Ndugu zangu,
Rais Jakaya Kiwete yuko Bungeni hivi sasa akihutubia Bunge Maalum la Katiba. Yapo mengi anayoyaeleza, lakini suala la muundo wa Muungano kwa uelewa wangu mdogo nadhani anatoa mwelekeo wa namna mjadala unavyotakiwa uwe.
Inavyoelekea haonekani kuunga mkono muundo wa serikali tatu akisema itakuwa kazi serikali ya Muungano kupata nguvu kwani itategemea zaidi serikali washirika.
Anaonekana kuunga mkono serikali mbili, na hata wajumbe (wanaounga mkono hasa CCM) wamelipuka kwa shangwe kusikia hoja hiyo.
Hofu yangu ni kwamba, isije ikatafsiriwa moja kwa moja kwamba kauli ya Rais ndio mwelekeo wa mjadala, kwamba muundo sahihi ni wa serikali mbili.
Katiba ya sasa ina upungufu na ndiyo maana imeandaliwa rasimu hii mpya, sasa basi, lazima tuzingatie hayo na kuliwazia taifa kwa miaka 50 au 100 ijayo, siyo sasa.
Niwaombe tu wajumbe, kwamba busara zitumike zaidi katika mjadala huo wa Katiba na kusiwe na shinikizo la kiitikadi, ikiwa kweli tunataka tupate katiba itakayoliongoza taifa hili kwa amani.
Ni hayo tu ndugu zangu,
Daniel Mbega
Iringa, Tanzania
0715 070109
No comments:
Post a Comment