| Meneja wa Huduma za kijamii wa Tigo Woinde Shisael akizngumza na wanahabari wakati wa Uzindizi wa shindano hilo leo Jijini Dar es salaam |
Kampuni ya simu ya Tigo kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Reach For change wamezindua shindano la Tuzo ya mwaka ya kidigitali ya Tigo Change Makers,shindano linalolenga kuwatambua na kuwasaidia wajasiriamali jamii kwa kutumia zana za kidigitali na Technologia katika kuboresha Jamii pamoja na matokeo yake kwa Vizazi vya Baadae,ambapo kwa mwaka huu Tigo inaangalia ubunifu uliojikita katika mtazamo wa elimu kupanua kujumuisha kidigitali na ambao unalenga kusaidia shiughuli za Ujasiriamali.





