Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot
Aidha miradi iliyozinduliwa ni pamoja na kukamilika kwa jengo la utawala lenye ukubwa wa Orofa mbili ambapo ujenzi wake umegharimu kiasi cha Shs. 1,044,064,462.96 pamoja na ununuzi wa mitambo minne ya ujenzi wa barabara yenye thamani ya Shs. 1,196,740,472.
Akizungumza kabla ya kuzindua miradi hiyo ,Ghasia aliipongeza halmashauri hiyo kupitia baraza la madiwani kwa ubunifu uliowezesha kupatikana kwa kiasi hicho cha fedha kupitia miradi yake mbalimbali iliyojiwekea ikiwemo ya ugawaji wa viwanja .
Waziri huyo alitoa onyo kwa halmshauri zingine ambazo zimekuwa hazitumii vizuri fedha za serikali kwa kubuni miradi ya kutafuna fedha za halamshauri ,kwa kueleza kuwa kwa sasa serikali ipo makuni na haitazifumbia macho na zitashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
''nawapongeza sana madiwani wa halmashauri yenu kwa kubuni miradi na kutumia vizuri fedha zinazopatikana ingekuwa madiwani wengine wangebuni ziara ya kwenda kujifunza hata matumizi yah ii mitambo ilimradi tu watumie hizo fedha ,ila hapa kwenu hamkufanya hivyo,' 'alisema Ghasia.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Felix Lumato, alitaja mitambo mine iliyozinduliwa na waziri ghasia kuwa ni pamoja na Caterpillar Vibratory lenye thamani ya Shs. 187,790,000. Hyundai
Crander Excavater (Shs. 291,600,000),
Alisema mitambo hiyo itasaidia sana kuinua hali ya uchumi kwa halmshauri na wananchi kwa ujumla,ambapo alisisitriza kuwa itakuwa inakodishwa kwa wananchi mbalimbali pamoja na kukarabati miundo mbinu ya barabara katika halmashauri hiyo.
Alisisitiza kwa kuiomba serikali ihakikishe fedha wanazoziomba kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ya maendeleo katika halmashauri zitolewe kwa wakati ili kurahisisha utekelezaji wa miradi hiyo kwa wakati waliojipangia.
Katika hatua nyingine mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi Goodluk Ole Medeye aliitaka serikali kuhakikisha inasaidia kugawanywa kwa wilaya ya Arumeru, vijiji, vitongoji na kata ili kurahisisha huduma kwa wananchi na utekelezaji wa maendeleo.
Alisema hivi sasa katika wilaya hiyo kumekuwepo na changamoto kubwa kwa wananchi kupata mahitaji yao muhimu kutokana na umbali ya maeneo ya huduma kwa kueleza kuwa baadhi ya maeneo yapo mbali sana na huduma za msingi.
No comments:
Post a Comment