Katika
medani ya siasa nchini msimamo wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kuhusu
Muungano na muundo unafahamika. Ni muundo wa kutaka Serikali mbili
ambao chama hicho unakipigania kwa udi na uvumba.
Hata
hivyo, msimamo huo ni kinyume na mapendekezo au matakwa ya wengi kama
ilivyoainishwa kwenye Rasimu ya Pili ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba.
Tume
hiyo iliyokuwa chini ya Jaji Joseph Warioba ilikusanya maoni ya
wananchi na ilipendekeza muundo wa Muungano wa Serikali tatu.
Hivi
karibuni akifungua Bunge Maalumu la Katiba, Rais Jakaya Kikwete akaunga
mkono msimamo wa chama chake, jambo lililoibua mjadala unaoendelea hadi
sasa.
Hoja ya Serikali mbili
Kwanini CCM wanataka Serikali mbili na siyo tatu au moja kama ilivyo
maoni ya wananchi walio wengi kwa mujibu wa maelezo ya Tume ya Warioba?
Makala haya yanachambua hoja hiyo.
Profesa
Bakar Mohammed ni Mhadhiri Mwandamizi na Mkuu wa Idara ya Siasa na
Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anayesema msimamo wa CCM wa
kudai Serikali mbili unatokana na hofu ya uhafidhina wa kuogopa
mabadiliko.
Anasema
viongozi wengi wa CCM wanasumbuliwa na hofu na woga wa mabadiliko na
kwamba wanakuwa wagumu kuyakubali yanapotaka kutokea.
“Kama
mtu unaangalia madaraka zaidi, lazima kunakuwa na woga, na hii ni hulka
ya binadamu kuwa na woga wa kuacha kile ulichokizoea… Lakini ukiangalia
masilahi ya nchi na kuacha yale yanayokusukuma kusingekuwa na wasiwasi
huu unaoonekana sasa,” anasema.
Anasema
CCM inachofanya ni kuhakikisha haking’oki madarakani, huku viongozi
wake wakiamini kuwa wana sifa za kuongoza na siyo wengineo.
Profesa
Bakari anailinganisha hofu ya sasa ya CCM na ile waliyokuwa nayo
viongozi wa chama hicho miaka ya 1990 zilipoanza vuguvugu za mabadiliko
ya siasa za vyama vingi. Anasema CCM kiliendesha propaganda kuwa mfumo
wa vyama vingi haukuwa na tija na ungeleta vita.
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment