Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 30 April 2014

LIGI YA MABINGWA MIKOA KUANZA KUTIMUA VUMBI MEI 10


Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) msimu wa 2013/2014 itakayochezwa kwa mkondo mmoja inaanza kutimua vumbi Mei 10 mwaka huu katika vituo vitatu vya timu tisa kila kimoja.

Timu itakayoongoza katika kila kituo cha ligi hiyo itakayomalizika Juni 2 mwaka huu ndiyo itakayopata tiketi ya kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa msimu ujao wa 2014/2015. Vituo hivyo ni Mbeya, Morogoro na Shinyanga.

Kituo cha Morogoro ambapo mechi zitachezwa Uwanja wa Jamhuri kitakuwa na timu za Abajalo FC ya Dar es Salaam, African Sports (Tanga), Bulyanhulu FC (Shinyanga), Kariakoo SC (Lindi), Kiluvya United (Pwani), Mji Mkuu FC (Dodoma) Mshikamano FC (Dar es Salaam), Navy FC (Dar es Salaam) na Pachoto FC (Mtwara).  

Uwanja wa Sokoine ndiyo utakaotumika katika kituo cha Mbeya chenye timu za AFC ya Arusha, Magereza FC (Iringa), Mpanda United SC (Katavi), Njombe Mji FC (Njombe), Panone FC (Kilimanjaro), Tanzanite SC (Manyara), Town Small Boys (Ruvuma), Ujenzi (Rukwa) na Volcano FC (Morogoro).

Timu za Eleven Stars ya Kagera, Geita Veterans (Geita), JKT Rwamkoma FC (Mara), Mbao FC (Mwanza), Milambo SC (Tabora), Mvuvumwa FC (Kigoma), Simiyu United (Simiyu), Singida United (Singida) na Wenda FC (Mbeya) zitacheza katika kituo cha Shinyanga kwenye Uwanja wa Kambarage.

Orodha ya usajili wa wachezaji wa timu zote kwa ajili ya RCL imetumwa kwa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa na klabu zote za RCL, FDL na Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kwa ajili ya kipindi cha pingamizi ambacho kinamalizika Mei 4 mwaka huu.

Hata hivyo, katika usajili uliowasilishwa na baadhi ya klabu imebainika kuwa kuna wachezaji walioshiriki VPL, FDL na wale U20 za VPL waliocheza ligi msimu wa 2013/2014.

Kiongozi yeyote atakayebainika katika udanganyifu kwenye usajili huo, awe wa klabu au chama cha mpira wa miguu cha mkoa atachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni ikiwemo kufikishwa katika vyombo vya kimaadili vya TFF kwa hatua zaidi.

Ligi ya Mabingwa haina mdhamini, hivyo timu shiriki zitajitege.

CHANZO, MPENJA BLOG

TBC NA CRI YAZINDUA TAMTHILIYA YA KICHINA ILIYOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI

PIX 1
Mkurugenzi Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Clement Mshana akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwajili ya kuzindua rasmi Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
Na Benedict Liwenga – MAELEZO
SHIRIKA la Utangazaji Tanzania (TBC) na Shirika la Radio ya Kimataifa ya Jamhuri ya Watu wa China (CRI) leo kwa pamoja yameshirikiana katika sherehe ya Uzinduzi wa Tamthiliya ijulikanayo kwa jina laMAPENZI NA FURAHA YA KIJANA (Jin Tai Lang)  ambayo imechezwa na China na kuwekwa sauti kwa lugha ya Kiswahili na wasanii wa Tanzania.
Sherehe hiyo imefanyika leo katika Viwanja vya TBC ikishuhudiwa na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Gabriel akiwemo Mwakilishi wa Balozi toka Ubalozi wa China nchini Tanzania, Wajumbe wa Bodi ya Wakaurugenzi TBC, Mkurugenzi Mkuu Star Media Tanzania, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara mbalimbali na wafanyakazi.
PIX 2
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Gabriel akitoa hotuba yake mbele ya viongozi mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
Hatua ya uzinduzi wa sherehe hiyo ni matokeo ya utekelezaji wa Sera ya Serikali ya kujenga mahusiano na ushirikiano na nchi rafiki kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo habari, Utamaduni na michezo.
“Pamoja na kutekeleza sera za Serikali pia TBC tunatambua umuhimu wa kuwa na michezo ya kuigiza ambayo inazingatia utamaduni wa Watanzania na niwahakikishie kuwa Tamthiliya hizi zimeonesha hali hiyo.”. Alisema Mkurugenzi Shirika la Habari Tanzania Clement Mshana.
Mashirika ya habari ya TBC na CRI yamekuwa mstari wa mbele katika kuimarisha ushirkiano nah ii ni mara ya tatu kuwa na Tanmthiliya ya Kichina iliyowekwa sauti kwa lugha ya Kiswahili ambapo mwaka 2012 kulikuwa na tamthiliya ya MAU DOU DOU NA VISA VYA MAMA WAKWE ZAKE, ikifuatiwa na tamthiliya mbili nyingine ya MAISHA YA MAMA na FURAHA YA BABA ambazo zote zimepata umaarufu.
PIX 4
Mtendaji Mkuu Kampuni ya Star Media (T) Ltd Bw. Jack Czhou akieleza jambo wakati wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
PIX 6
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Gabriel akifurahi mara baada ya kukata utepe ikiwa ishara ya kukamilika kwa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
PIX 7
Mkurugenzi Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Clement Mshana (kushoto) pamoja na Mshauri wa mambo ya Utamaduni Bw. Lzu Dong (kulia) wakipeana zawadi mara baada ya Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
PIX 5
Baadhi ya wafanyakazi toka Kampuni ya Star Media (T0 Ltd na wasanii waliotumika kuweka lugha ya Kiswahili katika Tamthiliya ya Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) wakisikiliza kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi leo wakati wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
PIX 9
PIX 10
PIX 11
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi, Watendaji na Viongozi mbalimbali mara baada ya Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.*PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA).
CHANZO, MO BLOG

PSPF WASHIRIKI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA USALAMA NA AFYA DUNIANI KWA WAFANYAKAZI VIWANJA VYA MNAZI MMOJA DAR

IMG_4021 - Copy
Ofisa muendeshaji wa Mfuko wa Pesheni wa Mashirika ya Umma (PSPF),  Bw. Hadji Jamadary (kushoto) akimwelekeza kujaza fomu Shabani Maganga wakati wa maaadhimisho ya siku ya usalama na afya kazini yaliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam.
pspf 1 - Copy
Ofisa muendeshaji wa PSPF, Hadji Jamadary (kushoto) akiwapatia maelezo ya jinsi ya kujiunga na PSPF wakati wa mahadhimisho ya siku ya usalama na afya kazini yaliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam.
pspf3 - Copy
Afisa Muendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PSPF) Bw. Lule Kasembwe (kushoto) akitoa maelekezo kwa wazee waliotembelea banda lao kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja
CHANZO, MPENJA BLOG

DILI LIMEKAMILIKA! DIDIER KAVUMBAGU AMWAGA WINO AZAM FC





Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

DIDIER Kavumbagu kwaheri Yanga. Hii ni baada ya mchana wa leo kusaini mkataba wa mwaka mmoja na mabingwa wapya wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya Azam fc, lakini kuna kipengele kinachosema ataongezewa mwaka mwingine kama atafanya kazi nzuri.

Taarifa hii imethibitishwa na meneja wa Azam fc, wana Lambalamba, Jemedari Said.

“Kavumbagu is a done deal! Tumemalizana nae na amesaini rasmi mkataba wa mwaka mmoja, so tutakuwa nae msimu ujao kwenye kampeni ya kutetea ubingwa wetu pamoja na michuano ya klabu bingwa ya Afrika,” alifunguka Jemedari.

Mshambuliaji huyo hatari na nahodha wa timu ya Taifa ya Burundi ameamua kumwaga wino Azam baada ya Uongozi wa Yanga kusuasua kumpa mkataba mwingine baada ya ule wa miaka miwili kumalizika.

Kavumbagu mara kadhaa alikaririwa na vyombo vya habari kuhitaji mkataba mpya katika klabu ya Yanga, lakini viongozi wa kalbu hiyo hawakuonesha nia na leo hii imeamua kuanza maisha mapya Chamazi.

Katika maelezo yake, Kavumbagu alieleza kuwa mpira ni sehemu ya maisha yake na kazi yake, hivyo yuko tayari kuichezea klabu yoyote yenye nia ya kumsajili kwa masharti ya kukidhi mahitaji yake ya msingi.

Azam fc wenye nia ya kufanya vizuri katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika mwakani, wamekusudia kuongeza nguvu katika kikosi chao.

Kocha mkuu, Mcameroon, Joseph Marius Omog ameenda likizo kwao Cameroon , lakini uongozi wa Azam ulithibitisha kupokea taarifa ya mapendekezo yake na tathimini ya msimu uliomalizika aprili 19 mwaka huu.

Usajili huu unathibitisha kuwa Kavumbagu alikuwa katika rada za Omog na aliwaachia viongozi mpango mzima.

Kuzugazuga kwa Uongozi wa Yanga kumemfanya nyota huyo kuangukia mikononi mwa matajiri wa Azam fc japokuwa alikuwa tayari kumwaga wino tena katika klabu ya Yanga.

Mkataba aliosaini Azam fc unasemekana kuwa na masilahi bora zaidi ya ule wa Yanga.

Nyota huyo mwenye uchu wa mabao alijiunga na Yanga mwaka 2013 akitokea klabu ya Atletico ya nchini Burundi.


Kavumbagu amesaini mbele ya Katibu Mkuu wa klabu ya Azam, Nassor Idrisa makao makuu ya klabu, Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Nassor amekaiririwa na Tovuti ya klabu akisema; “Tumepata mshambuliaji mzuri, ambaye tayari ana uzoefu wa kucheza Ligi Kuu ya Tanzania kwa misimu miwili, mchezaji huyu ni chaguo la kocha wetu Joseph Omog, ambaye alivutiwa naye baada ya kumuona akichezea klabu yake zamani, Yanga SC,”alisema.

Kwa upande wake, Kavumbangu ameiambia Tovuti ya Azam kuwa; “Mimi ni mchezaji, kazi yangu ni mpira. Nimemaliza mkataba Yanga, lakini viongozi hawaniambii kitu, nimepata ofa nzuri Azam nikaamua kusaini,”.

Mshambuliaji huyo mrefu mwenye nguvu amesema sasa akili yake anaipeleka kwa mwajiri wake mpya, Azam FC ambako pia amepania kwenda kushinda mataji na kuiwezesha timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika.  

“Mimi sasa ni mchezaji wa Azam, nafurahi kujiunga na klabu hii kubwa. Kawaida yangu huwa nashabikia klabu nayochezea, sasa mimi ni mshabiki namba moja wa Azam,”amesema.   

Kavumbangu alitua Yanga mwaka 2013 akitokea Atletico ya Burundi na katika mechi misimu miwili ya kuichezea klabu hiyo, amefunga mabao 31 katika mechi 63 za mashindano yote, moja tu la penalti.

Kila la heri Kavumbagu katika maisha mapya Azam fc.

CHANZO, MPENJA BLOG

BAYERN WAVULIWA UBINGWA UEFA, WALIMWA 5-0 NA REAL MADRID, `MNYAMA` RONALDO AVUNJA REKODI YA MESSI


BAYERN Munich wamevuliwa ubingwa wa UEFA kwa kipigo cha mbwa mwizi baada ya kufungwa mabao 5-0 na Real Madrid katika mechi mbili za nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Mechi ya kwanza katika dimba la Santiago Bernabeu, Real Madrid walishinda bao 1-0 na leo hii katika nusu fainali ya pili kwenye uwanja wa Allianz Arena mjini Munich, kikosi cha Carlo Ancelotti kimeibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Real Madrid walitumia dakika 16 tu kufunga goli ambapo Luca Modric alichonga kona kutoka winga ya kulia na Sergio Ramos kujitwishwa mpira huo na kuuzamisha kimiani.

Dakika nne baadaye, beki huyo wa kati aliwamaliza Bayern baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu ndogo uliochongwa na Gareth Bale.


 Baadaye Real Madrid walifanya shambulizi la kushitukiza ambapo Cristiano Ronaldo alifunga bao safi baada ya Bale kumpatia pasi murua.

Bao hilo liliwafanya Real wahitimishe dakika 45 za kipindi cha kwanza kwa mabao 3-0.

Bao la dakika ya 90 la Cristiano Ronaldo kwa njia ya adhabu ndogo lilitia chumvi katika kidonda cha Bayern na kuvuliwa ubingwa kwa wastani wa mabao 5-0.

Kabla ya mechi hii, nyota wa zamani wa soka la Ujerumani, Stefan Effenberg alionesha wasiwasi wake kama falsafa ya Pep Guardiola itaisaidia Bayern Munich kutwaa ubingwa wa UEFA,  wakati huu ambapo mchezaji muhimu Frank Ribery yupo katika kiwango cha chini.

Effenberg anaamini falsafa ya sasa ya Bayern ya kupiga pasi nyingi haikuweza kuwasaidia Bernabeu na alikuwa na wasiwasi katika mechi ya leo.

Kipigo cha mabao 4-0 kimethibitisha mawazo ya gwiji huyo wa soka la Ujerumani.

Tangu enzi za Zinedine Zidane, Luis Figo, Roberto Carlos na Raul, Real Madrid hawajacheza fainali na sasa wamefanikiwa kuelekea La Decima mjini Lisbon mwezi ujao.

Kabla ya mechi, watu walikuwa wanasema Real Madrid wanahitaji bao 1 zaidi au suluhu ili kuwashinda Bayern, lakini wameweza kushusha mvua kubwa ugenini.

Baada ya mechi hiyo, Gareth Bale amesema kipigo walichotoa leo hii ni sababu mojawapo ya yeye kujiunga na klabu kubwa duniani majira ya kiangazi mwaka jana.

“Ni matokoe mazuri mno kwetu. Nadhani tumejituma, tulitumia vizuri mbinu zetu na kucheza vizuri usiku huu, hivyo tulistahili ushindi”. Bale amezungumza na ITV.

“Walicheza mpira sana, waliacha nafasi za kushambuliwa kwa kushitukiza, nasisi tunapenda hivyo”.
“Tuna wachezaji wenye kasi na tunatumia nafasi kama hizo. Tulikuwa katika kiwango bora na tumefurahi kufika fainali”, “Lakini kuna hatua nyingine mbele”.

“Kiukweli hii ndio sababu ya kwanini nilijiunga na Madrid. Ndio maana niliamua kuja kujiunga na klabu kubwa zaidi duniani”
“Lengo ni kushinda makombe na mechi kubwa. Tunatakiwa kushinda taji, tutakuwa na fainali ngumu kwa timu yoyote itakayopita kesho”.


 article-2616240-1D74F53100000578-959_634x429

Ronaldo baada ya kufunga mabao mawili usiku huu amevunja rekodi ya Lionel Messi kwa kufikisha mabao 16 katika msimu mmoja wa UEFA.

Real Madrid wamefuzu kwa mara ya kwanza fainali tangu walipofanya hivyo mwaka 2002 na kutwaa kombe na sasa wanatarajia kukutana na Chelsea au Atletico Madrid ambazo zitapambana kesho katika uwanja wa Stamford Bridge.

Mechi ya kwanza katika dimba la Vicente Calderon mjini Madrid, Chelsea walilazimisha suluhu ya bila kufungana, hivyo wanahitaji bao 1-0 ili kufuzu fainali.


CHANZO, MPENJA BLOG

Tuesday, 29 April 2014

NANI ATANYAKUA UBINGWA KATIKA LIGI KUU YA UINGEREZA?

CHEKI PICHA 11 ZA WANAMICHEZO MAARUFU ENZI ZAO WAKIWA WATOTO

0

Wengi kati yao sura zao hazijabadirika sana tangu kipindi chao cha utotoni lakini picha hizi zitakuonyesha kwamba wanamichezo hawa wameanza kucheza michezo yao tangu wakiwa watoto.

Kwenye picha hizi kuna watu kama Cristiano Ronaldo,Lebron James,Lewis Hamilton,Tiger Woods,Michael Owen na wengine.
1

                                                                        Neymar

2

                                                                      David Beckham

3

                                                                     Michael Owen

4

                                                                     Lewis Hamilton

5

                                                                      Diego Maradona

6


                                                                               Messi

7

                                                                   Lebron James

8

                                                                       Tiger Woods

9

                                                            Serena na Venus Williams

10

                                                                    Cristiano Ronaldo


CHANZO, MILLARDAYO

MAMA SALMA AZINDUA CHANJO YA KUZUIA MAAMBUKIZO YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KWA WASICHANA WENYE UMRI WA MIAKA 9 HADI 16. HUKO MOSHI.

IMG_0089
IMG_0127 IMG_0147 IMG_0164 IMG_0168 IMG_0185 IMG_0228 IMG_0236 IMG_0303 IMG_0332 IMG_0350 IMG_0373
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anaonekana akitoa chanjo ya matone kuzuia ugonjwa wa polio kwa mtoto Ahmad, miezi 10, aliyefika kwenye sherehe ya uzinduzi wa chanjo ya kuzuia maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana huko Pasua, Moshi tarehe 28.4.2014.

 PICHA NA JOHN  LUKUWI.
CHANZO,FULL SHANGWE