Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Tuesday, 25 March 2014
KESI YA MHARIRI WA BURKINA FASO YAANZA KUSIKILIZWA ARUSHA
Na Mwandishi wa Brotherdanny5.blogspot, Arusha
Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu imefanikiwa kusikiliza kesi ya Lohe Issa Konatev mhariri wa gazeti la wiki la L'Ouragan la nchini Burkina Faso kwa tuhuma za kutoa kauli za matusi kwa umma kufuatia makala mbili zilizochapishwa katka gazeti hilo Agosti mosi mwaka 2012.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema jana mara baada ya kusikilizwa kwa kesi hiyo,mratibu wa mahaka ya Afrika Bw.Jean Piere alisema kuwa kesi hiyo imesomwa kwa mara ya kwanza katika mahakama hiyo iliyopo jijini Arusha.
Piere alisema kuwa mwandishi huyo hakutendewa haki chini ya ibara ya 9 ya haki za binadamu na ibara ya 19 ya mkataba wa kimataifa wa kisiasa wa haki za watu ambapo mhariri huyo alikuwa na hatia katika mahakama ya Burkina Faso kwa kashfa kutokana na makala mbili kuchapishwa kwenye gazeti hilo mnamo tarehe moja Agosti mwaka 2012.
Aliendelea kuwa mahakama ya Burkina Faso ilimtaka Bw.Konate kulipa faini ya dola za kmarkani 300000 ambapo malipo hayo yote yanakiuka haki na uhuru wa kujieleza, na kuitaka mahakama ya Burkina Faso kumlipa fidia kutokana na mateso aliyoyapata.
Hata hivyo kesi hiyo iliwakilishwa na Bw.Yakare Oule,Bw.John RWD Jones,Steven Finizio huku wanasheria kutoka serikali ya Burkina Faso ni Antoinette Ouedrraogo ,Mahamoudou Sanogo pamoja naye Ouoba Dama ambapo kesi hiyo imeahirishwa mpaka hapo watakapoitaja tena.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment