WATU wawili wafariki dunia mkoani Iringa katika matukio mawili tofautu likiwemo tukio la mtu mmoja kufariki baada ya kupigwa na watu wasiojulikana na kukatwa sehemu zake za siri.
Akithibitisha kutokea kwa tukiuo hili kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa,Wankyo Nyegesa,alisema kuwa tukio hilo limetokea huko maeneo ya kijiji cha Nzivi katika msitu uliopo jirani na bwawa la Kasanga kata ya Igowole wilayani Mufindi.
Nyegesa alisema mwili wa marehemu ulikutwa msituni hapo ukiwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo kichwani,mikononi,huku umme wake ukiwa umeondolewa.
Alimtaja marehemu kuwa ni Luckness Mlongalile (25) na hata hivyo uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa marehemu alikuwa hana maelewano mazuri na wakazi wenzake,lakini pia watuhumiwa wanatafutwa na jeshi la polisi.
Katika tukio lingine huko maeneo ya kijiji cha Malagosi Wilaya ya Iringa vijijini mzee wa miaka 70 anaejulikana kwa jina la Alphonce Mkwambe alifariki dunia baada ya kunyongwa na watu wasifahamika.
Nyegesa alisema mzee huyo alikua ametoka katika msiba kijiji cha jirani akiwa na baiskel yake ghafla walitokea watu wasiojulikana na kumnyonga kwa kutumia shati lake hadi kufa na baadaye kumtupa kwenye korongo la maji.
Aliongeza kuwa chanzo cha tukio zima kinachunguzwa na watuhumiwa wanasakwa na jeshi la polisi mkoani hapa.
Mwisho.

No comments:
Post a Comment