Vibaka wapo, hata porini, ingawa inategemea ni vibaka wa aina gani.
Huku
mijini tumezowea kuona vibaka wakikwapua na hata wengine wakichomwa
moto. Lakini hali ni tofauti na hifadhini, hasa Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti.
Mbali
ya kupiga kelele kuhusu majambazi au majangili yanayopopoa maliasili za
taifa hili - vita inayoendeshwa kwa nguvu zote za serikali - lakini
wakazi wa pale Seronera yalipo makao makuu ya hifadhi hiyo, wanakabiliwa
na changamoto ya 'vibaka'.
Vibaka
hawa siyo binadamu, bali ni ngedere (Chlorocebus pygerythrus) na nyani,
wakati mwingine ndege wakubwa aina ya korongo (Greater adjutant stork).
Ngedere
ni wajanja sana, wanawaotea wakazi wa hapa wakitoka tu huku wakiwa
wameacha milango ama madirisha wazi, basi wao wanazama ndani na 'kuiba'
chakula - hasa ndizi, nyama na kadhalika.
Ndivyo
pia wanavyofanya nyani. Lakini nyani wanakwenda mbali sana, kwani ikiwa
watakuwa wamezowea eneo husika, basi wanajenga kiburi na kujifanya
wababe kuliko binadamu.
Wanaoonewa
zaidi ni wanawake, kwa sababu, kwa mujibu wa muhifadhi Miraji, wakati
mwingine wanaweza kuwachapa makofi akinamama na watoto na kuwapora
chakula.
Korongo
nao wanapatikana mpaka kwenye makazi ya binadamu. Ingawa wao wanatafuta
wadudu, bado hii haiwazuii kudokoa vyakula ikiwa tu wahusika wataacha
wazi bila kufunika.
Mara
kadhaa nilipata chakula kwenye kahoteli ka Impala hapo Seronera, ambapo
nilishuhudia akina dada wakijitahidi kuwafukuza korongo kama
wanavyowafukuza kuku. Maisha mengine ni raha sana jamani, onjeni muone.
Ngedere
wanatokea katika Domeni ya Eukaryota, Himaya ya Animalia (Wanyama),
Faila ya Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni); Ngeli ya
Mamalia (wenye viwele wanaonyonyesha watoto wao), Oda ya Primates
(Wanyama wanaofanana kiasi na binadamu), Nusuoda ya Haplorrhini (Wanyama
wanaofanana zaidi na kima), Oda ya chini ya Simiiformes (Wanyama kama
kima), Oda ndogo ya Catarrhini (Kima wa Dunia ya Kale), Familia ya juu
ya Cercopithecoidea, Familia ya Cercopithecidae (Wanyama walio na
mnasaba na kima), Nusufamilia ya Cercopithecinae (Wanyama wanaofanana na
kima), Kabila ya Cercopithecini (Kima), na Jenasi ya Chlorocebus
(Ngedere). Spishi zake ni C. aethiops (Linnaeus, 1758), C. cynosyros
(Scopoli, 1786), C. djamdjamensis Neumann, 1902, C. pygerythrus F.
Cuvier, 1821, C. sabaeus (Linnaeus, 1766), C. tantalus Ogilby, 1841.
Ngedere
au tumbili ni wanyama wa jenasi Chlorocebus katika familia
Cercopithecidae. Wanatokea Afrika kusini mwa jangwa la Sahara, lakini
spishi kadhaa zimewasilishwa katika sehemu nyingine za dunia.
Ndugu yenu,
Daniel Mbega
No comments:
Post a Comment