JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
|
Simu: 255 22
2460735/2460706-8
Faksi:
255 22 2460735/2460700 P.O.
BOX 3056
Barua pepe: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM
Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb Na: TMA/3000/5/Vol
II 17 Machi, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA WADAU WOTE
Yah: Maadhimisho ya Siku
ya Hali ya Hewa Duniani
Tarehe 23 Machi, 2014
Kila mwaka tarehe 23 Machi nchi wanachama wa
Shirika la Hali ya Hewa Duniani hujiunga na kuadhimisha kuzaliwa kwa Shirika
hilo lililoanzishwa tarehe 23 Machi, 1950 kulingana na kauli mbiu. Kauli mbiu
ya mwaka huu ni ’Ushirikishwaji wa Vijana
katika Masuala ya Hali ya Hewa’- ”(Weather and Climate: Engaging Youth)”.
Katika
kuadhimisha Siku ya Hali ya Hewa Duniani (WMO), Shirika la Hali ya Hewa
linawahamasisha vijana ulimwenguni kote kujihusisha na masuala ya hali ya hewa,
ili kupata maarifa na uelewa wa hatua za kuchukua katika kipindi hiki cha
mabadiliko ya hali ya hewa duniani. Hatua hii ya WMO ni muhimu kwa ustawi wa
kizazi hiki na kijacho ili kujenga jamii imara hapo baadae.
Siku ya
Hali ya Hewa Duniani ni siku ya kutafakari Juhudi zinazofanywa na Wanasayansi
Duniani katika kufahamisha Dunia kuchukua tahadhari juu ya mabadiliko ya hali
ya hewa duniani na athari zake. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inatoa wito
kwa vijana wote kubadilika na kuchukua hatua za kukabiliana na mabadiliko ya
hali ya hewa katika kizazi hiki na kuchukua tahadhari ili kizazi kinachokuja
waweze kufaidi dunia yenye mazingira bora zaidi. Vijana wote walioko
mashuleni vyuoni na wajasiriamali washiriki katika kuokoa dunia kutoka kwenye
majanga yaletwayo na mabadiliko ya hali ya hewa. Aidha chachu kubwa ni kuhakikisha
vijana wanakuwa mstari wa mbele katika kufuatilia taarifa za hali ya hewa
zitolewazo na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini.
Kama ilivyo kwa wanachama wengine, Tanzania
inaungana nao kuadhimisha siku hii inayofikia kilele tarehe 23 Machi, 2014 kwa
kuwakaribisha wananchi wote kutembelea vituo vya hali ya hewa nchini ili kuona
shughuli zitolewazo na Mamlaka kuanzia tarehe 21-23 Machi 2014. Aidha, Mamlaka
itambelea na kutoa elimu kwa vijana wa baadhi ya shule na vyuo mbali mbali kupitia
ofisi zake zilizopo nchini kuanzia tarehe 19-20 Machi 2014. Kutoa
statements/makala za siku hiyo kwenye
magazeti, vipindi kwenye radio, na
televisheni kuhusu ushirikishwaji wa vijana
katika masuala ya hali ya hewa.
Mamlaka inawatakia maadhimisho mema ya Siku ya
Hali ya Hewa Duniani
’Ushirikishwaji wa Vijana katika Masuala ya Hali
ya Hewa’
(Weather and Climate: Engaging Youth)
IMETOLEWA
NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
No comments:
Post a Comment