Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 4 July 2015

UONGOZI CCM NI 'ZABUNI', HUNA FEDHA KAFIE MBELE!


Na Daniel Mbega
“RUSHWA ni adui wa haki, sitatoa wala kupokea rushwa!” Hii ni ahadi namba 6 miongoni mwa Ahadi 10 za Mwana-TANU ambazo zilirithiwa na Chama cha Mapinduzi inayosisitiza kwamba mtu yeyote anayepewa uongozi hapaswi kuutumia kwa maslahi yake binafsi bali kwa maslahi ya wote.

CHADEMA YAANDAA KONGAMANO LA WAZEE, KUFANYIKA LEO HOTELI YA BLUE PEARL UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM

 Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Hashim Juma Issa (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusu kongamano litakalo wakutanisha wazee wote bila kujali itikadi za vyama vyao litakalo jadili mustakabali wa taifa kuelekea uchaguzi mkuu litakalofanyika  kesho ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl Ubungo jijini Dar es Salaam.

ZANTEL YATOA SH.MILIONI 5 KUSAIDIA CHAMA CHA MAALBINO TANZANIA KUTOA ELIMU KWA UMMA

Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose (katikati) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi kuhusu ushirikiano wao na chama cha Maalbino Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel,  Progress Chisenga, na Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Tanzania, Ernest Kimaya.
Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel,  Progress Chisenga (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Tanzania, Ernest Kimaya (katikati), akizungumza katika mkutano huo wakati akiishukuru Zantel kwa msaada huo kwa chama hicho.
Meneja wa Chapa ya Zantel, Arnold Madale (kulia), akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu msaada huo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose(wa nne kulia),   akikabidhi mfano wa  hundi ya shilingi milioni tano kwa Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Tanzania, Ernest Kimaya (kushoto) kwa ajili kusaidia chama cha Maalbino Tanzania kutoa elimu kwa umma kuhusu changamoto walizonazo. Wengine ni maofisa kutoka chama cha Maalbino na maofisa wa Zantel.

Na Dotto Mwaibale


Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo imekisaidia Chama cha Maalbino Tanzania katika mpango wake wa kusambaza elimu juu ya ulemavu wa ngozi kwa jamii pamoja na msaada wa jumla ya shilingi milioni 5 ambao unalenga kusaidia uendeshaji wa shughuli zake hapa nchini.

Zantel kwa kushirikiana na Chama Cha Maalbino kitajikita kutoa elimu hii kwa kusambaza ujumbe mfupi kwa wateja wake pamoja na kutumia vipindi vyake inavyodhamini ili kupeleka ujumbe kwa jamii kiujumla.


Pamoja na hiyo pia, Zantel inajipanga kutumia mikutano ya wafanyakazi pamoja na matamasha ili kuhakikisha ujumbe kuhusu ulemavu wa ngozi unawafikia watu wengi zaidi.


Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Pratap Ghose alisema mchango huo katika kuwawezesha Chama cha Maalbino ni sehemu ya huduma za kampuni yake kwa jamii.

“Tatizo kubwa ni ukosefu wa elimu miongoni mwa wanajamii, na kwa hakika hatua kubwa imepigwa katika kupambana na tatizo hili tayari, na sisi kama Zantel tunaamini kwa kutumia uwezo wetu kama kampuni ya simu tunaweza kushiriki kulimaliza tatizo hili la mauaji ya ndugu zetu’ alisema Pratap.

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, Tanzania ina jumla ya watu wenye ulemavu wa ngozi 5,200 na wengi wao wanaishi kanda ya ziwa, na toka mwaka 2009 jumla ya kesi 155 zinazohusu walemavu wa ngozi zimeripotiwa kwa vyombo vya sheria kwa mujibu wa taasisi ya Under the Same Sun.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Tanzania, Ernest Kimaya, ameipongeza kampuni ya Zantel kwa mchango wao akisema utasaidia sana katika juhudi zao za kupigania haki za walemavu wa ngozi nchini.

‘Watu wenye ulemavu wa ngozi ni kama binadamu wengine wa kawaida, hivyo tunaiomba jamii isiwatenge ndugu zetu hawa’ alisema Kimaya.

Bwana Kimaya pia aliomba wadau wengine wajitokeze kuwawezesha walemavu wa ngozi waweze kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo.


“Jamii yetu ya walemavu wa ngozi ina matatizo mbalimbali, hivyo tunazidi kuwaomba watu binafsi, serikali pamoja na makampuni mbalimbali wazidi kujitokeza kusaidia kundi hili la jamii’ alisisitiza Kimaya.

Chama cha Maalbino Tanzania kilianzishwa mwaka 1978 kikiwa na lengo la kulinda na kuwezesha watu wenye ulemavu wa ngozi nchini na kinahudumia zaidi ya wanachama 1,200.(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

RAIS WA ZANZIBAR ALI MOHAMED SHEIN AFUTARISHA MKANYAGENI PEMBA

a
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mkoani  Mkoa wa Kusini Pemba Bw.hemed Suleiman wakati alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Mkanyageni katika futari iliyoitayarisha kwa Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni  Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini  Pemba jana. [Picha na Ikulu.] 

JESHI LA MAGEREZA LAIBUKA MSHINDI WA KWANZA KATIKA UTENGENEZAJI WA SAMANI MAONESHO YA 39 YA BIASHARA KIMATAIFA (SABASABA) MWAKA 2015

mail.google.comMuonekano wa Samani za Ofisi ambazo hutengenezwa kwa Ustadi mkubwa katika Viwanda mbalimbali vinavyoendeshwa na Jeshi la Magereza zikiwa tayari zimekamilika kwa matumizi ya kiofsi kama inavyoonekana katika picha.
Na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza
Jeshi la Magereza limeibuka Mshindi wa kwanza kwa upande wa Utengenezaji bidhaa za Samani kwenye Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Jijini, Dar es Salaam Maarufu “SABASABA” kwa Mwaka huu 2015.
Akizungumzia ushindi huo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja amesema kuwa anajivunia ushindi huo kwani kulikuwa na ushindani mkubwa wa Makampuni mengi yanayoshiriki katika Maonesho haya ya Kibiashara yanayoendelea.

RAIS KIKWETE AONGOZA MAADHIMISHO MIAKA 50 YA USHIRIKIANO BENKI YA DUNIA NA TANZANIA, AFUNGUA MAONESHO YA 39 YA SABASABA

0000.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia moja ya shati la batiki lililoshonwa na mjasiria mali mwanamke Violet Mmanyi wakati Rais alipotembelea mabanda machache baada ya kufungua rasmi maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa Dar es Salaam maarufu kama sabasaba. (picha na Freddy Maro).

RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AZINDUA MAONESHO YA 39 YA BIASHARA YA KIMATAIFA

1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubua wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya 39 ya biashara ya Kimataifa ambapo aliwataka wafanyabiashara kutumia fursa ya maonesho haya kutangaza bidhaa wanazozalisha na kuanzisha mashirikiano ya kibiashara baina ya makampuni, leo Jijini Dar es Salaam.

NAIBU KAMISHNA ATEMBELEA BANDA LA TRA KATIKA MAONESHO YA 39 BIASHARA YA KIMATAIFA

01
Naibu Kamishna Mkuu wa Mmlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Lusekelo Mwaseba akiangalia chati ya ukusanyaji wa Kodi kwa upande wa Tanzania Bara, alipotembelea Banda la Mamlaka hiyo katika Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Jijini Dar es Salaam.

KATIBU MKUU KIONGOZI ATEMBELEA MABANDA KWENYE MAONESHO YA 39 YA BIASHARA YA KIMATAIFA

1
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipewa maelezo na maafisa wa Shirika la Bima la Taifa alipotembelea Banda hilo kwenye Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa leo jijini Dar es Salaam.

ROBOTI LAMUUA MFANYAKAZI WA KIWANDA CHA VOLKSWAGEN


Mfanyikazi mmoja katika kiwanda cha kutengeza magari aina ya Volkswagen nchini Ujerumani amefariki baada ya roboti kum'beba na kumuangusha katika chuma.

HII SASA KALI, UKITAKA KUBEBA MIMBA CHINA LAZIMA UOMBE RUHUSA!

Mwakamke mja mzito China
Kampuni moja ya Uchina inapanga kutoa masharti ambapo wafanyikazi wake watatakiwa kupata ruhusa kabla ya kuanza familia.

FERNABAHCE KUMSAJILI NANI WA MAN UNITED

Nani
Mchezaji wa klabu ya Manchester United Nani anatarajiwa kufanyiwa ukaguzi wa matibabu katika klabu ya Uturuki ya Fenerbahce baada ya vilabu hivyo viwili kukubaliana ada ya yuro milioni 6 kwa uhamisho wa mchezaji huyo.

NICHOLAS ANELKA KUINOA KLABU YA MUMBAI


Aliyekuwa mchezaji wa vilabu vya Arsenal na Chelsea Nicolas Anelka amechaguliwa kama mkufunzi wa klabu ya Mumbai City.

BIDHAA ZAUZWA BILA NEMBO YA TBS

Baadhi ya bidhaa zinazouzwa bila nembo ya ubora ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Soko la Tanzania limekuwa likipokea bidhaa kutoka ndani na nje ya nchi lakini baadhi ya bidhaa zinaarifiwa kuuzwa madukani huku zikikosa nembo za ubora.

BASATA YAMJULIA HALI MSANII RAMADHAN MASANJA (BANZA STONE)

Banza Stone

Timu ya watendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ikiongozwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Bi. Vivian Nsao Shalua mapema jana imemtembelea Msanii na mwimbaji wa muziki wa Bendi ndugu Ramadhan Masanja ‘Banza Stone” ambaye kwa muda sasa amekuwa akiugua nyumbani kwao maeneo ya Sinza  Jijini Dar es Salaam.

BRIGHTERMONDAY TANZANIA YATOA FURSA KWA WANAOTAFUTA AJIRA KUWATEMBELEA KWENYE MAONYESHO YA SABASABA

DSC_9352
Meneja Masoko wa kampuni ya Brightermonday Tanzania, Lugendo Khalfan ndani ya hema la banda la Jakaya Kikwete akiwa tayari kukuhudumia wewe mtanzania utakayetembelea banda lao katika viwanja vya maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara ‘Sabasaba’, yanayoendelea kurindima kwenye viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.( Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

UMOJA WA MATAIFA WAIBUKA KIDEDEA KATIKA UHABARISHAJI NA UTOAJI ELIMU KWENYE TUZO ZA MAONYESHO YA 39 YA SABASABA

DSC_0178
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkadhi Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) cheti na tuzo katika kipengele cha Uelimishaji bora kupitia Uandishi wa machapisho na mpangilio bora wa maonyesho, baada ya Umoja wa Mataifa kuibuka mshindi wa kwanza katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yalipozinduliwa rasmi. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko (kushoto) pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Dkt. Abdallah Kigoda (kulia).

SHAMRASHAMRA ZA USHINDI WA NSSF MAONESHO YA 39 YA BIASHARA


Baadhi ya wafanyakazi na maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii(NSSF) wakishangilia ushindi wa ngao tatu kwa pamoja katika vipengele tofauti kwenye Maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi na maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii(NSSF) wakishangilia ushindi wa ngao tatu kwa pamoja katika vipengele tofauti kwenye Maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam.

STARS KUWAVAA THE CRANES LEO


Taifa Stars inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premieum Lager leo Jumamosi saa 10 kamili kwa saa za Afrika Mashariki itashuka dimba la Nakivubo kucheza na wenyeji Uganda.(The Cranes).

Friday, 3 July 2015

KOMBE LA KAGAME: SIMBA YAONGOZA, MABAO 1776 YAFUNGWA KATIKA MECHI 745 TANGU MWAKA 1974

Kikosi cha Simba SC ambacho mwaka 1995 kilitwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa mara ya nne jijini Dar es Salaam. Waliosimama kutoka kushoto ni aliyekuwa mfadhili mkuu wa klabu hiyo Azim Dewji, Madaraka Kibode Selemani 'Mzee wa Kiminyio', Godwin Aswile Mlimba 'Scania', Mohammed Mwameja, Hussein Marsha 'Smart Boy', Mustafa Hoza na George Magere Masatu.
Walioinama mstari wa mbele ni Athumani Abdallah China 'Injini', Dua Said, Deo Mkuki, Idd Kibode Selemani 'Meya' na Edward Cyryl Chumila.


Na Daniel Mbega wa brotherdanny.com

‘WANYAMA wa Msimbazi’ Simba SC ya Tanzania wana rekodi ya pekee katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame, ikiwa ndiyo klabu iliyocheza mechi nyingi zaidi na kutwaa ubingwa mara nyingi pia tangu mashindano hayo yalipoanza rasmi mwaka 1974.

WAZIRI MKUU ETHIOPIA, RAIS KIKWETE WAZINDUA KIWANDA CHA DAWA ZA WADUDU

Waziri Mkuu Ethiopia, Hailemariam Desalegm pamoja na Rais Jakaya Kikwete wakiwasili katika uzinduzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Viuawadudu vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini Kibaha. Kiwanda hiki kinamilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa ushirikiano na Kampuni ya LABIOFAM ya nchini Cuba.

Waziri Mkuu Ethiopia, Hailemariam Desalegm pamoja na Rais Jakaya Kikwete wakiwasili katika uzinduzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Viuawadudu vya Kuua Viluwiluwi wa Mbu mjini Kibaha. Kiwanda hiki kinamilikiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa ushirikiano na Kampuni ya LABIOFAM ya nchini Cuba.

Thursday, 2 July 2015

MTUME MWINGIRA YAMEMKUTA KESI YA KUZAA NA MKE WA MTU, ATAKIWA KUPIMA UKIMWI NA DNA!!

Ile kesi ya zinaa inayomkabili Mtume na Nabii Josephat Mwingira wa Kanisa la Efatha ya kuzini na kuzaa na mke wa mtu bado inamwandama ambapo baada ya Mahakama Kuu kutoa hukumu dhidi ya mapingamizi yao kwa mlalamikaji Dk. William Morris, sasa anatakiwa kuwasilisha majibu ya Vinasaba (DNA) vya mtoto wa miaka 7 aliyezaa na mke huyo wa mtu, Dk. Phillis Nyimbi Morris. Lakini pia anapaswa kupima Ukimwi kwani wawili hao hawakufanya ngono salama na matokeo yake siyo tu kupata mtoto, bali hali ya afya zao kwa vile tayari afya ya mwanamke huyo inadaiwa kuzorota. SOMA ZAIDI HAPA:
PASTOR JOSEPHAT E. MWINGIRA OF THE EFATHA MINISTRY IN TANZANIA
PRESS RELEASE:
PASTOR JOSEPHAT MWINGIRA HEAD OF EFATHA MINISTRIES IN TANZANIA SUFFERS A MAJOR COURT DEFEAT IN THE ONGOING ADULTERY  CASE AGAIST HIM.

SUMAYE ULISHINDWA VIPI KUPAMBANA NA RUSHWA ILIYOMALIZA MASHIRIKA YETU!?

Mawaziri Wakuu wa zamani, Frederick Sumaye (kulia) na Edward Lowassa wakifurahi pamoja mjini Dodoma wakati wa kurejesha fomu za kuwania kuteuliwa kugombea urais kupitia Chaa cha Mapinduzi (CCM).

Na Daniel Mbega
“Sumaye ahofia nchi kuongozwa na wauza dawa za kulevya”, “Sumaye: Rushwa ikizidi CCM nitajiondoa,” “Rushwa kuiweka CCM njiapanda,” “Sumaye: Epukeni wanaotoa fedha kwa kutumia mgongo wa zawadi,” “Sumaye kukimbia ufisadi CCM,” “Sumaye aanika mambo mazito,” “Sumaye-Wanaokerwa na maneno yangu waache kula rushwa,” “Sumaye awaonya urais 2015,” “Sumaye: Sijawahi kutoa, kupokea rushwa,” “Sumaye amshangaa Kikwete, ni kuhusu rushwa,” “Sumaye: Rushwa kwenye chaguzi, ufisadi vyanichukiza,” “Sumaye: Rushwa ikizidi CCM nitajiondoa.”
Hivi ni baadhi tu ya vichwa vya habari ambavyo nimekuwa nikivishuhudia kwenye vyombo vya habari kwa kipindi cha miaka mitatu sasa. Habari hizi zote zinamnukuu Waziri Mkuu mstaafu Frederick Tluway Sumaye, akisema kwa uchungu sana kuhusu masuala ya rushwa kwenye chaguzi mbalimbali pamoja na ufisadi.

TFF YATUMA SALAM ZA RAMBI RAMBI KWA MWAKELEBELA, MWAMBUSI

Frederick Mwakalebela

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Mwesigwa Selestine ametuma salamu za rambi rambi kwa famili aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela kufuatia kufiwa na baba yake mzazi jana mjini Irinnga na mazishi yakitarajiwa kufanyika kesho mjini Iringa.

STARS YAWAFUATA THE CRANES

Kocha mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa (katikati) akiongea na waandishi wa habari leo

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager inaondoka nchini leo jioni kuelekea Kampala - Uganda kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano dhidi ya The Cranes siku ya Jumamosi.

SIKIKA JOB RE-ADVERTISED, DEADLINE JULY 13TH, 2015

Join us in advocating for quality health services for all Tanzanians 
                    
Introduction
Sikika is a non-governmental organization that advocates for quality health services for all Tanzanians. For more information on our work please visit us at www.sikika.or.tz. 

PROF. MWANSOKO: UTAMADUNI UNASAIDIA KATIKA ULINZI NA USALAMA WA NCHI


 Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Major General G.S Milanzi kulia akiongea na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Helmas Mwansoko kushoto kabla ya Prof. Mwansoko kutoa Mhadhara juu ya Utamaduni unavyochangia katika usalama na ulinzi wa Nchi kwa Viongozi wa Ulinzi na usalama wa ndani na nje ya nchi pamoja na Taasisi za umma.Mhadhara huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo.

BOSS WA UN, ALVARO RODRIGUEZ ATEMBELEA SABASABA, ASEMA MAONYESHO NI FURSA YA KUJIFUNZA

IMG_5941
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Jacqueline Mneney Maleko (wa tatu kushoto) akiongozana na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili katika viwanja vya maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara 'Sabasaba', barabara ya Kilwa, jijini Dar.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

ELUMELU CALLS FOR AN END TO ENERGY POVERTY

Pix 1
L-R: Former president of Ghana John Kufuor; President of Cote D'Ivoire Alassane Ouattara, Co-Chair of the Africa Energy Leaders Group (AELG); Tony O. Elumelu, Chairman of Heirs Holdings and Co-Chair of the AELG; Vice President of Nigeria Yemi Osinbajo during the inaugural meeting of the AELG held in Abidjan yesterday to discuss regional solutions to the electricity deficit in Africa.

Wednesday, 1 July 2015

MABIBO BEER YAIDAI TUME YA USHINDANI SHILINGI TIRIONI MOJA, YASEMA IMEKWAMISHWA KUJENGA VIWANDA VITATU NCHINI

 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, James Rugemalira akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu kupinga uamuzi wa Tume ya Ushindani (FCC)  na kuidai fidia hiyo ya Shs. 1 trilioni kutokana na hasara wanayoipata kwa kuruhusu bia ya Windhoek kuingia katika soko la Tanzania kiholela.

AIRTEL YAINGIA MKATABA NA FINCA WA KUTOA HUDUMA ZA KIFEDHA

 Meneja Mahusiano wa Kampuni ya simu ya Airtel, Jackson Mmbando (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu ushirikiano wa Airtel na Finca kutoa huduma za kifedha. Kutoka kulia ni , Vivian Temi na Meneja wa Huduma ya Airtel Money, Stephen Kimea.

WARSHA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA GFCS BARANI AFRIKA


 Baadhi ya wanawarsha kutoka Malawi na Tanzania wakati wa warsha ya kisayansi kuhusu huduma za hali ya hewa kupitia modeli ya ‘PRECIS’.

BENDERA AIPONGEZA TFF

Joel Bendera

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dokta Joel Bendera ameipongeza TFF kwa kuandaa mashindano ya ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 13 (U-13),  na maandalizi ya timu hiyo kwa ajili ya kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika za vijana chini ya miaka 17 zitakazofanyika mwaka 2019 nchini Tanzania.

CECAFA YATOA RATIBA YA KAGAME 2015

Leodgar Tenga, Rais wa Cecafa

Rais wa Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, Leodgar Tenga leo ametangaza kuanza kwa michuano ya kombe la Kagame itakayoanza kutimua vumbi Julai 18, 2015 na kumalizika Agosti 2 mwaka huu jijii Dar es salaam.

TBL YAKABIDHI MSAADA WA KISIMA CHA SH. MIL. 65 RUFIJI


 Mkuu wa Wilaya ya Rufiji , Nurdin Babu akiwa na Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakifungua maji ya bomba mara baada ya makabidhiano ya kisima kilichochimbwa na TBL kwa gahrama ya shilingi mil. 65 katika Kijiji cha Mwaseni Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani. Makabidhiano hayo yalifanyika kijijini hapo mwishoni mwa wiki.

MRATIBU MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA TANZANIA ATEMBELEA BANDA LA MODEWJIBLOG MAONYESHO YA SABASABA LEO

IMG_6278
Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akisalimiana na Mwandishi mwandamizi wa mtandao wa habari wa Modewjiblog, Andrew Chale alipotembelea katika banda la mtandao huo ambao mwaka huu mwezi Septemba unatimiza miaka 7 tangu kuanzishwa ambapo wametumia fursa ya maonyesho ya saba saba kukutana na wadau mbalimbali wanaotumia mtandao huo kupata habari mbalimbali sambamba na kubadilishana mawazo na ushauri wa maboresho ya kazi. Kushoto aliyefuatana naye ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu. Kulia ni mdau wa karibu na mshauri wa mtandao wa habari Modewjiblog, Lemmy Hipolite.

KESI YA ULAWITI YA NTIMIZI KUTAJWA TENA JULAI 6

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Uyui, Mussa Ntimizi
.
Na Hastin Liumba, TaboraKESI ya kulawiti inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Uyui mkoani Tabora Mussa Ntimizi imezidi kupigwa kalenda baada ya kuahirishwa tena hadi Julai 6 mwaka huu baada ya upande wa mashtaka kushindwa kukamilika kwa ushahidi.

LG YATOA PUNGUZO KABAMBE LA BEI YA BIDHAA ZAKE KIPINDI HIKI CHA RAMADHANI NA SABASABA

IMG_5470
Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya MeTL Group, Bi. Fatema Dewji-Jaffer akipokea taarifa ya shughuli mbalimbali zinazoendelea kwenye maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba” kwa mmoja wa maafisa wa kampuni ya bidhaa za LG Tanzania ambapo kampuni ya Mohammed Enterprises Limited Tanzania (MeTL) ndio msambazaji rasmi wa bidhaa hiyo nchini kabla ya hafla fupi ya uzinduzi wa friji mpya ya LG yenye milango pacha aina ya “Velvet Gardenia na Coral Irish”.

UN TANZANIA YAKUSANYA MAONI KUHUSU UTENDAJI WAKE NCHINI NDANI YA SABASABA, KARUME HALL

IMG_5730
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akimwelekeza Mkurugenzi wa kampuni ya Events World, Dimo Debwe Mitiki, jinsi ya kuwasilisha maoni yake kuhusiana na kazi za Umoja wa Mataifa na nini angependa Umoja huo ufanye zaidi kwa ajili ya watanzania kwenye viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa maarufu kama “Sabasaba”. (Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).

NSSF YATOA HUDUMA ZA AFYA BURE MAONESHO YA SABASABA 2015

Dk. Suzan Lymo toka Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam (wa kwanza kulia) akimuhudumia mteja akipatiwa huduma za afya bure zinazotolewa na NSSF.  
Dk. Suzan Lymo toka Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam (wa kwanza kulia) akimuhudumia mteja akipatiwa huduma za afya bure zinazotolewa na NSSF.

HIKI NDICHO KIVUMBI CHA WAGOMBEA URAIS 42 WA CCM!

Raisi wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akikabidhi fomu ya kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar kupitia CCM kwa katibu mkuu wa chama hicho Zanzibar Vuai Ali Vuai, baada ya kukamilisha taratibu za kutafuta wadhamini katika Mikoa ya Zanzibar.Picha na Mwinyi Sadallah 
Na Kalunde Jamal
Dar. Hiki ni kivumbi. Kati ya wagombea 42 waliojitokeza kuwania urais kupitia CCM, anatakiwa kubaki mmoja tu na mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu unafungwa kesho.

ETI UNAWEZA KUISHI UKIWA UCHI!?

Mwandishi Mark Haskel Smith
Watu wengi wasingejihisi vyema kuvua nguo zao zote na kusalia uchi wa mnyama katika maeneo ya uma,lakini kwa wengine ni maisha yao.

NDEGE YA JESHI YAUA 100 INDONESIA


Takriban watu 100 wameuawa baada ya ndege ya uchukuzi wa kijeshi ya Indonesia kuanguka mapema leo katika maeneo yenye makazi ya watu huko Medan Sumatra.

WARUNDI 10,000 WAKIMBIA NCHI JUMAPILI

Wakimbizi wa Burundi
Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa{UNHCR} linasema karibu raia 10,000 wa Burundi walikimbia nchi hiyo wikendi iliyopita kabla ya uchaguzi wa ubunge.