Na Mwandishi wa Brotherdannyblog, Arusha
MAGONJWA yasiyoambukiza yakiwemo Vichomi na Almonia bado ni tatizo kubwa mkoani Arusha linaloendelea kuzwaathiri wananchi hasa walioko mbali na huduma za afya .
Hayo yameelezwa jana katika kikao cha mkoa cha wadau wa afya ,walipokuwa wakichangia nama bora ya kuboresha huduma za afya na kukabiliana na magonjwa hayo yasiyoambukiza ili kuyatokomeza.
Wamesema licha ya malaria kuongoza kwa vifo pia magonjwa yasiyoambukiza yameendelea kupoteza maisha ya wananchi hasa maeneo ya wilaya za wafugaji ambao kutokana na mazingira wapo mbali na huduma za afya .
Wajumbe hao wakapendekeza kila halmashauri kuweka mkakati maalumu wa kupambana na magonjwa hayo yasiyoambukiza na hatimae kuyatokomeza
walidai kama Halmashauri zote za mkoa wa Arusha zitaweza kuzingatia hilo basi magonjwa hayo ambayo hayaambukizi yatapungua na kisha kupunguza vifo vya jamii nzima kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment