IMEELEZWA kuwa tabia ya wauguzi, madaktari, na wataalamu wa afya kukosa roho ya upendo na wagonjwa wao ni kwa kuwa hawana roho ya Mungu lakini kanisa la sasa linapaswa kuhakikisha kuwa linaingia kwenye maombi juu ya suala hilo.
Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji kiongozi wa kanisa la Angilikan St James, Andrew Kajembe wakati akizungumza kwenye ibada rasmi ya siku ya walemavu iliyofanyika kanisani hapo mapema wiki hii.Kajembe alisema kuwa kwa sasa inashangaza sana kuona kuwa watalamu wa sekta ya afya ambao ndio hao hao wakristo wanakosa roho ya huruma na wagonjwa hasa wale ambao wanaletwa kwa haraka kwenye hospitali ili kuweza kuokoa maisha yao.
Alifafanua kuwa shetani anawatumia wataalamu hao na kisha kusababisha mauti ya wagonjwa jambo ambalo kwa sasa kanisa linatakiwa kuinuka na kisha kupinga kabisa roho hiyo ambayo si nzuri kwenye jamii.
Alidai kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa kanisa kuweza kusimama kwenye maombi na kisha kupinga roho hiyo ambayo inaua watu wengi sana wakati watu hao wana nafasi kubwa sana ya kuokoa maisha ya watu.
"Tuwaombee hawa watu kuanzia sasa kamwe shetani asiweze kuwatumia tena badala yake hata wale ambao hawajaweza kumpokea Yesu waweze kumpokea kuanzia sasa na wawe marafiki wa wagonjwa ili kuwaepusha wengine na vitu kama vile Ulemavu ambao wakati mwingine unasababishwa na ukosefu wa huduma za haraka," aliongeza Kajembe.Wakati huo huo, Muhubiri wa siku hiyo ya walemavu ambaye naye ana ulemavu kutoka katika kituo cha maombo cha Radio safina Jijini ArushaElisante,eliakunda alisema kuwa kuna umuhimu kwa watu wwenye ulemavu mbalimbali kuhakikisha kuwa wanajiwekea uataribu wa kuongeza kiwango cha imani kila mara.
Elisante alisema kuwa imani ni nzuri hata kama wewe ni mzima kwani kwa kupitia imani unaweza kupata mahitaji yako ya kila siku na pia kamwe huwezi kumkufuru Mungu kutokana na hali ya ulemavu ambayo inakukabili kwa sasa.
"imani ni kipatanisho baina ya mtu na mungu sasa sisi wenye ulemavu kamwe htupaswi kukata tamaa bali tunatakiwa kumshukuru mungu kwa kila hatua ambayo kwa sasa tunaipitia" aliongeza Elisante.
No comments:
Post a Comment