Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 5 July 2016

TIGO YAFANA MAONYESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA 40


Wateja wa Tigo wakipata huduma za Tigo pesa katika banda la tigo  
kwenye maonesho ya 40 ya kimataifa ya biashara (sabasaba) jijini Dar Es Salaam jana.

MAONESHO YA 40 YA BIASHARA YA KIMATAIFA (SABA SABA) YAPANUA WIGO WA USHIRIKI


Na Immaculate Makilika- MAELEZO
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), imekua ikiandaa maonesho haya ya biashara ya kimataifa kila mwaka. Maonesho ya 40 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam yameanza tarehe 28 Juni hadi tarehe 8 Julai, mwaka huu katika uwanja wa maonesho wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam yameendelea kuwa maonesho makubwa na yenye mafanikio katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

BARAZA LA WAWAKILISHI LAWACHAPA MAVETERANI WA KIKWAJUNI 1-0 KOMBE LA JAZEERA

Waziri wa Habari Michezo Mhe Nape Moses Nnauye akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya TAYI Tanzania Ndg. Abdalla Othman Miraji wakati akihudhuria fainali za Kombe la Masauni and Jazeera lililofanyika jana usiku katika viwanja vya Mnazi Mmoja kati ya Kilimani na Kisimamanjongoo, kabla ya mchezo huo kulikuwa na mchezo wa utangulizi kati ya Maveterani wa Kikwajuni na Timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, katika mchezo huo timu ya Baraza imeshinda bao 1--0. 

DK. KIGWANGALLA AKUTANA NA BALOZI WA KOREA KUJADILI KUHUSU HOSPITALI YA MLONGANZIRA

Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na balozi wa Korea nchini, Song Geum-young kuhusu uhusiano wa Tanzania na Korea na jinsi ambavyo nchi hiyo imepanga kuendelea kuisaida Tanzania katika kuboresha huduma za kiafya nchini. (Picha zote na Rabi Hume, MO Blog)

Kwa muda mrefu Tanzania imekuwa na urafiki na Korea na katika kulidumisha hilo, Balozi wa Korea nchini, Song Geum-young amemtembelea Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla na kuzungumza mambo mbalimbali kuhusu ushirikiano wa Korea na Tanzania zaidi katika sekta ya afya na jinsi Korea ambavyo imekuwa ikisaidia uboreshwaji wa huduma za kiafya nchini.

KAMPUNI YA EMOTEC YAJIPANGA KUTOA HUDUMA BORA ZA TEHAMA

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Emotec Limited, Bw. Moses Hella, akielezea moja kati ya gunduzi za kampuni yake kwa wageni (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kuazimisha miaka minne ya Chinese Alumni Association.

WAJASIRIAMALI WATAKIWA KUJITOKEZA WAWEZESHWE KUWEKEZA KWA AJILI YA MAENDELEO

Mkurugenzi wa kitengo cha Africa wa JICA, Hideki Watanabe akielezea Jinsi JICA wanavyofanya shughuli za Maendeleo Afrika

MKUU WA MKOA WA MWANZA AWAKUMBUKA WENYE UHITAJI.

Siku chache kabla ya kusherehekea Siku Kuu ya Idd, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella (pichani), amekabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ikiwemo vyakula kwa watoto ajili ya yatima pamoja na wazee mkoani Mwanza.
Na BMG
Jana Mhe. Mongella alikabidhi mbuzi 20, mafuta ya kula ndoo 20, kila moja lita 20, mchele mifuko 20, kila mmoja ukiwa na kilo 50 pampja na sukari mifuko 20, kila mmoja ukiwa na kilo 25.

CUF YAZINDUA TAWI LA WANAFUNZI WANACHAMA WA CUF LA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (JIVICUF UDSM)

 Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa , Juvicuf, ambaye pia ni Mbunge wa Mchinga Hamidu Bobal (kushoto), akizungumza na wanafunzi wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (JIVICUF UDSM), Dar es Salaam jana wakati akizindua tawi la wanafunzi hao katika chuoni hapo.

UN YASHINDA KWENYE MAONYESHO YA 40 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DAR ES SALAAM 2016

Rais wa Rwanda Paul Kagame, (wa pili kulia) akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, (wa kwanza kulia), akimkabidhi tuzo ya mwoneshaji bora kwenye kategori ya habari, machapisho, uchapishaji na vifaa vya ofisini, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez, wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 1, 2016. Wapili kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mh. Charles Mwijage.

Shirika la Umoja wa Mataifa limenyakua tuzo ya mwoneshaji bora kwenye kategori ya habari, machapisho, uchapishaji na vifaa vya ofisini katika sherehe za uzinduzi wa maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

BONGO FLEVA TOP 10 YA MAISHA BASEMENT WIKI HII

IMG-20160703-WA0000
1.Bill Nass- Chafu Pozi 
2.Raymond - Natafuta Kiki 
3.Darasa ft Rich Mavoko -Kama Utanipenda 
4.Rich Mavoko - Ibaki Story 
5.Namjua – Shetta 
6.Ali Kiba - Aje 
7.Mr Blue na Ali Kiba - Mboga Saba 
8.Ben Pol - MOYO MASHINE 
9.Nuh Mziwanda Ft. Alikiba - Jike shupa 
10.Dogo Janja-My Life 

Kupendekeza wimbo uingie katika top 10 ya Jumapili hii endelea kutembelea page yetu ya Instagram ya Global Publishers na Maisha Basement

KAMPUNI YA SIMU YA TIGO, MILVIK KUSHIRIKIANA KUTOA BIMA WATAKAYOIMUDU WATANZANIA

 Meneja wa Milvik Tanzania,Tom Chaplin (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Tigo Kijitonyama Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akitangaza ushirikiano kati yao na Tigo kutoa bima watakayoimudu watanzania. Kutoka kushoto ni Meneja wa Promosheni wa Tigo, Mary Rutta, Mkuu wa Huduma za kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel na Meneja Maendeleo ya Biashara wa Resolution Insurance, Zamaradi Mbega.

EPZA YATENGENEZA AJIRA 36,000

 Ofisa Mwamasishaji Mwandamizi wa Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA), Nakadongo Fares (kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu mambo mbalimbali yanayofanywa na mamlaka hiyo. Kushoto ni Meneja Uhamasishaji Uwekezaji,  Grace Lemunge.

MULTICHOICE TANZANIA KUBADILI MAISHA YA WATOTO YATIMA DAR

Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande akizungumza kuhusu msaada ambao wameutoa kwa kituo cha Al--Madina.

Zikiwa zimesalia siku kadhaa kabla ya kusherekea sikukuu ya Eid El Fitri, Kampuni ya Multichoice Tanzania ambao ndiyo wasambazaji wa ving'amuzi vya DSTV nchini imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto yatima ambao wanaishi katika kituo cha Al-Madina kilichopo Tandale kwa Tumbo, misaada ambayo kwa namna moja au nyingine inaweza kusaidia kubadilisha maisha ya watoto hao.

MFALME WA AFRO POP TWENTY PERCENT ARUDI KWENYE GEMU KWA KISHINDO NA SAUTI YAKE YA GHARAMA

Producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water (chini kushoto) akiweka saini kwenye hati ya mkataba wa lebo ya KOMBINENGA kurasimisha usimamizi wa kazi za msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) akishuhudiwa na Wakili msomi Iddi M. Gogo wa Alpha Attorneys  (juu kulia) aliyefanikisha zoezi hilo, pamoja na meneja uzalishaji wa Combination Sounds, Rowel Moses (juu kushoto) kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.

Na Sultani Kipingo
Mfalme wa Afro Pop nchini Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) anavunja ukimya na kurejea kwa kishindo kwenye anga ya muziki,  huku akiwa msanii wa kwanza kusaini mkataba na lebo mpya ya KOMBINENGA inayoendeshwa na producer nguli John Shariza a.k.a Mann Water.

Saturday, 2 July 2016

MADC WAPYA MKOANI TANGA WATAKIWA KUSIMAMIA SHUGHULI ZA MAENDELEO KWA UMAKINI MKUBWA

Katibu Tawala Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi akizungumza kwenye halfa ya kuapishwa wakuu wa wilaya wapya wa mkoa wa Tanga kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella na Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Othumani Shijja.

Msama awatahadharisha wauza CD Feki

Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam imewatahadharisha wanaouza kazi feki za wasanii mbalimbali hapa nchini kuachana na mfumo huo kwa sababu kuanzia mwezi huu  watawakamata wanaofanya biashara hiyo ndani ya mwezi mmoja.
Akizungumza jana, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama alisema wametoa siku 30 kwa wanaofanya biashara hiyo kuachana nayo kabla hawajawashukia.

Friday, 1 July 2016

TAASISI YA METDO YAHIMIZA WAZEE WANAOLELEWA KATIKA KITUO CHA BUKUMBI KUSAIDIWA

Ashraph Omary (wa pili kushoto) akizungumza jambo kwa niaba ya Wanachama/Wafanyakazi kutoka Taasisi ya METDO (Mining and Environmental Transformation For Development Organisation, walipotembelea Kituo cha Wazee Bukumbi kilichopo Misungwi mkoani Mwanza.

Wafanyakazi wa METDO wakiambatana na Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa daladala Kanda ya Ziwa, Hassan Dede pamoja na Wanafunzi wa Geita International School, waliwakabidhi wazee wanaolelewa katika kituo hicho msaada wa mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula.

KOCHA SERENGETI ASEMA HATABADILI KIKOSI KESHO


Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, Bakari Nyundo Shime, amesema hatarajii kuwa na mabadiliko makubwa ya kikosi katika mchezo dhidi ya vijana Shelisheli utakaopigwa kesho Jumamosi Julai 2, 2016 kwenye Uwanja wa Stade Linite mjini Victoria.

Mshindi wa Nyumba ni Nelly Mwangosi wa Iringa

NYUMBA (1)
Meya wa Wilaya ya Temeke, Abdallah Chaurembo akisoma jina la mshindi wa nyumba, ambaye ni Nelly Mwangosi kutoka Iringa.

Kampuni ya Resolution Insurance LTD yafturisha wadau mbali mbali pamoja

Mkurugenzi Mkaazi wa Kampuni ya Resolution Insurance Ltd Oscar Osir akipata iftar pamoja na Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam Sheikh Alhadi Musa Bin Salum katika iftar kwa ajili ya wateja na wafanyakazi wake iliyoandaliwa na kampuni ya Resolution Insurance LTD jijini Dar es Salaam.