Na Krantz Mwantepele, KAHAMA
Mkutano mkuu wa
Kijiji cha Nyandekwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga uliofanyika mwishoni wa
mwezi wa tisa umeazimia kuwashikinikiza wazazi wa kijiji hicho kuwapeleka
watoto wao shule Azimio hilo Pia
limeelekezwa kwa vijana wanaokaa
vijiweni kuwataka kushirki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na sio kukaa
vijiweni pia kushiriki katika mikutano mbali mbali ya kijiji kujua maendeleo ya
kijiji Iikihusisha mapato na matumizi.
Mkutano huo
umepitisha maazimio matano yanayolenga
kurejesha nidhamu Na heshima kijijini Nyandekwa hatua hiyo imefikiwa Kutokana
Na wananchi wa kijiji hiki kutoona umuhimu wao kuchukua hatua za kujikwamua
kiuchumi na pia Kuwa na ujasiri wa kuhoji mapato na matumizi kwa ajili ya
kijiji chao .
Hali hiyo
inatokana na juhudi za dhati bila kukata tamaa zilizofanywa waraghabishi na watetezi wa haki za binadamu wa kijiji
hicho akiwemo Miriam Stefano, Boniface Izengo , Matilda Peter ,Na Mwenyekiti Wa
kitongoji cha Busolwa Bi Ana Alphonce kuwapa
ujasiri na elimu ya uraia wananchi
wenzao ili wawe chachu ya maendeleo.
Kwa mujibu wa bi
Anna Alphonce ambaye pia ni mwenyekiti wa kitongoji cha Busolwe aliweza kuongea na mtandao wa
Mwanaharakati Mzalendo Blog alisema kupitia mikutano mbalimbali ya kijiji
aliweza kutoa hamasa kwa wanawake na wanaume wa kijiji hicho kushiriki katika
uchaguzi mkuu uliopita katika kusikiliza sera za viongozi na mwishowe kushiriki
kupiga kura.Na kwa muda mfupi aliweza kufanikisha wanawake wengi kushiriki
katika maamuzi ya kijiji pia kuwa na ujasiri wa kuhoji katika mikutano ya
kijiji.
Wengi wa
wanakijji ambao wamekuwa waraghabishi katika kijiji hiki waliweza kupata
mafunzo haya ya uraghabishi ambapo waliweza kujua baadhi ya haki zao na kuwa na
uajasiri wa kuhoji mapato na matumizi ya kijiji hicho ambapo mwanzoni walikuwa
hawapati fursa hiyo kwa wakati .Waraghabishi hawa wamekuwa chachu ya maendeleo
ya kijiji cha Nyandekwa katika sekta za kiuchumi ,kisiasa na kijamii kwa kuwaelimisha
wanakijiji wenzao haki na wajibu wao kwa nafasi kubwa .
“Viongozi wa
kijiji hiki hawakuweza kutupa mrejesho wa kila jambo linalofanyika kwa kijiji
hcetu hasa katika mikutano ya kijiji na sisi tulipoanza kuhoji tulikosa
ushirikiano kwao lakini mwishowe wananchi wengi waliona umuhimu wa
kushirikishwa” alinukuliwa bw. Boniface Izengo mmoja wa waraghabishi wa
kijiji hiki alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii.
Katika hatua
nyingine mmoja wa waraghabishi wa kijiji hiki bi Matilda Peter amekuwa ni mmoja
wa vijana wanaotoa elimu ya uzazi wa mpango kwa makundi rika ambapo hukutana na
vijana hasa wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari na kuwajuza kuhusu
mabadiliko ya mwili yao na pia kuwashauri jinsi ya kuepuka maambukizi magonjwa
ya ngono na mimba zisizotarajiwa.
Maazimio yaliyopitishwa kuwa ni vijana
wanaokaa au kusimama ovyo barabarani na maeneo mengine bila shughuli maalum
kuwajibishwa na pia kuweza kuwawezesha kuwashirikisha katika shughuli za kijiji
hicho ikiwemo kushiriki katika shughuli mbalimbali za uzalishaji kijijini hapo
Pia mkutano wa
kijiji hiki uliazimia kuwa mapato na matumizi kuweza kujadiliwa kwa uwazi na
pia kubandikwa katika mbao za matangazo hapo kijijini kuwezesha wananchi hao
kuweza kusoma na kuelewa kila kinachoendelea kijijini kwao katika swala la
maendeleo ya uchumi .
.
No comments:
Post a Comment