TAARIFA KWA UMMA WA WATANZANIYAA...
TAARIFA
YA PINGAMIZI LA MGOMBEA WA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE .FABIAN LEONARD
SKAUKI – MGOMBEA CHAMA CHA WANANCHI –CUFDHIDI YAMATHAYO MANG’UNDA
TORONGEY – MGOMBEA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO
-CHADEMA13.03.2014Mimi FABIAN L. SKAUKI, mgombea ubunge wa uchaguzi
mdogo jimbo la CHALINZE kwa Ticket ya THE CIVIC UNITED FRONT (CUF)
ninamwekea Pingamizi mgombea wa chama cha demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kwamba amepoteza sifa za kuwa mgombea kwa sababu zifuatazo.
1. Ndugu MATHAYO. M. TORONGEY amejaza Taarifa za uongo kwenye Fomu yake kwamba kazi anayoifanya ni BIASHARA.
Sio kweli, kwa sababu hajaweka vielelezo vya yeye kufanya hiyo kazi.
Hajulikani anafanya kazi gani.
2. Ndugu MATHAYO .M. TORONGEY amejaza katika fomu kwamba anajua kusoma na kuandika Kiswahili na kiingereza.
Taarifa
hizi ni za uongo, mgombea huyu hajui kusoma wala kuandika Kiswahili
wala kiingereza, na kwamba amedanganya na amepoteza sifa za kuwa
mgombea.
3.
Ndugu MATHAYO .M.TORONGEY amedanganya kwa kughushi/kufoji sahihi za
wadhamini,ambao amewaorodhesha kwenye fomu ya kuomba kuthibitishwa kuwa
mgombea.
Ambapo
katika fomu hizo wadhamini wote sahihi zao zimefojiwa na hazifanani na
zile zilizokuwepo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kwamba
sahihi zote hizi zimesainiwa na mtu mmoja ambaye sio muhusika.
Hivyo anapoteza sifa ya kuendelea kuwa mgombea.
4.
Ndugu MATHAYO.M.TORONGEY ameshindwa kutimiza mahitaji ya kisheria ya
kuwa na wadhamini wasiopungua 25, badala yake amedhaminiwa na wadhamini
28 ambao kati yao wadhamini 7 sio wapiga kura halali wa jimbo la
CHALINZE, na kwamba Taarifa zao na namba zilizojazwa hazifanani.
Hivyo anabakiwa na wadhamini halali 21 ambao kisheria hawatoshi kutimiza matakwa ya kisheria.
Majina
ya wadhamini hao ambao hawakidhi matakwa ya kisheria na namba zao ni
JINA LA MDHAMINI NAMBA YA KADI KURA 1. HABIBU ALLY SAIDI * 16886275*2.
MOHAMMED RAMADHANI *30376567*3. ABDULKADIR ALLY *49264905*4. SHABANI
SULEYMAN *16984045*5. JUMA MRISHO *48759563*6. RAJABU ALLY *16872368*7.
MANENO MIRAJI *16872059*
Wananchi
wenye namba na majina hayo hapo juu waliojazwa kama wadhamini kuanzia
namba 1 hadi 7 kwenye fomu yake hawana sifa za kupiga kura kwenye maeneo
ambayo wamejazwa wanatokea.
Hii
ni kutokana na ukweli kwamba idadi halali ya wadhamini wanaobaki
ukiwaondoa hao saba watabaki 21, hawakizi vigezo vya kuwa wadhamini.
5.
Ndugu MATHAYO.M.TORONGEY amedanganya Uraia wake, na kwamba yeye si
Mtanzania wa kuzaliwa ndio maana hana vielelezo halali vinavyohusu uraia
wake. Hivyo anakosa sifa ya kuwa mgombea.
Hivyo
ninaomba Tume ya Uchaguzi kutengua uteuzi wa mgombea wa chama cha
demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ndugu MATHAYO.M.TORONGEY kwa kuwa
anakosa sifa za yeye kuendelea kuwa mgombea.
Wako katika ujenzi wa Taifa FABIAN LEONARD SKAUKI …………………………………………………….. MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE.
THE CIVIC UNITED FRONT+255 786 189 070/+255 754 849 450
No comments:
Post a Comment