Taarifa
zinasema waandishi hao wawili wanafanyakazi katika vyombo vya habari
binafsi na mwingine yuko Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete.
Tayari
waandishi hawa mashuhuri nchini wamefanya ziara katika nchi za Rwanda,
Kongo (DRC), Ufaransa, Ubelgiji, Uganda na Uingereza, ambako pamoja na
kukutana na raia wa Rwandwa wanaoishi nchini humo, wamekutana pia na
"majasusi ya Kagame."
Aidha, waandishi
wamekutana na rais Paulo Kagame, Joseph Kanambe Kabila, Yoweri Museveni
na rais wa Ufaransa kwa shabaha ya kumsaidia Kagame kuidhoofisha
Tanzania.
“Nakuambia hivi kijana wangu.
Wanaosaidia na Kagame kumtukana rais Kikwete, wako humuhumu ndani ya
nchi. Kundi ni kubwa mno; lakini ndani yake kuna waandishi wa habari
watatu wandamizi nchini,” ameeleza kiongozi mmoja serikalini.
Kupatikana
kwa taarifa hizi kumekuja mwezi mmoja baada ya mtandao mashuhuri nchini
Rwanda, NEWS of Rwanda (NR), kuchokomoa kinachoweza kuitwa, "Maisha
binafsi ya Rais Kikwete."
Katika taarifa hiyo,
mtandao huo wa Rwanda unadai mke wa Rais (Mama Salma Kikwete), ni ndugu
wa Hayati Jevenalis Habyarimana, aliyewahi kuwa rais wa Rwanda; na
kwamba Rais Kikwete mwenyewe ni mtu dhaifu katika masuala ya mapenzi.
Rais
Kikwete na Paul Kagame wamekuwa na vita ya maneno kwa muda mrefu sasa;
huku Rwanda ikiituhumu Tanzania kutumiwa na mabeberu wasioitakia mema
nchi hiyo.
Tayari waandishi hawa mashuhuri
nchini wamefanikiwa kupenya mitego ya maofisa usalama wa taifa mkoa wa
Mwanza waliokuwa wanafuatilia nyendo zao, wakati walipokutana na watu wa
RPF - Chama cha Kagame, nchini Uganda, miezi mitano iliyopita.
Hiki
kilikuwa kipindi ambacho rais Kikwete alifanya ziara mkoani Kagera,
ambako pamoja na mengine, aliagiza kutekelezwa “operesheni wahamiaji
haramu."
Ugomvi wa Kagame na Kikwete kwa kiasi
kikubwa unatokana na serikali ya CCM kukisaidia chama cha upinzani cha
Democratic Green Party of Rwanda ili kimuondoe madarakani Kagame na RPF
yake.
No comments:
Post a Comment