Wakati michezo miwili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikifanyika kesho Jumatano Novemba 9, 2016, mchezo kati ya Young Africans na Ruvu Shooting utafanyika Alhamisi Novemba 10, 2016 kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, imefahamika.
Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Tuesday, 8 November 2016
KABAGO, MKONGWE KWENYE MUZIKI WA KUCHANA NCHINI KUACHIA WIMBO MPYA
Kupitia vyombo mbalimbali vya redio, kesho jumatano Novemba 09, 2016 mkongwe wa muziki wa kuchana nchini, Filbert Kabago "Kabago", ataachia wimbo wake mpya uitwao Tanzania akiwa amemshirikisha Hadmad.
MKUU WA MKOA WA MWANZA AZINDUA KITUO CHA HUDUMA SHIRIKISHI DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA NA WATOTO
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha One Stop Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure, hii leo.
MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI OKTOBA 2016, UMEBAKI KUWA ASILIMIA 4.5
DKT. POSSI AIPONGEZA UNESCO KUPUNGUA KWA UKATILI DHIDI YA ALBINO
SALAMU ZA RAMBI RAMBI KIFO CHA MZEE SITTA - CCM
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa majonzi na simanzi kubwa taarifa za kifo cha Mhe. Samuel John Sitta, Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichotokea usiku wa jana tarehe 6/11/2016 katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani alipokuwa akitibiwa.
BENKI YA TWIGA YATOKA KIFUNGONI YAAANZA KUTOA HUDUMA ZAKE TENA
| Gavana wa Benki Kuu. Profesa Beno Ndulu. |
Na Dotto Mwaibale
BENKI ya Twiga Bancorp Ltd (Twiga)ambayo ilikuwa imefungwa kwa muda na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) itaanza kufanya kazi baada ya mchakato wa kuifanyia tathmini ya kifedha kukamilika.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana benki hiyo itaanza kutoa baadhi huduma za kibenki kwa umma kuanzia kesho Novemba 8, 2016.
MKUU WA WILAYA YA NYAMAGANA AFURAHISHWA NA KONGAMANO LA WANAWAKE JIJINI MWANZA
Mtangazaji wa Kipindi cha THE MBONI SHOW kinachoandaliwa na Kampuni ya Chocolate Princes na kurushwa na TBC1, Mboni Masimba, akizungumza kwenye Kongamano la SAUTI YA MWANAMKE lililofanyika jana Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.
Sunday, 6 November 2016
KAMPENI YA BINTI WA KITAA YAFIKA WILAYA YA TEMEKE JIJINI DAR, WAKAZI WAPATA ELIMU JUU YA KUZUIA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI
Afisa Mtendaji wa Wilaya ya Tandika Hija Kipeleka akizindua Rasmi kampeni ya Binti wa kitaa katika Wilaya ya Temeke, ambapo aliwashukuru wanaoendesha kampeni hiyo na kuahidi kushirikiana nao katika kupinga mimba na ndoa za utotoni.
Saturday, 5 November 2016
LIGI YA VIJANA KUANZA KUPIGWA NOVEMBA 15, 2016
Ligi ya Vijana ya Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF) wenye umri wa chini ya miaka 20, inatarajiwa kuanza Novemba 15, 2016 mwaka huu kwa uzinduzi rasmi utakaofanyika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera kwa timu za vijana za Kagera Sugar na Young Africans ya Dar es Salaam kuchuana siku hiyo.
AZAM SPORTS FEDERATION CUP KUZINDULIWA TANGA NOVEMBA 19, 2016
Azam Sports Federation Cup (ASFC) itakayoshirikisha timu 86 msimu huu, itaanza rasmi Novemba 19, 2016 kwa uzinduzi rasmi utakaofanyika mkoani Tanga.
ELIGIBILITY OF CONGO U17 PLAYERS
Following various reports circulating in the social media regarding the eligibility of Republic of Congo U17 players in the just ended Afcon U17 qualifiers Tanzania Football Federation wishes to state as follows:
MCHEZO KATI YA BULYANHULU, GREEN WARRIORS UTATA
Mchezo Na. 4 wa Ligi Daraja la Pili kati ya Bulyanhulu na Green Warriors ulikuwa ufanyika jana Novemba 4, 2016 kwenye Uwanja wa CCM-Kambarage, mkoani Shinyanga haikufanyika.
MSUVA MCHEZAJI BORA WA VPL MWEZI OKOTOBA
Winga Simon Msuva wa Young Africans amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu ya Vodacom.
BUNGE LAPITISHA RASMI MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI WA 2016
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye alipokuwa akitoa hoja kabla Kamati ya Bunge zima kujadili Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 ambao umepitishwa leo mjini Dodoma.
KAMBI YA UPINZANI YAUKUBALI MUSWADA WA HABARI KWA KUWEKA BIMA YA AFYA KWA WANAHABARI
Msemaji Mkuu wa Kambi Bungeni katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Joseph Mbilinyi akiwasilisha hotuba ya kambi hiyo kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Kambi Rasmi ya upinzani Bungeni yaikubali Bodi ya Ithibati, Baraza Huru la Habari pamoja na Bima ya Afya kwa waandishi wa habari nchini.
Akiwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni mjini Dodoma, Msemaji Mkuu wa Kambi hiyo katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Joseph Mbilinyi amesema kuwa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 unamaufaa kwa wanahabari nchini.
MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI WASOMWA MARA YA PILI BINGENI
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akiwasilisha Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 leo Bungeni mjini Dodoma.
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Muwada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 umesomwa mara ya pili Bungeni mjini Dodoma ukiwa na lengo la kuifanya tasnia ya habari nchini kuwa taaluma kamili.
MAGUFULI: VYOMBO VYA HABARI SIMAMIENI KUJENGA MAADILI NA UTAMADUNI WA MTANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Wahariri, Watangazaji na Waandishi wa Vyombo mbalimbali vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam jana Novemba 4, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli ametoa wito kwa vyombo vya Habari nchini kuwa mbele katika kusimamia Maadili na kuutangaza Utamaduni wa Mtanzania.
TWIGA STARS KUIPIMA UBAVU CAMEROON
Waandaaji wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake 2016, wameipa heshima Tanzania na kuona kuwa Twiga Stars – Timu ya Taifa ya Wanawake inafaa kuipima ubavu kabla ya kuanza kwa fainali hizo Novemba 19, mwaka huu.
MAZUNGUMZO YANGA, SIMBA KUHUSU HASSAN KESSY YAENDELEA VEMA
Mazungumzo kati ya Viongozi wa Young Africans na Simba, katika shauri la madai, yanaendelea vema na mwishoni mwa wiki hii huenda wakakamilisha kwa kuridhiana.
AFRICAN LYON KUIKABILI SIMBA YA MSIMBAZI KESHO
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), mzunguko wa 15 unaomaliza duru la kwanza kwa msimu huu, inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa timu 12 kuchuana kwenye viwanja sita.
MKWASA ATAJA TAIFA STARS ITAKAYOIVAA ZIMBABWE NOVEMBA 13
Kocha Mkuu wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa jana Novemba 04, 2016 ametaja majina ya nyota 24 watakaounda kikosi ambacho kitasafiri wiki ijayo kwenda Harare, Zimbabwe kucheza na wenyeji kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Novemba 13, mwaka huu.
AGA KHAN YAWAPIGA MSASA WABUNGE, WADAU UBORESHAJI ELIMU NCHINI
Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Kitila Mkumbo akielezea kwenye mkutano wa wadau wa elimu mjini Dodoma, mambo mbalimbali yanayokwamisha maendeloeo ya elimu na jinsi ya kuiboresha. Mkutano huo ambao pia walishirikisha wabunge umeandaliwa na Chuo Kikuu cha Aga khan (AKU).PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
Mwenyekiti wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Zungu na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi wakisikiliza kwa makini mada kuhusu uboreshaji wa elimu nchini.
Washiriki wakiwa katika mkutano huo wa kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu nchini na jinsi ya kuziboresha
FILAMU NA TAMTHILIA ZA KITANZANIA ZAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM ZITARUSHWA NA DSTV
WASANII KUTOKA NIGERIA KUNOGESHA FAINALI YA TAMASHA LA FIESTA 2016, KESHO VIWANJA VYA LEADERS JIJINI DAR ES SALAAM
Msanii kutoka Nigeria, Yemi Alade (kushoto) , akisalimiana na msanii Snura Mushi alipokuwa amewasili ukumbi wa mikutano wa Kampuni ya Simu ya Tigo kuzungumza na wanahabari wakati akijitambulisha kwao Dar es Salaam leo jioni, kuhusu uwepo wake kwenye hitimisho la Tamasha la Fiesta litakalofanyika kesho viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
EU YAWEKEZA EURO MILIONI 1.7 KITUO CHA UTAMADUNI MAKUMIRA
Umoja wa Ulaya (EU) umewekeza zaidi ya Euro milioni 1 na laki 7 katika kituo cha Utamaduni cha Makumira kitengo kilichoko ndani ya Chuo Kikuu cha Makumira ambapo chuo kikubwa cha sanaa kinajengwa pamoja na kumbi ya burudani itakayogharimu kiasi hicho.
Friday, 4 November 2016
SHIRIKA LA WOTESAWA LATAMBULISHA MRADI WAKE WA SAUTI YA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI.
Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani WOTE SAWA lililopo Jijini Mwanza, Angela Benedicto, akizungumza hii leo wakati wa kutambulisha mradi wa "SAUTI YA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI" utakaofanya kazi kwenye Kata za Igogo, Mkuyuni, Butimba na Nyamagana Jijini Mwanza.
TAASISI YA ANSAF YAWANOA WADAU WA KILIMO KANDA YA ZIWA
Katibu Tawala Msaidizi idara ya Uchumi na Uzalishaji mkoani Mwanza, Joanen Kukwami akifungua mkutano wa wadau wa kilimo Kanda ya Ziwa unaofanyika Jijini Mwanza kwa siku mbili, jana Novemba 03 na leo Novemba 04, 2016.
Mkutano huo uliandaliwa na Jukwaa la Wadau wa Kilimo nchini ANSAF, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kuhakikisha kunakuwa na kilimo chenye tija katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ili familia ziweze kujikimu kiuchumi na kichakula.
HAYA NDIYO MAJIBU YA SERIKALI YA HOJA ZA WABUNGE KUHUSU MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA NA MWONGOZO WA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2017/2018
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (Kulia wanaoshuka ngazi), akizungumza jambo na Mbunge wa Kasulu Mjini, Mhe. Daniel Nsanzugwanko, baada ya kumalizika kwa mjadala wa mchana kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2017/2018, Bungeni Mjini Dodoma.
WANANCHI KIJIJI CHA MKALAMA WAUNGA MKONO KAMPENI ZA MKUU WA WILAYA YA HAI ZA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA
NYUKI WAZUA KIZAA ZAA KATIKA MCHEZO WA RUVU SHOOTING NA AFRICAN LYON
Wachezaji wa timu za Ruvu Shooting wenye jezi rangi ya bluu na wa African Lyon wakiwa wamelala chini ikiwa ni kujihami na makundi ya nyuki ambayo yalikuwa yanapita uwanjani hapo hivyo wachezaji, waamuzi na mabenchi ya wachezaji wa akiba wote walilazimika kulala chini ikiwa ni kujinusuru kutokana na hali hiyo. Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Shooting iliibuka na ushndi wa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji mwenye nguvu za miguu Issa Kanduru kunako dakika ya 19.
SEKTA YA DAWA YA BINADAMU NCHINI YAPATA WAWEKEZAJI
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage
Na Jacquiline Mrisho -
MAELEZO, Dodoma
Wizara
ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wamefanikiwa
kuhamasisha baadhi ya wawekezaji kuwekeza katika sekta ya dawa ya binadamu na
vifaa tiba ili kupunguza uagizaji wa dawa kutoka nje ya nchi.
Thursday, 3 November 2016
WATAKIWA KUJIEPUSHA NA SIASA KATIKA KUJADILI MUSWADA WA HABARI
Na Mwandishi Wetu.
Dar es Salaam.
2.Nov.2016.
WADAU wa tasnia ya habari nchini wametakiwa kujiepusha na itikadi za kisiasa kwa kisingizio cha ufinyu wa muda katika kujadili muswada wa sheria ya huduma za habari kwa kuwa sheria si kitabu takatifu kisichoweza kufanyiwa marekebisho.
MWAKA MMOJA WA JPM SEKTA YA UTALII YATOA MCHANGO MKUBWA KWENYE UCHUMI NCHINI
Na Beatrice Lyimo - MAELEZO
Mnamo Novemba Tano mwaka huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli atatimiza mwaka mmoja tangu alipoapishwa kuongoza Nchi hii katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
UN NA EU ZATOA EURO LAKI NANE KUSAIDIA WATOTO WA KIKE
Shirika la Umoja wa Mataifa la UN kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU) wametoa Euro laki nane kuwasaidia watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu na wahanga wa mimba za utotoni waishio kwenye kituo cha Faraja Young Women Development Unit .
Subscribe to:
Posts (Atom)
























