Profesa Muhongo siku alipotangaza kujiuzulu Januari 24, 2015
Na Daniel Mbega
RAIS Dk.
John Magufuli amemrejesha Profesa Sospeter Muhongo katika Wizara ya Nishati na
Madini huku akijaza sura ngeni nyingi katika Baraza lake jipya la Mawaziri
lenye wizara 18 tu.
Profesa
Muhongo alijiuzulu uwaziri Januari 24, 2015 kufuatia kashfa ya ufisadi wa fedha
za akaunti ya Tegeta Escrow na akasema
siku hiyo kwamba uamuzi wake ulikuwa wa nia njema kabisa ili kupoza mvutano
uliokuwepo baina ya serikali na Bunge.
Lakini
waziri huyo atakumbukwa kutokana na mvutano uliowahi kutokea baina yake ya
wawekezaji wazawa kuhusu ukodishaji wa vitatu vya mafuta na gesi Kusini mwa
Tanzania, hivyo kurejea kwake kunaonyesha kutowafurahisha baadhi ya mahasimu
wake ambao walisherehekea pindi alipojiuzulu.
Wakati
Muhongo akireshwa Nishati na Madini, Dk. Magufuli amewachukua mawaziri 12 tu
waliokuwa kwenye serikali iliyopita huku wengi akiwapandisha kutoka unaibu hadi
uwaziri kamili.
Mawaziri
waliorejea tena katika baraza jipya ambalo bado halijawapata mawaziri wanne ni
George Simbachawene aliyekuwa Nishati na Madini, ambaye sasa atakuwa Ofisi ya
Rais pamoja na Angela Kairuki wakishughulikia Utumishi na Utawala, Jenista
Mhagama yeye amebaki Ofisi ya Waziri Mkuu akiwa ameongezewa majukumu ambapo sasa
atashughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu na hana msaidizi.
January
Makamba, ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
sasa ni waziri kamili wa Ofisi ya Makamu wa Rais akishughulikia Muungano na
Mazingira ambapo atasaidiwa na Luhaga Mpina.
William
Lukuvi amebaki kwenye Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi ambapo atasaidiwa na
Angelina Mabula wakati ambapo Dk. Hussein Mwinyi amebaki kwenye Wizara ya
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Charles
Kitwanga, Mbunge wa Misungwi, amepewa Wizara ya Mambo ya Ndani wakati Dk.
Harrison Mwakyembe amekwenda Wizara ya Katiba na Sheria.
Mwigulu
Nchemba, ambaye alikuwa naibu waziri wa fedha, sasa amepandishwa na kuwa Waziri
wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, ambapo naibu wake ni William Tate Ole Nashon,
wakati Charles Mwijage, ambaye alikuwa naibu katika Wizara ya Nishati na
Madini, amepandishwa na kuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Ummy
Mwalimu amerejeshwa katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
lakini sasa atashughulikia pia Afya na Wazee. Atasaidiwa na Mbunge wa Nzega
Vijijini, Dk. Hamis Kigwangalla.
Wizara ya
Sayansi, Teknolojia, Elimu na Ufundi bado haijapata waziri, lakini naibu wa
wizara hiyo ni Injinia Stella Manyanya.
Wizara ya
Maliasili na Utalii haijapata waziri, lakini naibu ni Injinia Ramo Makani.
Wizara ya Fedha na Mipango nayo haina waziri bado, lakini naibu wake ni Dk.
Ashantu Kijachi, wakati Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano iliyokuwa
ikiongozwa na Magufuli mwenyewe bado nayo haina waziri ingawa naibu wake ni
Edwin Ngonyani.
Mawaziri
wapya walioingia ni Balozi Augustino Mahiga ambaye ataongoza Wizara ya Mambo ya
Nje na EAC na Uhusiano wa Kimataifa huku naibu wake akiwa Dk. Suzan Kolimba.
Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa NEC ya CCM, Nape Nnauye, amepewa Wizara ya Utamaduni,
Sanaa na Michezo ambapo anakabiliwa na changamoto kubwa ya kusimamia sekta hizo
zinazoonekana kudorora kwa muda mrefu sasa.
Orodha
kamili ya baraza hilo ni:
Wizara ya Mambo ya Nje na EAC/ Kimataifa
Waziri -
Augustino Mahiga
Naibu
Waziri - Dk. Suzan Kolimba
Wazara wa Utamaduni, Sanaa na michezo
Waziri-Nape
Nnauye
Wizara ya Nishati na Madini
Waziri -
Sospeter Muhongo
Naibu
Waziri-Medard Kalemani
Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu
Waziri
-Jenista Mhagama
Wizara ya ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala
Mawaziri
wawili – George Simbachawene na Angela Kairuki
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
Waziri -
January Makamba
Naibu
waziri - Luhaga Mpina.
Wizara ya Mambo ya Ndani
Waziri ni
Charles Kitwanga
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi
Waziri - William
Lukuvi
Naibu - Angelina
Mabula
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Waziri – Dk.
Hussein Mwinyi
Wizara ya Katiba na Sheria
Waziri -
Harrison Mwakyembe
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Waziri-
Mwigulu Nchemba
Naibu
Waziri- William Tate Ole Nashon
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
Waziri -
Charles Mwijage
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto
Waziri -
Ummy Mwalimu
Naibu - Dk
Hamis Kigwangalla
Wizara ya Sayansi, Teknolojia, Elimu na Ufundi
Waziri -
bado hajapatikana
Naibu
Waziri - Stella Manyanya
Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri -
bado hajapatikana
Naibu
Waziri - Injinia Ramo Makani
Waziri wa Fedha na Mipango
Waziri -
bado hajapatikana
Naibu
Waziri - Dk. Ashantu Kijachi
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Waziri -
bado hajapatikana
Naibu
Waziri -Edwin Ngonyani
No comments:
Post a Comment