Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 5 November 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMEONGOZA MATEMBEZI YA HISANI KWA AJILI YA KUSOMESHA WAUGUZI WAKUNGA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki mazoezi ya viungo kabla ya kuanza kwa Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga kwenye viwanja vya Green Ground ,Oysterbay jijini Dar es Salaam.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki mazoezi ya viungo pamoja na umati uliojitokeza kabla ya kuanza kwa Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga kwenye viwanja vya Green Ground ,Oysterbay jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiongoza Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga ambapo alitembea kwa kilometa 4.3 kuanzia viwanja vya Green Ground na kupitia barabara ya Toure na kurejea na barabara ya Msasani ,Oysterbay jijini Dar es Salaam wengine pichani ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) na Mkurugenzi Shirika la AMREF Health Africa Dkt. Florence Temu (kulia).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa jiji la Dar es salaam waliojitokeza kwenye   Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga kwenye viwanja vya Green Ground ,Oysterbay jijini Dar es Salaam
 Sehemu ya Umati uliohudhuria na kushiriki Matembezi ya Hisani ya Kusomesha Wauguzi  Wakunga kwenye viwanja vya Green Ground.
                                     ..................................................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameongoza mamia ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam katika matembezi ya hisani ya kilomita 4.3 ya kuchangia fedha kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya mafunzo ya wauguzi, wakunga 400 katika ngazi mbalimbali kupitia mafunzo ya kimtandao yaani e-learning nchini.


Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika matembezi hayo katika viwanja vya Green Ground, Oysterbay Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wananchi kuwa Serikali ya awamu ya Tano imeweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto mbalimbali katika sekta ya Afya ikiwemo kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto kwa kuongeza idadi ya wataalamu wa Afya na kuimarisha miundombinu pamoja na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kote nchini.


Amesisitiza kuwa ili kuhakikisha huduma za Afya zinazotolewa kwa wananchi zinakuwa na ubora unaotakiwa Serikali itaendelea kusimamia uwajibikaji kwa watumishi na watoa huduma za Afya mpango utaenda pamoja na kuongeza vitanda kwenye wodi za wazazi na utoaji wa huduma ya Afya bure kwa makundi maalum.

Makamu wa Rais pia amehimiza wadau wa sekta binafsi waendelee kushirikiana na Serikali katika utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi nchini ili kufikia malengo ya kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto.


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametumia sehemu ya hotuba yake kwa kulipongeza Shirika la AMREF Health Africa Tanzania kwa mipango yake ya kusaidia jamii ya Kitanzania kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika hilo ukiwemo mpango wa kugharamia masomo kwa njia ya ufadhili kwa wanafunzi wanaotoka kwenye familia duni kwa lengo la kuwawezesha kusomea cheti ya uuguzi ukunga.



Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa mipango na mikakati ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha vifo vya wanawake wajawazito na watoto nchini vinapunguzwa kwa kiwango kikubwa kutokana na Serikali kuendelea kutenga bajeti ya kutosha kwa Wizara ya Afya kwa ajili ya kununua vifaa tiba na kuongeza idadi ya wataalamu.
Katika harambee hiyo, Jumla ya shilingi milioni 290 zimechangwa na wadau wa maendeleo na lengo ni kukusanya shilingi milioni 500 fedha ambazo zitatumika kusomesha wauguzi 400 wakiwemo 50 kwa ngazi ya cheti na 350 kwa ngazi ya diploma kupitia mafunzo ya kimtandao yaani e-learning.


No comments:

Post a Comment