocheza na Jessica Lange.

Ujumbe wa Moderator: Tutumie picha na tarehe yako ya kuzaliwa, nasi tutaitundika wakati unapofika.

BAO PEKEE LA MASSA LAWAVUSHA UGANDA HATUA INAYOFUATA, RWANDA YAIKANYAGA LIBYA 3-0

Football - 2014 Fifa World Cup Qualifier - Uganda Vs Angola - Mandela Stadium - Namboole - Kampala
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

UGANDA The Cranes imefanikiwa kusonga hatua inayofuata katika michuano ya kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka tiketi ya kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika, AFCON 2015 nchini Morocco baada ya kufanikiwa kuiondosha Madagascar kwa wastani wa mabao 2-2, lakini Uganda wamenufaika kwa faida ya bao la ugenini.
Uganda jioni hii wameibuka na ushindi wa bao 1-0 mjini Kampala katika mchezo wa marudiano, na mechi ya kwanza walilala kwa mabao 2-1 nchini Madagascar.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
CHANZO FULL SHANGWE

HUZUNI! MBEYA CITY FC YACHAPWA 1-0 NA VICTORIA UNIVERSITY ROBO FAINALI

DSCF5413Na Baraka Mpenja wa fullshangweDar es salaam
 WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya CECAFA Nile Basin Cup, Mbeya City fc wameaga mashindano hayo baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Victoria University ya Uganda katika mchezo wa robo fainali uliomalizika dakika chache zilizopita mjini Khartoum.
Mbeya City wametolewa katika michuano hiyo wakiwa wameshinda mechi moja, kufungwa moja na kutoka suluhu mechi moja katika hatua ya makundi.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

CHANZO FULL SHANGWE