Na Mwandishi wa Brotherdannyblog, Arusha
IMEELEZWA kuwa mfumo dume katika Jiji la Arusha umesababisha jumla ya wanawake 5609 kushindwa kujua kusoma na kuandika hali ambayo ndio chanzo cha umaskini kwa baadhi ya familia.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa elimu ya watu wazima mkoa wa Arusha, January Mboya wakati akiongea na vyombo vya habari kuhusiana na maendeleo ya mkoa wa arusha kwenye idara ya elimu ya watu wazima
Aidha Mboya alisema kuwa idadi hiyo ya wanawake wasiojua kusoma lakini pia kuandika ni kubwa sana na inazidi kuongezeka tofauti na miaka ya nyuma ambapo idadi hiyo ya wasiojua kusoma na kuandika ilikuwa ni ndogo sana kwa miaka iliyopita
Alifafanua kuwa hali hiyo inasababishwa na mfumo dume uliopo kwennye baadhi ya familia ambapo asilimia kubwa ya wanawake huachwa nyuma kwenye elimu wakati wengine wakikosa elimu kabisa kwa kisingizo kuwa ni wanawakejambo ambalo ndio chanzo cha ongezeko hilo .
“hapo awali kwa jiji hili la Arusha idadi ilikuwa ni ndogo sasa imekuwa sana kutokana na mifumo dume iliopo kwenye jamii na sisi tunahakikisha kuwa tunaweka mikakati mbalimbali ya kuweza kuwasaidia wanawake hawa kwani kwa kutojua kusoma lakini pia kuandika ndiyo chanzo kikubwa dha umaskini kwenye jamii”aliongeza Bw Mboya
Pia alidai kuwa kwa sasa ndani ya Jiji la Arusha kuna wanaume 2969 ambao nao hawajui kusoma wala kuandika ambapo mpaka sasa idara hiyo ya Juma la elimu ya watu wazima tayari wameshaweka mikakati mbalimbali ya kuwasaidia
Katika hatua nyingine Bw mboya alisema kuwa idara ya elimuya watu wazima kwa jiji la Arusha bado inakabiliwa na changamoto lukuki hali ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa sana wasiojua kusoma na kuandika kufikiwa na huduma kwa haraka
Alitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ukosefu wa gari maalumu kwa ajili ya idara hiyo hali ambayo inachangia sana baadhi ya wadau wa elimu hiyo hasa wale waliopo mbali kidogo na mji kufikiwa
Pia alitaja changamoto nyingine kuwa ni uhaba wa bajeti ambapo napo bajeti iliopo ni ndogo sana hivyo inasababisha wakati mwingine baadhi ya huduma katika ofisi hiyo ya elimu ya watu wazima kusimama.
No comments:
Post a Comment