Bilionea Mark
Zuckerberg
KUFIKIA kiwango cha utajiri wa Dola
1 bilioni siyo mashindano, lakini baadhi wanafikia hapo haraka na kwa urahisi
tu. Kati ya mabilionea 1,645 walioko kwenye orodha ya Forbes, 31 wana umri wa
chini ya miaka 40. Kundi hilo haliwahusishi vijana matajiri wa Google, Sergey
Brin na Larry Page, ambao tayari wamekwishavuka miaka 40.
Katika orodha ya mwaka huu 2014,
yupo bilionea mdogo zaidi mpya. Perenna Kei, binti ambaye hajulikani sana,
amempiga kumbo muasisi mwenza wa Facebook Dustin Moskovitz ambaye alikuwa
bilionea mdogo zaidi.
Akiwa anatokea Hong Kong, Kei ana
asilimia 85 kwenye kampuni ya Logan Property Holdings kupitia kwenye kampuni
kadhaa pamoja na mfuko wa familia. Baba yake, Ji Haipeng, ndiye mwenyekiti na
Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo ambayo imeandikishwa kwenye Soko la Hisa la Hong
Kong, ambayo ilianza kuuza hisa zake mwezi Desemba 2013.
Mabilionea 39 wadogo waliomo kwenye
orodha ya mwaka 2014 wana utajiri wa pamoja wa Dola 115.7 bilioni. Wafanyakazi wa
Facebook, wakiwemo Sean Parker, Mark Zuckerberg na Jan Koum wa WhatApp – wana asilimia
42 ya kiasi hicho. Koum, ambaye ni mpya kufuatia Facebook kuamua kuinunua WhatsApp, ana
utajiri wa Dola 6.8 bilioni. Aliiuza kampuni yake hiyo ya mtandaoni kwenye
kampuni ya Menlo Park, ya California kwa Dola 19 bilioni katika hisa na fedha
taslimu mwezi Februari 2014.
Matajiri ‘watoto’ 13 kwenye orodha
hiyo wanatokea Marekani. Ifuatayo ndiyo orodha kamili kwa mwaka 2014:
1: Perenna Kei & familia
Umri: 24
Utajiri: Dola 1.3 bilioni
Taji la bilionea mdogo kabisa
duniani linakwenda kwa Bi. Perenna Kei, ambaye ana asilimia 85 kwenye kampuni
ya Logan Property Holdings kupitia kwenye kampuni kadhaa pamoja na mfuko wa
familia. Baba yake, Ji Haipeng na ndiye mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Logan
Property Holdings. Zamani akijulikana kwa jina la “Ji Peili,” Kei siyo mkurugenzi
mtendaji kwenye kampuni hiyo, ana shahada
katika uchumi na fedha kutoka Chuo Kikuu cha London.
Umri: 29
Utajiri: Dola 6.8 bilioni
Kwa sasa siye bilionea mdogo duniani,
Dustin Moskovitz atatimia miaka 30 mwaka huu. Rafiki mkubwa wa Mark Zuckerberg
waliyekuwa wakiishi chumba kimoja, Moskovitz alisaidia kuanzishwa kwa mtandao
wa kijamii wakitokea kwenye bweni lao katika Chuo Kikuu cha Harvard, akiacha
chuo baada ya miaka miwili na kufanya kazi ya kudumu kama mwajiriwa wa tatu wa
Facebook. Aliachana na Facebook mwaka 2008 na kuanzisha Asana, kampuni ya
software ambayo inawasaidia watu kuboresha kazi zao katika miradi. Alioa mwaka
jana kwa mpenzi wake wa miaka mingi Cari Tuna.
3: Mark Zuckerberg
Umri: 29
Utajiri: Dola 28.5 bilioni
Facebook imetimia miaka 10 mwaka huu
na hakuna aliyekuwa anasherehekea kwa nguvu kama Mtendaji Mkuu Mark Zuckerberg.
Baada ya kuinusuru kampuni yake katika kipindi kigumu cha IPO Mei 2012, Zuckerberg
ameisaidia kampuni hiyo kutoka Menlo Park, California kuendelea kupaa. Hisa za Facebook
zimepanda hadi kufikia 130% kwa mwaka jana tu hadi kufikia katikati ya Februari
mwaka huu. Hii imefanya utajiri wake uongezeke mara mbili pamoja na kutoa hisa
18 milioni mwishoni mwa Desemba. Aliuza zaidi ya hisa 41 milioni na kupata
mbadala wa hisa 60 milioni katika kipindi hicho hicho.
4: Anton Kathrein, Jr
Umri: 29
Utajiri: Dola 1.35 bilioni
Anton Kathrein, Jr. ni uzao wa nne kuongoza
kampuni ya familia ya Kathrein-Werke AG– ”kampuni kongwe na kubwa zaidi ya
uzalishaji wa antenna duniani,” kwa mujibu wa wavuti ya kampuni hiyo. Kampuni hiyo
pia inatengeneza antenna za radio na TV, satellite na mfumo wa mawasiliano na
vifaa vinginevyo ulimwenguni. Kampuni hiyo ina vituo 18 duniani, wafanyakazi
6,800 na pato la Dola 1.8 bilioni kwa mwaka 2012 ilianzishwa na babu yake
Kathrein mwaka 1919. Anton Sr aliiongoza kampuni hiyo kuanzia mwaka 1972 hadi
2012 alipofariki.
5: Drew Houston
Umri: 30
Utajiri: Dola 1.2 bilioni
Umri: 30
Utajiri: Dola 3.8 bilioni
Japokuwa alionekana kwa mara ya
kwanza kwenye orodha ya mabilionea ya Forbes akiwa na miaka nane, Albert von
Thurn und Taxis, prince wa 12 katika familia ya kifalme, alirithi rasmi utajiri
mwaka 2001. Rasilimali zake ni pamoja na majengo, sanaa na hekta 36,000 za miti
nchini Ujerumani, mmoja ya misitu mikubwa barani Ulaya. Bado hajaoa na anaishi
katika hekalu la familia mjini Bavaria, katika eneo la Schloss Emmeram, na
anapenda kuendesha magari yaendayo kasi.
7: Scott Duncan
Umri: 31
Utajiri: Dola 6.3 bilioni
Scott Duncan ni mmoja wa mabachela
wakongwe wa Texas na mmoja wa warithi wanne mradi mkubwa wa bomba la nishati
uliojengwa na marehemu baba yao, Dan Duncan. Utajiri wake umeongezeka kwa Dola
1.2 bilioni kulinganisha na mwaka uliopita katika bei ya hisa ya Enterprise
Products Partners. Baba yake, ambaye alikuwa tajiri mkubwa kuliko wote jijini Houston,
alifariki mwaka 2010 akiwa na umri wa miaka 77.
8: Eduardo Saverin
Umri: 31
Utajiri: Dola 4.1 bilioni
Mvumbuzi mwenza wa Facebook Eduardo
Saverin, ambaye alizaliwa nchini Brazil, amekuwa akiishi nchini Singapore tangu
alipoukana uraia wake wa Marekani mwaka 2012.
9: Yang Huiyan
Umri: 32
Utajiri: Dola 6.9 bilioni
Mwanamke tajiri kuliko wote nchini
China, Yang Huiyan ni makamu mwenyekiti wa kampuni ya uendelezaji majengo ya Country
Garden. Alipewa sehemu ya mali za baba yake kwenye kampuni ya Country Garden kabla
ya kampuni hiyo kuanza kuuza hisa mwaka 2007, mwaka ambao pia aliingia kwenye
orodha ya Forbes akiwa Mchina tajiri kwa kumiliki Dola 16 bilioni.
10: Fahd Hariri
Umri: 33
Utajiri: Dola 1.2 bilioni
Fahd Hariri ndiye mtoto wa mwisho wa
kiume wa Waziri Mkuu wa Lebanon, Rafik Hariri. Alipata shahada ya uhandisi
katika Chuo Kikuu cha Ecole Spéciale d’Architecture de Paris mwaka 2004. Wakati
inaripotiwa kwamba hajawahi kukanyaga ardhi ya Beirut tangu baba yake alipouawa
mwaka 2005, anaendelea majengo ya makazi huko kwa heshima ya baba yake.
Umri: 33
Utajiri: Dola 2.7 bilioni
Marie, 33, pamoja na ndugu zake Emmanuel,
43, na Jean-Michel, 46, walirithi kampuni kubwa ya maziwa Ufaransa ya Lactalis,
wazalishaji wa maziwa ya Président brie pamoja na siagi za aina mbalimbali,
maziwa na mtindi. Wote kwa pamoja wanamiliki asilimia 100 ya kampuni hiyo
ambayo babu yao aliianzisha katika miaka ya 1930.
12: Sean Parker
Umri: 34
Utajiri: Dola 2.4 bilioni
Mwezi Juni 2013, muasisi wa Napster na
rais wa zamani wa Facebook Sean Parker alimuoa mwimbaji Alexandra Lenas katika sherehe
ya kifahari iliyofanyika kwenye msitu wa Big Sur, California. Harusi hiyo
iligharimu Dola 4.5 milioni.
Mabilionea wengine wadogo, umri na utajiri wao kwenye mabano ni: Julia Oetker (Miaka: 35 na Utajiri: Dola 1.65 bilioni); Robert Pera (Miaka: 35 na Utajiri: Dola 2.7 bilioni); Ayman Hariri (Miaka: 35 na utajiri wa Dola 1.2 bilioni); Naruatsu Baba (Miaka 36 na utajiri wa Dola 2.2 bilioni); Yvonne Bauer & family (Miaka 36 na utajiri wa Dola 3.5 bilioni); Lawrence Ho (Miaka 37 na utajiri wa Dola 3 bilioni); Yoshikazu Tanaka (Miaka 37 na utajiri wa Dola 1.6 bilioni); Alejandro Santo Domingo
Davila & family (Miaka 37 na utajiri wa Dola 11.1 bilioni); Jack Dorsey (Miaka 37 na utajiri wa Dola 2.2 bilioni); Jan Koum (Miaka 38 na utajiri wa Dola 6.8 bilioni).
Wengine ni Nicholas Woodman (Miaka 38 na utajiri wa Dola 1.3 bilioni); Chase Coleman, III (Miaka 38 na utajiri wa Dola 1.6 bilioni); Yusaku Maezawa (Miaka 38 na utajiri wa Dola 1.25 bilioni); Rahel Blocher (miaka 38 na utajiri wa Dola 2.9 bilioni); John Arnold (Miaka 39 na utajiri wa Dola 2.9 bilioni); Jon Oringer (Miaka 39 na utajiri wa Dola 1.35 bilioni); Liu Qiangdong (Miaka 39 na utajiri wa Dola 2.7 bilioni); Ryan Kavanaugh (Miaka 39 na utajiri wa Dola 1 bilioni); na Miriam Blocher (Miaka 39 na utajiri wa Dola 1.1 bilioni).
Chanzo: Forbes
No comments:
Post a Comment