Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 18 March 2014

TFDA ARUSHA WATEKETEZA SHEHENA YA MIKATE


MAMLAKA ya chakula na dawa nchini TFDA, kanda ya kaskazini jana imeteketeza shehena kubwa ya Mikate na Skonzi katika kiwanda cha kuokea mikate cha Manyara Loef Company limited, kilichopo Sombetini jijini Arusha, kwa kukikuka maelekezo ya mamlaka hiyo na kuoka mikate katika mazingira yasiyo salama hivyo kukiuka sheria ya usalama wa chakula ya mwaka 2005.

Kaimu meneja wa TFDA,kanda ya kaskazini Salma Muhando,amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya kiwanda hicho kukaidi maelekezo ya mmlaka hiyo yaliyomtaka mmiliki wake kutekeleza mapungufu yaliyojitokeza wakati wazoezi la ukaguzi lililofanywa na mamlaka hiyo march 11 mwaka huu .

Amesema katika zoezi hilo la ukaguzi kiwandani hapo TFDA, ilibaini mapungufu kadhaa ambayo ni pamoja na kiwanda kutokusajiliwa na mamlaka hiyo kwaajili ya kuoka mikate na sikonzi, kutokuwepo mtaalam aliyesomea maswala ya vyakula ,vifaa vinavyotumika kuokea mikate kuwa ni hafifu na hivyo havikidhi viwango, watumishi hawana vifaa vya kufanyia kazi, pia hata choo chenyewe nacho hakikidhi viwango.

Amesema kulingana nasheria kabla ya kuanzashughuli za uokaji wa mikate lazima kiwanda kisajiliwe na mamlaka yachakula na dawa ndipo uzalishaji uanze nasi vinginevyo kwa kuwa mamala yachakula na dawa ndio chombo chenye jukumula kuhakikisha vyakula vyote  vinavyoingizwa sokoni viwe vimekidhiviwango..

Mhando, amesema mara baada ya ukaguzi huo mamlaka ilimtaka mmiliki wa kiwanda hicho ,kusitishashughuli zote za kiwanda mpaka atakapomaliza kuyafanyia marekebishomapungufu hayo na mamlaka uitarejea kufanya ukaguzi ndipo aruhusiwe.

Amesema cha kushangaza mmiliki wa kiwanda amekaidi kutekeleza  maelekezo hayo na kuendelea na uzalishaji kama kawaida ,hivyo mamlaka ililazimika tena marchi 13 mwaka huu kuendesha zoezi lingine ilikuangalia kama maelekezo yametekelezwa lakini chaajabu hakuna hata moja lililotekelezwa na kiwanda kinaendelea na uzalishaji kama kawaida .

Mhando, amesema kuwa mamlaka ya chakula na dawa itaendelea kufanya ukaguzi katika viwanda , maduka ya vyakula na vipodozi na kwenye taasisi mbalimbali ili kudhibiti vyakula visivyo na viwango visiingizwe  na kuathiri afya za watu .

Ameswema kutokana na mmiliki huyo kukaidi maelekezo hayo mamlaka imeamua kuteketeza kwa moto shehena yote iliyokutwa imeshazalishwa tayari kwa kupelekwa kwenye masoko,na hivyo kuepusha watu kutokula vyakula ambavyo vinazalishwa kwenye mazingira yasiyo rafiki ambayo sio salama kwa afya zawalaji.

Katika hatua nyingine msimamizi  wa kiwanda alikimbia mara baada ya kuwaona mamlaka yachakula na dawa na kuwaacha vibarua pekee  wakiendelea na kazi.

Ambapo vibarua hao wakizungumza katika tukio hilowalisema wao hawaelewi chochote na wanahofia malipo yao kwa kuwa hawaelewi hatima ya kiwanda hicho .

No comments:

Post a Comment