Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, imeaanza kutekelezakwa vitendo Mpango wa Taifa wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) kwa kukamilisha miradi mbalimbali ikiwemo maji, nishati na mabwawa kwa lengo la kuwaondolea wananchi kero .
Taarifa ya mkuu wa wilaya hiyo, Jowika Kasunga, imesema kuwa Monduli, inatekeleza mpango huo ambao ulizinduliwa na rais Jakaya Kikwete, Februari mwaka huu mpango ambao unakusudia kuwepo na huduma bora zaidi na kuwaondolea wananchi kero zilizokuwa hazijapata majawabu ya kudumu ya utatuzi wake.
Amevitaja vijiji hivyo kuwa niEngaruka, Selela, Moita, Kilorit, Naalarimi, Lendikinya, ambavyo vinatekeleza mradi wa maji mtiririko, huku vijiji vya Looisimingori, Loiksale, na Mbuyuni, vinatekeleza mradi wa maji ya mabwawa .
No comments:
Post a Comment