Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Saturday, 29 March 2014
TASO ARUSHA YAANZA MCHAKATO WA KUWAPATA VIONGOZI WAPYA
Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha
CHAMA cha wakulima na wafugaji kanda ya kaskazini TASO, kimeaanza mchakato wa kupata viongozi ngazi za kata katika uchaguzi unaoendelea ambao umeaanza February mwaka huu kwa ajili ya kusogeza huduma kwa wananchi waishio vijijini ambao huwa hawapati fursa ya kushirikimaonyesho ya kilimo ya ngazi ya kanda.
Hayo yamebainisha na Katibu mkuu wa Taso, Peter Ngasamiakwi,mapema jana wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya maonesho hayo kwa mwaka huu.
Alisema kuwa uchaguzi huo unatokana na mabadiliko ya katiba ya TASO, yanayoelekeza lazima viongozi wa chama hicho wapatikane kuanzia ngazi za kata bada yawilaya kama ilivyokuwa kabla.
Alifafanua kuwa Kulingana na mabadiliko hayo kila halmashauri ya wilaya inatakiwa inapaswa kuwa na viwanja vya maonyesho ya shughuli zawakulima na wafugaji ili kuwzesha wataalam wa ugani kutoa elimu sahihi itakayosaidia kuleta mapinduzi katika kilimo na mifugo.
"Kupatikana kwa viongozi hao kuanzia ngazi za kata kutahamasisha uboreshaji wa shughuli za kilimo na mifugo na kuwezesha walengwa kubadilisha shughuli zao na kuwa ni zenye tija na kuepuka kuziendesha kwa mazoea," aliongeza Ngassa.
Hataivyo alidai kuwa wakulima pamoja na wafugaji wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatumia vema chama hicho kwa ajili ya kuongeza na kuimarisha ufanisi kwenye kilimo kwanza
Ngassa alisema kuwa lengo la chama hicho ni kuona kuwa makundi hayo mawili yananufaika kila msimu wa mwaka na wala sio kwa msimu wa maonesho ya nane nane kama ilivyo kwa baadhi ya wananchi
"Tunatamani sana kuona kuwa haya makundi mawili yanabadilika sana yaani yanafikia malengo tunatamani kuona kuwa wanakuja hata hapa ofisini kwetu na kisha wakapewa elimu ya shamba darasa kama wakifanya hivyo nchi itabadilika sana"aliongeza Ngassa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment